Saturday, 30 April 2016

Bana matumizi.

JIFUNZE KUBANA MATUMIZI.

1.Epuka kununua vitu vya rejareja kwa "Mangi".Ukinunua  nusu nusu kwa Mangi unauziwa bei ya juu japo utaona ni hela ndogo!

2.Weka daftari la matumizi nyumbani��. kila kinachotumika kiandikwe iwe ni pesa au kiasi cha unga, mchele kilichotumika: itasaidia kudhibiti matumizi.

3.Dhibiti pesa za "chenji" zinazorudi dukani hasa sarafu kwa kuziweka mahali maalum.Hizi wengi "huzipotezea" na ukipata dada wa kazi mjanja�� basi hizi hizi mpaka mwisho wa mwezi anajikuta amekusanya nusu ya mshahara ��wake bila wewe kujua! Ndio unashangaa�� unakaa nae miaka na miaka,Wewe unajisifu"nimeishi nae mwaka wa 7 huu,tunaishi kama ndugu��‍❤️‍��"

....lol ndugu my foot��!! ndugu zake wako kijijini huko, hapo yeye anapiga hela wewe kaa tu unashangaa shangaa, kashangae kigamboni daraja jipya ila wezi wa zamani!

4.Nunua mizani ndogo⚖ ya kupimia uzito(bei rahisi) ili kupimia vitu nyumbani.Kuna wakati unapika chakula kingi kwa kukosa kipimo sahihi.

5.Kuwa mbunifu kwa kupendelea mapishi yanayobana matumizi mf: badala ya chips kuku����, unaweza kupika viazi rosti, utakuwa umefidia mafuta! utajiuliza ukipika rosti si nyanya, vitunguu vitahitajika? hata chips kuku utahitaji tomato source/kachumbari

6.Usinunue soda��, tengeneza juice "simpo" mfano juice ya ukwaju��. Watu10 ukiwanunulia soda utakuwa umetumia gharama zaidi kuliko ukitengeneza juice ya ukwaju

7.Mgeni asikulazimishe uharibu bajeti yako, Usijivimbishe kiduva kama alama ya kuuliza kwa kuleta ufahari na kulijaza friji ndiii! yani mpaka mgeni akiondoka una madeni kwa mangi ya mishahara miwili��!.Simaanishi usimkirimu mgeni ila "cheza kwa step"

8.Usinunue maandazi au mkate�� kwa jirani, pika hata chapati za maji asubuhi,utabana matumizi kuliko kununua vitafunwa nje.

9.Usizoeshe watoto tabia ya kuwapa hela hovyo!Kuwa na utaratibu maalumu,sio huyu amekuja anasema umpe mia ya pipi huyu anataka miatano ya chips��..Hata kama unazo jifunze kuwapa kwa utaratibu na hakikisha unaandika✍��.

10.Kama nyumbani nyote mnaondoka asubuhi��,mwambie dada wa kazi azime umeme�� na awashe tu pale anapohitaji!Mara nyingi kuna kuwa na "lose connections" ambazo wakati mwingine zinakula umeme bila kujua, na hii ni kwa sababu hatuna utamaduni wa kufanya checkup ya mifumo ya umeme!

11.��Taa izimwe kila mtu atokapo chumbani, taa iwashwe pale tu watu walipo. mf kwa nini taa ya chooni iwashwe wakati chooni hakuna mtu?haimaanishi tu giza likiingia basi kila taa iwashwe��.Vitu vinavyotumia umeme vizimwe kabla ya kulala isipokuwa vya muhimu kama friji na taa za nje za usalama.

12.Nunua vifaa original����☎-itakupunguzia gharama za matengenezo mara kwa mara

13.Jifunze kufanya matengenezo madogo madogo������ wewe mwenyewe sio hata bulb�� ikiungua kubadilisha mpaka uite fundi.

KAMA MNATAKA MALI.

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI".

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake, nasisitiza, kama mnataka mali mtaipata shambani.

Thursday, 21 April 2016

Fufua message zako!

Jinsi Ya Kufufua Meseji Zilizofutika Katika WhatsApp Kwa Android!

