Friday, 30 June 2017

Uhusiano wa akili na Roho

AKILI NA ROHO (SEHEMU ~I)

Bwana Yesu asifiwe wapendwa!!!

Tunakukaribisha katika kufuatilia mfululizo huu wa somo la akili na Roho, ambalo tumesimamia neno kutoka 1Kor 14:15

"Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia."

���� Wakristo wengi tunachanganya nafasi ya roho na akili katika kufanya maamuzi au kung'amua mambo.

���� Na wengine wamefika hatua wanafikiri kufanya maamuzi kwa kutumia akili zao watakuwa wamemkufuru Roho mtakatifu.

���� Wapo wanaousimamia mpaka mistari ya Biblia kuzifisha akili zao, mstari wanaopenda kuutumia ni huu unaosema

Mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote wala usitegemee akili zako mwenyewe. Mithali 3:5.

Hii ni tafsiri mbaya ya neno la Mungu inayowafanya wengi wawe maskini mwilini na rohoni.

Katika mstari huu neno la Mungu halituambii tusitumie akili zetu, bali linatuasa tusitegemee akili zetu WENYEWE, Hii ina maana tusiegemee katika kutumia akili TU,

Bali baada ya kumtumaini Bwana KATIKA AKILI zetu tunahitaji pia kumtumaini kwa Moyo.

Tafsiri ya Neno KWA MOYO ni kutoka ndani hii inamaana kutumaini Bwana kwa kumaanisha. Biblia inatuambia moyo ndiko chemichemi za uzima zinakotoka hivyo ukimtumaini Mungu kwa moyo hakuna kitakacho kutoa katika tumaini hilo hata mwisho.

Mtu asiemtumaini Mungu kwa moyo wake wote ni mbabaishaji au muigizaji neno  watu hawa wananiheshimu kwa midomo lakini Mioyo yao iko mbali nami.

Mungu anataka mioyo yetu tuisogeze kwakwe kila tunachokifanya tukifanye kwa moyo.

Hivyo umtumaini Bwana kwa si kwa akili yako au uelewa wako mwenyewe bali umtumaini kutoka ndani ya Moyo.

Neno linatuambia;  
Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, KWA AKILI ZAKO ZOTE ‘na’ kwa nguvu zako zote.’ Marko 12:30

Kila jambo lililotajwa hapo juu lina umuhimu wake, na uzito wake ndio maana ametumia kiunganishi ‘na’  hajatumia ‘au’ ambayo inakupa option yaani kuchagua.

Hivyo ni lazima utumie nguvu, roho, akili na Moyo.

Kumpenda Mungu kwa nguvu inamaanisha kujitoa kwa ajili ya Bwana kwa muda na mali yako.

↩  KWENYE KIINI CHETU CHA SOMO

AKILI ni nini?

Ni uwezo wa kung'amua jambo/ kitu fulani, ni uwezo wa kuwa na ujuzi na kitu/jambo flani,
 
Kuna aina kadhaa za akili,

�� Akili za kuzaliwa,

Hizi ni akili ambazo kila mtu anazo, kila mtu anazaliwa na akili ambazo zinamsaidia yeye kujua mambo mbalimbali pasipo kugundishwa na mtu. Kila mtu amejaliwa akili hizi tofauti ipo katika kuzitumia tu.

Uvivu wa kufikiri na kukubali kuongozwa na akili ya mtu mwingine au kuiga iga ndo kinafanya watu wengine waonekane wamependelewa. Mfano Wazungu

�� Akili za darasani,

Hizi zinapatikana kwa kuongezewa maarifa na mtu mwingine, akili hizi mara nyingi tunazipata ili zitusaidie kuweza kupata mambo fulani/kufika viwango fulani, inabidi uingie darasani na awepo mtu wa kukufundisha/kakuongezea ujuzi/akili.

Wengi hawafanikiwa pamoja na kuwa elimu za darasani, moja ya sababu kubwa ni Upumbavu.

Upumbavu maana yake kuwa na  maarifa na kushindwa kuyatumia kwa upuuzi. Hii ni tofauti na ujinga ambapo ujinga ni kukosa maarifa.

�� Akili za maisha,

Huu ni ujuzi ambao unaupata kutokana na mazingira yanayokuzunguka, maisha tunayoyaishi  yamekuwa yakifufundisha vitu vingi sana, na ndio maana kuna watu hawajawai kwenda shule au wameishia viwango vya chini vya elimu  lakini wamefanikiwa, ni kwa sababu ya akili ya maisha ambayo wameipata katika mazingira yanayowazunguka, wana uzoefu na mambo mengi tofauti na mtu ambaye emeenda shule.

Ni muhimu sana kuwa na akili ya maisha kuliko ya darasani, Kwa sababu kama una akili tu ya darasani hauna akili ya maisha, hiyo ya darasani ina asilimia ndogo sana kuweza kukusaidia!

