Sunday, 30 October 2016

Disable Copy and Paste in your blog!

How to Disable Copy Paste In Your Blogg


In internet there are easy way to copy text from your websites and paste it to their site without your permission. There are many blogger site which often doesn't make it possible for us to copy the content on the websites. Admin protected his/her websites post content by pasting code on their websites.

Today,your likely blog  songea computer lab will share a magical tips which protect your content from copy and paste.

Disable Copy Paste in Blogger

Step 1: Go to Blogger

Step 2: Then click on your site and go to Layout

Step 4: After selecting Layout then click on Add a Gadget

Step 5: Then it will open a window and select HTML/JavaScript

Step 6: Then paste following code into the box
<!- www.codiblog.com start disable copy paste --><script type='text/javascript'> if(typeof document.onselectstart!="undefined" ) {document.onselectstart=new Function ("return false" ); } else{document.onmousedown=new Function ("return false" );document.onmouseup=new Function ("return false"); } </script><!-- www.codiblog.com End disable copy paste -->Step 7: Now Save the open window and done.

Now see your site and you can not copy your post content. That's it. Happy Comment & share on This Post! on your result that have been checked





Monday, 24 October 2016

Vyakula vinavyo ongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa!

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume.

Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.

Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa.  Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:

1. PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta mgusu wa hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa unapata hisia kila sehemu ya mwili.

2. MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI 
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol).  Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.

Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido) kidogo.

Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa kula milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.

3. NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu.

Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.

Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

4. TANGAWIZI
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumiwa kama chai.

5. ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.

Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.

6. KARANGA
Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu (vascular system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua.

Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.

7. CHAZA (OYSTERS) NA PWEZA
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.

Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume.  Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa kwa wanaume.

8. SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada.

Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.

9. CHOKOLETI
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.

10. PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni.

Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

Tuesday, 18 October 2016

Nchi mpya kuanzishwa angani!

Wanasayansi hao wanataka kuunda taifa anga za juu ambalo litaitwa Asgardia

Kundi la wanasayansi mjini Vienna, Austria wameanzisha mpango wa kuunda taifa la amani la aina yake ambalo litakuwa na jina Asgardia.

Taifa hilo litaundwa katika anga za juu, eneo.

Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo litakuwa nje ya udhibiti wa mataifa yoyote ya sasa na litakuwa katika mzingo wa dunia, eneo ambalo vyombo vya anga za juu huzunguka dunia.

Wanasayansi hao wanapanga kurusha satelaiti ya kwanza, ya kuanzisha taifa hilo, mwishoni mwa mwaka ujao.

Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja hivi karibuni watatambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Lakini baadhi ya wataalamu wanatilia shaka uwezekano wa mpango huo kufanikiwa ikizingatiwa kwamba sheria za kimataifa huzuia mataifa kudai umiliki wa maeneo anga za juu.

"Raia" wa Asgardia, ambao watachunguzwa kwa makini kabla ya kukubaliwa, mwishowe watapewa hata pasipoti, anasema Lena de Winne, mmoja wa maafisa wakuu wa mradi huo ambaye alifanya kazi kwa miaka 15 katika Shirika la Anga za Juu la Ulaya (EPA).

Maelfu ya watu tayari wameonyesha nia ya kutaka kujiunga na taifa hilo

Mradi huo unaongozwa na shirika la Aerospace International Research Center, ambalo lilianzishwa na mwanasayansi Mrusi, ambaye pia ni mfanyabiashara, Dkt Igor Ashurbeiyli.

Mashindano yanaandaliwa kuamua bendera na wimbo wa taifa wa nchi hiyo mpya.

Profesa Sa'id Mosteshar, mkurugenzi wa Taasisi ya Sera na Sheria za Anga za Juu ya London, amesema itakuwa vigumu kwa Asgardia kutambuliwa kama taifa ikizingatiwa kwamba haitahusiana na taifa lolote linalojitawala duniani, na pia 'raia wake' wengi watakuwa ardhini.

Tayari zaidi ya watu 50,000 wamewasilisha maombi mtandaoni kutaka kuwa raia wa taifa hilo!

Sunday, 16 October 2016

Zijue hatua 10 za kumpata mchumba sahihi.

Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ruth aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.

Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.

Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.

NB: Kumbuka kumuomba MUNGU akupe chaguo sahihi. Ameen!

Utata mtihani wa Taifa wa darasa la pili.

MKANGANYIKO umeibuka kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa mtihani wa taifa wa darasa la pili.

Wakati wapo baadhi ya wazazi wanaosema wamejulishwa kuwepo kwa mtihani huo, wengine wanasema wamepokea barua kutoka katika shule wanazosoma watoto wao kuhusu kuahirishwa kwake.

Hata hivyo, alipozungumza na gazeti hili hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mtihani huo haupo kabisa.

Utata huo umeibua mkanganyiko kwa wazazi wengi, ambao watoto wao wanasoma katika shule mbalimbali za msingi nchini kutokana na kuwepo kwa shule ambazo uongozi wake, ulishatoa taarifa kwa wazazi juu ya kuwepo kwa mtihani huo, unaotolewa ili kupima uwezo wa wanafunzi kwenye KKK yaani Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.

Wakizungumza na gazeti hilo kwa nyakati tofauti Dar es Salaam, baadhi ya wazazi walisema wamepokea barua inayowaeleza uwepo wa mtihani huo wa taifa, utakaofanyika Novemba 17 na 18, mwaka huu kwa lengo la kupima uelewa wa KKK.

“Nina barua nyumbani tulipewa shuleni kwa mwanangu anasoma Atlas School, barua inazungumzia mambo mengi pamoja na hilo la mtihani wa taifa wa darasa la pili na kwamba katika kutimiza hilo, wanafunzi wamepewa mtihani wa majaribio na wameufanya Oktoba 11 hadi 13, mwaka huu,” alisema mzazi mmoja.

Alisema mwanawe huyo anayesoma darasa la pili, hivi sasa anajiandaa na mtihani huo na wazazi wanafahamu kuwa mtihani huo upo kwa sababu walitangaziwa na shule.

Alisema, hata hivyo, hivi sasa wanafunzi wa darasa la kwanza na pili shuleni hapo, wanasoma masomo saba ambayo ni Kiswahili, Kuandika, Kusoma, Kuhesabu, Sayansi, Stadi za Kazi, Haiba na Michezo, hatua inayozidisha mkanganyiko.

Wakati mzazi huyo akisema hayo, mzazi mwingine ambaye mtoto wake anasoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Tusiime, alisema awali wazazi walitaarifiwa kuhusu uwepo wa mtihani huo; na wanafunzi walianza kujaza fomu, lakini baadaye waliambiwa haupo.

‘’Nakumbuka shuleni kwa mwanangu waliambiwa kuhusu mtihani huo wa darasa la pili, na walianza kujaza fomu, ila baadaye wakaambiwa haupo, hatujui utafanywa lini,” alisema.

Mzazi mwingine ambaye mtoto wake anasoma Shule ya Mountain Hill jijini Dar es Salaam, alisema katika kikao cha wazazi cha Septemba, mwaka huu wazazi waliambiwa kuwa mtihani huo wa taifa kwa darasa la pili, umeahirishwa hadi mwakani.

“Nilienda kwenye kikao cha wazazi cha Septemba shuleni Mountain Hill na mwanangu anasoma darasa la pili, tuliambiwa mtihani wa darasa la pili wa taifa wa KKK haupo, bali utafanywa mwakani,” alisema.

Hata hivyo, Waziri Ndalichako alisema serikali haijawahi kuwa na mtihani wa darasa la pili; na kwamba watoto hao bado ni wadogo, hivyo hawastahili kupewa mtihani.

“Mtihani wa darasa la pili hatujawahi kuwa nao, halafu hawa watoto wadogo unaanza kuwapa mtihani, ni wadogo,” alisema Profesa Ndalichako, hatua ambayo inazidisha sintofahamu kwa suala hilo.

Thursday, 6 October 2016

Kagera tenaa, moto wawaka ardhini km volcano!


Wakazi Kagera wataharuki moto ardhini wakidhani volcano, wataalam watoa ufafanuzi!!!