WhatsApp ndio App inayotumika sana katika kutuma na kusoma meseji. Uzuri wa App hii ni kwamba ni rafiki kwa watu kwani ni rahisi sana kuitumia. Kwa hili watu wanaipenda lakini vipi kama ukiwa unataka kupata meseji zako zilizofutika?
Usiwe na wasiwasi itphidel niko  nawe. 

Kama ikikutokea kuwa unahitaji kupata meseji zako ulizozifuta kwa bahati mbaya hata kwa makusudi kuna njia mbadala ambayo unaweza ukaitumia katika kupata meseji hizo.
Jinsi Ya Kufufua Meseji Zilizofutika Katika WhatsApp.


Hapa ntakupa njia mbili ambazo zinaweza zikakusaidia. Njia hizi zitajalisha kama meseji zako zimefutika muda mrefu uliopita au hivi karibuni. Njia mbili zote hizo zina namna yake ya kufanya.


Njia Moja Wapo Ya Kufufua Meseji Za WhatsApp Kwa Kutumia ‘Back Up’
Kama Meseji Imefutika Hivi Karibuni
Ni rahisi sana kufufua meseji katika mtandao wa WhatsApp kama zimefutika ndani ya siku 7. Kila siku WahtsApp huwa wanafanya ‘back up’ ya meseji zako zote na kuzihifadhi katika memori kadi yako. 

Unaweza ukaitumia ‘back up’ hiyo kufufua meseji zako zilizofutika
Ili kulipata meseji zako zilizofutika katika WhatsApp kwa kutumia ‘back up’ uliyoihifadhi fanya hivi; futa WhatsApp yako na kisha ipakue tena katika simu yako. Ukishamaliza kuipakua wakati wa kufungua mtandao huo utakuomba urejeshe taarifa zako. 

Unaweza kurejesha mpaka meseji za siku saba tuu kwa kutumia njia hii
Kama Meseji Imefutika Zaidi Ya Siku 7 zilizopita.


Hapa itakubidi utumie njia nyingine kabisa katik akuhakikisha unapata kuzifufua meseji zako. Taarifa zote ambazo hazikuhifadhiwa hazitaweza kupatikana tena kwa kutumia njia hii
Njia:

1. Shusha ‘File Manager’ kutoka google Play
2. Futa WhatsApp Katika Kifaa chako
3. Kwa kutumia ‘File Manager’ nenda katika faili la /sdcard/WhatsApp
4. Utaona mafaili ambayo yanafana hivi
Mfano Jinsi Faili Hilo Litakavyo Onekana
5. Chagua tarehe yeyoteili kufufua faili la tarehe hiyo. Baada ya hapo badilisha jina la faili hilo kwenda msgstore.db.crypt
6. Weka WhatsApp tena katika kifaa chako na kisha chagua kurudisha taarifa zako (restore). Hapo faili la msgstore.db.crypt ndio litakalojirudisha katika simu yako hivyo utapata meseji zote za siku hiyo kwa mara nyingine tena.


Mpaka hapo utakuwa unaweza kufufua meseji zilizofutika katika WhatsApp. Hii itaweza kukusaidia sana kama kuna meseji ambazo unataka kuzifuta kwa muda au hata zile ambazo umezifuta kwa bahati mbaya. Cha msingi ni kwamba kabla hujafuta WhatsApp yako hakikisha umehifadhi taarifa zako vizuri.

Sunday, 10 April 2016

Wokovu ni nini?

Swali: "Wokovu ni nini?

Jibu: Wokovu ni ukombozi kutokana na hatari au mateso. Kuokoa ni kukomboa au kulinda. Neno wokovu hubeba wazo la ushindi, afya, au kuhifadhi. Wakati mwingine, Biblia inatumia maneno kuokolewa au wokovu kwa kutaja muda, ukombozi wa kimwili, kama vile ukombozi wa Paulo kutoka gerezani (Wafilipi 1:19).

