Monday, 20 March 2017

Maneno huumiza kuliko matendo!

"Siku moja usiku, nilipokuwa mtoto, nakumbuka kumwona mama yangu akituletea chakuka mezani nikiwa na baba. Mama aliniwekea sahani ya chapati laini, huku akimwekea baba sahani yenye chapati iliyoungua.

Nilijaribu kumtulizanishia macho baba ili kuona atafanyeje. Bila kuonesha tofauti, baba alianza kula chapati ile iliyoungua huku akiniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni.

Sikumbuki nilichomjibu. Ninachokumbuka, ni kumsikia mama akimtaka radhi baba kwa kuunguza chapati. Na kamwe sitasahau majibu ya baba pale alipomjibu mama kwa kumwambia, 'Oh, usijali mpenzi. Huwa napenda pia chapati za kuungua.'

Baadaye usiku huo, nilipokwenda kumbusu baba kwa ajili ya kumtakia usiku mwema, ndipo nilipomuuliza kama ni kweli hupendelea chapati za kuungua.

Alinikumbata mikoni mwake na kuniambia, 'Leo, mama yako alitingwa mno na majukumu ya kazini hata akawa amechoka sana, ndipo akaunguza chapati.

Lakini, kwa bahati, chapati iliyoungua haiwezi kumuumiza mtu kiasi cha kumchoma moyoni, walakini maneno makali yanaweza kumuumiza. Hivyo, sikuwa na sababu ya kumshutumu kwa maneno makali. Hata kama sipendi chapati za kuungua, ila kumjibu vile kumemfanya awe huru. Unajua maisha nayo hayako kamili kama tusivyo kamili sisi wanaadamu.

Kwahivyo, ili kudumisha furaha na kuboresha mahusiano na maelewano baina yetu, ni lazima tujifunze kuyakubali na kuyakabili mapungufu yetu - Chapati za kuungua hazidumu milele, zikishasagika tumboni utakwenda kuzitoa msalani. Lakini, maneno makali huacha majeraha ya kudumu.

Saturday, 11 March 2017

Hama mtandao bila kubadili line yako ya simu!

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezindua mpango maalum unaomuwezesha mteja kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu, na kueleza hatua 13 za kufuata ili kupata huduma hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jana jijini Dar es Salaam, alisema huduma hiyo ni ya hiari na ili mtu aweze kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine ni lazima afuate hatua 13.

Mhandisi wa Mawasiliano wa TCRA, Mwesigwa Felician, alitaja hatua ya kwanza ya kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine kuwa ni kufika kituo cha mauzo au kwa wakala anayetambuliwa na mtoa huduma anakotaka kuhamia na kumueleza dhumuni lake.

Hatua ya pili, alisema Felician, ni kujaza fomu maalum ya maombi ya kuhamia mtandao aliotaka kuhamia.

Felician alitaja hatua ya tatu kuwa ni kujaza tamko la kukubali kuwa mteja anakubali kuwajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma alizokuwa akipata kwa mtoa huduma wa awali kama yatakuwapo.

Felician alitaja hatua ya nne ni kuwa ni kuwasilisha kitambulisho chenye picha ambacho kinaweza kuwa cha taifa, kadi ya mpiga kura, leseni ya udereva, pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika.

Alisema pia mteja anatakiwa kuwa na simu ya kiganjani inayofanya kazi yenye namba inayotakiwa kubaki baada ya kuhama mtandao.

Hatua ya tano, Felician alisema ni kuhamisha fedha zilizopo kwenye akaunti ya simu kabla ya kuhama ili kuepuka usumbufu.

Katika hatua ya sita, Felician alisema, mwenye namba ya simu atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno HAMA kwenda namba 15080 ambayo ni namba maalum ya kuhama.

Alisema katika hatua ya saba, mteja atapokea ujumbe mfupi wa maneno utakaomjulisha kuwa ombi lake limekubaliwa.

“Hatua ya nane, iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana na kutokamilisha malipo ya madeni ya mtoa huduma wako wa awali, maombi yako yatashughulikiwa na utajulishwa kwa ujumbe mfupi wa maneno maendeleo ya mchakato huo,” alisema Felician.

KAMA KAWAIDA
Alisema katika hatua ya tisa, mtoa huduma za simu za kiganjani atampatia mteja wake mpya laini mpya ya simu.

Hatua ya 10, Felician alisema, ni kusitishwa kwa huduma za kifedha kwa muda mpaka namba ya mteja itakapohamishwa kwa mtoa huduma mpya. Kuanzia hapo mwenye namba atatumia huduma za kifedha za mtandao mpya kama huduma zipo.

