Wednesday, 31 August 2016

Kupatwa kwa jua, chukua tahadhari!

Tukio la kupatwa kwa jua nchini Tanzania kushudiwa!

Tahadhari imetolewa kwa wakazi wa mikoa ambayo itashuhudia kupatwa kwa jua kuwa kutazama jua moja kwa moja bila kutumia kifaa chochote kunadaiwa kuwa na madhara kwa mtazamaji kutokana na mionzi ya jua hilo.

Kupatwa kwa jua kunatarajiwa kutokea katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ya Njombe wilaya ya Wang'ing’ombe katika kijiji cha Litundu, Mbeya wilayani Mbarali katika kijiji cha Mpungarelini na mkoani Katavi ambako kupatwa kwa jua kutaonekana vizuri kwa zaidi ya asilimia 97.

Tahadhari hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani humo ikiwa zimebaki siku chache kutokea kwa tukio hilo la kihistoria.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa kuna jitihada mbalimbali zinazofanywa na halmashauri ya Waning'ombe kwa ajili ya kuweza kupata vifaa mahususi kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo bila kuacha madhara yoyote.

Tukio hilo la kupatwa kwa jua lilizinduliwa Julai 10 mwaka huu katika kijiji cha Litundu kwa mkoa wa Njombe ambapo macho ya dunia nzima kitalii yatatazama katika eneo hilo.

Polisi wapiga kambi Ofisi ya Chadema!

Polisi wapiga kambi Chadema

NI mwendo wa doria. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya askari polisi kulazimika kupiga kambi katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zilizopo Mtaa wa Ufipa, Dar es Salaam.

Polisi hao tangu jana asubuhi walikuwa wakifanya doria katika eneo hilo huku wengine wakizingira ofisi za chama hicho wakiwa wamevaa kiraia.

Kutokana na hali hiyo, MTANZANIA ilituma timu ya waandishi ambao kutwa nzima ya jana waliwashuhudia askari polisi wakiwa nje ya ofisi za chama hicho na wengine wakiwa ndani ya magari ya doria.

Hatua hiyo ilionekana kuzua taharuki kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa juu wa chama hicho ambao walijikuta wakishindwa kufanya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kwa hofu ya kuzuka vurugu.

Ilipotimu saa tano asubuhi, timu ya walinzi wa Chadema ‘Red Brigade’ waliongezeka na kusimama nje ya ofisi za makao makuu huku wakionekana kuwa tayari kwa lolote, ikiwamo kujihami kwa kuwalinda viongozi wao; mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye ambao waliwasili katika ofisi hizo kwa ajili ya kikao.

Kikao hicho kilikuwa ni cha mwandelezo baada ya kile cha juzi kushindwa kumalizika na baadhi ya viongozi wa chama hicho kukamatwa na polisi.

Pamoja na hali hiyo, ilipotimu saa 9 alasiri, viongozi hao wakiongozwa na Lowassa walitoka nje na kuelezwa kuwa kikao kimeshindwa kufanyika kwa kuwa hali ya usalama si nzuri, hasa baada ya kuonekana askari kanzu wakiingia ndani ya ofisi hiyo na wengine kujifanya ni wanachama wa chama hicho.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na Katibu Mkuu, Dk. Vicent Mashinji, walilazimika kuondoka mapema na kwenda katika kikao cha pamoja kati yao na viongozi wa dini ili kutafuta mwafaka, kuhusu Operesheni Ukuta inayotarajiwa kufanyika kesho licha ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi.

Kikao hicho cha viongozi wa dini kilichofanyika katika Hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine kilijadili kwa kina mkwamo wa kutafuta suluhu kati ya viongozi wa Chadema na Serikali kuhusu kuzuiwa maandamano ya kesho.

MTANZANIA ilipomtafuta Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Mashinji ili kupata ufafanuzi kuhusu kuzingirwa kwa ofisi zao na maofisa wa polisi, alikiri kutokea kwa hali hiyo.