Mara nyingi zaidi, neno "wokovu" huzungumzia umilele wa, ukombozi wa kiroho. Wakati Paulo alimwaambia Mfilipi mfungwa kile lazima akifanye ili aokolewe, alikuwa akimaanisha hatima ya milele ya askari (Matendo 16:30-31). Yesu alilinganisha kuokolewa na kuingia ufalme wa Mungu (Mathayo 19:24-25).

Sisi tumeookolewa kutoka kwa? Katika mafundisho ya kikristo ya wokovu, sisi tumeokolewa kutoka kwa "ghadhabu," yaani, hukumu ya Mungu kwa dhambi (Warumi 5:9, 1 Wathesalonike 5:9).

Dhambi yetu imetutenganisha na Mungu, na matokeo ya dhambi ni mauti (Warumi 6:23). Wokovu wa kibiblia wahusu ukombozi wetu kutokana na matokeo ya dhambi na kwa hiyo unahusisha kuondolewa kwa dhambi.

Nani anaokoa? Mungu tu ndiye anaweza kuondoa dhambi na atuokoe na adhabu ya dhambi (2 Timotheo 1:9, Tito 3:5).

Ni namna gani Mungu anaokoa? Katika mafundisho ya kikristo ya wokovu, Mungu ametuokoa kwa njia ya Kristo (Yohana 3:17).

Hasa, ni kifo cha Yesu msalabani na kilichofuatwa na kufufuka kwake ndio kilifikia mafanikio ya wokovu wetu (Warumi 5:10, Waefeso 1:7).

Maandiko yako wazi kwamba wokovu ni neema, zawadi tusiyostahili kutoka kwa Mungu (Waefeso 2:5, 8) na unapatikana tu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo (Matendo 4:12).

Je, sisi hupokea wokovu namna gani? Sisi tumeokolewa kwa imani. Kwanza, ni lazima tuisikie injili- habari njema ya kifo cha Yesu na ufufuo wake (Waefeso 1:13). Basi, ni lazima tumwamini -kikamilifu Bwana Yesu (Warumi 1:16).

Hii inahusisha toba, mabadiliko ya akili juu ya dhambi na Kristo (Matendo 3:19), na kulitia jina la Bwana (Warumi 10:9-10, 13).

Ufafanuzi wa kikristo wa mafundisho ya wokovu itakuwa "ukombozi, kwa neema ya Mungu, kutokana na adhabu ya milele ya dhambi ambayo ni nafasi kwa wale ambao hukubali kwa imani masharti ya Mungu ya toba na imani katika Bwana Yesu."

Ukombozi unapatikana katika Yesu peke yake (Yohana 14:6; Matendo 4:12) na Mungu anategemewa kuutoa, uhakikisho na usalama.

UBARIKIWE SANA. Ameen!

Saturday, 9 April 2016

15 HACKING OS.


Today we are discussing about top 15 advanced operating systems which has great penetration testing or ethical hacking tools. the top Os on this list is my favorite Linux distro Kali Linux because it is very popular in pentesting and it is developed by the same team of BackTrack (Offensive security). i am not including BackTrack on this list because it is no more available officially on their website and the next version of BackTrack is Kali Linux. 

The listed operating systems are here based on Linux kernel so it is all free operating systems. (Included download links for all Os) :)

I am recommending you to read my earlier post to understand more about Linux distros related to hacking security: Linux Powerful Distros For Hacking Or Security: Kali, Tails And Qubes

Recommended: Become a Hacker: Best 20 Tips for Beginners to Start Learning

1. Kali Linux


Kali Linux is a Debian-derived Linux distribution designed for digital forensics and penetration testing. It is maintained and funded by Offensive Security Ltd. Mati Aharoni and Devon Kearns of Offensive Security developed it by rewriting BackTrack. Kali Linux is the most versatile and advanced penetration testing distro. Kali updates its tools and it is available for many different platforms like VMware and ARM. if you want to know more about Kali Linux then i recommend you read my previous article: An Introduction To Hacker’s OS Kali Linux And Setup Tutorial.

