Sunday, 25 September 2016

Jiepushe na dark website hatari!

Simu au Computer yako ina hizi tabia?
1. Kukuletea matangazo ya Kudownloada vitu usivyovijua?
2. kupokea emails nyingi za watu wanaomba account yako wakutumie hela?
3. kuletewa matangazo bila mpangilio wakati upo mtandaoni?
4. Kujiconnect kwenye website bila taarifa?Kama unatatizo hata moja hapo, basi wewe ni muhanga wa hiki kitu ninachokieleza hapa chini;

Hii ni elimu muhimu kwako sababu itakuongezea usalama ktk mambo yako ya muhimu na siri zako unazotunza ktk mitandao kwa kutumia SIMU au COMPUTER yako.

Duniani kuna website za aina nyingi sana na zinafanya kazi kwa mifumo tofauti, na baadhi yetu hupenda kusafu mitandaoni kila siku kwa kutembelea website nyingi na kwa wingi.

Website hizo zinamilikiwa na watu tofauti na zipo kwa malengo tofauti na pia zinafanya kazi kwa mifumo tofauti, Leo nitaongelea Website za aina fulani inayojulikana kwa jina la “Dark websites” yaani website giza au website nyeusi.

Sasa basi ninaomba niende moja kwa moja hapa kwenye mfumo unaotumika ktk hizi Dark Websites wakati wa utanyaji kazi; mara nyingi huwa zinaomba ujaze vitu vifuatavyo kabla haujaendelea na chochote; 1. Jina lako2. Email yako 3. Password zako Mfano mzuri ni kama (facebook, sasa basi naomba nieleweke kuwa kuna “Dark Website SALAMA” na pia kuna “Dark WebsiteHATARI“)

Licha ya kuwa Facebook ni aina ya “Dark website salama” lakini kuna watu walikwisha tengeneza website zinazofanana na facebook kwa kila kitu na hizo tunaziita “Dark websiteHATARI“Huo ni mfano mmoja tu, LAKINI zipo website za namna hiyo nyingi sana (Itafika siku nitakuonyesha ni namna gani Hackers huingilia Account za watu za Facebook)

Kwa leo ninaomba tuendelee na hiki kitu ;“Dark websites HATARI” hufanya kazi kama Dark website salama, na hizo Darkwebsite hatari nazo huwa zinaomba ujaze vitu kama jina, email, password ili uweze kupata unachohitaji, lakini wengi wetu hatufahamu madhara yake, Leo nitakwambia kwa ufupi sana kuhusu wale watu Wanaoingilia account za watuwengi bila wahusika kufahamu hutumia mbinu gani,Wao huleta kitangazo kizuri sana tena kina picha nzuri nzuri zikikwambia “download” au “open” au “get this” na wewe kweli masikini bila kujielewa unabonyeza!

Ukifanya hivuo unapelekwa sehemu hatari bila kufahamu, na ukiingia huko utakuta kuna sehemu zinakutaka ujisajili, na wengi wetu huwa tunajaza tu data zetu bila kuelewa tunapelekwa/zinapelekwa wapi.

Nikupe siri sasa, “Dark websites HATARI” ni website feki zinazotumiwa na wahalifu kukusanya data au taarifa za watu, na mara nyingi kwa wale wanaopenda kudownload vitu wasivyovijua. Ukiwa ndani ya Dark website hatari wala hautagundua chochote hadi uwe na software/antivirus ya kukujulisha kuwa upo hatarini!

Mara nyingi ukiwa humo huwa kuna mdudu anaitwa “Malware” anajidownload bila wewe kufahamu na anaingia ktk simu au Computer na anajificha.Kazi yake kubwa ya huyu mdudu ni kuiba data zako muhimu na kuzituma kwa mmiliki wa hiyo Dark website Hatari, (Wataalamu wa IT wengi huwa wanaweza kuziset hizi Dark website HATARI hivyo ninaamini wananielewa vizuri)

Namna ya kuepuka; Njia ya kwanza; Ukiwa na simu au Computer unaweza kutumia Antivirus inayoitwa Eset Node 32 Antivirus ambayo ina protection nyingi zikiwemo hizo za kuzuia Dark websites HATARI, kwa wenye simu mtaipata play store kwa kuandika neno “eset” na kubonyeza search/go, itatokea ya kwanza kabisa imeandikwa “Mobile Security & Antivirus”

Na wenye Computer mtaipata hapa ⇒  https://maxitclub.wordpress.com/antivirus-nzuri/mimi binafsi huu ni mwaka wangu wa 3 ninaitumia na nipo salama), kwa wenye Computer ninawashauri muachane na kutumia Antivirus nyingine hizo zinazo wasumbua ku update kila siku.

Njia ya pili; Epuka kupokea simu, sms na email zinazotoka sehemu zisizo julikana “Unknown sources” nafahamu wenye Smartphones mnajua hiki kitu, kuwa kuna sehemu imeandikwa “Allow installations from unknown sources”, hawa jamaa wanafahamu kila kitu na ndio maana wamekuachia jukumu ujiamulie mwenyewe.

Njia ya tatu; Epuka kudownload au kubonyeza hovyo matangazo usiyokuwa na taarifa nayo, na mara nyingi huwa yanakuwa ni matangazo ya Ngono, Miziki, Biashara n.k, acha hiyo tabia ya kubonyeza kila uachokiona.Hitimisho;Hasara ya kuingia kwenye Dark Website HATARI, utakuwa unaona text au email zinaingia kila siku na nyingi huwa zinakuja na majina ya kike zikiomba ujibu na pengine mtumiane picha, au nyingine zikikudanganya kuwa kuna hela zipo sehemu hivyo basi usaidie kwakutuma account namba yako ya benki ilizihamishiwe kwako.