Mhandisi wa Mawasiliano wa TCRA Felician alisema katika hatua ya 11, huduma za kupiga na kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno zitaendelea kama kawaida.

Alisema katika hatua ya 12, mteja atakuwa amehama mtandao mmoja kwenda mwingine na kama patakuwa na ucheleweshaji, ni wa saa kadhaa, lakini ndani ya siku mbili pekee.

“Wakati huo namba yako ya zamani itakuwa imehamishwa kwa mtoa huduma wako mpya na laini yako ya awali haitatumika tena na utapokea ujumbe mfupi wa maneno kuwa uhamaji umekamilika,” alisisitiza Felician.

Katika hatua ya 13, mteja atatakiwa kuweka laini yake aliyopewa kwenye simu na endapo elimu zaidi itahitajika, mteja atatakiwa kwenda kwa mtoa huduma kujua namna ya kutumia huduma hiyo mpya.

MASHARTI NA VIGEZO
Mbali na kuelezea hatua hizo za kujiunga, Felician alisema masharti na vigezo vitavingatiwa ambavyo alivitaja kuwa ni mteja kutoweza kuhama na namba iliyofungiwa au kusitishiwa huduma kwa walipaji wa kabla ya huduma.

Alisema pia mteja hataweza kuhama na salio lililopo na atatakiwa kutumia salio lake kwanza kabla ya kuhama kwani vinginevyo, litapotea.

Pia alisema mteja hataweza kuhama iwapo ana mkopo kutoka kwa mtoa huduma wa awali, mikopo mingine kwa njia ya muda wa maongezi na pesa mtandao.

Felician alisema pia mteja hataweza kuhama iwapo namba yake inahusishwa na uhalifu na imefungiwa.

Kwa wateja wanaotumia utaratibu wa malipo baada ya kutumia huduma, watatakiwa kulipa madeni ya matumizi yao kabla ya kuhama, alisema.

Wateja hao, watatakiwa pia kukamilisha masharti ya mkataba ya mtoa huduma wake na kutizama masharti ya malipo kila mwezi kwa mujibu wa mkataba kabla ya ku

Friday, 3 March 2017

Soma ukue Kiroho!

1⃣ SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE.

DAY 1⃣

SOMO:  UTATUZI WA MATATIZO YATOKANAYO NA HALI YA KIROHO YA ARDHI.

Lengo la somo hili ni kupata ufumbuzi wa matatizo yatokanayo na hali ya kiroho ya ardhi nakujua namna ya kuyatatua

2 NYAKATI 7; 14-15
Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao.. 15; sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza maombi ya  watu waombao mahali hapa.

Neno kuu  "NCHI'
Tunaona katika tafsiri ya Biblia za kiingereza neno nchi limetafsiriwa kama ardhi yenye mipaka halali ya umiliki.

Katika Biblia kuna tofauti kati ya nchi na Taifa. Neno hili halijatumika kama Taifa.
Taifa halihusiani na ardhi na ukumbuke pia kuwa Taifa linaweza kuwa ndani ya ardhi ya Taifa jingine kama vile taifa la Israel lilivyokuwa ndani ya ardhi ya Taifa la Misri'.

Taifa linahusisha watu waaina flani walioamua kujitawala kwa namna moja.
Ndani ya Taifa pia utapata kabila; koo na familia
Hapa ndipo unapogundua kuwa haya yote hayahusiani na ardhi.

Kwa mfano ni kwamba kuna maombi ambayo hayajibiwi mpaka watu washughulike na matatizo yaliyoko katika ardhi husika iwapo ardhi hiyo ina shida..

MATATIZO YATOKANAYO NA ARDHI.

1> Tabia mbaya zinazopata msaada kutoka kwenye hali ya kiroho ya ardhi.

>Ikiwa kuna jambo ambalo Mungu atahitaji ushiriki wako uwe na uhakika kuwa atakutafuta kwa namna na gharama yoyote ile.

          Joshua 2;1
          Matahyo1;1-17
           Joshua 6;25
Hapa tunaona ya kuwa kutoka Ibrahim mpaka Yesu yapata vizazi 42

>Uwe na hakika kuwa Mungu alijua vizazi hivi vyote pamoja na jaribu ambalo shetani alitaka kuliinua kupitiaukahaba wa Rahabu.
shetani alitaka kumfanya Rahabu hata kushindwa kujifikiria kuingizwa katika kusudi la Mungu juu yake

> Mungu huangalia mwisho tangu mwanzo.