Click here to download


2. BackBox 


It includes some of the most used security and analysis Linux tools, aiming to a wide spread of goals, ranging from web application analysis to network analysis, from stress tests to sniffing, including also vulnerability assessment, computer forensic analysis and exploitation.

The power of this distribution is given by its Launchpad repository core constantly updated to the last stable version of the most known and used ethical hacking tools. The integration and development of new tools inside the distribution follows the commencement of open source community and particularly the Debian Free Software Guidelines criteria.

Click here to download

3. Parrot-sec forensic os


Parrot Security is an operating system based on Debian GNU/Linux mixed with Frozenbox OS and Kali linux in order to provide the best penetration and security testing experience. it is an operating system for IT security and penetration testing developed by the Frozenbox Dev Team. It is a GNU/Linux distribution based on Debian and mixed with Kali. 

Parrot uses Kali repositories in order to take latest updats for almost all the tools, but it also has its own dedicated repository where all the custom packets are kept. This is why this distro is not just a simple Kali “mod” but entire new concept which relies on Kali’s tool repositories. As such, it introduces a lot of new features and different developing choices.Parrot uses MATE as a Desktop Environment. Lightweight and powerful interface is derived from famous Gnome 2, and thanks to FrozenBox highly customizable with captivating icons, ad-hoc themes and wallpapers. System look is proposed and designed by the community members and also members of Frozenbox Network, who are closely following the development of this project.

Click here to download

4. DEFT



Deft is Ubuntu customization with a collection of computer forensic programs and documents created by thousands of individuals, teams and companies. Each of these works might come under a different licence. There Licence Policy describe the process that we follow in determining which software we will ship and by default on the deft install CD.

Click here to download

5. Live Hacking OS


As i am said before Live Hacking OS is also based on linux which has big package of hacking tools useful for ethical hacking or penetration testing. It includes the graphical user interface GNOME inbuilt. There is a second variation available which has command line only, and it requires very less hardware requirements.

Click here to download

6. Samurai Web Security Framework


The Samurai Web Testing Framework is a live linux environment that has been pre-configured to function as a web pen-testing environment. The CD contains the best of the open source and free tools that focus on testing and attacking websites. In developing this environment, we have based our tool selection on the tools we use in our security practice. We have included the tools used in all four steps of a web pen-test.

Click here to download

7. Network Security Toolkit (NST)


Network Security Toolkit (NST) is a bootable live CD based on Fedora Core. The toolkit was designed to provide easy access to best-of-breed open source network security applications and should run on most x86 platforms. The main intent of developing this toolkit was to provide the network security administrator with a comprehensive set of open source network security tools. 

What we find rather fascinating with NST is that we can transform most x86 systems (Pentium II and above) into a system designed for network traffic analysis, intrusion detection, network packet generation, wireless network monitoring, a virtual system service server, or a sophisticated network/host scanner.

Click here to download

8. Bugtraq


Bugtraq is an electronic mailing list dedicated to issues about computer security. On-topic issues are new discussions about vulnerabilities, vendor security-related announcements, methods of exploitation, and how to fix them. It is a high-volume mailing list, and almost all new vulnerabilities are discussed there.

Bugtraq team is experienced freaks and developers, It is available in Debian, Ubuntu and OpenSuSe in 32 and 64 bit architectures.

Click here to download

9. NodeZero


It is said the necessity is the mother of all invention, and NodeZero Linux is no different. There team is built of testers and developers, who have come to the census that live systems do not offer what they need in their security audits. Penetration Testing distributions tend to have historically utilized the “Live” system concept of linux, which really means that they try not to make any permanent effects to a system. Ergo all changes are gone after reboot, and run from media such as discs and USB’s drives. However all that this maybe very handy for occasional testing, its usefulness can be depleted when your testing regularly. Its there believe that “Live System’s” just don’t scale well in a robust testing environment.

All though NodeZero Linux can be used as a “Live System” for occasional testing, its real strength comes from the understanding that a tester requires a strong and efficient system. This is achieved in our belief by working at a distribution that is a permanent installation, that benefits from a strong selection of tools, integrated with a stable linux environment.