Ikiwa zimepita wiki kadhaa tangu tetemeko la ardhi litokee Kagera, leo October 6 2016 kupitia kituo cha runinga cha ITV kimeripoti habari kutokea hukohuko Kagera ambapo wananchi wa bonde la Katarabuga wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka moto ardhini wakidhani volcano. Wakala wa jiolojia, Prof Mruma amesema moto huo ni wa kawaida tu hivyo wananchi wasiwe na taharuki yoyote, Prof. Mruma amesema…….

Huu moto unaunguza ardhi ambayo umejaa vipandevipande vya miti mikavu majani, mizizi mithili ya mtu anayetengeneza mkaa’

Volcano haiwezekani hapa, volcano ni uji wa miamba na ya chini kabisa ya volcano degree 400 kwa hiyo degree 400 centigrade ikiungua hapa hata huu mti usingesalia, volcano mara nyingi inatoka na majimaji na mvuke’

huu ni moto wa kawaida, moto kama huu unatokea kwenye ardhi ambayo ina uozo wa majani mengi sasa yale majani yakiungua yanatoa kitu kama hiki, moto wa namna hii mara nyingi inatokea kwenye makaa ya mawe mtu anapita anaangusha moto mkaa unalipuka panaanza kuungua na ardhi inachubuka chubuka hivihivi!

Sunday, 2 October 2016

Je umekuwa addicted na simu yako? Jizuie na uraibu huo!

Jinsi Ya Kujizuia Na Uraibu (Addiction) Wa Kutumia Simu Janja Kila Mara!

Tafiti nyingi zimefanyika na ukweli umegundulika ni kwamba wengi wetu tumepata na uraibu (addiction) juu ya smartphone zetu pengine kuliko vitu vingine.

Kumbuka kuna wengine wanazipenda sana simu zao na hata zikidondoka wao ndio huumia Hahaha! .
Kwa karne hii wengi wanatumia simu janja (smart phone) sana kuliko zile simu zingine (mwanga wa sabuni).

Ukaribu wao wa kupitiliza na simu hizo pengine ndio unaosababisha uraibu (addiction) huo.
Katika tafiti iliyofanyika huko British, ilidai ya kwamba katika kila watu watatu (3) basi lazima kuna mmoja ambaye lazima atakuwa anatumia simu yake usiku wa manane.
Sasa kama ukijihisi una uraibu na simu yako nini cha kufanya? Njia ni hii hapa.

1. Weka Simu Yako Mbali Na Ulipo
Ndio! kama simu iko mbali na wewe ulipo hutaweza kuitumia sio? Kuna wengine hapa bado ni changamoto kwani hawawezi kukaa mbali kabisa na simu zao. Lakini kuna wale waliobarikiwa (Kama rafiki yangu, Mmaryson ) wao wanaweza hata kusahau kabisa walipoweka simu zao mpaka atokee mtu abipu hiyo simu.

2. Futa Baadhi Ya App
Kama unasumbuliwa na uraibu wa simu basi hapo huna budi kufuta baadhi ya App. Na itakua ni vizuri kufuta zile unazozipenda kwani hamu ya kushika simu na kuzifungua mara kwa mara itapungua au itaisha kabisa. Kwa kifupi ni kwamba utashindwa kushika shika simu yako kila mara.

3. Zima Simu Janja Yako
Hivi mara yako ya mwisho kuzima simu yako ni lini? Kuna wengine wanachanganyikiwa kabisa kama simu zao zikizima. Unaweza ukajiwekea katabia ka kuzima simu yako, pengine labda ukiwa bize au ukiwa unalala. Hii kwa kiasi kikubwa itapunguza uraibu kwani hutapoteza muda kupepesa machi katia simu yako hiyo.

4. Jiwekee Muda Maalamu Wa Kutotumia Simu Yako
Wengine wanajiuliza Je, ni kweli inawezekana? Lakini mimi naamini kila kitu kinawezekana. Ukijiwekea muda maalumu ambao hutaweza kugusa simu kabisa itakua ni vizuri na uraibu utapungua kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano unaweza ukajiwekea katabia kwamba kila ifikapo saa mbili usiku hutakua unatumia simu mpaka kesho yake.

