Jifunze kutatua tatizo la kushidwa kupakua (Download) App toka Google Playstore.
Kunamara nyingine unaweza kukuta simu yako inashidwa kupakua (Download) App toka Google Play na kukuonesha ujumbe wa “Error 491” jifunze jinsi ya kutatua tatizo hili kwa kufata hatua zifuatazo.
Njia ya kwanza ya kufata ni kwakufuta cache zote zilizopo kwenye Google Play. fata hatua hizi.
Fungua kitufe cha “Settings” kutoka kwenye simu yako.
Tafuta kitufe kilicho andika “Apps” au “Application Manager” hii hutegemeana na aina ya simu unayotumia
Shusha chini mpaka ukutane na chaguo liloandikwa “All apps” kisha ubonyeze kitufe cha “Google Play Store app”
Fungua sehemu ya maelezo ya App bonyeza kitufe cha kusimamisha shuhuli zote za App hiyo ” Force stop button”
Bonyeza chaguo lililo andikwa “Clear cache”
Kwa kufanya hivyo utakuwa umetatua tatizo lako kabisa, kama bado itaonekana tatizo linaendelea jaribu kubadilisha barua pepe ya Google (Email) unayotumia kwenye simu yako kwa kuweka barua pepe mbadala toka Gmail njia hiyo pia huondoa tatizo.
Always visit my blog and learn a lot
elisanteblog.blogspot.com
No comments:
Post a Comment