Thursday, 7 December 2017

Ushuhuda wa kijana mkristo.

Mafundisho ya Neno la Mungu

MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI


Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote ASIUDHARAU ujana wako, bali uwe KIELELEZOkwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’(1Timotheo 4:12 & 14).

Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo.

Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14 kwenye toleo la kiingereza la ESV unasema ‘Keep a close watch on yourself and on the teaching. Persist in this, for by so doing you will save both yourself and your hearers’. Kwa mujibu wa dictionary ya kigiriki na kiebrania neno ‘save’ lina maana ya kuweka huru (deliver), kulinda (protect), kuponya (heal), kutunza (preserve), kuokoa (save). Jambo muhimu ambalo Mtume Paulo alikuwa akilisisitiza hapa ni hili; jambo muhimu si tu kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako, bali kila mwamini ana kazi kubwa ya kufanya ili KUULINDA NA KUUTUNZA WOKOVU WAKE.

Moja ya changamoto kubwa sana ambazo zinawakabili vijana wengi waliokoka leo ni kuipenda dunia. Kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana wengi na kwa sababu ya kuipenda dunia; (a) Mahusiano ya vijana wengi na Mungu wao yameharibika (b) Maisha ya vijana wengi yamekosa uelekeo (c) Kutokana na uovu wao jina la Bwana Yesu limekuwa likitukanwa.

Katika kile kitabu cha 1Yohana 2:16 ni dhahiri kwamba dunia imejaa TAMAA YA MWILI, TAMAA YA MACHO NA KISHA KIBURI CHA UZIMA. Tamaa ina nguvu ya kuvuta pamoja na kudanganya, naam inamuingiza mtu kwenye jaribu. Hii ina maana tamaa ni mlango, naam mlango huu unapaswa kufungwa mapema usikupoteze. Hebu tujifunze kutokana na anguko la mfalme Daudi na mke wa Bathssheba (Samweli 11:1-2).

Tunaona anguko la Daudi lilisaabishwa na kumpa Ibilisi nafasi kwa kutokwenda vitani. Mkristo akipoa katika kuvipiga vita vya kiroho inakuwa rahisi kwake kuanguka dhambini             (Yakobo 1:14-15), naam kumbuka kwamba siku zote tamaa inalenga kumfurahisha mtu binafsi (self-pleasing) bila kujali matokeo yake.

Hivyo katika nyakati tulizonazo sasa suala la kuipenda dunia ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu miongoni mwa vijana wetu. Ujumbe huu mfupi unalenga kueleza kwa namna gani kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana na nini vijana wafanye ili kuikabili na kuishinda changamoto husika.

Pia katika waraka 2Timotheo 2:15 Mtume Paulo anaendelea kumwambia kijana Timotheo Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungumtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli’.

Pengine kila mmoja wetu atafakari maisha yake kwa kuhusianisha na maelekezo ya Paulo kwa Timotheo. Naomba jiulize na kujijibu kwa uaminifu kwamba mosi, je, ujana wako wako unaheshimika au unadharauliwa? Pili, je, kwa waamini wenzako umekuwa kielelezo cha kweli kwa habari ya imani, upendo, usafi, usemi na mwenendo au la?

Binafsi  nimekuwa nikijiuliza ni kwa namna gani kijana atahakikisha kwamba (a) Ujana wake haudharauliwi (b) Anakuwa kielelezo kwa waamini wenzake (c) Anathibitisha kwamba kweli amekubaliwa na Mungu. Naam katika kusoma na kutafakari neno la Mungu nimejifunza kwamba zifuatazo ni njia ambazo zitatusaidia sisi vijana wa leo kuifikia kweli hii ya neno la Mungu.

Kijana adumu katika kuomba na kusoma (kutafakari + kulitenda) neno la Mungu

Katika Zaburi 119:9 & 11 Biblia inasema ‘Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii AKILIFUATA neno lako’. Pia kwenye ule mstari wa 11 inasema ‘moyoni mwangu nimeliweka neno lako, NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI’.

Naam katika Mathayo 26:41 imeandikwa ‘Kesheni, mwombe, MSIJE mkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu’. Yohana 17:17 inasema ‘uwatakase kwa ile kweli ;neno lako ndiyo kweli. Mambo haya mawili yanapaswa kwenda kwa pamoja nakijana akidumu katika kuomba na kusoma neno la Mungu ushindi ni lazima.

Kijana asimpe Ibilisi nafasi.

Kijana anapaswa kujiuepusha na mazingira yenye kumfanya aiepende na kuifuatisha namna ya dunia hii. Katika kitabu cha 1Wakorinto 6:12 imeandikwa ‘Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote VIFAAVYO; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya UWEZO wa kitu chochote’.  Ni vizuri ukahakikisha kwamba ufahamu wako hautawaliwi na mambo yasiyo ya msingi (non-essentials of life) – Je ufahamu wako umetawaliwa ni nini?

Hii ndiyo sababu iliyomfanya Paulo awaambie Waefeso ‘Wala msimpe Ibilisi nafasi’ (Waefeso 4:27) na pia awaambie Warumi “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili hata kuwasha tamaa zake’. Toleo la KJV linasema ‘But put ye on the Lord Jesus Christ, and MAKE NOT PROVISION for the flesh, to fulfill the lusts thereof’.  Na toleo la ESV linasema ‘But put on the Lord Jesus Christ, AND MAKE NO PROVISION FOR THE FLESH, TO GRATIFY ITS DESIRES’ (Warumi 13:14).  Je hivi leo ni kwa namna gani vijana wanaungalia mwili na kumpa Ibilisi nafasi? – Mitandao ya kijamii, kuangalia na kusoma vitu vichafu, hasira, mawazo, mazingira.

Kijana azikimbie tamaa za ujanani

Katika 2Timotheo 2:22 imeandikwa ‘LAKINI ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi’. Kijana anawezaje kuzikimbia tama za ujanani? Hebu tuangalie mfano wa Yusufu. Ushindi wa Yusufu dhidi ya mke wa Uria (Mwanzo 39:2-9). Hii ni habari ya kijana Yusufu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mali za Potifa.

Pamoja na ushawishi aliokutana nao Yusufu alijibu kwamba ‘Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?’ Mwanzo 39:12 inasema ‘huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake akakimbia akatoka nje. Ili kuzikimbia tamaa za ujanani kijana anapswa (a) ajiepushe na mazingira/marafiki wabaya (Mithali 1:10 & 1Wakorinto 15:33) (b) Ajitenge na uovu (Mithali 16:17, Zaburi 1:1).

Ni muhimu ukakumbuka kwamba hukupewa mwili kwa ajili ya zinaa maana miili yenu ni ni viungo vya Kristo na tena hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorinto 6:15 & 19), tena yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye (1 Wakorinto 6:17) maana tena imeandikwa ‘Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili’(1Wakorinto 6:13b). Tena imeandikwa‘Lakini uasherati USITAJWE kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu’   (Waefeso 5:3).

Kijana ajifunze kuenenda kwa roho na si kwa mwili

Katika wagalatia 5:16 imeandikwa ‘Basi nasema ENENDENI KWA ROHO, wala HAMTATIMIZA kamwe TAMAA ZA MWILI. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayoyataka’.

Je kuenenda kwa Roho ndio kukoje?

Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli yote (Yohana 16:13) na pia imeandikwa ‘kwa kuwa wote WANAOONGOZWA na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu’ (Warumi 8:14). Kuenenda kwa Roho ina maana ya kuishi kwa kufuata utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yako (Warumi 8:2).

Naam kadri unavyokuwa mtiifu kufuata utaratibu wake ndivyo unavyokuwa mbali na sheria ya dhambi na mauti ambayo ni mwili.Kumbuka imeandikwa ‘kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waiufuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia mwili ni mauti bali nia ya roho ni uzima na amani (Warumi 8:5-6) na pia Wafilipi 4:8.

Naam imeandikwa ‘Kila mmoja wenu ajue KUUWEZA MWILI wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu HAKUTUITIA UCHAFU, bali tuwe katika utakaso’ (1Thesalonike 4:4-5, 7). Ni jambo la ajabu sana kwamba kwamba tumepewa fursa ya kuiweza miili yetu. Ndio tunapaswa kuuweza mwili kwa maana ya kuudhibiti kwa kuuongoza na kuufanya ufuate nia ya roho.

Kijana mwenzangu kama umechagua kumpa Yesu maisha yako kwa njia ya wokovu,  nakusihi na kukushauri zingatia haya ili kuwa na maisha yenye kielelezo na ushuhuda mzuri maana imeandikwa  ‘Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa’ (2Petro 2:20-21).

Neema ya Kristo iwe nanyi, na tuzidi kuombeana.

Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.

 

Saturday, 25 November 2017

Dhambi isiyo sameheka!


DHAMBI ISIYO SAMEHEWA...! ! !

DHAMBI ISIYO SAMEHEWA...! ! !

Bwana Yesu amesema kwamba: "...Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwakumkufuru Roho Mtakatifuhawatasamehewa." - (Mathayo 12:31)

Je! Nini maana ya KUMKUFURU Roho Mtakatifu?

 Tukianza na neno KUFURU, maana yake ni: Kusema maneno yakumtukana Mungu au kufanya matendo yanayomtukana Mungu. Tukiendelea kusoma Mathayo 12:32 tunaona Bwana Yesu anasema kwamba:

"Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa,bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao." (Mathayo 12:32)

Ni kweli kuwa Yesu ni Mungu; lakini, Je! Yesu anamaanisha nini kuhusu dhambi isiyosamehewa ya KUMKUFURU Roho Mtakatifu?
Kumkufuru Roho Mtakatifu maana yake ni hii; Biblia Takatifu inasema kwamba:

"Kwa maana HAO WALIOKWISHA KUPEWA NURU, na KUKIONJA KIPAWA CHA MBINGUNI, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo,HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKITUBU; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, naKUFEDHEHESHA kwa DHAHIRI." (Waebrania 6:4-6)

Kumkufuru Roho Mtakatifu ni kuzitukana kazi za Mungu ambazo hakika kazi hizo ziliwahi kuyagusa maisha yako. Hapa namaanisha ya kwamba: mf. Yawezekana mtu alikuwa ni Mkristo na analijua neno la Kristo vizuri; mtu huyo baadae akaja akakengeuka na kuanza kuutukana Ukristo pamoja na matendo ya Mungu ambayo yanatendeka kwa uwezo wa Roho Mtakatifu; mtu huyo atakuwa ANAMKUFURU Roho Mtakatifu na KAMWE HATASAMEHEWA.

Tumeona hapo Biblia Takatifu imesema kuwa: "...wakaanguka baada ya hayo,HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKITUBU..." (Ebr 6:6) ni kwa sababu wamefanya "...KUFEDHEHESHA kwa DHAHIRI." Wamezitukana kazi za Mungu kwa makusudi; dhambi hiyo ndiyo Yesu anasema kamwe haitasamehewa. Biblia Takatifu inazidi kusema kwamba:

"Maana, kama TUKIFANYA DHAMBI KUSUDI baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAITABAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI; bali kunakuitazama hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma... Mwaonaje?Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidimtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya aganoALIYOTAKASWA KWAYO kuwa ni kitu ovyo, na KUMFANYIA JEHURI Roho wa neema?" (Waebrania 10:26-29)

Kuzitukana kazi za Mungu ni dhambi ambayo kamwe haiwezi kusamehewa. Tunapaswa tuwe makini sana juu ya hili. Leo hii tumepewa neema ya wokovu; na pia tumeziona kazi za Mungu maishani mwetu; isije ikatokea siku mmoja wetu akakengeuka na kuutukana Ukristo.Hilo ni jambo la kutisha na KAMWE HALITASAMEHEWA.

