Thursday, 20 April 2017

Ijue jinsi ya kuroot simu yako!

ANDROID NI NINI..??

Android ni Mfumo wa simu (Operating System) ambao unaboreshwa siku hadi siku. Mfumo huu una majina tofauti kutegeana na toleo lake.

Haya ni Matoleo (Versions) mbalimbali ya Android kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho:

1. Cupcake (1.5)

2. Donut (1.6)

3. Éclair (2.0 – 2.1)

4. Froyo (2.2 – 2.2.3)

5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)

6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)

7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)

8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)

9. KitKat (4.4 – 4.4.4)

10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)

11. Marshmallow (6.0>>>>>>

Matoleo haya huboreshwa kadri yanavyozidi kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda;
Settings – About phone – Android Version. Ukikuta Jelly Bean, KitKat, marshmallow au Lollipop hongeara, kwani unatumia matoleo ya mwisho yalioboreshwa!!

Mfumo huu wa Android unafaa kufanyiwa settings mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili kumfanya mtumiaji aifurahie simu yake kwa asilimia 100, lakini shida huja kwamba sio kila PROGRAM inayowekwa katika mfumo huu wa Android inakubali kufanya kazi!!

Wapo watengenezaji wengi wa program (Software Designers) ulimwenguni, watengenezaji wa mfumo huu wa Android wamezuia Program ambazo hazijatoka kwao zisifanye kazi kwenye mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA TUTAPATA KUELEWA MAANA YA KU ‘ROOT SIMU' kuwa ni kuifanya simu ikubali Programu zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android Developers).

Ukishai ‘root’ simu yako sasa utakua na uwezo wa kuweka program zinazohitaji ‘root permission’ kwenye simu yako.

JINSI YA KU ‘ROOT’ SIMU YAKO.

Kuna aina za simu ni rahisi sana ku root, lakini nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa kutosha. Zipo program nyingi sana zinazoweza kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni kama vile:
1. KingRoot.

2. Vroot.

3. Kingoapp Root.

4. SRSRoot.

5. Framaroot.

6. Root Master.

7. z4root.

8. Universal root.

9. Iroot.

10. Easy root, nk.

Baadhi ya Program hizi zitahitaji Computer, nyingine hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa simu kutumia Program iitwayo KingRoot ambayo inakubali kufanikisha zoezi hili kwenye asilimia kubwa ya simu za Android.

Program hii haihitaji Computer. Kuipata nenda Google kisha isearch na kui download. Kwa msaada uliza……

Maandalizi:

(i) Charge Simu yako, angalao ijae kwa 50%

(ii) Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa kawaida. Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa 100%.

Sasa kuifichua nenda Settings>About phone>Build number.

Baadhi ya simu (LG na HTC) nenda Settings>About phone>Software information>Build number.

Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a Developer”

(iii) Sasa nenda Settings>Developer options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama haipo)

(iv) Nenda settings>Security>Unknown Sources. Weka tiki hapo.

Hapo maandalizi yatakua ni tayari. Sasa download KingRoot 4.0 (or above) kwa kui search kwenye Google kisha Install kwenye simu yako. Baada ya ku install gusa ‘Open’. Baada ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu yako automatically—Model ya Simu na Toleo lake. (Mf. Model: H6 Android 4.4.2). Kama simu yako haijawahi kuwa rooted utaona ‘Root access is unavailable’.

Chini gusa ‘START ROOT’. Hapo KingRoot itakua inakomboa simu yako kutoka kwenye kifungo cha maisha…kuwa na subira zoezi hilo litachukua muda kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…mpaka utakapoona ‘ROOT SUCCSSFULLT’ DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!!

Ili kuhakikisha kama simu yako imeshakuwa rooted, nenda PlayStore kisha download Root Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa ‘VERIFY ROOT’. Ukiona ‘’Congratulations! Root access is properly installed on this Device” HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!

FAIDA ZA KU ROOT SIMU:

1. Utaweza ku update toleo la mfumo wa simu yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android 4.4.2 (KitKat) unaweza kui update kwenda Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi kuflashiwa bila kuwa rooted!