Click here to download

10. Pentoo


Pentoo is a Live CD and Live USB designed for penetration testing and security assessment. Based on Gentoo Linux, Pentoo is provided both as 32 and 64 bit installable live cd. Pentoo is also available as an overlay for an existing Gentoo installation. It features packet injection patched wifi drivers, GPGPU cracking software, and lots of tools for penetration testing and security assessment. The Pentoo kernel includes grsecurity and PAX hardening and extra patches - with binaries compiled from a hardened toolchain with the latest nightly versions of some tools available.

Click here to download

11. GnackTrack


GnackTrack is an open and free project to merge penetration testing tools and the linux Gnome desktop. GnackTrack is a Live (and installable) Linux distribution designed for Penetration Testing and is based on Ubuntu.

Backtrack is not only a single player in the field of ethical hacking, so you can try some other distribution as well, if you are Gnome lover than must try this, however backtrack 5 is also available on Gnome platform. Just like backtrack, Gnacktrack comes with multiple tools that are really helpful to do a effective penetration testing, it has Metasploit, armitage, wa3f and others wonderful tools.

Click here to download

12. Blackbuntu



Blackbuntu is distribution for penetration testing which was specially designed for security training students and practitioners of information security. Blackbuntu is penetration testing distribution with GNOME Desktop Environment. It's currently being built using the Ubuntu 10.10 and work on reference Back|Track.

Click here to download

13. Knoppix STD


Knoppix STD (Security Tools Distribution) is a Live CD Linux distribution based on Knoppix that focused on computer security tools. It included GPL licensed tools in the following categories: authentication, password cracking, encryption, forensics, firewalls, honeypots, intrusion detection system, network utilities, penetration, packet sniffers, assemblers, vulnerability assessment and wireless networking. Knoppix STD version 0.1 was published January 24, 2004, on Knoppix 3.2. Thereafter, the project stagnated, lacking updated drivers and packages. A release date for version 0.2 has not yet been announced. A list of tools is available on the official website.

Click here to download

14. Weakerth4n


Weakerth4n is a penetration testing distribution which is built from Debian Squeeze.For the desktop environment it uses Fluxbox.This operating system is ideal for WiFi hacking as it contains plenty of Wireless tools. It has a very well maintained website and a devoted community. Built from Debian Squeeze (Fluxbox within a desktop environment) this operating system is particularly suited for WiFi hacking as it contains plenty of Wireless cracking and hacking tools.

Tools includes: Wifi attacks, SQL Hacking, Cisco Exploitation, Password Cracking, Web Hacking, Bluetooth, VoIP Hacking, Social Engineering, Information Gathering, Fuzzing Android Hacking, Networking and creating Shells.

Click here to download

15. Cyborg Hawk


The most advanced, powerful and yet beautiful penetration testing distribution ever created. Lined up with ultimate collection of tools for pro Ethical Hackers and Cyber Security Experts. It has 700 + tools while Kali have 300+ and also dedicated tools for and menu for mobile security and malware analysis . Also it is easy to compare it with Kali as to make a better OS than Kali we have to outperform it. It is a new operating system based on Ubuntu linux, i am not tested this OS that is why i placed it in the last of this list.

Cyborg Hawk is developed by Team Cybord led by Vaibhav Singh and Shahnawaz Alam from Ztrela Knowledge Solutions Pvt. Ltd.

Click here to download

Also Read:

Best 10 Lightweight Portable Operating Systems Available In 2016Become a Hacker!, What does Exactly Mean by a Hacker ?The Reason Behind Why Hackers Using Linux As Their Primary OS

SHARE THIS:

    

30 Helpful Nmap Commands For Pentester or System Admins

Become A Hacker: Top Books To Learn Ethical Hacking

How to Spoof Caller ID to Make Free Calls - VoIP Pentesting

The World Of Software

You Can Also CheckTop 10 Penetration Testing / Hacking OS Operating System 2016



"Penetration testing " is best way for removing all weak points,.








JIFUNZE IT

Je, unapenda kutengeza kitu chako ambacho umekitolea jasho?

Je, unapenda kujifunza technology mbalimbali hususani za kompyuta?

