Shaloom!
Bwana Yesu Kristo Asifiwe milele kwa kutupa nafasi ya kuuona na kuuingia mwaka huu mpya!
Mioyo yetu imejaa shukrani sana kwa Mungu, kwa sababu ya neema yake katika Kristo Yesu; inayotupa kuendelea kumtumikia katika kizazi cha nyakati zetu hizi.
Jambo ambalo Roho Mtakatifu ameliweka kwa uzito wa kipekee ndani ya mioyo yetu katika mwanzo huu, wa mwaka huu mpya – ni juu ya uhusiano wa utumishi na uaminifu!
Kuna baraka za kuwa mwaminifu na kuna gharama za kutokuwa mwaminifu katika kumtumikia Mungu kwenye eneo lolote analokupa – hata kama si katika kuhubiri.
Elewa maana ya neno Mwaminifu.
Neno hili “Mwaminifu” linatokana na neno la kiingereza lisemalo “Faithful”. Na ukifuatilia neno hili “uaminifu”, utaona limetokana na neno la Kiingereza la “Faithfulness”.
Kwa tafsiri ilivyo nyepesi, neno “faithful” na neno “faithfulness” – ni maneno mawili mawili lakini yaliyoungwa pamoja.
“Faithful” ni Full of Faith na Faithfulness “Fulness of Faith”. Kwa tafsiri ya Kiswahili maana yake “kujaa Imani”. Kwa hiyo, mtu aliye mwaminifu au aliye “faithful” ni yule aliye – jaa Imani au “full of faith”.
Nasi tunajua ya kuwa kutokana na Warumi 10:17 – “Imani, Chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo”. Hii ina maana ya kuwa mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatekeleza maelekezo ambayo Mungu amempa. Kwa mantiki hii mtumishi mwaminifu ni yule ambaye anakijua alichoambiwa na Mungu akifanye – na amekifanya alivyotakiwa!
Mistari Kadhaa ya kutafakari
juu ya Utumishi na Uaminifu.
Mathayo 24:45 – 47 inasema hivi:
“Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote”.
Luka 16:10 inasema hivi:
“Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia”.
Luka 16:12 inasema hivi:
“Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?”.
Luka 19:17 inasema hivi:
_“Akawaambia, vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi”._
1Wakorintho 4:1,2 inasema hivi:
_“Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndivyo mtu aonekane kuwa mwaminifu”._
Unaona nini ndani ya mistari hiyo?
Ni maombi yetu kwa Mungu ya kwamba atakupa uwezo ndani ya moyo wako kuona baraka na umuhimu wa uaminifu katika kufanya kile ambacho anakupa kufanya kwa mwaka huu.
Ni dhahiri ya kuwa ukipoteza uaminifu, pia unapoteza na kuyakosa mengi ambayo Mungu ameyaunganisha na uaminifu.
Semina zilizo mbele yetu.
Tunaamini Mungu atakupa kuhudhuria au kutusikiliza “live” semina zetu ambazo tunatarajia kuzifanya hivi karibuni.
Tarehe 21 January tutakuwa Dar es Salaam , Ukumbi wa Diamond Jubilee Kwenye semina ya Kupanda na Kuvuna.
Tuzidi kuombeana. Kumbuka Yesu Kristo karibu anarudi kuja kulichukua kanisa lake; kwa hiyo tuzidi kufanya bidii kukifanya na kukimaliza, kila anachotuagiza kufanya.
Ni sisi katika utumishi wa Kristo
Christopher na Diana Mwakasege.
Asant mtumishi Mungu akuongeze
ReplyDeleteAMEEN
ReplyDeleteBulk Fresh Fullz/Pros/Leads Available
ReplyDeleteHigh Credit Scores Fullz 700+
CC Fullz (USA/UK/CANADA)
SSN DOB DL Fullz
Office365 Leads
Dumps With Pin
Business EIN Fullz
Leads for Tax Return/PUA USA
ICQ/TG - @killhacks
WA - +92 317 2721122
Email- exploit dot tools4u at gmail dot com
All Spamming & Hacking Tools
Carding Methods/Loan Methods
Mailers/Senders/Shells/Brutes
C-panels/RDP's/SMTP's
Onion Web Links
I.p's/Proxies/Server I.P's
Combos/Premium account Logs
Fr**d B**le 201/2022/2023 Updated
ICQ- 752822040
Telegram - @killhacks