NB: Huwezi kufanikiwa ukiwa na akili za darasani pekee unahitaji akili za maisha, lakini inawezekana kufanikiwa ukiwa na akili za maisha bila kuwa na za darasani. AMKA!

Aina nyingine ni akili ya kiungu,

Hii ndo akili bora kuliko zote, akili hii hauzaliwi nayo, hauipati darasani wala mtaani (maisha ya kawaida) utapata kutoka kwa Mungu tu.!

Akili hii ni bora Kwa sababu ukiipata inauwezo wakubadilisha maisha yako muda wowote!

Habari hizi za akili ya kiungu utazipata zaidi ukisoma habari za Yusufu (Mwanzo 41:37-41) na Danieli 5:10-14).

�� Akili za kiungu

Zinapatikana kwa wewe ambaye ni mwana wa Mungu na ukimuomba kwa bidii akupatie anakupatia!

�� Ukimuomba Mungu Roho ya hekima, maarifa na ufahamu utaipata akili hii.

Roho ni nini?

Ni nafsi hai inayoifanya nafsi kuwa hai, kuna tofauti kati ya nafsi na nafsi hai, Nafsi haiitwi nafsi hai isipoungana na roho. Ukisoma mwanzo 2;7 neno linasema Akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

➡ Nafsi inaonekana lakini haiishi pasipo roho. Roho ni nafsi isiyoonekana lakini ni hai.

Kwa hiyo ukiitenga nafsi na roho nafsi hio haitobaki hai tutaizika, itarudi mavumbini.

���� Hapo tumezungumzia roho ya mwanadamu kuna aina mbalimbali za Roho ambazo pia ni muhimu kuzielewa na kuzitofautisha; Roho wa Mungu, Roho ya/za Mungu, na roho za shetani.

�� 1. ROHO MTAKATIFU (Roho WA  Mungu)

Huyu tunampokea kwa namna mbili, kila ujio una kazi tofauti;

1⃣ Uvuvio Wa Roho

Huyu tumempokea kutoka kwa Mungu mwenyewe kwa njia ya kuvuviwa, Yohana 20:21 naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho mtakatifu.

Tukimpokea hutuongoza dhamiri zetu katika kweli;

Warumi 9:1 nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu.

Pia Yohana 16:8 anasema Naye akiisha kuja, huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki na hukumu, Hutufundisha, kutukumbusha; Yohana 14:26

kutuongoza; Yohana 16:12

kwa kifupi kwa njia ya uvuvio Roho huja kama msaidizi.
���� Wote tumepata Neema ya kuvuviwa ingawe wengi hawajui, na kutokujua na kuamini Roho yuko ndani yake hupotea.
Wasiomtambua huyu dhamiri zao huwa dhaifu hivyo rahisi kunajisika.

2⃣ Kujazwa Roho

Ujio huu wa Roho Mtakatifu ni wa nguvu, Ambapo anapokujilia unasikia hali ya tofauti na unapokea nguvu. ukisoma Matendo 1:8 anasema.

"Lakini mtapokea nguvu Roho akishawajilia juu yenu".

Katika ujio huu Roho mtakatifu hushuka na nguvu zake naye huleta roho za Mungu na nguvu ama upako.

Mtu hujazwa Roho kwa kuwekewa mikono ama kuongozwa maombi ama kujitenga na kuomba kwa Mungu.

Huja na ishara mbalimbali mfano kunena kwa lugha mpya. Matendo 2:4

Kwa kifupi kwa njia ya kujazwa Roho huja kwa nguvu akiambatana na matendo ya Muujiza na roho za Mungu zinazotusaidia kuifanya kazi ya Bwana.

Kwa Neema Ya Mungu, Mungu Humvuvia Roho Wake Kila Amwaminiye Amfundishe, Amuongoze, Kumkumbusha,

Lakini Hii Haitoshi Neno La Mungu Linasema; *MTAKENI MUNGU NA NGUVU ZAKE Zaburi 105:4

⚡ Hivyo Unahitaji Ujazo Wa Roho Mtakatifu Katika Huduma Yako Ili Umtumikie Mungu Kwa Ujasiri Matendo 4:31

⚡ Unahitaji Ujazo Wa Roho Mtakatifu Ili Upokee Nguvu Itakayokuwezesha Kutumia Mamlaka; Kumkemea Mapepo, Kuombea Wangonjwa Na Matendo Yote Ya Miujiza N.K.

✅ ya kwanza ya somo hili la AKILI NA ROHO inaishia hapa, leo tumeweka msingi,

Mungu akipenda kwa sehemu inayofuata tutaingia ndani zaidi. Roho mtakatifu atakufundisha utaelewa zaidi endelea kufauatilia kuna namna Roho mtakatifu anataka kukuvusha.

���� Mungu akubariki sana!