Je, unapenda kujua jinsi website zinavo fanya kazi.Basi hii thread ina kufaa?

Habari marafiki?

Katika hii course ningependa kuelekeza jinsi ya kutengenza website na iliyokua na ubora wa hali ya juuambayo inyoweza kuonekana na kila kifaa ikiwemo simu na Kompyuta.

BAADA YA KUJIFUNZA HII TEKNOLOJIA UTAPATA NINI.

1. Baada ya kujifunza hii lugha utakua una uwezo wa kutengeneza page yako amboya una weza kuweka taarifa zako.

2. Utaweza kuweika page au website yako online ili iweze kuonekana na kila mmoja.

3. Utaweza kupata ujuzi wakuandika html na css code.

4. Utaweza kua freelancer wa kudesign pages za aina mbalimbali.

HII COURSE IME MLENGA NANI ?

Hii course ime mlenga mtua mbaye hajui chochote kuhusu website wala code ila anachojua ni ana kompyuta na ana itumia kwa matumizi ya kawaida tu.

Hii course ime mlenga mtu ambaye anae hitaji kujua nini maana ya html na css na nini maana ya website.

VIFAA UNAVO TAKIWA KUWA NAVYO

1. Uwezo wa kutumia kompyuta.

2. Uwe na kompyuta.

3. Uwe na notepad ya kompyuta au notepad++ kwa kudownload.

UTANGULIZI WA HTML.

Nini maana ya HTML ?

HTML ni lugha inayo eleza nyarakaka za mtandao (web documents) au kurasa zinazo patikana mtandaoni (web pages).

HTML kirefu chake ni HYPER TEXT MARKUP LANGUAGE.

Nyaraka za HTML zina vitambulisho vya HTML (html tags).

Kila vitambulisho(tag) vinaeleza nyaraka zilizomo.

Mfano wa html.

<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title>Ni website yangu ya kwanza</title>
</head>
<body>

<h1>Karibu katika page yangu</h1>
<p>katika page hii nitaeleza kuhusu jinsi ya kutengeneza website</p>

</body>
</html>

MAELEZO YA MFANO.

· !DOCTYPE inaelezea aina ya nyaraka (document) na hiyo ni html.

Kati ya nakala <html> na </html> inaelezea nyaraka (document) za HTML.

Kati ya nakala <head> na </head> inaeleza taharifa kuhusu nyaraka (document).

Kati ya nakara <title> na </title> inaeleza (title) kichwa cha nyaraka(document).

Kati ya nakala <body> na </body> inaeleza kurasa inayoonekana (visible page).

Kati ya nakala <h1> na </h1> inaeleza viongozi (heading).

Kati ya nakala <p> na </p> inaeleza aya (paragraph).

Kutumia maelezo haya browser inaweza kuonesha nyaraka na viongozi (heading) na aya (paragraph).

HTML Tags.

Tags ni vitambulisho.

HTML tags ni maneno (keywords) au (jina la vitambulisho ) tags name lililo zunguukwa na pembe mabano (angle brackets).

<jina la kitambulisho> yaliyomo </jina la kitambulisho>

HTML tags kwa kawaida zina kuja kwa jozi(pairs) kama <h1> na </h1>.

Tag ya kwanza kwenye jozi(pair) ni tag ya kuanza nay a pili ni yaku funga.

Tag yakufunga inaandikwa kama ya kufungua ila ina wekwa alama ya / kabla ya jina la kitambulisho aut tag.

WEB BROWSERS.

Kazi ya web browsers ni kusoma kusoma nyaraka za HTML na kuzionesha.

Browser hai oneshi html tags lakini inazitumia ili kuonesha nyaraka (document).

Mfano hapo juu utaonekana kama hivi.

Karibu katika page yangu

katika page hii nitaeleza kuhusu jinsi ya kutengeneza website

Browser in onesha sehem ya <body></body> tu.

Huitwaji wa <!DOCTYPE>

Huitwaji wa <!DOCTYPE> unasaidia browser kuonesha kurasa za mtandao (Web page) kuonesha sawia.