“Ni kweli tumeahirisha mkutano wetu wa Kamati Kuu mpaka hapo baadaye, Ofisi zetu za Makao makuu zilizingirwa na askari wa kila aina, wengine walivaa baraghashia, kanzu na kila aina ya nguo kwa lengo la kuvunja na kutawanya mkutano wetu wa ndani, tumeuahirisha mpaka wakati mwingine, tutawajulisha.

“Askari hao wamekuwa wakipiga kambi katika ofisi zetu kwa muda wa wiki sasa, lakini kadiri siku zinavyokwenda idadi yao inazidi kuongezeka kama ilivyokuwa leo (jana),” alisema Dk. Mashinji.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa wajumbe wa Kamati Kuu walikutana ili kujadili mambo mbalimbali ikiwamo suala la maandamano yanayotarajiwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho.

VIONGOZI WA DINI

Viongozi wa dini nchini wameendelea kukuna vichwa kutafuta suluhu kati ya Serikali na vyama vya siasa vinavyojiandaa na Operesheni Ukuta iliyopangwa kufanyika kote nchini kesho.

Viongozi hao walijichimbia jana Hoteli ya Courtyard katika kikao cha siri ambacho kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, Katibu Mkuu wake, Mashinji na mawaziri wakuu wa zamani; Sumaye na Lowassa.

Taarifa za ndani zinasema kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana aliwasili hotelini hapo saa nne asubuhi, lakini aliondoka punde baada ya kupokea simu ambayo inadaiwa alipigiwa na Rais Dk. John Magufuli.

Kikao hicho kilichoanza saa mbili asubuhi hadi saa tisa alasiri ni cha tatu kufanyika, ambacho mbali kuhudhuriwa na viongozi dini, pia kilihudhuriwa na vyama vitano vyenye uwakilishi bungeni huku agenda kuu ikiwa ni hali ya kisiasa nchini.

Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti Mwenza wa mkutano huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema kuwa ulimalizika salama na kukubaliana na kwamba watatoa taarifa rasmi ya kikao hicho leo kwa umma.

“Kikao chetu tunamshukuru Mungu tumemaliza salama na kwa pamoja tumeweza kukubaliana mambo mbalimbali, ikiwamo ya hali ya kisiasa nchini, wabunge wa upinzani kususia vikao vya Bunge pamoja na Operesheni Ukuta, ambayo tutayazungumza kwa waandishi wa habari kesho (leo) ili Watanzania waweze kuyajua,” alisema Sheikh Alhad.

Pamoja na mambo mengine, alisema kwa sasa hali ni nzuri na wanaamini mkutano huo utaweza kurudisha hali ya utulivu, umoja na mshikamano kwa wananchi wote bila ya kujali tofauti zao za kisiasa, dini au kabila.

KAULI YA MASAJU

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa mkutano huo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo, aliliambia MTANZANIA kuwa Serikali iwaache wafanye mambo kwa wakati wanaoona unafaa.

Dk. Shoo alikuwa akizungumzia kauli iliyotolewa juzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, akiwataka viongozi wa dini kuliombea taifa lisiingie kwenye uvunjifu wa amani kutokana na Operesheni Ukuta na kwamba huu si wakati mwafaka wa kukaa meza ya majadiliano.

“Sisi tunafanya vitu kwa wakati tunaoona unafaa, siyo yeye atuamuru cha kufanya, namuomba ayaache haya mambo hivi hivi kwani tunaujua wajibu wetu kwa Serikali na wananchi ambao ni waumini wetu.

“Kwa sasa haya mambo tuyaache yabaki kama yalivyo, sisi tunazungumza kuhusu masuala hayo hayo na tumefikia mahali pazuri, mtayasikia kesho (leo), bado kikao hakijaisha,” alisema Dk. Shoo.

Monday, 29 August 2016

Lema agoma kula!

Lema Aendelea Kugoma kula akiwa mahabusu.

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ameendelea kugoma kula kwa siku ya tatu mfululizo tangu alipokamatwa Oktoba 26 mwaka huu, nyumbani kwake mjini hapa, akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.

Lema alikamatwa siku hiyo saa 12 alfajiri akiwa nyumbani kwake, Njiro,  na hadi sasa anashikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha polisi mjini Arusha.