Wapendwa; Tusonge mbele katika wokovu. Tuishi maisha ya toba kila wakati; na pia, tuzidi kuihubiri kweli ya neno la Mungu bila ya kujitakia maslahi binafsi.

"Ee Bwana Yesu, nakuomba uwe nasi daima; kamwe asije akatokea mmoja miongoni mwetu akazikufuru kazi Zako. Naomba Roho Mtakatifu uwe nasi daima; utuongoze na kutulinda katika jina la Yesu Kristo. Amina."





 

Akili na Roho, soma ujue!

UHUSIANO KATI YA AKILI NA ROHO

AKILI NA ROHO (SEHEMU ~I)

Bwana Yesu asifiwe wapendwa!!!

Tunakukaribisha katika kufuatilia mfululizo huu wa somo la akili na Roho, ambalo tumesimamia neno kutoka 1Kor 14:15

"Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia."

���� Wakristo wengi tunachanganya nafasi ya roho na akili katika kufanya maamuzi au kung'amua mambo.

���� Na wengine wamefika hatua wanafikiri kufanya maamuzi kwa kutumia akili zao watakuwa wamemkufuru Roho mtakatifu.

���� Wapo wanaousimamia mpaka mistari ya Biblia kuzifisha akili zao, mstari wanaopenda kuutumia ni huu unaosema

Mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote wala usitegemee akili zako mwenyewe. Mithali 3:5.

Hii ni tafsiri mbaya ya neno la Mungu inayowafanya wengi wawe maskini mwilini na rohoni.

Katika mstari huu neno la Mungu halituambii tusitumie akili zetu, bali linatuasa tusitegemee akili zetu WENYEWE, Hii ina maana tusiegemee katika kutumia akili TU,

Bali baada ya kumtumaini Bwana KATIKA AKILI zetu tunahitaji pia kumtumaini kwa Moyo.

Tafsiri ya Neno KWA MOYO ni kutoka ndani hii inamaana kutumaini Bwana kwa kumaanisha. Biblia inatuambia moyo ndiko chemichemi za uzima zinakotoka hivyo ukimtumaini Mungu kwa moyo hakuna kitakacho kutoa katika tumaini hilo hata mwisho.

Mtu asiemtumaini Mungu kwa moyo wake wote ni mbabaishaji au muigizaji neno  watu hawa wananiheshimu kwa midomo lakini Mioyo yao iko mbali nami.

Mungu anataka mioyo yetu tuisogeze kwakwe kila tunachokifanya tukifanye kwa moyo.

Hivyo umtumaini Bwana kwa si kwa akili yako au uelewa wako mwenyewe bali umtumaini kutoka ndani ya Moyo.

Neno linatuambia;  
Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, KWA AKILI ZAKO ZOTE ‘na’ kwa nguvu zako zote.’ Marko 12:30

Kila jambo lililotajwa hapo juu lina umuhimu wake, na uzito wake ndio maana ametumia kiunganishi ‘na’  hajatumia ‘au’ ambayo inakupa option yaani kuchagua.

Hivyo ni lazima utumie nguvu, roho, akili na Moyo.

Kumpenda Mungu kwa nguvu inamaanisha kujitoa kwa ajili ya Bwana kwa muda na mali yako.

↩  KWENYE KIINI CHETU CHA SOMO

AKILI ni nini?

Ni uwezo wa kung'amua jambo/ kitu fulani, ni uwezo wa kuwa na ujuzi na kitu/jambo flani,
  
Kuna aina kadhaa za akili,

�� Akili za kuzaliwa,

Hizi ni akili ambazo kila mtu anazo, kila mtu anazaliwa na akili ambazo zinamsaidia yeye kujua mambo mbalimbali pasipo kugundishwa na mtu. Kila mtu amejaliwa akili hizi tofauti ipo katika kuzitumia tu.

Uvivu wa kufikiri na kukubali kuongozwa na akili ya mtu mwingine au kuiga iga ndo kinafanya watu wengine waonekane wamependelewa. Mfano Wazungu

�� Akili za darasani,

Hizi zinapatikana kwa kuongezewa maarifa na mtu mwingine, akili hizi mara nyingi tunazipata ili zitusaidie kuweza kupata mambo fulani/kufika viwango fulani, inabidi uingie darasani na awepo mtu wa kukufundisha/kakuongezea ujuzi/akili.

Wengi hawafanikiwa pamoja na kuwa elimu za darasani, moja ya sababu kubwa ni Upumbavu.

Upumbavu maana yake kuwa na  maarifa na kushindwa kuyatumia kwa upuuzi. Hii ni tofauti na ujinga ambapo ujinga ni kukosa maarifa.

�� Akili za maisha,

Huu ni ujuzi ambao unaupata kutokana na mazingira yanayokuzunguka, maisha tunayoyaishi  yamekuwa yakifufundisha vitu vingi sana, na ndio maana kuna watu hawajawai kwenda shule au wameishia viwango vya chini vya elimu  lakini wamefanikiwa, ni kwa sababu ya akili ya maisha ambayo wameipata katika mazingira yanayowazunguka, wana uzoefu na mambo mengi tofauti na mtu ambaye emeenda shule.

Ni muhimu sana kuwa na akili ya maisha kuliko ya darasani, Kwa sababu kama una akili tu ya darasani hauna akili ya maisha, hiyo ya darasani ina asilimia ndogo sana kuweza kukusaidia!

NB: Huwezi kufanikiwa ukiwa na akili za darasani pekee unahitaji akili za maisha, lakini inawezekana kufanikiwa ukiwa na akili za maisha bila kuwa na za darasani. AMKA!

Aina nyingine ni akili ya kiungu,

Hii ndo akili bora kuliko zote, akili hii hauzaliwi nayo, hauipati darasani wala mtaani (maisha ya kawaida) utapata kutoka kwa Mungu tu.!

Akili hii ni bora Kwa sababu ukiipata inauwezo wakubadilisha maisha yako muda wowote!

Habari hizi za akili ya kiungu utazipata zaidi ukisoma habari za Yusufu (Mwanzo 41:37-41) na Danieli 5:10-14).

�� Akili za kiungu

Zinapatikana kwa wewe ambaye ni mwana wa Mungu na ukimuomba kwa bidii akupatie anakupatia!

�� Ukimuomba Mungu Roho ya hekima, maarifa na ufahamu utaipata akili hii.

Roho ni nini?

Ni nafsi hai inayoifanya nafsi kuwa hai, kuna tofauti kati ya nafsi na nafsi hai, Nafsi haiitwi nafsi hai isipoungana na roho. Ukisoma mwanzo 2;7 neno linasema Akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

➡ Nafsi inaonekana lakini haiishi pasipo roho. Roho ni nafsi isiyoonekana lakini ni hai.

Kwa hiyo ukiitenga nafsi na roho nafsi hio haitobaki hai tutaizika, itarudi mavumbini.

���� Hapo tumezungumzia roho ya mwanadamu kuna aina mbalimbali za Roho ambazo pia ni muhimu kuzielewa na kuzitofautisha; Roho wa Mungu, Roho ya/za Mungu, na roho za shetani.

�� 1. ROHO MTAKATIFU (Roho WA  Mungu)

Huyu tunampokea kwa namna mbili, kila ujio una kazi tofauti;

1⃣ Uvuvio Wa Roho

Huyu tumempokea kutoka kwa Mungu mwenyewe kwa njia ya kuvuviwa, Yohana 20:21 naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho mtakatifu.

Tukimpokea hutuongoza dhamiri zetu katika kweli;

Warumi 9:1 nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu.

Pia Yohana 16:8 anasema Naye akiisha kuja, huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki na hukumu, Hutufundisha, kutukumbusha; Yohana 14:26

kutuongoza; Yohana 16:12

kwa kifupi kwa njia ya uvuvio Roho huja kama msaidizi.
���� Wote tumepata Neema ya kuvuviwa ingawe wengi hawajui, na kutokujua na kuamini Roho yuko ndani yake hupotea.
Wasiomtambua huyu dhamiri zao huwa dhaifu hivyo rahisi kunajisika.

2⃣ Kujazwa Roho

Ujio huu wa Roho Mtakatifu ni wa nguvu, Ambapo anapokujilia unasikia hali ya tofauti na unapokea nguvu. ukisoma Matendo 1:8 anasema.

"Lakini mtapokea nguvu Roho akishawajilia juu yenu".

Katika ujio huu Roho mtakatifu hushuka na nguvu zake naye huleta roho za Mungu na nguvu ama upako.

Mtu hujazwa Roho kwa kuwekewa mikono ama kuongozwa maombi ama kujitenga na kuomba kwa Mungu.

Huja na ishara mbalimbali mfano kunena kwa lugha mpya. Matendo 2:4

Kwa kifupi kwa njia ya kujazwa Roho huja kwa nguvu akiambatana na matendo ya Muujiza na roho za Mungu zinazotusaidia kuifanya kazi ya Bwana.

Kwa Neema Ya Mungu, Mungu Humvuvia Roho Wake Kila Amwaminiye Amfundishe, Amuongoze, Kumkumbusha,

Lakini Hii Haitoshi Neno La Mungu Linasema; *MTAKENI MUNGU NA NGUVU ZAKE Zaburi 105:4

⚡ Hivyo Unahitaji Ujazo Wa Roho Mtakatifu Katika Huduma Yako Ili Umtumikie Mungu Kwa Ujasiri Matendo 4:31

⚡ Unahitaji Ujazo Wa Roho Mtakatifu Ili Upokee Nguvu Itakayokuwezesha Kutumia Mamlaka; Kumkemea Mapepo, Kuombea Wangonjwa Na Matendo Yote Ya Miujiza N.K.

✅ ya kwanza ya somo hili la AKILI NA ROHO inaishia hapa, leo tumeweka msingi,

Mungu akipenda kwa sehemu inayofuata tutaingia ndani zaidi. Roho mtakatifu atakufundisha utaelewa zaidi endelea kufauatilia kuna namna Roho mtakatifu anataka kukuvusha.

���� Mungu akubariki sana!

MUNGU KATUPENDELEA SANA

mpaka shetani amenuna

��������������

Madhara ya kutosamehe!

Je, wajua kusamehe ni kutii amri ya Mungu?

SOMO: - MSAMAHA

Tukisoma kitabu cha WAEFESO 4:31,32 tunaona Biblia Takatifu inasema kwamba:

"Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, MKASAMEHEANE kamana Mungu katika Kristo ALIVYOWASAMEHE ninyi." (Efe 4:31,32)

Je! Nini maana ya neno MSAMAHA na kuna faida zipi katika KUSAMEHE; na kwa nini tunapaswa KUSAMEHE?

