"Siku moja usiku, nilipokuwa mtoto, nakumbuka kumwona mama yangu akituletea chakuka mezani nikiwa na baba. Mama aliniwekea sahani ya chapati laini, huku akimwekea baba sahani yenye chapati iliyoungua.
Nilijaribu kumtulizanishia macho baba ili kuona atafanyeje. Bila kuonesha tofauti, baba alianza kula chapati ile iliyoungua huku akiniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni.
Sikumbuki nilichomjibu. Ninachokumbuka, ni kumsikia mama akimtaka radhi baba kwa kuunguza chapati. Na kamwe sitasahau majibu ya baba pale alipomjibu mama kwa kumwambia, 'Oh, usijali mpenzi. Huwa napenda pia chapati za kuungua.'
Baadaye usiku huo, nilipokwenda kumbusu baba kwa ajili ya kumtakia usiku mwema, ndipo nilipomuuliza kama ni kweli hupendelea chapati za kuungua.
Alinikumbata mikoni mwake na kuniambia, 'Leo, mama yako alitingwa mno na majukumu ya kazini hata akawa amechoka sana, ndipo akaunguza chapati.
Lakini, kwa bahati, chapati iliyoungua haiwezi kumuumiza mtu kiasi cha kumchoma moyoni, walakini maneno makali yanaweza kumuumiza. Hivyo, sikuwa na sababu ya kumshutumu kwa maneno makali. Hata kama sipendi chapati za kuungua, ila kumjibu vile kumemfanya awe huru. Unajua maisha nayo hayako kamili kama tusivyo kamili sisi wanaadamu.
Kwahivyo, ili kudumisha furaha na kuboresha mahusiano na maelewano baina yetu, ni lazima tujifunze kuyakubali na kuyakabili mapungufu yetu - Chapati za kuungua hazidumu milele, zikishasagika tumboni utakwenda kuzitoa msalani. Lakini, maneno makali huacha majeraha ya kudumu.
No comments:
Post a Comment