Walio wengi huwa wanafanya hivyo, lakini hatari yake ni kubwa, ipo siku utafanyiwa kitu kinaitwa“HACKING” kwa kiswahili ni “KUINGILIWA KWENYE ACCOUNT ZAKO BILA KUFAHAMU“ Ushauri; kwa wafanyakazi mnaofanya kazi kwenye makampuni makubwa kama yanayojihusisha na mambo ya Fedha, Usalama, Huduma za Afya, Wahasibu Vyuoni au Mashuleni, Viongozi wakubwana wadogo Au watoa huduma zozote za muhimu ktk jamii mnatakiwa muache kabisa tabia ya kujaza hovyo data zenu mahala msikokujua.

Aidha kwa wasio wafanyakazi pia mnapaswa kuacha ili kuwa salama zaidi.

Wednesday, 21 September 2016

After work, is what determines your Life! Change ur Life forever by doing this 5 things!

Kalyana SundaramBusiness Development Manager - SAP

After work, is what determines your future! Spend one hour per day doing these 5 things and your life will change forever!

May 19, 2016 • 35213 Likes • 2726 Comments

You finish work at 6 pm, go to bed at 12 midnight.

Within these six hours, how do you spend them?

Watching TV?

In fact, the activities you do between 6 am and 12 midnight,

the importance of it is beyond your imagination.

Too many people believe that,

your career is determined by the 8 hours of hard work and effort you put at work,

and your future and career progression depend on the boss and the company.

But the reality is that for most people, this thing, you are on your own…..

 

Read on…

 

“Cultivation”, it’s forever dependent by yourself.

If you found yourself not progressing in life,

you cannot blame and put the responsibility on your company for not grooming you.

 

1. What you do every night is important

My major in college was marketing, but I expect to become a designer.

So I practiced day and night,

picking up some freelance work to improve my design skills.

It took me a long time.

When I became a boss, I no longer need to involve myself in design work,

So I went back to the Marketing field.

Every day, when my children are sleeping,

I began learning to gain more knowledge, this again took me a long time,

But I begin to realise my returns.

 

If I rely on my working hours to gain skills,

then I will never have become a creative director and a product manager,

or like today, teaching MBA students on Marketing.

What I rely on, is myself giving myself “lessons”.

And the most successful people I knew, walked the same path as I am.

I have a friend who is a History graduate,

but he is interested in technical sales,

In the day, he does telemarketing, at night he learns how to code,

Finally, he became the vice president of sales in a startup company.

Now, he’s a CTO.

I have another friend, he received a degree in political science.

But he’s very interested in entrepreneurship.

he learnt a lot of knowledge on how to start up a company,

eventually, he founded a company and sold it,

Now he has reaped the rewards.

 

For them, what they do between 6 pm till 12 midnight,

is what determined their future.

Clearly, we need to balance life and work.

If you have a wife and children, every night, you have to stay with them.

Even if you are single, you also need a reasonable allocation of time to go to the gym, to meet with friends, or be alone to meditate and so on.

Of course, watching movies, playing games is good.

But there are things you do not need to do.

For example, watching the new season of a Netflix drama,

14 hours per week watching television (This is the average amount of time watching television).

 

The time spent playing the game Candy Crush.

 

Or spending time stalking your high school alumni on Facebook,

it does not seem to be good.

So what should you do?

 

2. Read more, anything will do!

My college mentor was born in Alabama,

A poor African family.

He was admitted to West Point Military Academy, and he became the first person in the family to go college.

Before going to Havard for his MBA, he’s a trained officer.

When I met him, he has already developed his career in the city of Colorado Springs.

 

I asked him, what’s his biggest success?

He replied, because he kept the habit of reading,

and he never stopped.

He believed that if you want to get what you want in life,

knowledge is the key.

He often asked his interviewees what book are they reading now,

the excellent ones can give an answer immediately.

Reading can give you a good headstart,

this is often what your peers cannot obtain.

Compared to others,

you are more likely to know other industries strategies and tactics,

and that may be helpful to your company.

 

You can transfer your knowledge within the organization,

create new possibilities for your company.

Moreover, your conversation topics will become more interesting.

 

Anthony Robbins said:

“If you spend one hour a day to learn about a topic,

a year later, in this regard,

the knowledge you gain will be more than 99.999% of the world’s people.”

Even if you have 30 minutes every night,

each week you can easily read a book.

You may not be an expert, but I promise,

you’ll know more than what your peers know.

 

3. Do some projects

You can apply the knowledge learnt to real work scenario,

this is only an ideal state.

If your company did not give you this opportunity,

create opportunities for yourself.

You can do some volunteer projects. They can bring you fame.

Working with a team,

you’ll understand how things work.

In the practical application of the industry,

and how it ultimately affect actual customers.

You’ll learn how to perform the task and meet deadlines,

and get feedbacks on what you are doing,

and benefit from it.

 

When you are not strong enough, these experience may not have any value to you.

But you are still a novice.

these experiences are far more valuable than the miserable pay you are getting.

If you can really convince others of your pockets of fruits of labour,

Then go try it. But do not let these private jobs affect your work.

 

4. Actively build your connections

In your career path,

a strong network of connections will make everything accelerate.

If you have not set up your own personal connections,

you’ll need to divide a portion of your time to do this.