Kutokana na kuendelea kugoma kula, Wakili wake, John Mallya amesema leo saa sita mchana atakwenda Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kufungua kesi ya kutaka mteja wake afikishwe mahakamani.

Malya jana alisema katika kesi hiyo atashirikiana na Chadema kuwashtaki mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, Mkoa wa Arusha.

Tangu mbunge huyo akamatwe amegoma kula kwa  kile anachodai kupinga udhalilishwaji aliofanyiwa na polisi wakati wa kukamatwa.

Pia, Lema anasema alinyanyaswa mbele ya watoto wake nyumbani kwake huku wakijua yeye ni kiongozi na amechaguliwa na wananchi.

Neema, mkewe Lema,jana alithibitisha kwamba  mumewe amegoma kula.

“Anaendelea kugoma kula mpaka sasa kwa sababu  hata sasa nimetoka polisi asubuhi kumpelekea chakula, lakini amekataa kula.

“Lakini nilipouliza pale polisi kuwa wanampeleka lini mahakamani, nilijibiwa wanaendelea kumhoji,”alisema Neema.

Juzi, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa alihojiwa dhidi ya matamshi ya uchochezi na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika   uchunguzi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, Lema anatuhumiwa kuwachochea wakazi wa Arusha kuandamana Septemba mosi, mwaka huu kuhamasisha kile kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).

Thursday, 25 August 2016

Mwanafunzi ampa mimba mwalimu wake, atuzwa milioni 600.

Mwanafunzi atunzwa M600 kwa kumpachika mimba mwalimu.

Mahakama moja ilimtunuku mwanafunzi Sh600 milioni kwa kumtia mimba mwalimu wake akiwa na miaka 16

–Mwalimu huyo alifungwa kwa mwaka mmoja lakini alikaa jela kwa miezi sita pekee. Binti wao ana miaka mitatu

Mwanafunzi mmoja California, Marekani, atatunzwa Sh600 milioni kwa kuhusika kimapenzi na mwalimu wake na kumtia mimba.

Mwalimu huyo Laura Whitehurst, 31, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo akiwa na miaka 16 ambapo alipata mimba na kumzalia binti miezi tisa baadaye.

Hukumu hiyo ilitolewa miaka mitatu baada ya Whitehurst kutambulika kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wake.

Mahakama iliambiwa kuwa mwalimu huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wengine wawili ambao hawakutambulishwa.

Ilisemekana mwalimu huyo alikuwa akishiriki ngono darasani akiwa na mvulana huyo, na nyumbani kwake kwa mwaka mmoja kabla ya tukio hilo kujulikana.

Mwanafunzi huyo alidai kuwa usimamizi wa shule yake, Redlands Unified School District, ulikuwa ukijua kuhusu uhusiano huo lakini ukakataa kuchukua hatua yoyote.

“Ushahidi unaonyesha kuwa usimamizi ulijua vyema kuhusiana na suala hilo lakini ukakataa kuchukua hatua yoyote,” alisema wakili wa mwanafunzi huyo Vince Finaldi.

Whitehurst alifungwa mwaka mmoja 2013 kuhusiana na kisa hicho lakini alikaa jela kwa miezi sita pekee kwa kuonekana kuwa na tabia njema.

Have a nice day all my viewers!!

Wednesday, 24 August 2016

UDOM na wataalamu wa mafuta na gesi.

UDOM kuongeza wataalam wa mafuta na gesi.

Chuo Kikuu cha UDOM kimeandaa mtaala wa elimu kwa ajili ya shahada ya uzalimili katika sekta ya mafuta na gesi ili kutoa watalaam wengi zaidi wa masuala ya athari za kimazingira zinazoweza kusababishwa na uchimbaji wa rasimali hiyo.

Kaimu Makamu mkuu wa chuo hicho Dkt. Peter Msofe amesema hayo mjini Dodoma katika uifunguzi wa mkutano wa wadau wa elimu kutoka nchi za Uganda na Tanzania wanaoandaa mtaala wa unaolenga kuzinufaisha nchi mbalimbali za Afrika.