Kuna aina ya nyaraka mbalimbali mtandaoni.

Kuonesha nyaraka sawia,browser inahitaji kujua aina na version.

Uitwaji wa doctype sio kesi nyeti (case sensitive),kesi zote zina kubalika.

Mfano.

<!DOCTYPE HTML>

<!DOCTYPE html>

<!DOCTYPE Html>

Uitwaji wa kawaida.

HTML 5

<!DOCTYPE html>

HTML 4.01

<!DOCTYPE HTML PUBLIC "-//W3C//DTD HTML 4.01 Transitional//EN" "http://www.w3.org/TR/html4/loose.dtd">

XHTML 1.0

<!DOCTYPE html PUBLIC "-//W3C//DTD XHTML 1.0 Transitional//EN" "http://www.w3.org/TR/xhtml1/DTD/xhtml1-transitional.dtd">

Kwenye course hii tutatumia HTML 5.

AINA ZA HTML | HTML VERSIONS

Version

HTML

Year
1991

Version
HTML 2.0
Year
1995

Version
HTML 3.2
Year
1997

Version
HTML 4.01
Year
1999

Version
XHTML
Year
2000

Version
HTML5
Year
2014

Itaendelea .... usually visit my blog

elisanteblog.blogspot.com

Tuesday, 5 April 2016

Whatsap privacy and security.


WhatsApp Calling lets you talk to your friends and family, even if they're in another country. Just like your messages, WhatsApp calls are end-to-end encrypted so WhatsApp and third parties can't listen to them.

Messages that Stay with You
Your messages should be in your hands. That's why WhatsApp doesn't store your messages on our servers once we deliver them, and end-to end encryption means that WhatsApp and third parties can't read them anyway.

See for Yourself WhatsApp lets you check whether the calls
you make and messages you send are end- to-end encrypted. Simply look for the indicator in contact info or group info.

Get the Details Read an in depth technical explanation of WhatsApp's end-to-end encryption, developed in collaboration with Open Whisper Systems.

Privacy and Security is in our
DNA From day one, we built WhatsApp to help you stay in touch with friends, share vital information during natural disasters, reconnect with separated families , or seek a better life .

Some of your most personal moments are shared with WhatsApp, which is why we built end-to-end encryption into the latest versions of our app. When end-to-end encrypted, your messages, photos, videos, voice messages, documents, and calls are secured from falling into the wrong hands.

Security by Default WhatsApp's end-to-end encryption is available when you and the people you message use the latest versions of our app.

Many messaging apps only encrypt messages between you and them, but WhatsApp's end- to-end encryption ensures only you and the person you're communicating with can read what is sent, and nobody in between, not even WhatsApp.

This is because your messages are secured with a lock, and only the recipient and you have the special key needed to unlock and read them.

For added protection, every message you send has its own unique lock and key. All of this happens automatically: no need to turn on settings or set up special secret chats to secure your messages.

Usually visit my blog and enjoy!

Whatsapp sasa yaboreshwa.

WhatsApp yaboreshwa: Sasa Mazungumzo yako Yapo Salama Zaidi.

WhatsApp leo wamewatangazia watumiaji wake juu ya maboresho waliyoyafanya ambapo kwa sasa si wao (WhatsApp) wala mitandao ya simu/serikali itaweza kuona chats au kusikiliza maongezi ya watu wanaotumia huduma hiyo.

Kupitia teknolojia inayofahamika kama end to end encryption maboresho hayo yameifanya huduma hiyo ya WhatsApp kuwa moja ya app zenye usalama zaidi kama vile Telegram na iMessage iliyo kwa watumiaji wa iOS.

Kupitia end to end encryption data zote zinazopita katika huduma ya WhatsApp hufichwa kwa password spesheli kwenye app ya mtumiaji na kishwa kusafirishwa huku ikiwa ni data isiyoweza someka kwa mtoa huduma wa intaneti na mitambo ya WhatsApp na kisha data hizo zinapopokelewa kwa mlengo app ya mtumiaji hiyo itasoma data hizo na kuzionesha kwa mtumiaji.

