Thursday, 3 March 2016

Ajifungulia kwenye beseni, nesi adundwa!

Ajifungulia kwenye beseni, nesi adundwa

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo

SUZAN Anatory aliyeenda kujifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana-Butimba na watoto wake wawili kufariki, kumesababisha Mariam Mkankule, nesi wa hospitali hiyo kudundwa.

Hatua hiyo iliibua vurugu na kusababisha Jeshi la Polisi Jijini Mwanza kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi kutuliza fujo hizo.

Tukio hilo limetokea leo katika hospitali hiyo baada ya muuguzi, Mariam kudaiwa kukataa kumpatia huduma mama huyo mjamzito.

Inaelezwa kuwa, chanzo kikubwa cha kutokea kwa vurugu hizo ni baada ya muuguzi huyo kumtolea lugha chafu na za vitisho mgonjwa huyo kitendo ambacho kiliibua hasira kwa wagonjwa wengine.

Pia inaelezwa kuwa, wakati muuguzi huyo akiendelea kutoa lugha hizo, Suzan alihisi maumivu na kwenda msalani ambako alijifungulia kwenye beseni watoto mapacha wawili ambao walikufa papo hapo.

Inadaiwa kuwa, baada ya wagonjwa kuona hali hiyo walianza kufanya vurugu muuguzi huyo, kabla ya polisi kufika na kupiga mabomu ya machozi na hatimaye kumwokoa muuguzi huyo.

Hata hivyo, Mariam na wenzake watano wanashikiliwa na polisi mjini hapa kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo.

Baadhi ya wagonjwa waliokuwepo katika hospitali hiyo na kushuhudia wamesema kuwa, muuguzi huyo alikuwa akiwaambia haogopi chochote.

Taabu Abdallah amesema, “mimi nilikuwepo hapa na niliona kila kitu, yule mjamzito alifika hapa kwa lengo la kujifungua na akamueleza muuguzi muda wake umefika lakini alikataa kumhudumia.”
Amesema, wakati wakivutana huku muuguzi huyo akidai kwamba haogopi chochote na hawezi kumhudumia mama huyo.

Suzan amesema kuwa, msaada kukosa kutoka kwa wauguzi ndio chanzo kilichosababisha kufa kwa watoto wake.

Amesema, sababu zilizokuwa zikitolewa na muuguzi huyo kwamba siku zake za kujifungua hazijafika sio kweli.

“Mimi baada ya kuvutana na huyo muuguzi, nilikwenda msalani baada ya kujisikia vibaya nikiwa najisaidia haja ndogo ghafla nilijifungua mtoto wa kwanza ambaye alikuwa ametanguliza makalio.

“Pia mtoto wa pili nilijifungua akiwa mzima lakini msaada kutoka kwa wauguzi ndio ulisababisha huyu mtoto akafariki na kama angepata msaada asingefariki,” amesema Suzan.

Magesa Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema tume imeundwa kuchunguza suala hilo na kwamba hatua zitachukuwa juu yake pamoja na wenzake pale itakapobainika kuhusika kwao.

“Muda huu tume hii iliyoundwa wakati ikiendelea kuchunguza suala hili, hatua zaidi zitaendelea kuchukuliwa,” amesema Mulongo.

Hata hivyo, Mulongo aliwasimamisha kazi madaktari Ngusa Masanja, Vivian Moshi na Mariam kwa uchunguzi zaidi.

Kikwete aishukuru symbion power ya Marekani

Dar es Salaam. Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ameishukuru Kampuni ya Symbion Power ya Marekani kwa kujenga kituo cha ukuzaji wa michezo kilichoko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.

Kikwete aliyasema hayo juzi katika uzinduzi wa ligi ya mpira wa kikapu ya vijana ya NBA Basketball League iliyofanyika kwenye kiwanja hicho.

Kikwete aliwataka vijana wajitume na wawe na nidhamu kipindi chote watakachokuwa wanajifunza kupitia katika kituo hicho.

Viongozi walioudhuria katika uzinduzi huo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Symbion Power, Paulo Hinks, makamu rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la NBA Afrika, Amadou Gullo, mchezaji wa zamani wa WNBA, Allison Feaster na Mbunge wa Ilala Mussa Zungu.

Akizungumza baada ya ufunguzi wa ligi hiyo, Gullo alisema wamefurahi kuzindua rasmi msimu wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana nchini Tanzania.