Dkt. Msofe amesema kuwa mtaala huo umekuja wakati muafaka wakati Tanzania imegundua gesi nyingi hivyo kuna uhitaji wa watalaam ambao wataweza kujua faida na athari za rasimali hiyo kimazingira na kiafya nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitivo cha Sayansi Asilia na Hisabati Said Ali Vuai, amesema kuwa mtaala huo unatarajiwa kuanza katika mwaka wa masomo 2017/2018.

Together we can, yes we can!

Saturday, 20 August 2016

Fanya haya ufikie malengo yako!

Mambo 8 Yatakayosaidia Kufikia Malengo Yako.

Kila wakati wengi wetu katika maisha, ni watu wa kujiwekea malengo. Mara nyingi huwa tunaweka malengo haya,  kwani kwa kujiwekea  malengo hayo ndiyo hutuongeza na kutuhakikishia  kule tunakotaka kufika kimafanikio. Kwa kujua hili, karibu kila mtu msaka maendeleo, kwake malengo huwa ni kitu cha lazima sio cha kuuliza tena.

Lakini hata hivyo, pamoja na kujiwekea malengo mazuri,  kwa bahati mbaya sana tena wengi wetu huwa bado hatuyafikii malengo hayo. Hapo ndipo maswali mengi sana ya kwanini huanza kuibuka vichwani kwetu? Kama mambo ni hivyo usikate tamaa, Kwa kufatilia makala haya utajifunza juu ya mambo muhimu yatakayokusaidia kufikia malengo yako.

1. Yajue malengo yako vizuri.                                                                      
Huwezi kufanikiwa kama huyajui malengo yako vizuri. Ni lazima malengo yako yawe ya wazi kwako. Ikiwezekana yaandike vizuri kwenye karatasi nayaweke sehemu inayoonekana. Kwa mafano kama lengo lako ni kufanya biashara ya ‘stationary’ liandike lengo hilo mahali na lionekane.  Kama pia lengo lako ni kufungua duka weka wazi lengo lako kwa kuliandika.

Watu wengi mara nyingi wanashindwa kufikia malengo yao kwa sababu malengo yao yanakuwa sio wazi sana. Siku zote mawazo yetu ya ndani hutusaidia kufikia malengo yetu, kama malengo hayo yana eleweka. Kinyume cha hapo, utakaa sana kusubiri malengo yatimie lakini wapi. Hivyo siri ya kufikia mafanikio jitahidi kuweka malengo yako wazi.

2. Jitoe kikamilifu.
Siri ya mafanikio ni kujitoa kikimalifu kwa kile unachokifanya. Hata malengo yako ambayo umeshajiwekea na yako wazi ili kuweza kuyafikia ni lazima ufanye juu chini kujitoa kikamilifu na wala sio nusunusu. Ikiwa utakuwa unayaendea malengo yako, huku ukiwa hujaamua kujitoa kikamilifu tambua ikatokea umeshindwa usishangae hapo kwa hilo.

Kwa kuwa unanajua malengo yako nini, kama kuna kazi unatakiwa kuifanya ifanye kweli kwa nguvu zako zote bila kuchoka. Weka juhudi na maarifa yako yote na kuhakikisha unajitoa kweli. mafanikio yako hayatakuja kirahisi eti kwa kufanya kazi kilegevu. Jitoe kwa kupiga kazi kwelikweli mpaka kieleweke.

3. Kamilisha majukumu yako kila siku.
Unaweza ukawa unayajua malengo yako na umejitoa kikamilifu, lakini huwezi kuyafikia malengo yako kama kila wakti unakuwa hukamilishi zile kazi zinazotakiwa  kukusaidi kuyafikia malengo yako. Hapa sasa ndipo unapotakiwa kujilazimisha na kuhakikisha kila jukumu ulilonalo  unalikamilisha  kwa siku husika.

Kwa mfano kama wewe ni mfnyabiashra ulitakiwa kupga mahesabu Fulani ya kukusidia, fanya hivyo bila kuacha. Halikadhalika akama wewe ni mwandishi na umejipangia kuandika kurasa mbili kwa siku, pia fanya hivyo bila kuacha wala kuahirisha. Kwa kukamilisha majukumu yako kila siku itakusaidia kufikia malengo yako kuliko ambavyo ungefanya mambo nusunusu.