5. Usitumie Simu Yako Ndani Ya Dk 30 Za Kwanza Baaya Ya Kuamka.
Ukishaamka asubuhi usifanye kuangalia simu yako kuwa ndio kitu cha kwanza kufanya. Fanya vingine vya muhimu unaweza fanya mazoezi pia na ukafanya maandalizi ya kuweza kupata chai. Haya yote yakitumia ndipo unapoweza rudi katika simu janja yako na kujua yale yaliyojiri.
Kama inavyofahamika kuwa uraibu wa aina yoyote ile una kazi sana kama mtu akitaka kuacha hicho kitu ambacho ana uraibu nacho. Hapa cha msingi ni juhudi na dhamira ndiyo itakayo saidia. Kwa Tanzania pengine jambo hili linaweza likachukuliwa Poa!

Lakini nina uhakika wapo watu amabao wanasumbuliwa na hili, ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini kama kuna njia yeyote ambayo sijaiandika na unahisi inaweza pia ikasaidia.


Saturday, 1 October 2016

Ongeza nafasi ktk disk yako!

Jinsi ya Kupata Nafasi ktk ‘Hard Disk’ Iliyojaa

Umejaza filamu na nyimbo kibao katika diski yako, labda ni magemu pia. Tamthilia je? Inaweza ikawa moja ya vitu hivi au ni mambo mengine kibao yamejaa kwenye kompyuta yako kiasi ya kwamba inakuwa ni vigumu ata pa kujua mafaili makubwa ya kufuta ni yapi hasa.

Unaangalia kompyuta yako na inakuambia diski C yako inakaribia kujaa kabisa na hivyo unatakiwa ufute baadhi ya mafaili, ila ndio hivyo tena kutokana na jinsi yalivyomengi hufahamu mafaili yapi ni makubwa au yapo wapi hayo makubwa kutokana na wewe kuwa na mafolda mengi kwelikweli. 

Leo tunakutambulisha kwa programu moja ya bure kwa watumiaji wa kompyuta/laptop za Windows, inaitwa WinDirStat.
Ndio kuna njia zingine za kupunguza nafasi katika diski yako kama vile kutumia programu wa Windows ifahamikayo kama ‘Disk Cleaner’, ila hiyo haikuoneshi mafaili yako mwenyewe. Yenyewe inasaidia mafaili ya system ya kompyuta tuu.

Programu ya WinDirStat inakupa uwezo wa kufahamu mafaili gani ni makubwa na ni kwa ukubwa gani na pia inakupa uwezo wa kuyafuta kwenda kwenye ‘Recycle Bin’ au kuyafuta moja kwa moja kabisa bila kupitia Recycle Bin.


Pia kwa kutumia rangi mbalimbali utaoneshwa mafaili muhimu ambayo si vizuri uyaguse ukapoteza vitu vya msingi!

Linda data zako kwa njia hizi 5 uwe salama!!!

Njia Tano za Kulinda Data Zako Sasa

Je, wewe ni moja wa watu walio na msukumo mkubwa wa kulinda data na maisha yako ya kidijitali? Hii inakuhusu sana.
Mara nyingi tunasikia ya kwamba mitandao mbalimbali na huduma za mtandaoni zinavamiwa na wahalifu wa mitandao na katika nyakati hizo mtu wa kawaida hauna mengi unayoweza kuyafanya kukabiliana na matatizo kama hayo. Watu husema kinga ni bora kuliko kutibu yaliyojiri, hivyo kuna vitu rahisi unavyoweza kufanya kabla ya majanga ili kujilinda na uhalifu wa mitandao kama:

1. Ruhusu Roboti Kumudu Pasiwedi Yako
Kwa kawaida, akili ya binadamu haina uwezo mkubwa wa kukumbuka pasiwedi na hata kutengeneza nzuri, yenye ugumu wa kudhibiti kuvamiwa.
Mara nyingi tunatumia pasiwedi ileile kwenye tovuti mbalimbali. Hili sio jambo zuri. Linamaanisha kwamba kama mhalifu akigundua na kuvamia akaunti mojawapo unayomiliki, anaweza kuingia kwenye akaunti zako zingine.
Hili ni tatizo kubwa hasa ukizingatia watu wengi wanasemekana kufanya hivyo kwenye akaunti zao za Facebook, Google, Twitter na hata akaunti za benki za mtandaoni.
Suluhisho la jambo hili ni kutumia huduma moja ya kumudu pasiwedi zako za kompyuta na simu ambayo itaipa kila tovuti uliojisajili passiwedi isiyo na mpangilio maalumu mara kwa mara na kui-’synchronise’ kwa vitumi vyako vyote. Mifano ya huduma kama hii na ambayo inajulikana sana ni kama 1Password na LastPass.

