IFANYE/SET KOMPYUTA YAKO IJIANZISHE YENYEWE AU KUZIMA KWA MUDA UTAKAO
Ukiwa na computer yako unaweza kuset izimime baada Muda flani. Au kuianzisha tena baada ya muda flani. Yani kwa mfano unataka kuiset izimike baada ya masaa mawili basi waweza set kwa kutumia CMD. Fuata hatua zifuatazo kuset kompyuta yako:-
1.kuipata CMD bonyeza alama ya window bila kuachia na R (WIN+R)
2. Kitatokea kibox cheupe cheupe upande wa kushoto mwisho mwa screen yako
3. Katika hilo box andika cmd.exe na ubonyeze ENTER
4.kitakuja kibox cheusi chenye maandishi meupe
5. Utakua umemaliza kuipata CMD. Ndani ya hiyo cmd andika shutdown /t 60 /s Bonyeza ENTER.
/t=time
/s=shutdown
60 ni muda unaotaka kompyuta yako izime.
Kumbuka muda unauweka kwa mfumo wa seconds yani ukitaka kompyuta yako izime baada ya dakika moja unaweka 60 ikiwa na maana kwamba dakika 1=60 sekunde.
KOMPYUTA KUJIANZISHA KWA MUDA UNAOUTAKA YANI KUJI RESTART/REBOOT
Hata hivyo waweza ianzisha kompyuta yako kwa kutumia CMD kuipata cmd fuata hatua ya 1 hadi ya 4 hapo juu. Kisha andika
shutdown /t 60 /r kisha bonyeza ENTER
/r ikiwa na maana ya restart
Pia ukitaka ku logoff
Log off(/l)
shutdown t/ 60 /l
Ukitaka izime,logoff,restart kwa muda huo huo bila sekunde au muda uliopangwa.
shutdown/s kisha ENTER
shutdown/r Kisha ENTER
Shutdown/l kisha ENTER
**********MWISHO********
Mshirikishe na mwenzio usisahau kumwambia endelea kufuatilia maujanja zaidi
Visit my blog and learn more!
No comments:
Post a Comment