MSAMAHA:

Neno “MSAMAHA” ni neno jepesi kulitamka lakini ni pana sana katika maana. Nisemapo "NI NENO JEPESI KULITAMKA" ninamaanisha kulitamka tu kwa kawaida na katika hali ya kawaida tu pasipo kukosewa, lakini kwa watu wengi; neno MSAMAHA ni neno gumu sana kulitamka toka rohoni mwao hususani pindi wanapokosewa. Nilifanya utafiti juu ya hili neno nikagundua zipo siri kubwa sana katika KUSAMEHE ambazo Shetani apendi watu wazifahamu.
Tukirudi kwenye neno “SAMEHE” maana yake ni: Kukoma / kuacha kuhisi hasira juu ya mtu ambaye amekuumiza, kakukwaza au kakuudhi; Pia, kukoma / kuacha kuhisi hasira juu yako wewe mwenyewe (kuto kujichukia).
Neno MSAMAHA, kwa maana nyepesi linamaanisha kama ifuatavyo;

Þ       Kutolipiza kisasi japokuwa unayo haki ya kulipiza kisasi.

Þ       Ni tendo la imani na tena la hiari kwa kuwa unayo sababu, uwezo, na haki ya kulipiza kisasi kutokana na yale uliyo umizwa.

Je! Unafahamu ni kwa nini watu wengi ni wagumu KUSAMEHE?

Watu wengi hushindwa kusamehe kwa sababu hawana Roho Mtakatifu ndaniyao; kwamba, wameruhusu maisha yaokutawaliwa na Shetani. 
Dhana hiyo inao ukweli mkubwa ndani yake na pia wapo watu wajiitao watumishi wa Mungu lakini nao wanashindwa KUSAMEHE. Si kwamba tu tunasamehe ili na sisi tupate kusamehewa; La, si hivyo tu, bali zipo faida nyingi sana zipatikanazo kwenye KUSAMEHE.

Siku zote mtu anapokosewa, ndani yake anazaa UCHUNGU, asipokuwa makini nao UCHUNGU unazaa CHUKI, na pia hasipojiadhari hiyo CHUKI inazaa HASIRA. Na hapo ndipo Shetani anapata mlango wa kumwingia mtu. Vitu hivyo vitatu; yaani, UCHUNGU, CHUKI na HASIRA mara zote huandamana. Usipoweza kuudhibiti UCHUNGU, unakuwa unaweka wazi mlango wa Shetani kukutawala.
Mtu kuokoka haimaanishi ndiyo mwisho wa makwazo na majaribu mbalimbali, bali tambua unapo mpokea Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako unakuwa umetangaza vita dhidi ya Shetani na majeshi yake ya pepo waovu. Shetani atajaribu kukuingia moja kwa moja, lakini akishindwa, anatafuta mbinu ya kumuingia mtu mwingine ili akukwaze; nawe ukikwazika ndipo Shetani anapata nafasi ya kukuingia na kukutawala kupitia UCHUNGU, CHUKI, na HASIRA.

Tumeona mifano mingi ya watumishi wa Mungu walio anguka kiimani kwa kushindwa KUSAMEHE; Huduma nyingi za kuhubiri Neno la Mungu zimekufa kwasababu ya KUTOSAMEHE; Makanisa mengi yamevunjika na kutengana kwa sababu tu ya KUTOSAMEHE; Ndoa nyingi na uchumba mwingi umevunjika kwasababu ya KUTOSAMEHE; Makampuni mengi yamevunjika kwa sababu ya KUTOKUSAMEHE, utaona mkurugenzi amekwazana na meneja alafu kampuni inapoteza muelekeo, utendaji unakuwa mbovu na hatimae kampuni inakufa. Yote hayo unaweza kukuta chanzo chake ni KUTOSAMEHE.
Siku zote unapokwazika Shetani anakuwa anakuletea hati ya mashtaka kwenye mawazo yako; utasikia siuti ikikwambia;

"YAANI FULANI AKUFANYIE HIVI KABISA ALAFU UMSAMEHE? HAPANA !!! LAZIMA UMKOMESHE. HAIWEZEKANI UMSAMEHE HIVI HIVI TU WAKATI AMEKUPA HASARA YOTE HII.”

 Ndipo nawe waweza ukajikuta yanakuingia akilini na ukaanza kusema: “Kweli; HAIWEZEKANI KABISA, TENA YAANI, ATANITAMBUA MIMI NI NANI."

Utaona Shetani anakukumbushia tukio jinsi ulivyo tendewa. Utasikia ushauri mwingi sana ndani ya fahamu zako. Tena maneno hayo yanaweza kukupa UCHUNGU sana kiasi cha kushindwa kula, na hata ukatokwa na machozi. Na akili ya mwanadamu ni rahisi kunasa mabaya kuliko mema; ni rahisi kukumbuka mabaya kuliko mema; hapo ndipo Shetani huchukulia point endapo usipokuwa makini. Ukimruhusu Shetani katika akili zako; ndipo utajikuta ukimtazama aliyekukwaza ni mtu wa karibu sana nawe, ambae ulitegemea angekuwa msaada kwako lakini amekurudisha nyuma na kuuumiza sanamoyo wako. Hauna raha, amani wala matumaini yoyote yale. 

Yawezekana akawa ni rafiki yako wa karibu sanaamesababisha ufukuze kazi kwa kosa ambalo hukulifanya. Kweli inauma sana; inaleta huzuni na uchungu ukiwaza utafanya nini na wale wanaokutegemea. Inaumiza sana.
Kwa wakati huo, ukijitizama uwezo wa kumdhuru unao, sababu ya kumdhuru unayo, na nia ya kumdhuru unayo. Na kila mtu unaemsimulia anakwambia:

"Mbona wewe mjinga hivyo? Ingekuwa ni mimi, kamwe siwezi kumlazia damu huyo, lazima angenitambua."

Kwa wakati huo moyo wako umejaa UCHUNGU, CHUKI na HASIRA. Lakini kwa mbali saaaana, unasikia sauti ndani ya moyo wako ikisema: MSAMEHE.
Nadhani ata wewe waweza kutambua ni jinsi gani ilivyo vigumu kuitii hiyo sauti isemayo SAMEHE kwa kuwa ukitazama ni kweli umeonewa, uwezo wa kulipa kisasi unao, na hata ukilipa kisasi au kudhuru wapo watu watakaosema "Kwa kweli umefanya vizuri kumkomesha. Ilimpasa hivyo."

Na kama ukitenda jambo baya juu yake; fahamu kwamba hiyo imetokana na wewe kuruhusu UCHUNGU ukutawale. Wengine hufikia hata hatua ya kujinyonga. Mawazo yatakujia; “Yaani fulani kabisa azini na mke wangu ! Tena fulani ni rafiki yangu kabisa ! Hapana. Lazima nimkomeshe.”

Hayo yote chanzo chake ni UCHUNU uliouruhusu uingie ndani ya nafsi (akili) yako. Tumeona Biblia Takatifu inatuambia kwamba: "Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu..." (Efe 4:31) Sasa; je! Nini maana ya neno UCHUNGU? Nivigumu kupambana na adui kama hatumfahamu adui yetu UCHUNGU ni nani.

UCHUNGU:

Kwa maana nyepesi neno UCHUNGU maana yake ni hii:

Þ       Ni hali ya kutokuwa na furaha, kujawa hasira zilizotokana na kutendewa mabaya.

Þ       Ni hali ya kuhisi huzuni nzito ambayo wakati mwingine inaweza kuchangamana na maumivu makali katika fahamu za mtu, ambayo yaweza kusababisha mwili kunyong'onyea na kusababisha akili kupoteza uwezo wa kufikiri vizuri.

Mara nyingi UCHUNGU husababisha akili kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Hiyo ndiyo maana halisi ya neno uchungu. Zifuatazo ni athali za kutosamehe;

MADHARA YA KUTOSAMEHE:

i/: KUHARIBU AFYA YAKO.

Kama nilivyojifunza hapo awali; UCHUNGU husababisha huzuni nzito. Hii huzuni inapomwingia mtu, huleta maumivu makali katika fahamu za mtu; Uwezo wa mtu wa kufikiri vizuri hupotea, na wakati mwingine huyu mtu anakuwa kama vile amedumaa akili. Unaweza hata ukamwuliza: “Jina lako ni nani?” Lakini mtu huyo badala ya kukujibu akabaki anakushangaa tu.

Uchungu unapomwingia sana mtu unaweza kumfanya apoteze hamu ya kula. Atahisi kila aina ya chakula kwake ni kibaya, atahisi vyakula vyote kwake havina radha. Na hata akijilazimisha kula ataona kama chakula ni kigumu kumezea. Matokeo yake, afya inaanza kuzorota na mwili unaanza kunyong'onyea. Ndipo chanzo cha madonda ya tumbo. Uchungu utokanao kwa hasira husababisha mwili uweze kuzalisha sumu ambayo inaleta madhara katika afya yako.

Pia, UCHUNGU husababisha mtu kuwa na mawazo yenye maswali yasiyo na majibu kwa wepesi; na tena tumaini huonekana kama vile limepotea kabisa. Uchungu huo ukidumu kwa muda mrefu husababisha mwili kutengeneza sumu itakayoharibu ule ute mwepesi unaopatikana katikati ya mifupa (Synovial fluid) pamoja na kuharibu afya yako kwa ujumla (Bila shaka hapa madaktari wananielewa vizuri.) 

UCHUNGU huo ukizidi kupita kiasi, mwili wa mtu huyo huonekana umekakamaa kakamaa sana. Na kwa kiasi kikubwa afya ya mtu huyu huanza kuharibika hatua baada ya hatua. Mwili wake hunyong'onyea na akili zake hushindwa kufanya kazi vizuri, hupoteza kumbukumbu na utambuzi wa mambo mbali mbali na kumfanya mtu afanye maamuzi ya pupa yanayompeleka kwenye hasara kubwa zaidi badala ya kuleta suluhu la matatizo yake.

Hivyo basi; Athali ya pili ya KUTOSAMEHE ni kama ifuatavyo:

ii/: KUTENGWA NA WATU.

KUTOKUSAMEHE kunasababisha GHADHABU na HASIRA. Na hivi vyote hutokea pale unaposhindwa KUUDHIBITI UCHUNGU USIKUTAWALE. Mlango mkubwa wa DHAMBI huanzia pale mtu anaposhindwa kudhibiti UCHUNGU. Kwa hiyo; UCHUNGU unapomtawala mtu, uchungu huo unazaa kitu kinachoitwa CHUKI. Ndani ya hii chuki ndimo kunakaa GHADHABU. 

GHADHABU ni hali ya mtu kuwa na maamuzi ya pupa pasipo kujali madhara yake. Hali hiyo yaweza kumfanya mtu kuwa na majibu ya mkato mkato, kutopenda kuulizwa ulizwa; humfanya mtu kuwa na hali ya UGOMVI mara kwa mara, kutopenda kuwa na subira (anataka afanyiwe vitu kwa haraka haraka la sivyo ananuna na kutoa maneno machafu, na wakati mwingine anakuwa na tabia ya kuzira). Katika hatua hii ndipo kunazaliwa kitu kiitwacho HASIRA. 