2. Pata U2F – na Tumia Uidhinisho wa Aina Mbili
Njia nyingine ya kulinda akaunti zako ni kuhakikisha kwamba hata kama mtu ataijua passiwedi yako, hatakuwa na idhini ya kuingia kwenye akaunti hiyo moja-kwa-moja.
Ili kuingia kwenye akaunti, inabidi awe na uidhinisho wa ziada, yani tofauti na pasiwedi. Kwenye baadhi ya tovuti, hii inaweza kuwa namba ya siri inayotumwa kwenye simu yako kutoka kwa tovuti/ huduma husika (kama unavyotumiwa na WhatsApp unapo-’sign-in’), au kuanzisha app maalumu ya ziada kwenye kifaa chako ambayo itatoa namba ya siri ya kutumika mara moja.
Moja ya njia mpya kabisa kama hizi za uidhinisho wa mara mbili ni ‘U2F security key’, ambayo ni kwa kutumia kitu kinachoonekana kama flashi ya USB ya kawaida. Bila ya kifaa hicho, huwezi kuingia kwenye akaunti flani kwenye kompyuta yoyote. Kifaa kama hiki kinaweza kugharimu kama dola 15 za kimarekani (TShs 30000) ambayo ni gharama ndogo ya kukuongezea usalama wa data zako. Tayari ishaonekana kwamba ndani ya miaka michache inayokuja, makampuni makubwa yataongeza matumizi ya U2F.

3. Wezesha ‘Disk Encryption’
Kama una laptopu au simu ya mkononi ambayo haijawezeshwa na ‘Data Encryption’ na ikaipotea, ujue kwamba mtu yeyote ambae ataipata ana uwezo wa kupata data zako kirahisi.
Data Encryption ni mbinu maalumu ya kuficha data zako kwenye kifaa kwa kuzipa data hizo mfumo usiosomeka iwapo mtu akiamua kuflash hicho kifaa na kujaribu kuibua data zako. Mbinu hiyo imewekwa moja kwa moja kwenye i-phone na iPad ila kwa Windows, Android na Mac OS inabidi utumie muda wako kidogo ili kuiwezesha. Jambo hili ni la msingi kwa wale walio na ‘unyeti’ wa data zao na maisha yao ya kidijitali.

4. Weka Stika kwenye Kamera ya Kompyuta
Imejulikana kwa muda mrefu kwamba kuna watu mtandaoni wana tabia ya kuwasha kamera zilizopo kwenye laptopu zisizo za kwao kwa makusudi ya kuchungulia kila unachofanya bila wewe kujua. Hiki kitu hakitokei mara milioni kwa mwaka ila bado kinatokea ni kitu kinachotokea mara kwa mara na cha kutisha. Unaweza kujilinda na wahalifu hawa kwa kuweka stika kwenye hiyo kamera uwapo huitumii.
Unaweza kujilida na wahalifu kwa kuweka stika kwenye hiyo kamera uwapo huitumii.

5. Encrypt Mawasiliano yako ya Simu na Ujumbe
Mawasiliano ya simu na meseji ambazo makampuni ya simu yanatoa yana uwezo wa kufuatiliwa na mtu yeyote mwenye nia . Hii ina maana kwamba serikali yako au ya nchi nyingine na watu wenye maslahi ya kuiba ujumbe na mazungumzo yako kwenye simu wanaweza kupata chochote wanachotaka bila ya nguvu nyingi. Baadhi ya app za intaneti kama WhatsApp na FaceTime zinaweza kuwa nzuri ila kama ungependa usiri zaidi, fanya tafiti kidogo kupata huduma zenye usalama wa hali ya juu kama Signal inayopatikana kwenye Apple Store.