A strong network of relationships, can enable you:

contact smart friends, and learn their opinionsget information and knowledge that are difficult to obtainhelp the company look for more potential partnersor income generating opportunities

Go get to know your work colleague or boss…..

 

If you are an entrepreneur,

your network connections will be your early customers,

your staffs are a source of capital

rather than go home, or going to a bar,

you should find some inner circles.

There are many small groups which are highly relevant to your career.

You should try to integrate into these circles.

Every week, you can drink coffee together with new friends,

go drinking or have breakfast.

 

You can also look into everyone’s career developments on LinkedIn.

And establish a network with mentors in those professional industries.

They may be your next job employer, who knows?

Your connections will be your most powerful asset in the workplace.

Since you have time to watch “The Voice of China”,

you have time to build a social network.

 

5. The CHANGE of your LIFE starts TONIGHT

6 pm to 12 am, you go home, though physically and mentally tired,

you are free to do anything and do not have to take orders from others.

During this time,

you can switch off like switching off your computer at your workplace, switch off your brain.

But you can also do something,

make you smarter, stronger, have a wider network of people.

From the start tonight, take an hour a day to do these things,

I guarantee that after a year,

your career, and life will change.


Tuesday, 20 September 2016

Mheshimiwa abambwa gesti na bintiye!

Mheshimiwa Abambwa Gesti na Mwanaye!

DAR ES SALAAM: CHAR/RB/1847/2016 KUJARIBU KUBAKA ni RB ya Kituo cha Polisi Mbagala Charambe jijini hapa  ikimhusu moja kwa moja mheshimiwa Damian Edward Kakuru, mkazi wa Mwandege wilayani Mkuranga, Pwani kufuatia askari wa kituo hicho na ‘makachero’ wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kumnasa ndani ya chumba namba 6 kwenye gesti iliyopo Mbagala, Dar akiwa na binti yake (16), jina tunalihifadhi kwa sasa, Wikienda tu linakujuza zaidi.

SIKU YA TUKIO

Mheshimiwa Kakuru alikumbwa na tukio hilo zito katika kumbukumbu za maisha yake, Septemba 15, mwaka huu akiwa kwenye chumba hicho katika harakati ambazo ziliashiria ni za nia ya kutaka kujaribu kumbaka binti huyo ambaye kisheria yuko chini ya miaka ya kujitambua kwa maamuzi, 18.

KWA NINI MHESHIMIWA?

Licha ya yale yaliyotokea, mzee Kakuru inadaiwa amekuwa mzee wa Kanisa la Truth Ministry International lakini pia

 Inatoka Uk. 2 anaheshimika katika jamii ya maeneo anayoishi. Sehemu ya mavazi yake ni zile suti za viongozi huku wengine wanaoonekana kuzivaa sana ni watu wa usalama wa taifa hali inayomfanya asilikwepe jina la mheshimiwa kwa watu wa Mwandege.

MWANAYE KIVIPI?

Kabla ya kuendelea na tukio hilo, muhimu kufahamu ni kwamba, mzee Kakuru ana wake wanne. Mmoja wa wake zake, anayeishi mkoani, ana mdogo wake wa kike, ndiye mwenye mtoto huyo. Hivyo, alipofika kuishi kwa mzee huyo, maana yake yupo kwa baba yake mkubwa. Na maisha yao nyumbani hapo ni ya mtu na mtoto wake; ‘shikamoo baba, marahaba mwanangu’!

SASA TWENDWE PAMOJA

Jumba bovu hilo ‘lilimwangukia’ mzee huyo baada ya binti yake kulalamika mara kadhaa kwa watu anaowaamini kuwa, baba yake huyo amekuwa akimshawishi kutenda tukio ambalo yeye anaamini ni la ‘watu wazima’ na wasio na uhusiano wowote. “Binti amedai kuwa kutokana na mazingira hayo kudumu kwa muda mrefu, aliwahi kumshtakia kwa mama yake lakini ilionekana kama mtoto ana uelewa mdogo katika kupokea mambo na kuyatafsiri, lakini pia ilibidi kuwe na kikao cha kifamilia ili kumaliza madai hayo,” kilisema chanzo kimoja.

KIKAO CHASHINDWA KUFUA DAFU

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo, licha ya kikao binti huyo alidai baba yake huyo aliendelea kumsumbua hali iliyomsukuma binti, safari hii kuhamishia malalamiko yake kwa walimu katika shule ya sekondari (jina lipo) ambapo binti huyo anasoma na sasa yupo kidato cha nne.

WALIMU WAPELEKEWA MALALAMIKO

Wikienda lilitajiwa orodha ya walimu ambao, binti huyo alifungua kinywa chake kuwatonya anachokutana nacho kwa baba yake huyo. Walimu hao walitajwa kuwa ni Mapunjo (jina moja, mwalimu mkuu), Adamu Nyema (mwalimu wa malezi), mwalimu Hokororo na mwalimu Said ambao binti huyo alidai wote wanafahamu malalamiko yake.

WALIMU NA MAMA MZAZI

Chanzo kikazidi kuweka wazi kuwa, baada ya kupokea malalamiko hayo, walimu hao waliwasiliana na mama wa binti aitwaye Goret Kabogwi ambaye anaishi Kamachumu wilayani Muleba, Kagera. “Lakini kinachoonekana ni kwamba, mawasiliano ya walimu na mzazi wa mtoto huyo hayakuzaa matunda kwa kuwa walimu walikuwa wakitaka kumchukua mwanafunzi huyo ili wakaishi naye mpaka atakapomaliza shule arudi kwa mama yake lakini taratibu za kisheria za kuishi na binti huyo zilionekana kuwa ngumu hivyo kumuacha njia panda.” Chanzo.