HASIRA umfanya mtu kuchukua maamuzi pasipo kujali. Mtu huyo kwa wakati huo anakuwa hatarini sana kuingiliwa na Shetani. Endapo asipodhibiti hiyo hasira yawezekana Shetani akamwendeshakama jinsi Shetani apendavyo. Hapo ndipo utaona MAGOMVI, MATUSI na KILA AINA YA UBAYA vinadhihirika kwa mtu huyo. Tena anafanya pasipo hata kujali. Mtu hukirihusu hasira ikutawale utakuwa umempa Shetani kibali cha kukutawala. Biblia Takatifu inasema kwamba:

"Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego." (MITHALI 22:24-25).

Mtego huo hutoka kwa Shetani ili akuingize dhambini. Hivyo basi; matokeo ya hasira ni KUTENGWA NA WATU. Kwa kuwa mtu huyo hufanya maamuzi bila kutumia akili, hekima wala busara.

Neno la Mungu linapotuambia: "UCHUNGU WOTE NA GHADHABU NA HASIRA NA KELELE NA MATUKANO YAONDOKE KWENU, PAMOJA NA KILA NAMNA YA UBAYA.." Mungu anatutaka vitu hivyo viondoke kwetu kwa ajili ya faida yetu wenyewe. Lakini ukishindwa kuvidhibiti, matokeo yake utafikia hatua itakayokupa hasara kimwili na kiroho pia. Na ufahamu kwamba; MTU KUSHINDWA KUDHIBITI UCHUNGU USIMTAWALE kunaweza kuwa CHANZO CHA MABAYA NA DHAMBI KUTOKEA. 

Ndiyo maana utaweza kuona mtu amegombana na mke wake nyumbani alafu anaondoka na hasira zake kisha unasikia amegongwa na gari barabarani. Sasa jiulize, kusamehe ni kwa ajili ya faida kwa Mungu au kwako wewe mwenyewe? Au yawezekana umedhurumiwa pesa zako na wafanya biashara wenzako kisha ukaingia ofisini mwako umejaa hasira, wateja wanapokuja wewe unawajibu vibaya; Je, biashara yako ikifa utamlaumu Mungu, Shetani au lawama ni juu yako wewe uliyeshindwa KUZUIA HUO UCHUNGU? Dawa ya kuushinda uchungu ni KUSAMEHE; hakuna tiba nyingine zaidi ya KUSAME. Ni kitu cha kushangaza hata watu wadunia wanataka kuwazidi akili baadhi ya watu wa Mungu. Katika accountance kuna kitu kinaitwa Bad Debt Account. 

Yaani ni deni lililoshindikana kulipwa aidha kwa kudhurumiwa au mdeni amekufa au kufirisika. Wahasibu hufungua account hiyo ambayo ni ishara ya kusamehe deni lililoshindikana kulipwa, kisha wanafanya mikakati mipya ya kusawazisha pengo hilo. Sasa je! Kuna tatizo gani linalowafanya watu wa Mungu washindwe KUSAMEHE?
Nikifungua Biblia kwenye kitabu cha WAEFESO 4:26 Biblia inasema:

"Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na UCHUNGU wenu bado haujawatoka." (Efe 4:26)

Unaona sasa; tatizo kubwa la watu ni kuruhusu UCHUNGU KUWATAWALA. Tunapoambiwa "MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.." Kumbe inawezekana kabisa mtu kupatwa na hasira kwa sababu makwazo na majaribu ni mengi tuyapatayo kila siku, lakini tumeambiwa “MWE NA HASIRA LAKINI MSITENDE DHAMBI”;  na tena tunaambiwa “...JUA LISIZAME TUKIWA BADO NA UCHUNGU NDANI YETU.” Tunalazimika KUSAMEHE kwa ajili  ya faida yetu sisi wenyewe. Ndiyo maana tukisoma WAEFESO 4:26 imeandikwa: "wala msimpe Ibilisi nafasi."

 Hivyo basi, kumbe KUTAWALIWA NA UCHUNGU NI NJIA YA KUMPA SHETANI NAFASI. Tunaposoma WAEFESO 5:17 tunaona imeandikwa:

"Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana". (Efe 5:17)

Bila shaka hadi hapo nimeeleweka vizuri. Sasa basi;  Athali ya tatu ya KUTOKUSAMEHE ni kama ifuatavyo:

iii/: MUNGU HATAKUSAMEHE DHAMBI ZAKO.

KUTOSAMEHE ni moja ya sababu ya KUTOSAMEHEWA. Neno DHAMBI, lina maana ya kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Dhambi ni kuvunja amri/sheria za Mungu. Mtu atendapo DHAMBI anakuwa haumkosei mwanadamu bali umemkosea Mungu. Hivyo basi, ni Mungu pekee ndiye awezaye KUKUSAMEHE. Kwa hiyo, Mungu hawezi kukusamehe wakati wewe hautaki KUSAMEHE wenzako. Neno la Mungu linatuambia kwamba:

"Nanyi, kila msimamapo na kusali, SAMEHENI, mkiwa na neno juu ya mtu; ILI NA BABA YENU ALIYE MBINGUNI AWASAMEHE NA NINYI MAKOSA YENU." (Marko 11:25)

Tukizidi pia kusoma ule mstari wa 26, tunaona Mungu anasisitiza kwa kusema:

"Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu." (Marko 11:26)

Mungu ametuweka wazi kabisa; ENDAPO KAMA SISI HATUSAMEHE, VIVYO HIVYO NA SISI HATUTASAMEHEWA. Sasa je! Ni nani asiyetenda makosa au kumkwaza mwenzake kwa namna yoyote ile? Bila shaka hapa jawabu ni HAKUNA. Kila mmoja wetu umkwaza mwenzake kwa namna fulani fulani. Kwa hiyo hatupaswi kuruhusu UCHUNGU ututawale hata kidogo ili Shetani asipate nafasi ndani yetu. Kwa kuwa sote huwa tunakoseana, ni lazima tusameheane ndipo na sisi tupate kusamehewa na Mungu.

Madhara mengine ya kutosamehe ni haya yafuatayo:

iv/: MUNGU HAPOKEI SADAKA ZAKO, NA WALA HAJIBU MAOMBI YAKO.

Nikifungua Biblia Takatifu kwenye kitabu cha MATHAYO 5:23,24 tunaona pameandikwa kwamba:

"Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako."

Mungu huchukizwa na sadaka za mwenye dhambi. Sadaka za mtu mwenye dhambi hazipokelewi mbele za Mungu. Ndiyo maana imeandikwa kuwa utii ni bora kuliko dhabihu. Mungu si masikini hata ababaishwe kwa sadaka zako. Tukisoma kitabu cha HOSEA 6:6 Mungu anasema:

"Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka...",

Mungu hababaishwi na hako kasadaka kako. Mungu si masikini hadi ababaishwe na uto tusadaka twako. Mungu anapenda sadaka za mtu mwenye moyo safi; Ndiyo maana Biblia inasema kwenye MITHALI 21:3

"Kutenda haki na hukumu humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka." (Mithali 21:3)

Mungu hupendezwa na moyo safi; ndiyo maana amesema "...IACHE SADAKA YAKO MBELE YA MADHABAHU, UENDE ZAKO, UPATANE KWANZA NA NDUGU YAKO, KISHA URUDI UITOE SADAKA YAKO." Kwahiyo, usipopatana (sameheana) na yule mliyekoseana, hakika Mungu hatapokea sadaka zako. Hivyo basi, KUTOSAMEHE umfanya mtu kukosa kibali mbele za Mungu. Naunapokosa kibali kwa Mungu maana yake unakuwa haujampendeza Mungu, vivyo hivyo kwa maana nyepesi unakuwa umetenda dhambi, kwa maana dhambi ni kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

Hivyo basi, ninapenda kuhitimisha somo hili kama ifuatavyo; Biblia inasema kwenye kitabu cha WAEFESO 6:10,12

"Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani."

Ninajua wapo watu ambao watauliza; Je, silaha za Mungu ni zipi?

Silaha kubwa kabisa kuliko zote ni NENO LA MUNGU lililomo ndani ya Biblia Takatifu; neno hilo la Mungu linapaswa kukaa kwa wingi ndani yako. Neno la Mungu likikaa kwa wingi ndani yako, ukilifanyia kazi na kulishika, ndipo Roho Mtakatifu atakaa ndani yako na kukuongoza namna ya kufanya. Pasipo Neno la Mungu, hatuwezi kuyajua mapenzi ya Mungu. Kwahiyo, silaha kuu ni NENO LA MUNGU. Ndiyo maana tukisoma WAEFESO 6:14-17 imeandikwa:

"Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu..."

Sasa soma hapa kwa makini zaidi, "...Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu."

Siku zote Shetani anataka kuona watu wanapotea na kukosa baraka za Mungu. Shetani analeta majaribu na makwazo mbalimbali ili watu waanguke na kuiacha njia ya uzima; Shetani anataka watu wawe na uchungu ili wakose baraka za Mungu. 

Hauwezi kusema umemsamehe mtu wakati bado unao uchungu moyoni mwako. Biblia inasema hakuna dhambi ndogo wala dhambi kubwa, ni kwa sababu muongo na muuaji wote hukumu yao ni kutupwa kwenye ziwa la moto na kupata humo mateso ya milele yote. Vivyo hivyo yeye asiyesamehe wenzake hukumu yake ni ile ile kwenye ziwa la moto sawa sawa na muuaji.
Nikisoma WAEFESO 6:12 imeandikwa

"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wagiza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."

Ndugu zangu tuweni macho na makinisana, Shetani hapendi kuona watu wanabarikiwa, hapendi kuona kazi ya Mungu inasonga mbele, na hapendi kuona watu wanarithi uzima wa milele.

SAMEHEANENI NA WALA UCHUNGU USIKAE MIOYONI MWENU. Mwenyezi Mungu awabariki nyote mnaotendea kazi haya mliyojifunza humu. Roho Mtakatifu awaongoze kwenye kweli yote, mbarikiwe katika jina la Yesu Kristo. Amina.

 

 

Thursday, 16 November 2017

BEST SET OF ADVICE.

This is one of the best set of advise l have ever read.

1. Take risks in your life. If you win, you can lead; if you lose, you can guide.

2. People are not what they say but what they do; so judge them not from their words but from their actions.

3. When someone hurts you, don't feel bad because it's a law of nature that the tree that bears the sweetest fruits gets maximum number of stones.

4. Take whatever you can from your life because when life starts taking from you, it takes even your last breath.

5. In this world, people will always throw stones on the path of your success. It depends on what you make from them - a wall or a bridge.

6. Challenges make life interesting; overcoming them make life meaningful.

7. There is no joy in victory without running the risk of defeat.

8. A path without obstacles leads nowhere.

9. Past is a nice place to visit but certainly not a good place to stay.

10. You can't have a better tomorrow if you are thinking about yesterday all the time.

11. If what you did yesterday still looks big to you, then you haven't done much today.

12. If you don't build your dreams, someone else will hire you to build theirs.

13. If you don't climb the mountain; you can't view the plain.

14. Don't leave it idle - use your brain.

15. You are not paid for having brain, you are only rewarded for using it intelligently.

16. It is not what you don't have that limits you; it is what you have but don't know how to use.

17. What you fail to learn might teach you a lesson.

18. The difference between a corrupt person and an honest person is: The corrupt person has a price while the honest person has a value.