‘Ni matumaini yetu kuwa hii ligi mpya iliyoanzishwa inahamasisha wavulana kwa wasichana kujibidisha na kuhamasisha wengine kuja na kufurahia mchezo wa mpira wa kikapu hapa kwenye kituo,” alisema Gullo.

Feaster alieleza kufurahishwa na vijana wengi kwani wana ari ya kucheza mchezo huo.

“Ni heshima kubwa kwangu mimi kuwa sehemu ya ufunguzi wa ligi hii ya vijana nchini Tanzania,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Symbion Power alisema, Shirikisho la Mpira wa Kikapu (NBA) na Symbion wameanzisha ushirikiano mkubwa barani Afrika unaolenga kukuza mpira wa kikapu.

“Ni jambo la kufurahia kuwa sehemu ya ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana. Ni faraja kuona hilo limtokea kwa kuwapo kituo cha michezo cha Symbion jijini Dar es Salaam,” alisema Hinks.

SERIKALI KUJIPANGA VINGUNGUTI

Serikali imejipanga kujenga machinjio ya kisasa katika eneo la Vingunguti  Jijini Dar es Salaam ili kuondoa changamoto zilizopo machinjioni hapo ikiwa ni pamoja na kulinda afya za wachinjaji na walaji wa nyama.
.
Akiongelea mipango hiyo kwa njia ya simu Msemaji wa Manispaa ya Ilala Bi.Tabu Shahibu amesema Halmashauri iko katika mchakato wa kutangaza zabuni kwa makampuni yatakayoweza kujenga machinjio hayo kwa kiwango kinachotakiwa.

“Tupo katika harakati za kutafuta mkandarasi wa kujenga machinjio na hivi karibuni tutatangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi huo”

“ Napenda kuwahakikishia kwamba tutafanya jitihada zote za kumpata mkandarasi mapema ili tuanze mapema ujenzi huu wa machinjio mapya na kuondokana na changamoto zinazokabili machinjio yaliyopo”Alisema Bi Tabu.

Aidha, Bi Tabu Shaibu amesema kuwa kabla ya kujenga machinjio mapya wanaendelea na ujenzi wa mabanda ya machinjio, njia za kushushia ng’ombe ,bucha na kupanua eneo la machinjio na wameshapima na kufanya tathimini ya gharama ambazo zitatumika katika marekebisho hayo.

Mpango huu umekuja mara baada ya ya agizo la mawaziri, akiwemo Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla na Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi TAMISEMI MHE. George Simbachawene walipotembelea machinjio ya Vingunguti Januari 2 mwaka huu.

Machinjio ya Vingunguti yalianza kutumika tangu miaka ya 1950 ikiwa inahudumia idadi ya watumiaji wa mazao ya wanyama waliokuwa kwa wakati ule. Machinjio hayondio bado  yanatumika hadi sasa wakati idadi ya watumiaji wa mazao ya nyama wameongezeka  hivyo kukumbana na changamoto mbalimbali. Ili kukabiliana na changamoto hiyo Serikali imepanga kuyarekebisha yaliyopo na kujenga mapya na ya kisasa.

Wednesday, 2 March 2016

RIFARO AFRICA SIO.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
ISO 9001:2008 CERTIFIED

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUTUMIKA RASILIMALI NAMBA MAALUMU 15420 NA KAMPUNI YA RIFARO BILA CHETI CHA MATUMIZI YA NAMBA CHA MAMLAKA YA MAWASILIANO


1.0   UTANGULIZI

1.1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni taasisi ya Serikali yenye jukumu la kusimamia huduma za Sekta ya Mawasiliano na Utangazaji nchini, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali namba kwa mawasiliano na anwani kuhakikisha matumizi sahihi.

1.2. ​Katika siku za hivi karibuni, Mamlaka imeona taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano. Yafuatayo ni maelezo ya Mamlaka kuhusu taarifa hizo:

1.3.​Mnamo tarehe 28 Julai, 2014 Mamlaka ilitoa kwa RIFARO AFRICA LIMITED Cheti cha Matumizi ya Rasilimali Masafa kwa ajili ya huduma za ziada za Mawasiliano kupitia SMS (VAS SMS CODE) namba maalumu 15420 kutumika katika kutengeneza mfumo wa Mawasiliano wa SMS kuunganisha na kupokea taarifa za mawakala wao wa kuuza na kusambaza muda wa maongezi kupitia wavuti yao (website);

1.4.​Mnamo tarehe 27 Julai, 2015 Cheti hicho kilimalizika muda wake na Kampuni ya RIFARO Africa Limited haikuomba kuongeza muda wa matumizi wa rasilimali namba maalumu 15420. Kuendelea kutumia rasilimali namba hiyo bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano ni ukiukwaji wa Kanuni ya 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano - (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