HADI KANISANI

Chanzo: “Wakiwa katika kutafuta nini cha kufanya, binti huyo aliendelea kutafuta ufumbuzi mwenyewe ambapo sasa alilipeleka suala hilo kanisani ambako ndiko alikotokea muumini mmoja aliyemuongoza binti huyo

kuwasiliana na OFM na kumhakikishia kwamba, suala lake litakuwa limekoma kama siyo kwisha kabisa! BINTI NA OFM Mungu si Kalimanzila, Septemba 14, mwaka huu, binti alifanikiwa kukutana na OFM uso kwa macho na kusema yote kuhusu mzee huyo huku akirekodiwa kwa sauti na picha kwa ajili ya kuboresha kazi.

USHAURI WA OFM

Baada ya maelezo yake hayo, OFM walimtaka binti huyo kama ni kweli, kufuata maelekezo kama siyo maagizo. Binti huyo alielekezwa na OFM kumkubalia baba yake huyo ili wanaswe wakiwa gesti, jambo ambalo litaongeza ukweli wa malalamiko yake. Binti: “Sawa, mimi nimewaelewa, lakini sasa nikirudi nyumbani, baba akaniambia tena maneno yake mimi nitawapataje ninyi? Maana sina simu!” OFM: “Sisi tutakupa simu na namba zetu zitakuwemo humo, sawa ee?” Binti: Sawa, nitashukuru sana. Maana nimekuwa sisomi nikaelewa, kisa ni

kusumbuliwa na baba.” OFM: “Usijali binti, yataisha hayo, OFM ni kazi yetu kuhakikisha maadili yanasimama sawasawa na inavyotakiwa.” BINTI NYUMBANI Baada ya kurudi nyumbani, kama kawaida, mzee huyo bila kujua kuwa, OFM wapo kazini, alimwambia binti yake yale maneno. Safari hii, binti alikubali kwa urahisi lakini akaomba eneo la tukio lisiwe nyumbani bali sehemu nyingine yoyote ili kutunza siri. Alipewa maelekezo kuwa, kesho yake, apande daladala kutoka Mwandege hadi Kituo cha Kokoto, Mbagala ambako atakutana na mzee huyo na kutafuta sehemu yenye utulivu kwa ajili ya ‘mazungumzo’ yao.

Binti akawasiliana na OFM, akaambiwa good!! SEPTEMBA 15, OFM POLISI Asubuhi ya siku ya tukio, binti huyo aliiambia OFM tayari baba yake ameshamuelekeza eneo la kukutana ambapo OFM nao wakaenda kumjulisha Mkuu wa Upelelezi Polisi Wilaya ya Mbagala (OC-CID), Tobias Walelo na kumueleza mpango mzima. Afande Walelo baada ya kusikiliza kwa umakini maelezo na kuambiwa OFM wanasubiri ushauri wake, alisema amegundua kuna kosa la jinai, aliwataka OFM kwenda Kituo cha Polisi Charambe ambapo ni karibu zaidi na eneo la tukio na kumtaarifu suala hilo mkuu wa kituo hicho.

OFM, ASKARI GESTI

Mipango ilisetiwa, maafande wa kituo hicho na OFM waliongozana kwenda gesti kwa maelekezo ya binti huyo kupitia simu ya mkononi ya OFM na kujibanza sehemu kwa siri. Baada ya dakika kadhaa, mzee Kakuru alionekana akiwasili eneo hilo akiwa amevaa suti iliyonyooshwa kwa pasi vizuri. Alimkaribia binti huyo na kumwonesha tabasamu laini kisha wakaanza kukata vichochoro, baba mbele binti nyuma. OFM na polisi wakiwafuata kwa nyuma kimtindo, wawili hao walimaliza vichochoro kadhaa kisha wakatokea kwenye  nyumba ya wageni iliyotulia, walizama ndani kwa pamoja.

POLISI KWA MHUDUMU

Polisi walisubiri kwa dakika chache kisha wakaenda kwa mhudumu wa gesti hiyo na kumtaka awaoneshe chumba walichoingia wawili hao. Kwa kutii amri ya jeshi la polisi, mhudumu huyo aliwaonesha chumba namba 6 ambacho alisema hadanganyi!

BINTI ALIVYOJIONGEZA

Kwa kuwa katika kuingia ndani ya chumba, binti huyo ndiyo alikuwa nyuma hivyo alitumia nafasi hiyo kuufunga mlango kwa geresha, kitendo kilichowasaidia polisi na OFM walipofika mlangoni kusukuma na kuingia ambapo wawili hao walikutwa nusu utupu!

BABU AJING’ATANG’ATA

Baada ya kunaswa laivu, baba huyo aliwatolea macho polisi na kuulizwa kwa nini yuko chumbani na binti huyo ambapo alisema alikuwa na binti yake kwa ajili ya kutatua tatizo fulani lililopo kati yao. “Hapa sisi tumekuja kusuluhisha mgogoro, ninyi mnataka nini? Hebu tuacheni.”

KWA NINI MGOGORO USULUHISHWE GESTI?

Mheshimiwa huyo alipoulizwa sababu ya kusuluhishia mgogoro gesti, awali alikaa kimya kisha akasisitiza walikuwa wakitaka kusuluhisha tatizo.