19. If you succeed in cheating someone, don't think that the person is a fool...... Realize that the person trusted you much more than you deserved.

20. Honesty is an expensive gift; don't expect it from cheap people.

This is very interesting post and I want all my friends and family to benefit.

Thursday, 2 November 2017

How to hack WhatsApp

3 Ways To Hack Whatsapp Account Today

 

At the moment, there are 1.3 billion Whatsapp users. This is a significant increase if you know that in 2016, the number was 1 billion.

Obviously, due to simplicity and functionality, we can only assume that the number of users will go in one direction only, up!

But, this also means that a higher number of people will want to hack Whatsapp account.

Yes, this is possible and there are three methods you can use.

Method 1: Using Copy9 to hack someone’s Whatsapp

Copy9 is the first method on our list. Basically, it is a full-size app which allows you to get a complete access to a targeted device.

In recent months, we have been able to see a huge increase in the number of users. They are parents, spouses and business owners, among others.

The main idea behind the app in question was to provide safety and security, rather than to use it for plain smartphone hacking, which is something we prefer.

Yes, you can still hack Whatsapp messages and read them whenever you want.

Perhaps all of this spends complicated, but the real procedure is more than just simple. In essence, you will have to:

Download the Copy9Install it on targeted deviceLogin to your control panel on a PCDone

As you can see, the entire process takes no more than 5 minutes of your time.

It is specifically developed to be simple enough for average users and those who don’t even fully understand smartphones and how they work.

The bottom line is yes, you will be able to use it without a problem.

Here it should be mentioned that there is no risk of being detected!

The app works by connecting to the operating system and literally becoming part of it.

As such, the app has all the access to the OS on your phone, obviously.

The app cannot be detected by antivirus, malware software or on any other way.

Hard reset of a device won’t delete the app as well. At the end, we can add Copy9 is the safest app to use.

Besides the hack Whatsapp online feature, Copy9 offers plenty of additional features!

Besides the fact you will be able to read Whatsapp messages, the app allows you to read messages and monitor calls performed via other apps. All messenger apps are supported.Tracking the GPS location is possible as well. The app will determine the exact location of a smartphone within a matter of seconds.It is accurate within 10 feet! Even if the GPS option isn’t activated on a smartphone, the Copy9 will activate it and use it. The feature is essential for severe and dangerous issues.Monitoring internet activities is just another feature. Although Whatsapp tracker option is associated with the internet, the feature here is a bit different.Basically, it allows for the user to block access to the web, limit it or check out what has been visited via the targeted device.The full list of features is significantly long. In general, you will be able to hack Whatsapp chat historymonitor call, all messages, internet activity, GPS, detecting when a SIM card is changed and many other features.

Customer support is guaranteed and also more than just decent, which isn’t a case with apps of this kind!

The best part, you get a free trial, without a need to enter your credit card. If you don’t like it, after 48 hours simply delete the app and you are done.

However, most users who tried the free trial, have been using Copy9 ever since.

Are you interested in our App?

You get a free trial, without a need to enter your credit card

Get 2-Day Free Trial

Method 2: Hack Whatsapp messages without access to phone

How actually safe Whatsapp and similar apps are?

You may believe that they are bulletproof, but they aren’t! As a matter of fact, both, Whatsapp and Telegram were able to be hacked by a single photo, yes, just one ordinary photo.

Both of these companies issue a new patch recently which should prevent this issue.

According to the latest details, hackers were able to hack these accounts by sending a photo to a user.

Of course, a photo had to be opened, after which hack would be performed.

The severity of this issue means that your account can be hacked within a matter of seconds.

If you are looking for a way how to hack someone’s Whatsapp without their phone this is the method for you.

So, how this method actually works?

Video Demonstration:

The researchers also provided a video demonstration, given below which shows the attack in action.

In order to complete it, you will have to insert a malicious code into a photo.

Once a user opens that photo, the code will infect the device, allowing you a complete access.

Within a matter of seconds, you can have a complete control over Whatsapp or Telegram, depending on which app you targeted.

The explanation lies in the process how both of these apps treat media files.

The same applies to videos and documents, by the way. In essence, Whatsapp doesn’t check the files for malware.

It directly allows to the users to open, view and store a photo or a video.

In other words, the app will literally allow access of malware into a device. After which the account is hacked.

A bit more detailed explanation is required here. Telegram, Whatsapp, and a few other apps use the same type of encryption.

It means that an app won’t be aware of the message or a file which is sent to a device until it validates it.

However, the opening is the first step here and only then a message is validated. In plain words, Whatsapp doesn’t realize what has been actually received until it is too late.

Still, want to know how to hack a Whatsapp account using this method?

Well, it may be still working among users who haven’t upgraded their Whatsapp.

Surprisingly, there are more than 60% of users who avoid or upgrade their apps as late as possible.

Just in case, you will need a piece of code which can be implemented into a photo or a video.

Once a victim opens the file, the code will spread through the device and infect it. Then, you will have a full control over the app.

You can read the messages check out the contacts, delete anything you want and get access to private images and files!

This method does require knowledge of coding and it is one of the most complicated out there, simply due to the fact you will have to adapt the code according to several parameters.

On the other hand, the main advantage is in the further hacking capabilities.

In essence, once a hacked user sends the same photo to another, he will be hacked as well.

This creates an impressive chain of hacked users, which can be more than just long.

Method 3: WhatsApp Backdoor allows Hackers to Intercept and Read Your Encrypted Messages

This method is perhaps the most appealing of them all. In essence, it uses a “backdoor” flaw.

Some say it is a severe mistake, while others claim it is an additional feature.

Anyway, it allows to you to hack Whatsapp and to read, by intercepting the messages between users. Backdoor is used by Whatsapp, Telegram, and a few more apps.

First of all, we should explain the end-to-end encryption. It means that you, as a user will send an encrypted message to another person.

Only after it is received, it will be decrypted and readable. Whatsapp introduced this feature in 2012 and then became the most secure app of them all. Sadly, it looks like it isn’t so secure.

Whatsapp is owned by Facebook, and if we know that this giant allows to the central intelligence agencies to spy on their users, we can deduce that Whatsapp shares the same flaw.

That’s why the backdoor feature exists. Originally, it has been developed for central intelligence agencies, but at the same time, it is something that hackers can use.

Furthermore, Whatsapp end-to-end encryption works on “trust”. The company uses a secure server to process the messages, but according to the user agreement, they can change any of the rules at any given moment.

Basically, Whatsapp can choose to share your messages with others and you won’t know about it!

How this actually works?

The vulnerability relies on the way WhatsApp behaves when an end user’s encryption key changes.

Basically, we have a scenario between users A and a person B.

When a person A sends a few messages to the person B, the Whatsapp on that device will decrypt the messages and allow for the user to read them.

But, when a user B replaces the device, he will also be able to get and read those messages.

This is possible due to the fact Whatsapp choose to update and modify the private keys, needed for decryption at any given moment, without informing the user.

Now, you as a hacker will be user C. You will modify the private key of a user B and insert your own.

By doing so, you will directly be able to read messages of user A. Whatsapp spy app that can do it for you isn’t so complicated to use, after all.

Here we have another advantage of this method. Facebook, which owns Whatsapp didn’t solve this issue since 2016. It is obvious that it will stay available in the future as well.

All of this means that you, as a hacker will be able to exploit this method in the near future. Using Whatsapp tracker onlineand using this method will give impressive results.

Some believe that backdoor feature is used as a feature to eliminate the need for constant privacy key verification, which is annoying. Instead, Whatsapp will do it instead of you.

But, Signal private messenger, which uses the same technology is immune to this issue, simply due to the fact it requires physical verification.

If you are a decent hacker, you will be able to exploit this method or better said this drawback of the Whatsapp.

After all, it is introduced to allow for agencies to spy on users, which means that hackers, including yourself, can use it for the same reason.

Conclusion:  The best way to hack Whatsapp is to use Copy9

At the end, we must choose the best or better said the most efficient way to spy on Whatsapp.

Obviously, it is Copy9 app. First of all, it is so easy to use that you don’t need any, precious knowledge or anything else.

Even if you are an average user, you won’t have any difficulties with it. Then we have the fact you will get additional features, which directly makes you the “owner” of a targeted device.

On average, you will need around 5 minutes from the time you will download the app, install it and read the first Whatsapp messages.

None of other two methods can provide you this. Once you are done with the process, you can remotely remove the app from the targeted device and there won’t be any pieces of evidence you have ever used it.

The second method is a bit more demanding. You will need to know the essence of coding.

But, this isn’t something you can learn at school or at some other place.

You will have to be born for this and you will need to understand the matter without the help of anyone else.

Also, once users upgrade the app, you won’t be able to use this method anymore.

The third, backdoor method is still possible and it will stay possible ever since, due to the fact Facebook refuses to change the privacy terms!

In other words, you will be able to use it as long as you want. But, this method is also complicated and probably even more demanding than the second one here.

So, if you choose to use it, take your time, learn the matter and only then try it. By the way, this method can be detected easily by users!

At the end, we should repeat that the best and the easiest way is to use Copy9. It doesn’t require any of the requirements other two methods do, but it offers even better result.

     











         

Friday, 30 June 2017

Uhusiano wa akili na Roho

AKILI NA ROHO (SEHEMU ~I)

Bwana Yesu asifiwe wapendwa!!!

Tunakukaribisha katika kufuatilia mfululizo huu wa somo la akili na Roho, ambalo tumesimamia neno kutoka 1Kor 14:15

"Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia."

���� Wakristo wengi tunachanganya nafasi ya roho na akili katika kufanya maamuzi au kung'amua mambo.

���� Na wengine wamefika hatua wanafikiri kufanya maamuzi kwa kutumia akili zao watakuwa wamemkufuru Roho mtakatifu.

���� Wapo wanaousimamia mpaka mistari ya Biblia kuzifisha akili zao, mstari wanaopenda kuutumia ni huu unaosema

Mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote wala usitegemee akili zako mwenyewe. Mithali 3:5.

Hii ni tafsiri mbaya ya neno la Mungu inayowafanya wengi wawe maskini mwilini na rohoni.

Katika mstari huu neno la Mungu halituambii tusitumie akili zetu, bali linatuasa tusitegemee akili zetu WENYEWE, Hii ina maana tusiegemee katika kutumia akili TU,

Bali baada ya kumtumaini Bwana KATIKA AKILI zetu tunahitaji pia kumtumaini kwa Moyo.

Tafsiri ya Neno KWA MOYO ni kutoka ndani hii inamaana kutumaini Bwana kwa kumaanisha. Biblia inatuambia moyo ndiko chemichemi za uzima zinakotoka hivyo ukimtumaini Mungu kwa moyo hakuna kitakacho kutoa katika tumaini hilo hata mwisho.

Mtu asiemtumaini Mungu kwa moyo wake wote ni mbabaishaji au muigizaji neno  watu hawa wananiheshimu kwa midomo lakini Mioyo yao iko mbali nami.