2. Huwa inatokea simu kuibiwa. Wewe unaesoma Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi (ukiokota mtafute mwenye nayo). Nitafute nikupe story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu yako wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka kwenye System ya simu yako baada ya kufanyiwa ‘Factory reset’ au kuflashiwa. Kama ume root simu yako, zipo Program za kuitafuta simu yako ambazo hata mtuhumiwa aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program hizo ni Cerberus.

3. Utakua na uwezo wa kuweka Program nyingi na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na kuboresha muonekano (performance and appearance). Pia kuna program za kutunzia chaji, Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k…. ambazo hazitafanya kazi bila root.

4. Utaweza kufuta chochote ktk simu yako! Mimi nimefuta hadi torch, kitu ambacho huwezi fanya km hujaroot simu yako!

5. Unaweza kuongeza RAM ktk simu yako!!!

TAHADHARI:
Rooting inaweza kuharibu kabisa simu yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa sitahusika kwa lolote). Usiogope, hii huwatokea wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo. Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za Marafiki zangu wasiopungua 20 bila madhara yoyote kutokea. Fanya utafiti kwanza ni program gani sahihi ku root simu yako, omba ushauri,…..

Pia Rooting inaharibu Warranty ya simu yako. Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako na ukaikuta na tatizo, ukiirudisha haitakubalika. Aidha, inawezekana pia ku’unroot’

MWISHO;

Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti, anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala hii, wale woote ambao tutaenda sambamba tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo zinahitaji ‘Root Permission’. Mie natumia Tecno L3 , baada ya kui root nimeifanyia Settings nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi sana!! ROOTING imeniwezesha hata kubadilisha muonekano wa maandishi system nzima.

Tembelea blog mara kwa mara ujifunze mengi!

Wednesday, 19 April 2017

Rudisha data zako ulizopoteza ktk simu yako!

Elisante blog, keep on reeding!

JE WEWE NI MUATHIRIKA WA KUPOTEZA DATA ZAKO KATIKA SIMU YAKO..??? 
EITHER ULIZIFUTA AU BAHATI MBAYA 


   Sasa ondoa shaka kabisa suluhisho limepatikana kupitia blog yetu hiiii sasa utaweza kurudisha data zako zote ikiwa ni sms mesenger au hata whatsapp kama inavyoonekana hapo.. 

     

 Vitu hivyo vyote unaweza ukavipata kama vilikupotea unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo    

  Nenda play Store Katafute app inaitwa GT RECOVER KAMA unavoiona hapo chiniiii 

   Baada ya hapo sasa unachotakiwa kufanya ni kuchagua unataka kurecover nini na utapata vitu vyako vyoteee...  

 Sehemu ya kuchagua vitu vya kurudisha ipo kama ifuatavyo na wewe utachagua unachotaka kurudisha tyuuuu

Na hapo itakua umefikia hatua ya mwisho kabisaaa asante kwa kutembelea blog yetu endelea kushare kwa wenzako na kama utakua na tatizo tutakusaidia 

    NB: Your phone must be rooted!


Thursday, 13 April 2017

Neno la Mungu by Mwakasege.

SEMINA YA NENO LA MUNGU  DODOMA.

NA MWL MWAKASEGE

FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA

TAR 3 APRIL 2017

Siku ya Pili

LENGO ni kuimarisha mahusiano yako na Mungu katika Kristo Yesu

Kuna mambo 2 ambayo yanaweza kutumika katika NDOTO

*JAMBO 1*
Shetani anaweza kutumia NDOTO kupandikiza mambo ambayo usipoyang'oa mapema yataharibu maisha yako

*JAMBO 2*
Kutazama ishara  zitakazo kuonyesha kuwa NDOTO zinahitaji kufuatiliwa

*ISHARA*
1. Kujisikia kufadhaika moyoni kwa ajili ya NDOTO uliyoota

Kufadhaika  maana yake ni mahangaiko unayoyapata  ndani ya Moyo wako( kuutibua moyo)