2.0   AMRI YA UTEKELEZAJI

Mnamo tarehe 24th Februari, 2016, Mamlaka ilitoa Amri ya Utekelezaji kwa kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kwa mujibu wa Kifungu cha 45 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania sura ya 172 kama ilivyorekebishwa na Kifungu cha 179 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta, na kuimauru kampuni hiyo kufika mbele ya Mamlaka ya Mawasiliano kujitetea kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuvunja na kukiuka Kanuni namba 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila Cheti cha kuruhusu matumizi yake kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

3.0 ​KUSIKILIZA SHAURI

​Katika kusikiliza shauri la utetezi wa RIFARO AFRICA LIMITED:

1. Walikubali kupewa kibali cha kutumia rasilimali namba maalumu 15420 na kukubali pia kuwa matumizi yake yaliisha muda wake mwezi Julai, 2015;
2. Aidha walikubali kuwa Cheti Cha Matumizi ya Rasilimali Namba Maalumu 15420 kilipokwisha muda wake hawakuomba kuongezewa muda wa matumizi yake;
3. Hali kadhalika walikiri wameingia mkataba wa kibiashara na Kampuni ya Zanzibar Telecom Limited (ZANTEL) kwa ajili ya huduma ya Ezzy Pesa kama mtoa huduma mkubwa wa kampuni hiyo (mobile money super dealership).

4.0 ​MAAMUZI YA MAMLAKA

RIFARO AFRICA LIMITED imekuwa ikitumia rasilimali namba maalumu (VAS SMS CODE) 15420 bila cheti cha Mamlaka kuwaruhusu kufanya hivyo kinyume na Kanuni ya 17 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

​Baada ya kutafakari utetezi wa Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED na matokeo ya utetezo wao, Mamlaka inatoa maamuzi kama ifuatavyo:

1. RIFARO AFRICA LIMITED kulipa kwa Mamlaka faini ya shilingi milioni 10 (TZS 10,000,000) kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano; na

2. RIFARO AFRICA LIMITED iache mara moja kutumia rasilimali namba maalumu 15420 kwa kuwa haina ruhusa ya kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuarifu umma kuwa RIFARO AFRICA Limited haina leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Kampuni hii ilikuwa na Cheti cha matumizi ya rasilimali namba maalumu 15420 ambacho kiliisha muda wake tangu mwezi Julai 2015.

Dkt. Ally Y. Simba
MKURUGEZI MKUU

02/03/2016

DKT. MAGUFULI AFANYA …

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano
hususani katika masuala ya kiuchumi.

Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.

Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na
miradi ya maendeleo inaharakishwa.

"Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi
wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa
tumetengana" Amesisitiza Rais Kenyatta.

Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina
kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda
utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.

"Wazee wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo" amebainisha Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga mahusiano na
ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi
wake.

Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka
Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania
itakapoongeza uzalishaji wa umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya,
halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake
Tanzania.

Kabla ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuzidisha
mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia
kuwa serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani
"Standard Gauge" ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.

Rais Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga
kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda
inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.

Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU Arusha
02 Machi, 2016

Tuesday, 1 March 2016

MATOKEO FORM IV 2015

MATOKEO FORM IV 2015

HEKA HEKA

March 1 2016 kwenye Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea hekaheka iliyotokea Magomeni Dar es salaam hii ni baada ya Mtoto kupigwa na Mama anayeishi naye, tukio ambalo limepelekea mpaka majirani na mjumbe wa eneo hilo kuingilia kati.

‘Naitwa Pilli Mdidi mjumbe wa shina namba 12 nakaa mtaa wa Kiembeni nilivyopata taarifa nimeacha kupika, maana mimi ni Mama Lishe ndio nimefika hapa ndio nikaadisiwa kwamba huyu mtoto katoka ndani analia kufika juu akaanguka mpaka kuzimia ikanibidi niende kwa mama anayeishi naye kumuhoji  kwanini kampiga yule mtoto‘>>>Mjumbe

‘Mimi nafanya biashara huko Mbeya yule sio Msichana wa kazi  nilikuwa naenda kwa Mama yake ndio tukawa kama ndugu huyu Msichana natoka naye Chombe ni mdogo wangu namfundisha kupika sasa leo kuna kitu kaniudhi nikamchapa, anatabia ukimchapa anajidondosha chini‘>>>Mama aliye mpiga mtoto