Mungu anataka mioyo yetu tuisogeze kwakwe kila tunachokifanya tukifanye kwa moyo.

Hivyo umtumaini Bwana kwa si kwa akili yako au uelewa wako mwenyewe bali umtumaini kutoka ndani ya Moyo.

Neno linatuambia;  
Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, KWA AKILI ZAKO ZOTE ‘na’ kwa nguvu zako zote.’ Marko 12:30

Kila jambo lililotajwa hapo juu lina umuhimu wake, na uzito wake ndio maana ametumia kiunganishi ‘na’  hajatumia ‘au’ ambayo inakupa option yaani kuchagua.

Hivyo ni lazima utumie nguvu, roho, akili na Moyo.

Kumpenda Mungu kwa nguvu inamaanisha kujitoa kwa ajili ya Bwana kwa muda na mali yako.

↩  KWENYE KIINI CHETU CHA SOMO

AKILI ni nini?

Ni uwezo wa kung'amua jambo/ kitu fulani, ni uwezo wa kuwa na ujuzi na kitu/jambo flani,
 
Kuna aina kadhaa za akili,

�� Akili za kuzaliwa,

Hizi ni akili ambazo kila mtu anazo, kila mtu anazaliwa na akili ambazo zinamsaidia yeye kujua mambo mbalimbali pasipo kugundishwa na mtu. Kila mtu amejaliwa akili hizi tofauti ipo katika kuzitumia tu.

Uvivu wa kufikiri na kukubali kuongozwa na akili ya mtu mwingine au kuiga iga ndo kinafanya watu wengine waonekane wamependelewa. Mfano Wazungu

�� Akili za darasani,

Hizi zinapatikana kwa kuongezewa maarifa na mtu mwingine, akili hizi mara nyingi tunazipata ili zitusaidie kuweza kupata mambo fulani/kufika viwango fulani, inabidi uingie darasani na awepo mtu wa kukufundisha/kakuongezea ujuzi/akili.

Wengi hawafanikiwa pamoja na kuwa elimu za darasani, moja ya sababu kubwa ni Upumbavu.

Upumbavu maana yake kuwa na  maarifa na kushindwa kuyatumia kwa upuuzi. Hii ni tofauti na ujinga ambapo ujinga ni kukosa maarifa.

�� Akili za maisha,

Huu ni ujuzi ambao unaupata kutokana na mazingira yanayokuzunguka, maisha tunayoyaishi  yamekuwa yakifufundisha vitu vingi sana, na ndio maana kuna watu hawajawai kwenda shule au wameishia viwango vya chini vya elimu  lakini wamefanikiwa, ni kwa sababu ya akili ya maisha ambayo wameipata katika mazingira yanayowazunguka, wana uzoefu na mambo mengi tofauti na mtu ambaye emeenda shule.

Ni muhimu sana kuwa na akili ya maisha kuliko ya darasani, Kwa sababu kama una akili tu ya darasani hauna akili ya maisha, hiyo ya darasani ina asilimia ndogo sana kuweza kukusaidia!

NB: Huwezi kufanikiwa ukiwa na akili za darasani pekee unahitaji akili za maisha, lakini inawezekana kufanikiwa ukiwa na akili za maisha bila kuwa na za darasani. AMKA!

Aina nyingine ni akili ya kiungu,

Hii ndo akili bora kuliko zote, akili hii hauzaliwi nayo, hauipati darasani wala mtaani (maisha ya kawaida) utapata kutoka kwa Mungu tu.!

Akili hii ni bora Kwa sababu ukiipata inauwezo wakubadilisha maisha yako muda wowote!

Habari hizi za akili ya kiungu utazipata zaidi ukisoma habari za Yusufu (Mwanzo 41:37-41) na Danieli 5:10-14).

�� Akili za kiungu

Zinapatikana kwa wewe ambaye ni mwana wa Mungu na ukimuomba kwa bidii akupatie anakupatia!

�� Ukimuomba Mungu Roho ya hekima, maarifa na ufahamu utaipata akili hii.

Roho ni nini?

Ni nafsi hai inayoifanya nafsi kuwa hai, kuna tofauti kati ya nafsi na nafsi hai, Nafsi haiitwi nafsi hai isipoungana na roho. Ukisoma mwanzo 2;7 neno linasema Akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

➡ Nafsi inaonekana lakini haiishi pasipo roho. Roho ni nafsi isiyoonekana lakini ni hai.

Kwa hiyo ukiitenga nafsi na roho nafsi hio haitobaki hai tutaizika, itarudi mavumbini.

���� Hapo tumezungumzia roho ya mwanadamu kuna aina mbalimbali za Roho ambazo pia ni muhimu kuzielewa na kuzitofautisha; Roho wa Mungu, Roho ya/za Mungu, na roho za shetani.

�� 1. ROHO MTAKATIFU (Roho WA  Mungu)

Huyu tunampokea kwa namna mbili, kila ujio una kazi tofauti;

1⃣ Uvuvio Wa Roho

Huyu tumempokea kutoka kwa Mungu mwenyewe kwa njia ya kuvuviwa, Yohana 20:21 naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho mtakatifu.

Tukimpokea hutuongoza dhamiri zetu katika kweli;

Warumi 9:1 nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu.

Pia Yohana 16:8 anasema Naye akiisha kuja, huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki na hukumu, Hutufundisha, kutukumbusha; Yohana 14:26

kutuongoza; Yohana 16:12

kwa kifupi kwa njia ya uvuvio Roho huja kama msaidizi.
���� Wote tumepata Neema ya kuvuviwa ingawe wengi hawajui, na kutokujua na kuamini Roho yuko ndani yake hupotea.
Wasiomtambua huyu dhamiri zao huwa dhaifu hivyo rahisi kunajisika.

2⃣ Kujazwa Roho

Ujio huu wa Roho Mtakatifu ni wa nguvu, Ambapo anapokujilia unasikia hali ya tofauti na unapokea nguvu. ukisoma Matendo 1:8 anasema.

"Lakini mtapokea nguvu Roho akishawajilia juu yenu".

Katika ujio huu Roho mtakatifu hushuka na nguvu zake naye huleta roho za Mungu na nguvu ama upako.

Mtu hujazwa Roho kwa kuwekewa mikono ama kuongozwa maombi ama kujitenga na kuomba kwa Mungu.

Huja na ishara mbalimbali mfano kunena kwa lugha mpya. Matendo 2:4

Kwa kifupi kwa njia ya kujazwa Roho huja kwa nguvu akiambatana na matendo ya Muujiza na roho za Mungu zinazotusaidia kuifanya kazi ya Bwana.

Kwa Neema Ya Mungu, Mungu Humvuvia Roho Wake Kila Amwaminiye Amfundishe, Amuongoze, Kumkumbusha,

Lakini Hii Haitoshi Neno La Mungu Linasema; *MTAKENI MUNGU NA NGUVU ZAKE Zaburi 105:4

⚡ Hivyo Unahitaji Ujazo Wa Roho Mtakatifu Katika Huduma Yako Ili Umtumikie Mungu Kwa Ujasiri Matendo 4:31

⚡ Unahitaji Ujazo Wa Roho Mtakatifu Ili Upokee Nguvu Itakayokuwezesha Kutumia Mamlaka; Kumkemea Mapepo, Kuombea Wangonjwa Na Matendo Yote Ya Miujiza N.K.

✅ ya kwanza ya somo hili la AKILI NA ROHO inaishia hapa, leo tumeweka msingi,

Mungu akipenda kwa sehemu inayofuata tutaingia ndani zaidi. Roho mtakatifu atakufundisha utaelewa zaidi endelea kufauatilia kuna namna Roho mtakatifu anataka kukuvusha.

���� Mungu akubariki sana!

Saturday, 13 May 2017

Je, unapenda kufanikiwa kimaisha?


Mambo Matatu Ya Yuyaepuka Katika Safari Yako Ya Mafanikio

Kuna wakati umekuwa unajilaumu kwamba maisha yamekuwa ni magumu, wengine husema wamelogwa, wengine husemwa hawana bahati na meneno mengine kama hayo.  Hizo sababu zinginezo ni woga binafsi ambao kimsingi kama utaendelea kuzibeba basi kufanikiwa kwako itakuwa ni ngumu. Lakini ukweli ni kwamba adui  namba moja wa maisha yako ni wewe mwenyewe.

Na adui huyu ni mbaya sana, kwani hatima ya maisha yako unayo mwenyewe, kwanini ubaki kuwanyoshea vidole watu wengine? Na ili hali wewe ndo mmliki mkuu wa maaumuzi yako? Nilichogundua ni kwamba watu wengi tunashindwa kufanikiwa kwa sababu ya mambo haya;

1.Kusubiri mtu mwingine akufanyie maamuzi.
kama tulivyosema hapo awali ya kwamba maisha  yako yapo mikononi mwako kwanini uache mtu mwingine afanye maamuzi juu ya maisha yako? Najaribu kuwaza kwa sauti ila sipati majibu.

Nasema hivyo kwa sababu maisha yetu yanakuwa ya kawaida kwa sababu tunapenda kuwaruhusu watu wengine watoe maaumuzi katika kutenda jambo fulani. Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kufanikiwa jaribu kutafakari juu ya maisha yako na uamue kutoa maaumuzi juu ya jambo hilo. Lakini pia baada ya kutafakari ni nini cha kufanya jambo la msingi ni kuhakikisha unapata mtu sahihi wa kukushauri ni nini ufanye katika jambo hilo ili uwe bora zaidi.

2. Kukata tamaa mapema.
Watu wengi sana huwa tunaathiriwa na ugonjwa huu wa ukataji tama mapema, na hii ni kwasababu wengi wengi wetu huwa tunapenda matokea ya papo kwa papo. Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya papo kwa papo hakuna labda uamue kucheza bahati nasibu. Ila kama unataka matokeo ya uhakika na yenye kuleta mafanikio ya kweli unachokihitaji ni kuwa mvumilivu kwa kila hatua ambayo unapiga kila siku katika jambo ambalo unalolifanya.

Hivyo niweke nukta katika maelezo haya kwa kusema ya kwamba kuwa mvumilivu kila wakati. Kwani mvulivu hala mbivu, ila  kumbuka kuongeza hatua za kiutendeji ambazo zitakufanya uweze kusonga mbele na si kukata tamaa. Kwani kukata tamaa ni chukizo mbele za Mungu wetu.

3. Kuridhika mapema.
Kuridhika mapema ni adui mkubwa wa mafanikio yako, naomba hili libaki kichwani mwako. Mafanikio hayana ukomo, kila siku na kila wakati ona kabisa bado hujafanikiwa hata kama watu wanasema umefanikiwa. Usibweteke na hali uliyonayo. Daima kumbuka ya kwamba "Mafanikio ni njaa isiyoisha" hivyo kuridhika ni kurudi nyuma katika hali ya kiutendeji.

Nimalizie kwa kusema tena mafanikio hayana ukomo, hivyo achana na tabia ya kuridhika mapema.

Thursday, 20 April 2017

Ijue jinsi ya kuroot simu yako!

ANDROID NI NINI..??

