Friday, 27 May 2016

U-geneous vs U-kichaa

Kumekuwa na theory nyingi mitaani kuwa watu wenye intelligence kubwa na ma-genius wengi wana tabia nyingi za ukichaa au ni vichaa kabisa, madaktari bingwa wengi kwenye mahospitali makubwa hapa nchini ambao wanategemewa wengi huwa ni "wehu".

Hata katika viunga vya vyuo vikuu maprofessor wengi wakubwa wa kuaminika wengi huwa ukikaa nao utagundua tu wana-"wehu" fulani.

Ukifuatilia biography nyingi za watu waliokuwa na uwezo mkubwa wa kiakili na wavumbuzi wengi wakubwa hapa duniani katika sayansi na katika sanaa utagundua historia zao zimegubikwa na uchaa wa hali ya juu.

Mtu kama Isaak Newton inasemekana alikua na magonjwa ya akili na saikolojia ambayo kwa sasa kitaalamu yanaitwa "schizophrenia", huu ni ugonjwa wa mtu kutokuweza kuishi na mtu yeyote,historia inaonesha Newton alikuwa ni mtu wa kujistukia muda wote kama mtu aliyeua vile, na mara nyingi aliwashutumu ndugu zake kuwa wanataka kumuwekea sumu kwenye chakula .Alipofika miaka 40 hali ilikua mbaya zaidi na alikua hawezi kuishi hata na ndugu zake wa karibu akajitenga completely .

Albeit Einstein yeye alikua na tabia ya uchafu uliopindukia, inasemekana chumba alichokuwa akiishi kilikua kama zizi la nguruwe, kula hapo hapo kujisaidia hapo hapo hakuna mtu wakawaida anayeweza kuingia ndani, kilikua kinanuka kwa uvundo lakini pia hata nguo zake alikuwa anaweza kuvaa miezi bila kufua na kutokana na tabia yake ya uchafu na kutokujipenda na kutopenda kunyoa wengi walijua ni mwehu, wataalamu wa magonjwa ya akili kwa sasa wanauita ugonjwa huu schizotype.

Alexander Graham Bell, huyu ni mvumbuzi wa simu, yeye alikua na tatizo la hisia kali za mapenzi , hisia zilizopitiliza mpaka alikuwa kero kwa mpenzi wake miss Hello.

Inasemekana alikua kama zombi kabisa kwa mpenzi wake kuna nyakati ilibidi mpenzi wake huyu amkimbie, lakini pamoja na kumkimbia huku siku alipovumbua tu simu neno la kwanza katika simu lilikua ni kutaja jina la mpenzi wake HELLO na hapo ndio utamaduni wa kuanza na neno HELLO kwenye simu ulipoanzia, japo watu wa kizazi hiki wanachukulia kama ni fashion lakini neno HELLO lilitajwa na mtu aliyekuwa na emotion breakdown wakati huo .

Martin Luther huyu alikua na tatizo la misongo ya mawazao iliyotukuka (chronical depression), lakini pia alikua ni mtu mwenye "mizuka ya ajabu, siku akiamka kichwa kimemtuma kufanya kazi anaeza fanya kazi hata 48 hrs non-stop, siku kichwa kikimtuma kusoma anaweza kusoma hata 36 hrs non-stop.

Mwaka 1517 kichwa kilimtuma kuandika Thesis za kupinga namna Kanisa Katoliki linavyoendeshwa, aliandika thesis 95 alipoona hawamuelewi akaamua kuzibandika mlangoni mwa kanisa la Wittenberg halafu akasepa, na hapo ndipo ikaanza movement ya protestant churches.

Wapo wengi kama Thomas Edson, Leonardo da Vinci, Michelangelo Buonarroti, Theodore Roosevelt,John Nash,Michael Faraday, Henry Ford na wengine kibao ambao historia zao zinapatikana kiurahisi, wote hawa wameonesha kuwa na degree fulani ya ukichaa ambayo ni tofauti na mtu wa kawaida kama ambavyo sayansi ina-define na wengi wamekuwa na tabia ya kuongea wenyewe muda wote.

Kuna vitabu vimeandika research ya hii kitu na wakafanya clinical trials wakagundua kuwa asilimia kubwa za watu wenye akili nyingi au ma-genius familia zao pia kuna vichaa wengi au watu wenye upungufu wa akili au wehu.

Moja ya kitabu kizuri ni cha mwanamama Nancy C. Andreasen, M.D., Ph.D. kinaitwa "The Creating BRAIN, Neurosciences of Geinus" kimejaribu sana kutafiti kwa kutumia technolojia nzuri ya MRI bongo nyingi za ma-genius na kimegundua zinafanana neuro-arrangement zake na kua sehemu za brain zao haziko developed kabisa.

Swali hapa linakuja je kuna uhusiano gani kati ya kuwa na Intelligence kubwa au kuwa genius au kuwa highly creative na UKICHAA??

Thursday, 26 May 2016

Madaktari Tz juu.

Tanzania inaendelea kupiga hatua katika nyanja ya afya baada ya madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.

Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu.

Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa Bashir Nyangasa ameambia BBC kuwa upasuaji huo wa kupandikiza mishipa ya damu nje ya mshine ni wa kihistoria nchini Tanzania.

“Mgonjwa anaweza kutolewa mishipa ya damu kutoka miguuni au mikononi baada ya kupewa dawa ya usingizi na mishipa hiyo kupandikizwa kwenye mshipa wa moyo uliokuwa umeziba ili kuruhusu mzunguko wa damu wa moyo kama kawaida bila kutumia mashine,” amesema.

Upasuaji huo wa moyo kwa njia ya kupandikiza umefanyika kwa watu wawili, ambao umeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hali zao zinaendelea vizuri .

Dkt Nyangasa amesema kwa sasa hakuna haja ya Watanzania wenye matatizo ya moyo kwenda nje ya nchi kwa kuwa wao kama wataalam wameweza kufanya upasuaji huo.

Anasema madaktari sasa wanaweza kuhudumia wagonjwa wengi zaidi wenye uhitaji na kupunguza gharama kwa serikali ya kusafirisha wagonjwa wa moyo nje ya nchi.

Mwandishi wa BBC aliyepo Dar es Salaam Esther Namuhisa anasema wengi wa wagonjwa wamekuwa wakisafiri hadi India ambapo wengi hukumbana na changamoto nyingi kupata huduma hiyo kifedha na hata kwenye upande wa lugha.

Wednesday, 25 May 2016

Malkia Elizabeth na nguvu zake!

Nguvu na uwezo alionao Malkia Elizabeth, yaan dahh!

1. Haitaji leseni ya gari, huendesha bila leseni

2.Husafiri bila passport nje ya nchi

3.Huwa anasherehekea siku ya kuzaliwa mara mbili, ile ya kweli 21 april na jumamosi ya jully

4. Ana mtunga mashairi wake maalumu.

5.Ana ATM mashine yake binafsi ya kutoa ela

6.Bila ruhusa yake hakuna muswada utapitishwa kuwa sheria

7. Ana uwezo wa kutolipa kodi

8.Ana uwezo wa kumuonya waziri yoyote, na hata kumwajibisha

9. Ni malkia wa Australia pia

10. Ukiacha ukuu wake katika UK na Australia pia anaongoza nchi zifuatazo Antigua and Barbuda, the Bahamas, Barbados, Belize, Canada, Grenada, Jamaica, New Zealand, Papua New Guinea, Saint Kitts and Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent and the Grenadines, Solomon Islands, na Tuvalu.

11.Ni mwenyekiti wa kanisa la Anglikana

12. Ana uwezo wa kuivunja serikali ya Australia

13. Anakinga ya kutoshitakiwa

14. Anamiliki ndege aina ya swans, kongoro katika mto thames

15. Ana uwezo wa kumteuwa spika kwa amri yake

Monday, 23 May 2016

Sifa 6 za mke mwema.

Mithali 14:1“Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu hibomoa kwa mikono yake mwenyewe”
Kuna mithali isemayo “MAJUTO MJUKUU”, ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo.

Matatizo mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu aliyeanzisha Ndoa. Baadhi ya sifa za Mwanamke mwenye Hekima – Pia Soma Mithali 31:10-31.

1. Hufumbua kinywa chake kwa hekima,
Na sheria ya wema I katika ulimi wake (31:26). Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRAna WIVU, akiona mumewe anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni Mbaya.

2. Hufanya kazi kwa Moyo na Huamka alfajiri na mapema
Kuna wanawake ambao ni wavivu kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaribu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haichelewi mwanaume kulipa fadhila kwa wema anaotendewa.

3. Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yake
Kuna wanawake ambao ni wachafu – usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala ni stoo ya nepi za mikojo na nguo chafu, wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti mwanamke awe msafi muda wote. Wanaume wote wanapenda Usafi, marashi hata ya mchina yasikose, Mwanamke hakikisha “Reception” inakuwa Safi na kuwa katika hali ya kumfanya Mume ajisikie kujipumzisha kwa Raha mstarehe.

4. Jali na timiza Mahitaji ya NDOA kwa mume wako
Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku”, kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama apanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani.

Wanaume ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya Ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.

5. Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho familia itafurahia.
Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula.

Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Test”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.

6. Mwamini Mume wako,
wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza Ndoa kwa Uadilifu na Upendo.

Sunday, 1 May 2016

Science & technology.

A technological revolution

By Paul Boutin

Special to msnbc.com

So many new technologies have appeared in the past half century that it’s impossible to list them all.  But these 10 high-tech breakthroughs stand out over the last 50 years because they’ve revolutionized the way Americans live.  We look back at their beginnings, as well as where they’ve taken us today.

10. Organ transplants. In 1954, Dr Joseph Murray removed the kidney from one human patient and implanted it in another.  The recipient accepted the kidney as its own rather than rejecting it as a foreign body.  It was more than skillful surgery:

Murray had chosen a pair of identical twins, Ronald Herrick and his terminally ill brother Richard, in hopes their similar genetic makeup would reduce the likelihood of Richard’s body rejecting Ronald’s liver.  Soon afterward, though, other researchers developed drugs that could squelch a transplant recipient’s immune system long enough for the new organ to become incorporated into its new body.  Today, some 25,000 Americans a year receive a new heart, kidney, liver, lung, pancreas or intestine — and a new lease on life.