_Mwanzoni 41:1-8"...... 8. Hata asubuhi roho yake IKAFAIDHAIKA akapeleka watu kuwaita waganga wote wa misri ..._

⏩Usifanye kosa kudharau NDOTO yoyote utakayoota Ukasema kumbe ni ndoto tu,  inabidi kuifuatilia  _Mwanzo 41. 7 b"Basi Farao akaamka , *kumbe ni NDOTO tu*._

_Mwanzo 40:5-6 "Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi, akawaona *wamefadhaika*._

Yusufu aliwaona wote wawili mnyweshaji na mwokaji wote WAMEFADHAIKA

⏩Mfadhaiko huja kama alarm,maana ukishaitega alarm ikilia lazima ushtuke.

2. Kuota NDOTO hiyo zaidi ya Mara moja au inayofanana na hiyo
⏩Mwanzo 41:25-32
Mst 32"...  _*Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi*_.

Unapoota Mara 2 au zaidi ni kukutaarifu unatakiwa kuifuatilia hiyo NDOTO
*Ayubu 33:14-15*
_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, *Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali*. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;_

Usipoifuatilia ndipo Mungu huirudisha Mara ya 2 au zaidi hadi utakapopata ufahamu wakulifanyia kazi

⏩Jiulize kama Mungu katumia NDOTO kusema na wewe kwa nini iwe vigumu kuelewa maana yake

_Warumi10:17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa *neno la Kristo*._

Ukiwa na Neno LA Mungu lazima utaisikia sauti yake.

⏩Mfano ukiwa na gari ni vema kujua baadhi ya vitu ili likipata shida uweze kulitengeneza sio lazima kila kitu unapeleka garage. Vivyo hivyo kwa watumishi, sio lazima kila tatizo lako unalipeleka kwa watumishi mengine yatatue mwenyewe Yale unayoona huyawezi ndio yapeleke huko, unapotaka kumweleza *Mtumishi jambo lako sikiliza Amani Ya moyo wako kwanza*

3. Ndoto uliyoota kukutia hofu
Daniel 4:5 na Ayubu 4:12-14

_Nikaota ndoto iliyonitia *hofu*; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha._
*DAN. 4:5*

_Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong’ono yake. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.  *Hofu* iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote._
*AYU. 4:12‭-‬14*

4. Ukiwa mambo uliyoota kwenye ndoto yanatokea katika mwili
Ayubu 4:12-16����

Mfano
⏩Ukiona umeota ndoto unakemea na ulivyoshtuka bado unakemea( fuatilia)

⏩Au ulikuwa unalia kwenye ndoto na umeamka unakuta macho yana machozi pia fuatilia

5. Ndoto kukunyima usingizi
Daniel 2:1
 
_Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, *usingizi wake ukamwacha*_. *DAN. 2:1*

6. Kwa na hamu ya kutaka kujua tafsiri ya hiyo ndoto
Mwanzo 40:7-8,41:7-8

_Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.MWA. 40:7‭-‬8 SUV_

_Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.   Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.MWA. 41:7‭-‬8_

Mstr 8 - alitaka kujua ndoto ile ilimaanisha nini

⏩Ndoto ya Farao ilibeba maisha ya miaka 14 ya dunia nzima,kama angepuuzia sijui ingekuwaje kwa hiyo miaka 14. Kwa hiyo  ule msukumo aliokuwa nao ndio ulisaidia utafsiriwa

7. Ndoto uliyoota kukuletea mahangaiko moyoni mwako juu ya Imani na utumishi ulinao kwa Mungu

_Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.KUM. 13:1‭-‬4_

⏩Usimwogope mtu Bali mwogope Mungu

⏩Usikubali jina au huduma yako ivume kuliko jina la Yesu

*Mfano*: Punda aliembeba Yesu alitembea juu ya nguo kwa sababu tu alikuwa kambeba Yesu lakini baada ya kumshusha Yesu alitembea chini kama kawaida. Dhamani uliyonayo ni kwa sababu unae Yesu ndani yako