MASHUHUDA WATAKA SHERIA IFANYE KAZI

Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na OFM waliitaka serikali kusimamia kikamilifu sheria iliyopitishwa kwa kishindo na wabunge mwezi Juni, mwaka huu ya kuwabana wale wote wanaotembea na wanafunzi  na watoto wa kike walio na umri chini ya miaka 18.

Friday, 16 September 2016

Je, huwa unakoroma? Je wajua sababu na jinsi ya kuzuia?

Sababu ya kukoroma na jinsi ya kuzuia hali hiyo!

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji.

Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?

Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:

• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.

• Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.

• Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.

• Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.

• Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake.

Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.

 Je, Dawa ya kukoroma ni nini?
Swali hilo limeuliwa sana na mimi katika kulijibu ningependa kusema kuwa, kujua sababu inayosababisha mtu akorome na kuitatua au kuiondoa sababu hiyo ndiko kunakotibu kukoroma. Sote tunajua adha inayotokana na kukoroma, na sauti hiyo inavyosumbua hasa iwapo anayekoroma ni mtu wako wa karibu kama vile mumeo, mwenzi wako au yoyote yule inayekubidi ulale naye karibu au katika kitanda kimojana hata chumba kimoja.

Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde kadhaa ambapo usingizi pia hukatika. Wanaokoroma pia hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. Vilevile tunapaswa kujua kuwa kukoroma kuna athari za kiafya za muda mrefu kwa mtu anayekoroma hivyo si jambo la kufanyia mzaha na ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa.

Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:

1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.

2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.

3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.

4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.

Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, unashauriwa ujaribu yafuatayo:

 Punguza uzito
 Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.
 Wacha kuvuta sigara.

 Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana. Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.

Wataalamu pia wanasema kwamba unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile
o Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.
o Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.
o Kutokunywa pombe kabla ya kulala.
o Kutotumia dawa aina ya antihistamines.
o Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na kurudisha ulimi nyuma kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa kulia na wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30.

Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini.

Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofauti zilizoelezwa, usife moyo jaribu kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo. Madakatari wataalamu wa magonjwa ya pua, masikio na koo au ENT wanaweza kukusaidia zaidi kutatua tatizo hilo.

Siku hizi kuna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa mahospitalini ili kuondoa kukoroma kama vile kifaa kinachowekwa kwenye meno, CPAP, kidude kinachowekwa mdomoni au hata kufanyiwa operesheni ili kuondoa tatizo hilo.

Friday, 9 September 2016

Utaratibu wa uhamisho kwa mtumishi wa umma!

UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

1. Mamlaka za Uhamisho

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003 Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na

Kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekasimiwa kwa;

Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na;Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja kwenda kingine ndani ya Halmashauri.

2. Aina za Uhamisho

Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;

Uhamisho wa Kuomba

Taratibu za Kuomba Nafasi:-

Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.

Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopoIwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho huo.

Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi.Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.

Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyo

Angalizo:

Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.

Upatikanaji wa Majibu:-

Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.

Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba.

Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.Uhamisho wa Kawaida

Uhamisho huu ni wa kawaida ambapo Mwajiri au Msimaimizi wa kazi anafanya uhamisho kwa sababu za kuboresha utendaji.

Hata hivyo ili uhamisho huo ufanyike pia Mamlaka za uhamisho zinatakiwa kujiridhisha uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri anayohamishiwa mtumishi wa hakusababishi upungufu katika Sehemu mtumishi anakotoka au anakohamia.

Uhamisho huu kwa kawaida unagharamiwa na Halmashauri inayompokea mtumishi na ile inayomruhusu kwa kumlipa gharama za kufunga mizigo kama ilivyoelezwa kwenye Kanuni L (8 na 13) ya Utumishi wa Umma ya Kudumu toleo la 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2010 kwa wakati. hivyo ni muhimu Mamlaka za Uhamisho kijiridhisha na uwezo wa Halmashauri kugharamia uhamisho huo ili kuepuka kuzalisha madeni kwa Serikali

Pamoja na utaratibu wa uhamisho kuwa ni uhamisho kufanyika mara mbili kwa mwaka, uhamisho huu wa kawaida unaweza kufanyika wakati wowote katika jitihada za kunusuru utendaji katika kituo alichopo mtumishi au anachohamishiwa mtumishi kwa manufaa ya umma.

Angalizo:

Mtumishi atakayebainika kughushi saini za viongozi, kuomba au kupokea rushwa katika ngazi yoyote atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumfikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ni muhimu kwa Waajiri kujiridhisha na majibu ya barua za uhamisho kutoka katika Mamlaka za uhamisho ili kuona kama maombi yake yalifuata taratibu sahihi na watumishi waliopata majibu wanatayarishiwa mapema data sheet na kumbukumbu za utumishi na mshahara ili kuepusha usumbufu kwa watumishi na waajiri wanaowapokea watumishi

Mambo 10 ambayo mwanaume hupenda kusikia toka kwa wenzi wao!

Fahamu Mambo 10 Ambayo Mwanaume Hupenda Kusikia Toka Kwa Mpenzi Wake!

10. Kukosolewa – “I think you are wrong”

Wanaume wanaweza kujikweza sana lakini daima hawachukii kurekebishwa. Wanachojali zaidi ni jinsi gani au njia gani imetumika kuwarekebisha. Mwanaume akikosea, anataka mpenzi wake amkosea lakini kwa mapenzi, sio kwa mikwaruzano au dharau au mbele ya kadamnasi. Mrekebishe au mkemee faragha, toa maoni yako na wala usimlazimishe, itamfanya aone unajali na unataka kumjenga.