Android ni Mfumo wa simu (Operating System) ambao unaboreshwa siku hadi siku. Mfumo huu una majina tofauti kutegeana na toleo lake.

Haya ni Matoleo (Versions) mbalimbali ya Android kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho:

1. Cupcake (1.5)

2. Donut (1.6)

3. Éclair (2.0 – 2.1)

4. Froyo (2.2 – 2.2.3)

5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)

6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)

7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)

8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)

9. KitKat (4.4 – 4.4.4)

10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)

11. Marshmallow (6.0>>>>>>

Matoleo haya huboreshwa kadri yanavyozidi kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda;
Settings – About phone – Android Version. Ukikuta Jelly Bean, KitKat, marshmallow au Lollipop hongeara, kwani unatumia matoleo ya mwisho yalioboreshwa!!

Mfumo huu wa Android unafaa kufanyiwa settings mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili kumfanya mtumiaji aifurahie simu yake kwa asilimia 100, lakini shida huja kwamba sio kila PROGRAM inayowekwa katika mfumo huu wa Android inakubali kufanya kazi!!

Wapo watengenezaji wengi wa program (Software Designers) ulimwenguni, watengenezaji wa mfumo huu wa Android wamezuia Program ambazo hazijatoka kwao zisifanye kazi kwenye mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA TUTAPATA KUELEWA MAANA YA KU ‘ROOT SIMU' kuwa ni kuifanya simu ikubali Programu zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android Developers).

Ukishai ‘root’ simu yako sasa utakua na uwezo wa kuweka program zinazohitaji ‘root permission’ kwenye simu yako.

JINSI YA KU ‘ROOT’ SIMU YAKO.

Kuna aina za simu ni rahisi sana ku root, lakini nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa kutosha. Zipo program nyingi sana zinazoweza kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni kama vile:
1. KingRoot.

2. Vroot.

3. Kingoapp Root.

4. SRSRoot.

5. Framaroot.

6. Root Master.

7. z4root.

8. Universal root.

9. Iroot.

10. Easy root, nk.

Baadhi ya Program hizi zitahitaji Computer, nyingine hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa simu kutumia Program iitwayo KingRoot ambayo inakubali kufanikisha zoezi hili kwenye asilimia kubwa ya simu za Android.

Program hii haihitaji Computer. Kuipata nenda Google kisha isearch na kui download. Kwa msaada uliza……

Maandalizi:

(i) Charge Simu yako, angalao ijae kwa 50%

(ii) Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa kawaida. Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa 100%.

Sasa kuifichua nenda Settings>About phone>Build number.

Baadhi ya simu (LG na HTC) nenda Settings>About phone>Software information>Build number.

Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a Developer”

(iii) Sasa nenda Settings>Developer options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama haipo)

(iv) Nenda settings>Security>Unknown Sources. Weka tiki hapo.

Hapo maandalizi yatakua ni tayari. Sasa download KingRoot 4.0 (or above) kwa kui search kwenye Google kisha Install kwenye simu yako. Baada ya ku install gusa ‘Open’. Baada ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu yako automatically—Model ya Simu na Toleo lake. (Mf. Model: H6 Android 4.4.2). Kama simu yako haijawahi kuwa rooted utaona ‘Root access is unavailable’.

Chini gusa ‘START ROOT’. Hapo KingRoot itakua inakomboa simu yako kutoka kwenye kifungo cha maisha…kuwa na subira zoezi hilo litachukua muda kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…mpaka utakapoona ‘ROOT SUCCSSFULLT’ DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!!

Ili kuhakikisha kama simu yako imeshakuwa rooted, nenda PlayStore kisha download Root Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa ‘VERIFY ROOT’. Ukiona ‘’Congratulations! Root access is properly installed on this Device” HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!

FAIDA ZA KU ROOT SIMU:

1. Utaweza ku update toleo la mfumo wa simu yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android 4.4.2 (KitKat) unaweza kui update kwenda Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi kuflashiwa bila kuwa rooted!

2. Huwa inatokea simu kuibiwa. Wewe unaesoma Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi (ukiokota mtafute mwenye nayo). Nitafute nikupe story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu yako wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka kwenye System ya simu yako baada ya kufanyiwa ‘Factory reset’ au kuflashiwa. Kama ume root simu yako, zipo Program za kuitafuta simu yako ambazo hata mtuhumiwa aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program hizo ni Cerberus.

3. Utakua na uwezo wa kuweka Program nyingi na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na kuboresha muonekano (performance and appearance). Pia kuna program za kutunzia chaji, Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k…. ambazo hazitafanya kazi bila root.

4. Utaweza kufuta chochote ktk simu yako! Mimi nimefuta hadi torch, kitu ambacho huwezi fanya km hujaroot simu yako!

5. Unaweza kuongeza RAM ktk simu yako!!!

TAHADHARI:
Rooting inaweza kuharibu kabisa simu yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa sitahusika kwa lolote). Usiogope, hii huwatokea wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo. Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za Marafiki zangu wasiopungua 20 bila madhara yoyote kutokea. Fanya utafiti kwanza ni program gani sahihi ku root simu yako, omba ushauri,…..

Pia Rooting inaharibu Warranty ya simu yako. Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako na ukaikuta na tatizo, ukiirudisha haitakubalika. Aidha, inawezekana pia ku’unroot’

MWISHO;

Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti, anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala hii, wale woote ambao tutaenda sambamba tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo zinahitaji ‘Root Permission’. Mie natumia Tecno L3 , baada ya kui root nimeifanyia Settings nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi sana!! ROOTING imeniwezesha hata kubadilisha muonekano wa maandishi system nzima.

Tembelea blog mara kwa mara ujifunze mengi!

Wednesday, 19 April 2017

Rudisha data zako ulizopoteza ktk simu yako!

Elisante blog, keep on reeding!

JE WEWE NI MUATHIRIKA WA KUPOTEZA DATA ZAKO KATIKA SIMU YAKO..??? 
EITHER ULIZIFUTA AU BAHATI MBAYA 


   Sasa ondoa shaka kabisa suluhisho limepatikana kupitia blog yetu hiiii sasa utaweza kurudisha data zako zote ikiwa ni sms mesenger au hata whatsapp kama inavyoonekana hapo.. 

     

 Vitu hivyo vyote unaweza ukavipata kama vilikupotea unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo    

  Nenda play Store Katafute app inaitwa GT RECOVER KAMA unavoiona hapo chiniiii 

   Baada ya hapo sasa unachotakiwa kufanya ni kuchagua unataka kurecover nini na utapata vitu vyako vyoteee...  

 Sehemu ya kuchagua vitu vya kurudisha ipo kama ifuatavyo na wewe utachagua unachotaka kurudisha tyuuuu

Na hapo itakua umefikia hatua ya mwisho kabisaaa asante kwa kutembelea blog yetu endelea kushare kwa wenzako na kama utakua na tatizo tutakusaidia 

    NB: Your phone must be rooted!


Thursday, 13 April 2017

Neno la Mungu by Mwakasege.

SEMINA YA NENO LA MUNGU  DODOMA.

NA MWL MWAKASEGE

FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA

TAR 3 APRIL 2017

Siku ya Pili

LENGO ni kuimarisha mahusiano yako na Mungu katika Kristo Yesu

Kuna mambo 2 ambayo yanaweza kutumika katika NDOTO

*JAMBO 1*
Shetani anaweza kutumia NDOTO kupandikiza mambo ambayo usipoyang'oa mapema yataharibu maisha yako

*JAMBO 2*
Kutazama ishara  zitakazo kuonyesha kuwa NDOTO zinahitaji kufuatiliwa

*ISHARA*
1. Kujisikia kufadhaika moyoni kwa ajili ya NDOTO uliyoota

Kufadhaika  maana yake ni mahangaiko unayoyapata  ndani ya Moyo wako( kuutibua moyo)

_Mwanzoni 41:1-8"...... 8. Hata asubuhi roho yake IKAFAIDHAIKA akapeleka watu kuwaita waganga wote wa misri ..._

⏩Usifanye kosa kudharau NDOTO yoyote utakayoota Ukasema kumbe ni ndoto tu,  inabidi kuifuatilia  _Mwanzo 41. 7 b"Basi Farao akaamka , *kumbe ni NDOTO tu*._

_Mwanzo 40:5-6 "Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi, akawaona *wamefadhaika*._

Yusufu aliwaona wote wawili mnyweshaji na mwokaji wote WAMEFADHAIKA

⏩Mfadhaiko huja kama alarm,maana ukishaitega alarm ikilia lazima ushtuke.

2. Kuota NDOTO hiyo zaidi ya Mara moja au inayofanana na hiyo
⏩Mwanzo 41:25-32
Mst 32"...  _*Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi*_.

Unapoota Mara 2 au zaidi ni kukutaarifu unatakiwa kuifuatilia hiyo NDOTO
*Ayubu 33:14-15*
_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, *Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali*. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;_

Usipoifuatilia ndipo Mungu huirudisha Mara ya 2 au zaidi hadi utakapopata ufahamu wakulifanyia kazi

⏩Jiulize kama Mungu katumia NDOTO kusema na wewe kwa nini iwe vigumu kuelewa maana yake

_Warumi10:17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa *neno la Kristo*._

Ukiwa na Neno LA Mungu lazima utaisikia sauti yake.

⏩Mfano ukiwa na gari ni vema kujua baadhi ya vitu ili likipata shida uweze kulitengeneza sio lazima kila kitu unapeleka garage. Vivyo hivyo kwa watumishi, sio lazima kila tatizo lako unalipeleka kwa watumishi mengine yatatue mwenyewe Yale unayoona huyawezi ndio yapeleke huko, unapotaka kumweleza *Mtumishi jambo lako sikiliza Amani Ya moyo wako kwanza*

3. Ndoto uliyoota kukutia hofu
Daniel 4:5 na Ayubu 4:12-14

_Nikaota ndoto iliyonitia *hofu*; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha._
*DAN. 4:5*

_Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong’ono yake. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.  *Hofu* iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote._
*AYU. 4:12‭-‬14*

4. Ukiwa mambo uliyoota kwenye ndoto yanatokea katika mwili
Ayubu 4:12-16����

Mfano
⏩Ukiona umeota ndoto unakemea na ulivyoshtuka bado unakemea( fuatilia)

⏩Au ulikuwa unalia kwenye ndoto na umeamka unakuta macho yana machozi pia fuatilia

5. Ndoto kukunyima usingizi
Daniel 2:1
 
_Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, *usingizi wake ukamwacha*_. *DAN. 2:1*

6. Kwa na hamu ya kutaka kujua tafsiri ya hiyo ndoto
Mwanzo 40:7-8,41:7-8

_Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.MWA. 40:7‭-‬8 SUV_

_Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.   Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.MWA. 41:7‭-‬8_

Mstr 8 - alitaka kujua ndoto ile ilimaanisha nini

⏩Ndoto ya Farao ilibeba maisha ya miaka 14 ya dunia nzima,kama angepuuzia sijui ingekuwaje kwa hiyo miaka 14. Kwa hiyo  ule msukumo aliokuwa nao ndio ulisaidia utafsiriwa