Suala la usalama wa data dhidi ya wadukuzi wa aina mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na vyombo vya usalama vya kiserikali limekuwa jambo lililopewa kipaumbele sana na makampuni ya simu na watoa huduma za kimtandao.

Uamuzi huu wa WhatsApp umepewa pongezi sana na watu wote wanaopigania haki ya usiri ya watumiaji wa huduma hizo. Kama utaingia kwenye WhatsApp na kuona kiujumbe kinachohusu ‘privacy’ katika hizi siku chache basi jua ni taarifa juu ya uwezo huu upya.

Unachotakiwa ni kutumia toleo la kisasa la WhatsApp.

Mazungumzo ya aina yote yatakuwa salama – kuchati na pia ata kupiga simu.

Usually visit my blog and enjoy!

Monday, 4 April 2016

Utaratibu wa uhamisho.

UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

1. Mamlaka za Uhamisho
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za
mwaka 2003 Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na
Kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekasimiwa kwa;

Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka
Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa
na; Mkurugenzi wa Halmashauri kwa
watumishi wanatoka kituo kimoja kwenda kingine ndani ya Halmashauri.

2. Aina za Uhamisho Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;

1.UHAMISHO WA KUOMBA.
Taratibu za Kuomba Nafasi:-
Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya
uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.

Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi.

Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi
kwa kumrejesha katika miongozo iliyopoIwapo
Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za
mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho
huo.

Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu
mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa
barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au
kuacha kazi.

Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na
kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba
uhamisho mwenyewe.

Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi
akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia
katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni
muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata
nafasi hiyo.

Angalizo:
Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au
Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho.

Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.

Upatikanaji wa Majibu:-
Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa
waajiri wao na sio vinginevyo.

Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kukataliwa
uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
yaani www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai
kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia
Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya
uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha
mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.

Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka
iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi
yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na
ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.

Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho
na hakupata majibu au hakuridhika na majibu
aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa
uhamisho yaani June au Desemba.

Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake
ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.

2.UHAMISHO WA KAWAIDA
Uhamisho huu ni wa kawaida ambapo Mwajiri au Msimaimizi wa kazi anafanya uhamisho
kwa sababu za kuboresha utendaji.

Hata hivyo ili uhamisho huo ufanyike pia Mamlaka za uhamisho zinatakiwa kujiridhisha uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri
anayohamishiwa mtumishi wa hakusababishi upungufu katika Sehemu mtumishi anakotoka au anakohamia.

Uhamisho huu kwa kawaida unagharamiwa na Halmashauri inayompokea mtumishi na ile inayomruhusu kwa kumlipa gharama za
kufunga mizigo kama ilivyoelezwa kwenye
Kanuni L (8 na 13) ya Utumishi wa Umma ya Kudumu toleo la 2009 na marekebisho yake
ya mwaka 2010 kwa wakati.

Hivyo ni muhimu Mamlaka za Uhamisho kijiridhisha na uwezo wa Halmashauri
kugharamia uhamisho huo ili kuepuka kuzalisha madeni kwa Serikali Pamoja na utaratibu wa uhamisho kuwa ni uhamisho kufanyika mara mbili kwa mwaka, uhamisho huu wa kawaida unaweza kufanyika
wakati wowote katika jitihada za kunusuru utendaji katika kituo alichopo mtumishi au
anachohamishiwa mtumishi kwa manufaa ya umma.

Angalizo:
Mtumishi atakayebainika kughushi saini za viongozi, kuomba au kupokea rushwa katika ngazi yoyote atachukuliwa hatua kali za
kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa ajili ya
kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ni muhimu kwa Waajiri kujiridhisha na majibu
ya barua za uhamisho kutoka katika Mamlaka za uhamisho ili kuona kama maombi yake
yalifuata taratibu sahihi na watumishi waliopata majibu wanatayarishiwa mapema
data sheet na kumbukumbu za utumishi na mshahara ili kuepusha usumbufu kwa
watumishi na waajiri wanaowapokea
watumishi.

Tuwe makini kudai haki zetu!