9. Kujali – “How was your day?”

Wanawake wengi hutaka wao tu ndio waulizwe kuhusu jinsi siku zao zilivyoenda kila siku, wanasahau kabisa hata wanaume nao walikua kwenye mihangaiko. Mzoeshe kumuuliza mpenzi wako siku yake ilikuwaje? utaona hata nuru ya mapenzi yenu itang’aa na mtakua marafiki, japo mwanzoni atakua hakuambii kila kitu lakini baada ya muda atazoea. Kila mtu anataka wa kumsikiliza, mtu atakayezungumza nae chochote kilichotokea ndani ya siku yake, na pengine kukuuliza ushauri.

8. Ucha Mungu – “Can we pray?”

Mwanaume, anayesali au kutosali, lazima huwa ana imani kwamba Mungu yupo. Mwanamke mcha Mungu siku zote huwa ni wazo la kila mwanaume endapo ana mpango wa kuoa. Mwanaume huwa na amani kwa kiasi fulani akiongozwa na mwanamke wake kwa upande huo wa sala.

7.  Msamaha – “I forgive you”

Vikombe kwenye sahani havikosi kugongana, vivyo hivyo na kwa wapenzi, kuumizana hisia hakuepukiki, iwe kwa makusudi au bahati mbaya, mwenzio akikosea sasa isiwe ndo adhabu, akiomba msamaha ukamwambia nimekusamehe na kweli umemsamehe, funika kurasa endeleeni na maisha. Usililete tena mezani jambo ulilosema umesamehe.

6. Sifa – “That was great sex”

Kama amefanya kazi nzuri, mwambie. Wote tunajua sio kila siku watu hufanya kiwango che Maradona au Pele, siku akiwa kwenye kiwango hicho hata yeye anajua, usisite kumpa sifa zake. Wazungu wanasema, ‘Yes, you can kiss and tell some of the times’. Na kama unaona kuna sehemu anahitaji kujisogeza, mwambie pia, tena kimahaba. Hii itawasaida nyote.

5. Upekee  – “I admire you. No other man is like you”

Ni kweli kwamba kuna wanaume ambao ni wazuri na wenye uwezo mkubwa zaidi ya huyo ulienaye, lakini kwake hujisikia vyema zaidi ukimwona yeye ni zaidi ya wote hao. Sio mbele ya macho yake tu, matendo yako na hata nyuma yake msifie kwamba yeye ndio mwanaume pekee duniani unayempenda na hakuna mwingine zaidi yake.

4. Uaminifu – “I trust you”

Mwanaume akijua anaaminika sana kwa mwanamke, na yeye hujiachia. Na kwa hili huwa anaweza kugombana na watu kabisa kwa ajili ya mwanamke wake. Japo wengine hulitumia hili kwa uchafu wao lakini wengi wao ni kitu chema kwao.

3. Mapenzi –  “Make love to me”

Ni mtazamo wa wengi kwamba mwanaume ndio siku zote awe mwanzilishi wa tendo. Lakini mwanaume kwa wakati mwingine hupenda mwanamke wake ampe vishawishi na yeye vya kumleta kwenye mood. Sio kila siku aanze yeye tu, wakati tendo ni la kuwafurahisha wote. Hata kama ni ngumu kusema kwa mwanamke, ishara kibao zipo za kumuonyesha mwenzi wako akaona ‘Leo baby anataka na yeye’.

2. Malengo -“What’s your dream?”

Mwanaume anaweza asionyeshe kama anahitaji msaada, lakini kwa kutumia njia za mapenzi, unakuta ni mwanaume tu anayehitaji uwepo  wa mwanamke anayempenda yeye. Mungu alimtengeneza mwanaume na kumpatia msaidizi kwa kumpatia mwanamke. Kuwa mwanamke mwenye msimamo na mpangilio mahiri usiotikisika, ambaye unauwezo wa kumuuliza anaenda wapi katika maisha yake, na akakukumbusha huko siko ni huku. Ndoto za mwanaume mara nyingi huendana na zile na mwenzi wake, na mwanamke huwa pale kuhakikisha ndoto za pamoja zinatimia.

1. Upendo wa dhati – “I love you”

Wanaume wengi hujiona wagumu kwenye kutamka neno ‘I love you’ kwa wanawake zao na hata akisema itakua ni mara chache chache hata kama kweli kutoka moyoni wanapenda, lakini haina maana hawataki kuambiwa na watu wanaowapenda, hii huwaaminishia nafasi yao kwenye moyo wa mwanamke.

Monday, 5 September 2016

Mambo 10 muhimu maishani

Katika dunia ya leo, ambayo ipo kwenye ushindani mkubwa ili uweze kufanikiwa unalazimika kujifunza mambo mengi ya kukusaidia kufanikiwa huko. Bila kufanya hivyo hautaweza kufanikiwa na kufikia viwango vya juu, zaidi utaishia kuwa na mafanikio ya kawaida kabisa.

Haijalishi uwe umeajiriwa au umejiajiri ni muhimu kujua mambo mengine ya ziada ambayo tena ni ya kawaida lakini, yanaendana na kasi ya ulimwengu wa sasa. Kwa jinsi utakavyojua mambo hayo utazidi kujiongezea thamani kubwa ambayo bila ubishi itazidi kukupa mafanikio.
Yafuatayo Ni Mambo 10 Ambayo Ni Muhimu Kuyafahamu Kwenye Maisha Yako.