8. Ukiona uliyoyaona kwenye ndoto yanapinga au ni tofauti ya mipango uliyonayo

Ayubu 33:14-17
_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;  Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,  Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;AYU. 33:14‭-‬17_

⏩unaweza kuota ili upangue kile kibaya ambacho kinaweza kutokea mbele,hivyo anapozungumza nawe anakusaidia usijeingia kwenye matatizo Fulani au kukuondoa katika mawazo uliyonayo

9. Kusikia msukumo moyoni wa kusimulia ndoto uliyoota
Mwanzo 37:5-11( Pale Yusuph alipowasimulia ndugu zake ndoto aliyoota)

Mathayo27:19  _Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, *Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake*._

⏩Unaweza kuota ndoto kwa ajili ya mtu mwingine hivyo pale unapopata msukumo moyoni wa kumwambia we mweleze ila omba hekima, na kibali kutoka kwa  ROho Mtakatifu

10. Kusikia msukumo moyoni wa kuandika ndoto uliyoota

_Habakuki 2:2-3 BWANA akanijibu, akasema, *Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao*, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.HAB. 2:2‭-‬3_

⏩Unaandika kwa sababu unaweza kuisahau asubuhi au kwa  ajili ya kufuatilia huko mbeleni

⏩Uwe unaandika ndoto zakusaidia baadae
Note:Kama huwa unasahau ndoto unazoota weka daftari na kalamu karibu ili unapoota tu uwe unaziandika na baadae iwe rahisi kuzifuatilia hatua kwa hatua.

11. Ukiwa umesahau ndoto uliyoota ila moyoni unajisikia msukumo wa kutaka kujua

Daniel 2:1-5
Baada ya Nebkadreza kusahau ndoto Daniel alienda kumweleza hiyo ndoto tena

⏩Ukiota ukasahau jitahidi kuifuatilia kwani ktk ulimwenngu wa roho imerekodiwa km ile ya Nebukadreza.

MAOMBI
⏩Toba kama kuna mojawapo ya ishara hizi 11 hukuzifuatilia( kwa kujua au kutojua) Mungu arudishe hizo
Ndoto ili aseme nasi tena haijalishi muda gani umepita

��������������
Bwana Yesu Asifiwe. Tunawakaribisha kwenye semina inayoendelea Dodoma mjini katika uwanja wa barafu. Semina imeanza jana tarehe 2 April itaendelea hadi jumapili tarehe 9 April.
Redio zinazorusha Semina inayoendelea Dodoma mjini ni;

1. Redio Sauti ya injili - 
Moshi, 92.2 FM
Arusha,96.1 FM.
Tanga 102.6FM  & 96.7 FM
Same 100.4 FM
Rombo 96.4 FM
Manyara 102.9 FM & 96.1FM
Morogoro 99.1 FM
Mara 96.1 FM
Unguja, Pemba na Mombasa 102.6 FM
Voi - Kenya 96.4 FM
Dodoma 102.9 FM
Pwani, Rufiji, Kiluvya, Tegeta, Ubungo, Manzese, Mbezi, na Ruaha  99.9 FM
Daraja la Mkapa (Lindi) 99.9 FM

2. Redio HHC Alive
Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga, - 91.9 FM.

3. Redio CG FM
Kigoma, Simiyu, Shinyanga, Tabora na Katavi 89.5 FM

4. Redio Baraka
Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa 107.6 FM

5. Radio Rungwe
Rukwa, Malawi,Mbeya na Njombe102.5 FM

6. Radio Info
Mtwara 92.1 FM

7. Redio Uzima
Dodoma 94.0 FM

8. Redio Bunda FM
Mwanza, Mara, Simiyu na Kagera 92.1 FM

9. Redio Mpanda FM
Katavi, Rukwa na Kigoma 97.0 FM

Unaweza kusikiliza live kupitia www.kicheko.com na www.mwakasege.org, unaweza kusikiliza na kuangalia  live kupitia www.ustream.tv/chanel/mwakasegemanaministry na www.youtube.com (jina la chanel ni Christopher Mwakasege)

Mungu awabariki sana wapendwa!