4. Yagawanye malengo yako.
Malengo yoyote ulinayo yanaweza kufikika. Haijalishi malengo hayo ni makubwa kivipi lakini uwezo wa kuyafanikisha upo, ikiwa tu lakini utafuata hatua za kuyakamilisha malengo hayo. Pengine unajiuliza kivipi au nitawezaje kuyakamilisha malengo yangu makubwa? Ni rahisi tu na hata wewe unaweza.

Kulielewa hilo vizuri ngoja nikupe kisa kimoja moja ambacho kinaelezea siku moja fisi mkubwa alimkuta fisi mdogo akimla tembo. Fisi Yule alivyoona vile alicheka sana na kumuuliza utamaliza lini? Fisi Yule mdogo alimwambia nitamla kidogo kidogo mpaka ataisha. Kwa kutumia mfano huo hivyo, ndivyo unavyotakiwa na wewe kufanya kwa malengo yako makubwa. Unajiona una malengo mkubwa yagawe vipande vipande mpaka uyafikie..

5. Tafuta msaada.
Ni rahisi kuyafikia malengo yako, kama utatafuta msaada wa kukusaidia kuyafikia malengo hayo. Acha kung’ang’ania kukamilisha malengo hayo ukiwa peke yake. Yaangalie malengo yako yana husu nini kisha baada ya hapo jiulize je, ni mtu gani au watu gani  ambao wanaweza kunisaidia kukamilisha malengo haya.

Kwa kujua watu ambao watakusaidia kukamilisha malengo yako itakusaidia sana kushirikiana nao kwa ukamilifu na kwa ubora wa hali ya juu hadi kufikia mafanikio yako. Tambua na elewa sio kwa sababu malengo ni yako, hivyo unatakiwa kuyakamilisha mwenyewe, hapana. Tafuta kile unachokosa, kisha omba msaada.

6. Kuwa chanya wakati wote.
Kuna wakati tunapokuwa tunajiwekea malengo huwa tunakutana na changamoto nyingi sana ambazo zinatukatisha tamaa. Sasa hali hii inapokutokea ni vyema ukajitahidi ukawa chanya wakati wote. Acha kukataa wala kujiona hufai, endelea kusonga mbele kati kati ya changamoto hizo ulizonazo wewe.

Kuwa chanya wakati unatafuta mafanikio inalipa sana. Tuchukulie kwa mfano unafanya biashara halafu ukapata hasara, hapo unafanyaje? Utaacha au itakuaje? Jibu ni kuendelea  na safari ya mafanikio kwa kutambua kwamba hiyo nayo ni hatua ya mafanikio pia. Ndiyo maana tunasema ni muhimu na lazima kuwa chanya ili kuyafikia mafanikio yako.

 7. Kuwa tayari kuyapitia malengo yako kila wakati.
Pamoja na kwamba umejwekea malengo vizuri, umejitoa kabisa kwenye malengo hayo, lakini hutakiwi kusahau kabisa kuyapitia malengo yako. Ni muhimu kuyapitia tena na tena malengo kwa kutambua wapi ulipofikia, nini kinachokukwamisha na ufanye nini ili uweze kusogea hapo ulipo kwa kasi zaidi.

Watu wengi wenye mafanikio wanayapitia malengo yao. Wanapita malengo yao asubuhi, wanapitia malengo yao mchana, wanapitia malengo yao jioni. Picha kamili ya malengo yao inakuwa ipo kichwani mwao tayari. Hiki ndicho kitu ambacho unatakiwa ukifanye hata wewe. Pitia malengo yako kila wakati ili yaumbieke vizuri na itakusaidia kuyakamilisha.

8. Jifunze kufurahia mafanikio kila hatua unayopitia.
Pamoja na kujiwekea malengo yetu makubwa, lakini kumbuka kuna yale malengo yetu madogo madogo ambayo huwa tunayashinda. Inapotokea umefanisha jambo fulani, hata kama kwako ni dogo ni vyema ukajifunza kulifurahia. Furahia mafanikio yako siku hadi siku kwa jinsi unavyoyapata.