1. Kuongeza maarifa.
Kila siku na kila wakati, jenga tabia ya kuongeza maarifa. Jifunze kupitia vitabu au semina mbalimbali. Kuunoa ubongo inatakiwa iwe sehemu ya maisha yako na  ni hatua muhimu sana ya kukusaidia kufikia mafanikio makubwa kuliko unavyoweza kuwaza au kufikiri. Watu wenye mafanikio wanajifunza sana kila siku.

Ongeza maarifa yako kila siku.

2. Kutengeneza bajeti.
Huhitaji kusomea uchumi ndio uweze kupanga bajeti. Katika maisha yako pia unahitaji kujifunza juu ya upangaji wa bajeti zako binafsi. Hiyo itakusidia kutokuwa na matumizi ya hovyo ya pesa zako. Pia bajeti itakusaidia kutunza pesa na kukusaidia kuwekeza kwa siku za baadae.

3. Kuwasikiliza wengine vizuri.
Ni vyema kujua namna ya kuwasikiliza wengine vizuri. Acha kuwa muongeaji tu kila wakati na kusahau kuwasikiliza wengine. Unapowasikiliza wengine inakusaidia kujifunza mambo ya msingi ambayo ingekuwa sio rahisi kwako kujifunza kama ungekuwa unaongea wewe tu.

4. Kongea mbele ya watu wengine.
Jambo lingine ambalo hutakiwi kukwepa kujifunza ni kuongea mbele za watu. Lazima uwe na maarifa ya kukusaidia kuogea mbele za watu. Ikiwa utakuwa unaogopa kuongea mbele za watu jiulize, ni nini kitatokea ikiwa utapewa jukumu hilo? Hivyo unalazimika kujifunza hili pia kwa faida yako.

5. Kujifunza lugha zingine.
Kwa dunia ya sasa jinsi ilivyo, si ya kukaa na kujivunia lugha ya aina moja. Ni vizuri ukawa na tabia ya kujifunza lugha nyingine za kigeni angalau hata moja pole pole. Hiyo itakusaidia hasa pale unapotaka kujifunza kitu kwa mfano kupitia vitabu haitakuwa tabu sana kwako kwa sababu lugha utakuwa unaijua.

6. Kuwa na mwonekano mzuri.
Moja ya kitu kizuri cha kukusaidia kukutambulisha ni mwonekano mzuri ulionao. Unapokuwa na mwonekanao mzuri inakusaidia kukutambulisha wewe ni nani. Pia Mwonekano wako unakuwa unakutangaza kwamba wewe ni mtu wa aina gani katika jamii husika.

7. Kulinda siri za wengine.
Ni vyema katika maisha ukajifunza pia kuwa mtu wa kutambua na kulinda siri za watu wengine. Usiwe mwongeaji sana wa mambo yasiyo kuhusu hasa ya watu wengine. Linapotokea jambo ambalo unaona linaweza likawa siri, ni vyema kukaa kimya kuliko ukawa mvujishaji wa mambo ya watu.

8. Kutumia kompyuta kwa ufasaha.
Haijalishi wewe ni bosi au muajiriwa. Ni muhimu sana kujifunza juu ya matumizi ya kompyuta. Hapa unatakiwa ujue program mbalimbali kama ‘Microsoft office au Excel’ ambazo zinaweza kukusaidaia. Pia kwa kujua kompyuta hata ikitokea umepata kazi sehemu, zipo ofisi ambazo hazihitaji sana secretary maarifa hayo yatakusaidia.

9. Kuendesha gari.
Unaweza ukaona ni kitu cha kawaida lakini lazima ujue kuendesha gari. Hii sio dunia ya kusubiri eti ununue gari ndio ujue kuendesha. Ni muhimu kujifunza kuendesha gari na hiyo itakusaidia kukuongezea wasifu kwenye mambo mengine kama ya kazi au kukupa uzoefu binafsi hata wewe.

10. Kupika.
Si vibaya ukawa na maarifa ya kupika pia. Haijalishi wewe ni mwanume au mwanamke ni muhimu kujua kupika hata kidogo. Jiulize kama hutaki kabisa kupika wale wanaokupikia siku wasipofanya hivyo utafanyaje? Naamini itakusumbua na itakuwa shida kwako. Hivyo ni muhimu kujua kupika na hilo jukumu lisibaki kwa wanawake tu hata kwa wanaume pia.

Hayo ni baadhi tu ya mambo machache ambayo unalazimika kuyafahamu katika maisha na mafanikio yako kwa ujumla. Unaweza ukajifunza mambo mengine zaidi kwa kadri unavyoweza.

Sunday, 4 September 2016

Majambazi yafanya tukio lingine!

Majambazi, hii sasa imezidi! Tunaomba serikali iangalie hili kwa jicho pevu!

Handeni. Siku moja baada ya majambazi kumuua mlinzi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu), Tanga, majambazi ambao idadi yao haijafahamika, wamefunga Barabara ya Segera – Chalinze katika Kijiji cha Kwachuma wilayani Handeni kwa zaidi ya saa mbili na kupora fedha na simu za abiria waliokuwa kwenye magari usiku wa kuamkia jana.

Katika tukio hilo, watu watano walijeruhiwa kwa mapanga na kupelekwa Hospitali ya Magunga Korogwe.

Juzi, majambazi yalivamia Sekomu na kulipua moja ya mabweni ya chuo hicho, kisha  kumuua Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Tele Security, Yohana Shemzigwa na kumjeruhi mlinzi mwenzake, Abuu Rajab.

Akizungumzia tukio la usiku wa kuamkia jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema majambazi hao walifunga barabara saa tano usiku kwa kutumia magogo kisha kuanza kuwapora mali watu waliokuwa wakipita kwa magari eneo hilo.