>Aliona mwaisho wa Rahabu asiye kahaba *"Mtumishi wake"* na hakukuwepo na namna ambayo wana wa Israel wanaweza kulifuta tena jina lake katika historia zao na uzao wao kwa sababu Mungu alikuwa na kusudi naye.

>Gharama ambazo Mungu hutumia kukufatilia ili uweze kurudi kwake hukuonyesha thamani halisi ya kitu alichokuitia kwake kwanihatokubali upotee hata kidogo.

>Kilichomfanya Mungu kwenda Yeriko ni Rahabu

>Alitafuta mtu mmoja tu pamoja na kuuangamiza mji mzima

>Mungu yuko tayari hata kuangamiza taifa zima ili ampate hapo mtu mmoja anayemhitaji kwa ajili ya kusudi lake

>Kama alikuwa tayari kumfata Rahabu aliyekuwa kahaba pamoja na shetani kuleta jaribu la ukahaba inashindikanaje kwako?

>Kama Rahabu alifuatwa basi tambua ya kwamba haijalishi umekufa kiasi gani atakufata tu kwa Roho wa ufufuo..Haijalishi una dhambi kubwa kiasi gani''

2> Mungu alishughulikana ardhi ya Yeriko ili kumfungua Rahabu kutoka kwenye ukahaba.

          Joshua 6;1-5

>Je? Kwa nini kwa nini Mungu alishughulika na ardhi ya Yeriko badala ya kushughulika na tabia "ukahaba" wa Rahabu?

>Baada ya Rahabu kuachilia imani yake na kuitoa nyumba yake kama sadaka hatukuona tena akifanya ukahaba.

>Familia yake pamoja na mali zake zote zilifunguliwa

> Hapa tunaona kuwa tabia ya mtoto inaweza ikazima mafanikio ya familia nzima

>Rahabu alipokwama familia yake pia ilikwama sababu Rahabu alikuwa lango la familia yake

> Kuna tabia shetani hukuletea ili kukukwamisha usiweze kufikia kiwango fulani cha maisha ambayo Mungu amekupangia'

VITU GANI VILIVYOMFANYA RAHABU KUFUNGULIWA?

1>Unyenyekevuwa Joshua kukubali kuwakuna vitu vya kiroho vilivyopo katika ardhi ambavyo hakuvijua;

Joshua 5;13-15
Yule malaika alimwonyesha Joshua kuwa kuna kitu katika ardhi ndio maana alimwambia vua viatu vyako.

>Wakati mwingine ni mtihani mkubwa sana kwa Mtumishi/ viongozi wa kifamilia/ viongozi wa serikali/ na wakubwa wa namna yoyote ile kukubali au kunyenyekea kuwa kuna vitu asivyovijua| .

>Pamoja na kwamba Joshua alikuwa kiongozi alionesha unyenyekevu wa hali ya juu wa kutii na kufahamu kuwa kuna mambo hakuyafahamu.

2>Imani ya wana wa Israel juu ya kutii kuuzunguka ule mji
        Ebrania 11;30"imani"
>Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka

>Kuomba kwakutembea pasipo kuwa na imani haiwezi kukusaidia chochote hata ufanye nini..

>Ilikuwa kazi ngumu sana kwa wale wazee kukubali kuuzunguka ule mji kila siku kama wasingekuwana imani.

3>Wapelelezi kutumia ishara yaagano na Mungu ili kumhakikishia Rahabu ukombozi
               
Joshua 2;12;17-18
"funga kamba hii" hii kamba ilikuwa yao wakampa

>Naye alionesha kwadai wale wapelelezi alama ya uaminifu
Kamba ilisimama badala ya kifungo
Nyekundu ilisimama badala ya damu

>Hii inaonesha ya kwamba wale wapelelezi walikuwa katika kifungo na Mungu wao na walipompa kamba walikuwawanamaanisha kwamba naye "Rahabu" aliingizwa katika agano na Mungu na kuanzia hapo basi mtu yeyote angemtazama basi angetambua moja kwa mojakuwa yeye ni wa Mungu yupi..

>Ile kamba ilimuingiza Rahabu moja kwa moja katika agano na Mungu wa wana wa Israel.

4> IMANI YA RAHABU  ILIYOKUWA INAJISEMEA NDANI YAKE AMBAYO ILIMJENGEA IMANI NDANI YAKE.

>Hakutaka ukahaba uamue hatma ya maisha yake
          Luka 22;20

>Ile kamba  ilirudisha heshima kwa yule dada kama ambavyo damu ya Yesu inavyotuletea heshima tulipodharaulika."Damu ya agano"

Jipime uelewa wako Kiblia!