Hiyo itakupa nguvu ya kufanikisha mambo mengine.
Kama kweli una nia njema ya kufikia mafanikio makubwa, basi hayo mambo ni ya msingi sana katika kukusaidia kufikia malengo yako makubwa uliyojiwekea. Jukumu lako kubwa ni kuhakikisha unayaweka kwenye vitendo mambo hayo.  Na kwa kufanya hivyo basi utaweza kufikia malengo yako na kutakuwa hakuna wa kukuzuia.

Friday, 19 August 2016

Saratani ya utumbo mpana!

(Colon Cancer) SARATANI YA UTUMBO MPANA NI HATARI.

SARATANI YA UTUMBO MPANA NI HATARI

Habari wadau,
Mnaweza shangaa leo kuja na uzi huu wa Saratani ya Utumbo mpana, kifupi mi si tatbibu na wala sina fani yoyote ya namna hiyo, bali mambo haya yakikukuta ndo utayajua, sometime kuliko daktari mwenyewe, hasa ukiwa mtafiti wa kwanini nimepata tatizo hili ama lile, yalinikuta, haikufika kuwa saratani, labda kwa kuwa Mungu hakutaka ifike huko, lakini cha moto nimekiona, hivyo nimeona bora tuelimishane kupitia blog hii ili sote tuwe na tahadhari ya aina fulani hasa kuhusiana na magonjwa haya ya kujitakia, ndio ni ya kujitakia, yanaitwa Lifestyle Diseases ama magonjwa yasababishwayo na mitindo yetu ya maisha.

"What you eat may play a role in your risk of colon cancer. Colon cancer may be associated with a high-fat, low-fiber diet and red meat. However, some studies have found that the risk does not drop if you switch to a high-fiber diet, so this link is not yet clear.
 
Smoking cigarettes and drinking alcohol are other risk factors for colorectal cancer." kwa mujibu wa U.S National Library of Medicine

Ndio maana nikasema ni ya kujitakia, tafiti zaonesha "90% of chronic diseases come from infection of gastrointestinal" na sababu kuu ni tatizo la kukosa choo, mi nilikuwa najiona sawa tu kama sijaenda haja siku moja au mbili, nikidhani ni kawaida, kumbe nilikuwa nalundika matatizo, mtu yeyote ambaye anapata mlo walau mlo mmoja kwa siku na kupitisha siku moja au zaidi bila kupata choo anatatizo la kukosa choo, sasa je weye unaye pata milo mitatu kwa siku bila kutoa uchafu huo je wadhani waenda wapi? kitaalumu tatizo hili lajulikana kama Constipation.

Wataalamu wanasema sababu ziko nyingi ikiwa ni pamoja na:-
Kukosa mlo kamili ama kula vyakula viingi vyenye kiwango kikubwa cha wanga na mafuta,
Kula vyakula vilivyokobolewa na vilivyo changanywa na madawa ili visiharibike,
mifumo hatarishi ya maisha (Dangeraous Lifestyles) kama vile matumizi ya pombe na sigara kwa wingi,

Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda katika milo yetu,
Maji yasiyo salama,
Kuvuta hewa chafu,

Hizi ni baadhi tu, na hadhari zake zaweza kuwa:-

Chakula kutomeng'enywa vizuri (poor function of digestion system)
Maumivi makali wakati wa kupata choo,
Uchafu uliokaa muda mrefu kugeuka sumu,
Bakteria wenye madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine mwilini.

Hii yaweza sababisha magonjwa sugu kama:
1. Saratani ya utumbo mpana (Colon Cancer)
2. Presha (Arteriosclerisis)
3. Kuongezeka uzito (Obesity)
4. Tumbo kujaa gesi
5. Magonjwa ya Ini
6. Figo kushindwa kufanya kazi vizuri,
7. Magonjwa ya ngozi,
8. Kukakamaa kwa mishipa ya damu,
9. Kisukari,
10. Magonjwa ya moyo n.k