Friday, 2 September 2016

Mawe katika kibofu cha mkojo!

Tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo (Gallstones).

Tatizo hili linazidi kushika kasi kwa kuwasumbua watu wengi kuliko ilivyokuwa awali. Vitu kama mitindo ya maisha na vyakula tunavyokula, vinatajwa kuwa chanzo kikuu cha tatizo hili.

Kwa kuzingatia hilo, makala haya yameandaliwa kujaribu kuchambua Gallstones ni nini, husababishwa na nini na matibabua yake.Gallstones ni nini?

Gallstones ni vimawe vidogovidogo vinavyopatikana kwenye kibofu cha mkojo au kwenye nyongo ambavyo humsababishia mgonjwa maumivu makali. Vimawe hivi vinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu.

Cholestrol Gallstones (Mawe ya Lehemu)

Haya husababishwa na ulaji uliokithiri wa vyakula vyenye Cholesrtol ambapo ikiingia kwenye mzunguko wa damu, hujikusanya na kisha kuganda kwenye kibofu ambapo baada ya muda hubadilika na kuwa vimawe vigumu.

Black Pigment ( Pigmenti nyeusi)

Haya husababishwa na kuharibiwa kwa kiwango kikubwa cha chembe nyekundu za damu (red blood cell) ambapo mabaki ya seli hizo hujikusanya kwenye kibofu na kuganda, kisha kutengeneza vimawe vigumu vyenye rangi nyeusi.

Brown Pigment (Pigmenti za Kahawia)

Haya husababishwa na kurundikana kwa uchafu katika kibofu cha mkojo. Wanywaji wa pombe na wavutaji wa sigara wapo katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya mawe kwenye kibofu.Uwepo wa mawe haya kwenye kibofu husababisha maumivu kama ya moto kuwaka tumboni, tumbo kujaa gesi na kunguruma, mwili kukosa nguvu, homa kali na kama mgonjwa asipotibiwa, husababisha kifo.

DALILI ZA TATIZO!

Tatizo hili linapoanza, huwa hakuna dalili za moja kwa moja, na mtu anaweza kukaa na mawe hayo kwa miaka kadhaa bila kuhisi chochote. Dalili huanza kuonekana yanapoongezeka ukubwa na kufikia kiwango cha milimita 8. Dalili za awali huwa ni kuhisi maumivu makali upande wa kulia, juu ya tumbo.

Maumivu haya huambatana na
kichefuchefu cha mara kwa mara na kutapika mfululizo. Dalili nyingine ni maumivu makali katikati ya mabega, upande wa mgongoni hasa nyakati za usiku.Pia kushindwa kula vyakula vyenye mafuta ni dalili nyingine ya tatizo hili.

Mtu mwenye mawe kwenye kibofu, anapokula chakula chenye mafuta, hata kwa kiwango kidogo, hupatwa na kichefuchefu, tumbo hujaa gesi na wakati mwingine hutapika nyongo.

MADHARA.

Uwepo wa mawe katika kibofu, husababisha ugonjwa uitwao Cholecystitis ambao huendana na kurundikana kwa nyongo katika kongosho, hali ambayo husababisha tatizo lingine la utumbo kushambuliwa na bakteria hususan Escherichia coli au Bacteroides.

Mawe haya husababisha madhara zaidi kwa kuziba mirija mbalimbali ndani ya mwili, ikiwemo mirija ya mkojo, hali ambayo kitaalam huitwa Cholangitis au Pancreatitis.

Hali hizi huwa hatari sana kwa uahi na husababisha kifo kwa mgonjwa endapo atachelewa kupatiwa matibabu

UCHUNGUZI WA TATIZO

Ugonjwa wa mawe katika kibofu au nyongo, hupimwa kwa kutumia mbinu za kitaalam ambazo ni:
Ultrasound: Mionzi maalum hutumika kuangalia viungo vya ndani ya tumbo, hasa kibofu na nyongo kuangalia kama kuna vitu visivyo vya kawaida. Majibu ya Ultrasound pekee hayatoshi kutoa majibu ya mwisho, bali daktari atayaunganisha na majibu ya vipimo vingine.

Oral Cholecystogram (OCG): 
Hii ni mbinu ambayo mgonjwa anapewa vidonge maalum ambavyo vikigusana na mawe ndani ya tumbo, hubadilika rangi na kufanya iwe rahisi kwa mawe hayo kuonekana kwenye kipimo cha tatu,

X- Ray.
X Ray: Baada ya mgonjwa kumeza vidonge, picha za X Ray zikipigwa huonesha mahali mawe yalipo, ukubwa na jinsi yalivyokaa.
Baada ya vipimo hivi, daktari anaweza pia kushauri mgonjwa apimwe damu ili kupata taarifa kamili juu ya afya yake.

MATIBABU!
Hakuna matibabu ya moja kwa moja ya tatizo hili. Baada ya uchunguzi wa tatizo, daktari na mgonjwa wataamua mbinu ya matibabu inayofaa lakini kama hali ya mgonjwa ni mbaya, hakuna mbinu nyingine inayoweza kufaa zaidi ya upasuaji ambapo kifuko cha nyongo hukatwa na kutolewa kabisa!

Kama mgonjwa ana hali ya kawaida, tiba mbadala kama kufunga (fasting), kunywa maji na juisi kwa wingi, kuepuka vyakula vyenye mafuta na sukari kwa wingi, husaidia sana kupunguza athari za ugonjwa huo.

Dawa za Acetaminophen pia hupunguza maumivu ingawa ni kwa muda.