MIMI NI NANI?

MAELEZO

Jibu maswali yote 50.

1. Nilikuwa wa kwanza kupanda shamba la mizabubu. Mimi ni nani?
a) Adam
b) Nuhu
c) Kaini

2. Mimi ni mji ambao Paulo alikuta madhabahu yaliyoandikwa kwa “Mungu asiye julikana”. Mimi ni nani?
a) Rumi
b) Galatia
c) Athene

3. Nilikata upindo wa nguo ya Sauli. Mimi ni nani?
a) Daudi
b) Jonathani
c) Samweli

4. Mtume Paulo alitutoa mimi na Iskanda kwa shetani ili shetani atufundishe. Mimi ni nani?
a) Anania
b) Himenayo
c) Baraba

5. Kwangu Mungu alinipulizia pumzi ya uhai. Mimi ni nani?
a) Masikio
b) Pua
c) Roho

6. Mimi ni amri ya kumi. Mimi ni nani?
a) Usitamani
b) Usiibe
c) Usizini

7. Nilisema “mpatie kaisari vilivyo vyake Kaisari na mpatie Mungu vilivyo vyake Mungu”. Mimi ni nani?
a) Mtume Paulo
b) Yesu Kristo
c) Petro

8. Siku Yesu alipoizidisha mikate na samaki watu wakala wakasaza aliniuliza “tununue wapi mikate ili hawa wapate kula?”. Mimi ni nani?
a) Yohana
b) Andrea
c) Philipo

9. Mimi ni mahali ambapo Sarah alifia. Mimi ni nani?
a) Merabu
b) Kaanani
c) Kiriath-arba

10. Nilikuwa mtoto wa mwana wa mfalme lakini nilijichukulia kama mbwa mfu, lakini niliitwa tena na mfalme daudi nikala naye chakula mezani pake. Mimi ni nani?
a) Absalom
b) Mefiboshethi
c) Ahithopheli

11. Nilipofuka nilipokuwa nikienda Damasca. Mimi ni nani?
a) Petro
b) Timotheo
c) Paulo

12. Mimi ni kaka yake Isaka. Mimi ni nani?
a) Esau
b) Ishimael
c) Yakobo

13. Ni kitabu kitakatifu ndani yangu yamo mafundisho juu ya kuutawala ulimi. Mimi ni nani?
a) Waebrania
b) Luka
c) Yakobo

14. Shem, Hamu na mimi ni watoto wa Nuhu. Mimi ni nani?
a) Yafethi
b) Mesharck
C) Jafeti

15. Mimi ni baba yake Raheli. Mimi ni nani?
a) Isaka
b) Manoha
c) Laban

16. Ni kitabu kitakatifu ndani yangu pameandikwa “kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu”. Mimi ni nani?
a) Mhubiri
b) Methali
c) Zaburi

17. Ni kitabu kitakatifu. Ndani yangu yameandikwa maneno: “Mungu ni Roho, na wote wamuabuduo wapaswa kumuabudu katika roho na kweli”. Mimi ni nani?
a) Luka
b) 1 petro
c) Yohana

18. Ni baba yake mfalme  Yothamu, mfalme wa Yuda. Mimi ni nani?
a) Ahazi
b) Hezekia
c) Uzia

19. Kwa mujibu wa kitabu cha methali, Yule atakaye niche/fear atakuwa hai. Mimi ni nani?
a) Dhambi
b) Uovu
c) Bwana

20. Ni kitabu kitakatifu. Ndani yangu yameandikwa maneno: “na kama vile watu wanawekewa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu”. Mimi ni nani?
a) Waebrania
b) Waefeso
c) Wagalatia

21. Kaini aliniua. Mimi ni nani?
a) Shemu
b) Abneri
c) Habili

22. Ni kitabu kitakatifu, maneno yangu yanasema moyo uliochangamka ni dawa nzuri. Mimi ni nani?
a) Methali
b) Wimbo ulio bora
c) Zaburi

23. Mimi ni kitabu katika sura yangu ya kwanza ukoo wa Yesu umetajwa. Mimi ni nani?
a) Luka
b) Marko
c) Mathayo

24. Ni mmoja wa wafalme ambao walikosa usingizi. Mimi ni nani?
a) Nebukadneza
b) Yeroboam
c) Ela

25. Mimi ni mwanamke wa kwanza niliyempokea Kristo kwa sababu ya mtume Paulo. Mimi ni nani?
a) Persisi
b) Tryphaena
c) Lidia