7. Ndoto uliyoota kukuletea mahangaiko moyoni mwako juu ya Imani na utumishi ulinao kwa Mungu

_Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.KUM. 13:1‭-‬4_

⏩Usimwogope mtu Bali mwogope Mungu

⏩Usikubali jina au huduma yako ivume kuliko jina la Yesu

*Mfano*: Punda aliembeba Yesu alitembea juu ya nguo kwa sababu tu alikuwa kambeba Yesu lakini baada ya kumshusha Yesu alitembea chini kama kawaida. Dhamani uliyonayo ni kwa sababu unae Yesu ndani yako

8. Ukiona uliyoyaona kwenye ndoto yanapinga au ni tofauti ya mipango uliyonayo

Ayubu 33:14-17
_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;  Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,  Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;AYU. 33:14‭-‬17_

⏩unaweza kuota ili upangue kile kibaya ambacho kinaweza kutokea mbele,hivyo anapozungumza nawe anakusaidia usijeingia kwenye matatizo Fulani au kukuondoa katika mawazo uliyonayo

9. Kusikia msukumo moyoni wa kusimulia ndoto uliyoota
Mwanzo 37:5-11( Pale Yusuph alipowasimulia ndugu zake ndoto aliyoota)

Mathayo27:19  _Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, *Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake*._

⏩Unaweza kuota ndoto kwa ajili ya mtu mwingine hivyo pale unapopata msukumo moyoni wa kumwambia we mweleze ila omba hekima, na kibali kutoka kwa  ROho Mtakatifu

10. Kusikia msukumo moyoni wa kuandika ndoto uliyoota

_Habakuki 2:2-3 BWANA akanijibu, akasema, *Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao*, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.HAB. 2:2‭-‬3_

⏩Unaandika kwa sababu unaweza kuisahau asubuhi au kwa  ajili ya kufuatilia huko mbeleni

⏩Uwe unaandika ndoto zakusaidia baadae
Note:Kama huwa unasahau ndoto unazoota weka daftari na kalamu karibu ili unapoota tu uwe unaziandika na baadae iwe rahisi kuzifuatilia hatua kwa hatua.

11. Ukiwa umesahau ndoto uliyoota ila moyoni unajisikia msukumo wa kutaka kujua

Daniel 2:1-5
Baada ya Nebkadreza kusahau ndoto Daniel alienda kumweleza hiyo ndoto tena

⏩Ukiota ukasahau jitahidi kuifuatilia kwani ktk ulimwenngu wa roho imerekodiwa km ile ya Nebukadreza.

MAOMBI
⏩Toba kama kuna mojawapo ya ishara hizi 11 hukuzifuatilia( kwa kujua au kutojua) Mungu arudishe hizo
Ndoto ili aseme nasi tena haijalishi muda gani umepita

��������������
Bwana Yesu Asifiwe. Tunawakaribisha kwenye semina inayoendelea Dodoma mjini katika uwanja wa barafu. Semina imeanza jana tarehe 2 April itaendelea hadi jumapili tarehe 9 April.
Redio zinazorusha Semina inayoendelea Dodoma mjini ni;

1. Redio Sauti ya injili - 
Moshi, 92.2 FM
Arusha,96.1 FM.
Tanga 102.6FM  & 96.7 FM
Same 100.4 FM
Rombo 96.4 FM
Manyara 102.9 FM & 96.1FM
Morogoro 99.1 FM
Mara 96.1 FM
Unguja, Pemba na Mombasa 102.6 FM
Voi - Kenya 96.4 FM
Dodoma 102.9 FM
Pwani, Rufiji, Kiluvya, Tegeta, Ubungo, Manzese, Mbezi, na Ruaha  99.9 FM
Daraja la Mkapa (Lindi) 99.9 FM

2. Redio HHC Alive
Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga, - 91.9 FM.

3. Redio CG FM
Kigoma, Simiyu, Shinyanga, Tabora na Katavi 89.5 FM

4. Redio Baraka
Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa 107.6 FM

5. Radio Rungwe
Rukwa, Malawi,Mbeya na Njombe102.5 FM

6. Radio Info
Mtwara 92.1 FM

7. Redio Uzima
Dodoma 94.0 FM

8. Redio Bunda FM
Mwanza, Mara, Simiyu na Kagera 92.1 FM

9. Redio Mpanda FM
Katavi, Rukwa na Kigoma 97.0 FM

Unaweza kusikiliza live kupitia www.kicheko.com na www.mwakasege.org, unaweza kusikiliza na kuangalia  live kupitia www.ustream.tv/chanel/mwakasegemanaministry na www.youtube.com (jina la chanel ni Christopher Mwakasege)

Mungu awabariki sana wapendwa!

Monday, 20 March 2017

Maneno huumiza kuliko matendo!

"Siku moja usiku, nilipokuwa mtoto, nakumbuka kumwona mama yangu akituletea chakuka mezani nikiwa na baba. Mama aliniwekea sahani ya chapati laini, huku akimwekea baba sahani yenye chapati iliyoungua.

Nilijaribu kumtulizanishia macho baba ili kuona atafanyeje. Bila kuonesha tofauti, baba alianza kula chapati ile iliyoungua huku akiniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni.

Sikumbuki nilichomjibu. Ninachokumbuka, ni kumsikia mama akimtaka radhi baba kwa kuunguza chapati. Na kamwe sitasahau majibu ya baba pale alipomjibu mama kwa kumwambia, 'Oh, usijali mpenzi. Huwa napenda pia chapati za kuungua.'

Baadaye usiku huo, nilipokwenda kumbusu baba kwa ajili ya kumtakia usiku mwema, ndipo nilipomuuliza kama ni kweli hupendelea chapati za kuungua.

Alinikumbata mikoni mwake na kuniambia, 'Leo, mama yako alitingwa mno na majukumu ya kazini hata akawa amechoka sana, ndipo akaunguza chapati.

Lakini, kwa bahati, chapati iliyoungua haiwezi kumuumiza mtu kiasi cha kumchoma moyoni, walakini maneno makali yanaweza kumuumiza. Hivyo, sikuwa na sababu ya kumshutumu kwa maneno makali. Hata kama sipendi chapati za kuungua, ila kumjibu vile kumemfanya awe huru. Unajua maisha nayo hayako kamili kama tusivyo kamili sisi wanaadamu.

Kwahivyo, ili kudumisha furaha na kuboresha mahusiano na maelewano baina yetu, ni lazima tujifunze kuyakubali na kuyakabili mapungufu yetu - Chapati za kuungua hazidumu milele, zikishasagika tumboni utakwenda kuzitoa msalani. Lakini, maneno makali huacha majeraha ya kudumu.

Saturday, 11 March 2017

Hama mtandao bila kubadili line yako ya simu!

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezindua mpango maalum unaomuwezesha mteja kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu, na kueleza hatua 13 za kufuata ili kupata huduma hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jana jijini Dar es Salaam, alisema huduma hiyo ni ya hiari na ili mtu aweze kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine ni lazima afuate hatua 13.

Mhandisi wa Mawasiliano wa TCRA, Mwesigwa Felician, alitaja hatua ya kwanza ya kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine kuwa ni kufika kituo cha mauzo au kwa wakala anayetambuliwa na mtoa huduma anakotaka kuhamia na kumueleza dhumuni lake.

Hatua ya pili, alisema Felician, ni kujaza fomu maalum ya maombi ya kuhamia mtandao aliotaka kuhamia.

Felician alitaja hatua ya tatu kuwa ni kujaza tamko la kukubali kuwa mteja anakubali kuwajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma alizokuwa akipata kwa mtoa huduma wa awali kama yatakuwapo.

Felician alitaja hatua ya nne ni kuwa ni kuwasilisha kitambulisho chenye picha ambacho kinaweza kuwa cha taifa, kadi ya mpiga kura, leseni ya udereva, pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika.

Alisema pia mteja anatakiwa kuwa na simu ya kiganjani inayofanya kazi yenye namba inayotakiwa kubaki baada ya kuhama mtandao.

Hatua ya tano, Felician alisema ni kuhamisha fedha zilizopo kwenye akaunti ya simu kabla ya kuhama ili kuepuka usumbufu.

Katika hatua ya sita, Felician alisema, mwenye namba ya simu atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno HAMA kwenda namba 15080 ambayo ni namba maalum ya kuhama.

Alisema katika hatua ya saba, mteja atapokea ujumbe mfupi wa maneno utakaomjulisha kuwa ombi lake limekubaliwa.

“Hatua ya nane, iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana na kutokamilisha malipo ya madeni ya mtoa huduma wako wa awali, maombi yako yatashughulikiwa na utajulishwa kwa ujumbe mfupi wa maneno maendeleo ya mchakato huo,” alisema Felician.

KAMA KAWAIDA
Alisema katika hatua ya tisa, mtoa huduma za simu za kiganjani atampatia mteja wake mpya laini mpya ya simu.

Hatua ya 10, Felician alisema, ni kusitishwa kwa huduma za kifedha kwa muda mpaka namba ya mteja itakapohamishwa kwa mtoa huduma mpya. Kuanzia hapo mwenye namba atatumia huduma za kifedha za mtandao mpya kama huduma zipo.

Mhandisi wa Mawasiliano wa TCRA Felician alisema katika hatua ya 11, huduma za kupiga na kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno zitaendelea kama kawaida.

Alisema katika hatua ya 12, mteja atakuwa amehama mtandao mmoja kwenda mwingine na kama patakuwa na ucheleweshaji, ni wa saa kadhaa, lakini ndani ya siku mbili pekee.

“Wakati huo namba yako ya zamani itakuwa imehamishwa kwa mtoa huduma wako mpya na laini yako ya awali haitatumika tena na utapokea ujumbe mfupi wa maneno kuwa uhamaji umekamilika,” alisisitiza Felician.

Katika hatua ya 13, mteja atatakiwa kuweka laini yake aliyopewa kwenye simu na endapo elimu zaidi itahitajika, mteja atatakiwa kwenda kwa mtoa huduma kujua namna ya kutumia huduma hiyo mpya.

MASHARTI NA VIGEZO
Mbali na kuelezea hatua hizo za kujiunga, Felician alisema masharti na vigezo vitavingatiwa ambavyo alivitaja kuwa ni mteja kutoweza kuhama na namba iliyofungiwa au kusitishiwa huduma kwa walipaji wa kabla ya huduma.

Alisema pia mteja hataweza kuhama na salio lililopo na atatakiwa kutumia salio lake kwanza kabla ya kuhama kwani vinginevyo, litapotea.

Pia alisema mteja hataweza kuhama iwapo ana mkopo kutoka kwa mtoa huduma wa awali, mikopo mingine kwa njia ya muda wa maongezi na pesa mtandao.

Felician alisema pia mteja hataweza kuhama iwapo namba yake inahusishwa na uhalifu na imefungiwa.

Kwa wateja wanaotumia utaratibu wa malipo baada ya kutumia huduma, watatakiwa kulipa madeni ya matumizi yao kabla ya kuhama, alisema.

Wateja hao, watatakiwa pia kukamilisha masharti ya mkataba ya mtoa huduma wake na kutizama masharti ya malipo kila mwezi kwa mujibu wa mkataba kabla ya ku