9. Robots and artificial intelligence. The term “robot” was coined by Czechoslovakian playwright Karel Capek in 1920 — “robota” being a Czech word for tedious labor — but the first real industrial robot was built in 1954 by George Devol.  Five years later, the Massachusetts Institute of Technology founded its Artificial Intelligence Laboratory in a quest to mechanically mimic human minds as well as hands. 

Today, robots assemble products better, faster and often cheaper than manual laborers, while more than 8 million U.S. airline flights a year are scheduled, guided and flown with the superhuman assistance of advanced software.  Still, some Americans eye such systems with the cynical view of novelist Kurt Vonnegut, whose 1952 story “Player Piano” warned that the machines might leave people without a purpose — or a job.

8. Electronic funds transfer.  The Federal Reserve Bank of San Francisco set up a paperless transfer system with the Los Angeles branch in 1972.  By the end of the decade, instantaneous transfers of millions of dollars in value between banks, insurance companies and other financial institutions had become common. 

The real appeal of EFT today is its trickle down to the individual: You get grab cash from your bank account anywhere in the world, and use PayPal to buy and sell stuff on eBay without sending money or checks through the mail.

7. Nuclear power. When the Queen herself threw the switch on the world’s first atomic power plant at Calder Hall outside London in 1956, nuclear reactors were seen as a source of cheap, pollution-free energy.  But a partial meltdown in 1979 at the Three Mile Island reactor in Pennsylvania soured Americans on nukes as safe power. 

Nonetheless, the United States today has about 100 active plants that generate 20 percent of the country’s electricity — second only to coal as a source of power — and have been steadily increasing their capacity.  Will the next 50 years bring a better alternative?

6. Mobile phones. The idea for cellular phone service dates back at least to 1947, but the first call was made from the sidewalk outside the Manhattan Hilton in 1973 by Martin Cooper, a Motorola researcher who rang up his rival at AT&T Bell Labs to test the new phone. 

Thirty years later, more than half of all Americans own one and cellular networks are beginning to serve Internet access at broadband speeds through thin air.

5. Space flight. Americans from 50 years ago would be disappointed to learn we never went further than the Moon — no Mars colony, no 2001 odyssey to Jupiter, no speed-of-light spaceships.  Even the Shuttle is in trouble.  But the space race against the Russians that dominated the national psyche (and a good chunk of the budget) in the ‘60s and ‘70s pushed the development of hundreds of enabling technologies, including synthetic fibers and integrated computer circuits, necessary to fly men to the Moon and back. 

And the astronauts brought back a lesson from space: “We saw the earth the size of a quarter, and we realized then that there is only one earth. We are all brothers.”

4. Personal computers. Before IBM recast the desktop computer from hobbyist’s gadget to office automation tool in 1983 — followed by Apple’s people-friendly Macintosh a year later — a “minicomputer” was the size of a washing machine and required a special air-conditioned room. 

But the trained technicians who operated the old mainframes already knew computers were cool: They could use them to play games, keep diaries, and trade messages with friends across the country, while still looking busy.  Today, thanks to the PC, we all look busy.

3. Digital media. “The camera doesn’t lie” went a saying not heard much since the release of Photoshop 1.0 in 1990.  Digitized audio, pictures, movies, and text let even an amateur edit reality — or conjure it from scratch — with a keyboard and a mouse.  A singer’s bad notes, a model’s blemishes, or an overcast sky in a movie scene can be fixed as easily as a spelling error. 

Just as important, digital media can be copied over and over nearly for free, stored permanently without fading, and sent around the world in seconds.  It rightly worries the movie and music industries, but how do you put the genie back in the bottle if there’s no bottle anymore?

2. Genetic engineering.  Everyone knows Watson and Crick, who unraveled the secret of DNA in 1953.  But have you heard of Boyer and Cohen, who constructed the first organism with combined DNA from different species in 1973?  They inserted toad genes into a bacterium that then replicated itself over and over, passing the toad’s genetic code down through generations of bacteria. 

Thirty years later, an estimated 70 percent of processed foods contain genetically modified ingredients, such as soybeans or corn engineered for higher crop yields.  Of course, the much bigger potential — good and bad — is in engineering humans.  It might prevent birth defects, and diseases later in life.  But the side effects could be disastrous and unknown.  Is there an ethical way to beta-test human beings?

1. The Internet. This one seems like a no-brainer, but the Net’s unique strength is that no two people will agree on why it’s so important.  The world’s largest and most unruly library, it’s also a global news channel, social club, research archive, shopping service, town hall, and multimedia kiosk. 

Add to that the most affordable mass medium ever, and a curse to anyone with a secret to keep.  Three-fifths of Americans now use the Net, but it remains to be seen whether the connections to one another will transform us, or prove that we’ll never change.

Paul Boutin is a technology writer for Wired magazine and Slate. He has worked as a software engineer and manager at MIT and in Silicon Valley.

© 2013 MSNBC Interactive.  Reprints