26. Baada ya kukutana na mtu Fulani moyo wangu ulibadilika na nikaamua kurudiha vitu vyote nilivyowiwa. Mimi ni nani?
a) Luka
b) Daudi
c) Zakayo

27. Mfalme wa babeli. Mimi ni nani?
a) Nebukadneza
b) Yeoakimu
b) Dario

28. Nilikuwa ni miongoni mwa miji minne iliyotajwa katika Biblia iliyoharibiwa kwa sababu ya hasira ya Mungu. Mimi ni nani?
a) Seboimu
b) Filipi
c) Damasca

29. Nilisema Yesu ataitwa Immanuel (Mungu pamoja nasi). Mimi ni nani?
a) Luka
b) Mathayo
c) Marko

30. Mimi ndiye niliyeanza kuandika kitabu cha Yeremia. Mimi ni nani?
a) Baruku
b) Neri
c) Yeremia

31. Yakobo alinizika betheli. Nilikuwa mlezi wa rebeka. Mimi ni nani?
a) Leah
b) Debora
c) Zilipa

32.  Ni kamanda wa jeshi la Sauli. Mimi ni nani?
a) Abneri
b) Ahinoamu
c) Naamani

33. Nilimpa Adamu tunda lililokatazwa. Mimi ni nani?
a) Hawa
b) Kaini
c) Nyoka

34. Ni kitabu kitakatifu. Ndani yangu pameandikwa askari 185000 walikufa kwa usiku mmoja. Mimi ni nani?
a) Waamuzi
b) 2 wafalme
c) 1 samweli

35. Ni kitabu kitakatifu. Ndani yangu yameandikwa maneno: “kesheni basi kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu”. Mimi ni nani?
a) Luka
b) Mathayo
c) Matendo ya mitume

36. Ni kitabu kitakatifu. Ndani yangu yameandikwa maneno: “kwa jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”. Mimi ni nani?
a) Mathayo
b) Luka
c) Yohana

37. Nilisema “kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana”. Mimi ni nani?
a) Yohana
b) Petro
c) Paulo

38. Nilimuoa dada yangu (binti wa baba yangu ila sio wa mama yangu). Mimi ni nani?
a) Lutu
b) Ibrahim
c) Labani

39. Mimi ni pango. Ndani yangu Daudi alijificha alipokuwa anamkimbia Sauli. Mimi ni nani?
a) Megido
b) Merare
c) Adulamu

40. Mimi ni mkate ambao Mungu aliushusha kutoka mbinguni ambao ulikuwa mweupe kama chembe za mtama na tamu yake kama maandazi yaliyotengenezwa kwa asali. Mimi ni nani?
a) Matzo
b) Pita
c) Manna

41.  Ni mmoja wa mitume, nilichukua nafasi ya Yuda msaliti. Mimi ni nani?
a) Barnaba
b) Simion
c) Mathiya

42.  Kila siku niliomba na kutoa sadaka kwa ajili ya kuwatakasa watoto wangu. Mimi ni nani?
a) Stefano
b) Ibrahim
c) Ayubu

43. Zaidi ya watu 40 waliapa  kutokula wala kunywa hadi watakapo niua. Mimi ni nani?
a) Paulo
b) Yakobo
c) Petro

44.  Mimi ni baba yake mfalme Ahabu. Mimi ni nani?
a) Omri
b) Zimri
c) Tibini

45.  Mazungumzo kati yangu na mwenzangu tukiwa njiani kuelekea Emau wakati Yesu amefufuka, yalikuwa ni ya kuvutia sana, japo katika agano jipya ni jina langu tu ndiyo lililotajwa. Mimi ni nani?
a) Kleopa
b) Petro
c) Dema

46. Ni mmoja wa wakamwana (daughter-in-law)  wa Naomi. Mimi ni nani?
a) Rebeka
b) Raheli
c) Orpa

47. Nilikuwa ni mchungaji nilikutana na mme wangu mtarajiwa nilipoenda kunywesha kondoo maji kisimani. Mimi ni nani?
a) Rebeka
b) Ruthi
c) Raheli

48. Nilitupwa kupitia dirishani kwa amri ya kapteni na mwili wangu uliliwa na mbwa. Mimi ni nani?
a) Yezebeli
b) Rahabu
c) Bathsheba

49. Mimi ni mtoto wa kwanza wa Nahori (ndugu yake Ibrahimu). Mimi ni nani?
a) Usi
b) Buzi
c) Hazo

50.  Mimi ni baba yake Yohana mbatizaji. Mimi ni nani?
a) Zakaria
b) Manoa
c) Malaki.