Thursday, 28 July 2016

Tumia hadi line 5 kwa simu moja kwa wakati mmoja!


TUMIA LAINI ZA SIMU MPAKA 5 KWA WAKATI MMOJA UKIWA NA KIFAA HIKI

Jinsi Siku zinavyozidi kwenda mbele nayo Teknolojia inazidi kukua kwa kasi sana. Kila kuchapo utapata mpya zinazojiri katika upande wa teknolojia. Tumezoea kutumia Simu zenye Laini moja ya Simu(Singe Simcard) pia hata Simu zenye laini mbili (Dual Simcard) katika Simu zetu iwe mfumo wa Android au iOS. Ulitamani hata utumie Simcard zaidi ya mbili kwenye simu yako katika simu yako kwa kuchoka kubadirisha laini na kuweka nyingine unayohitaji kuitumia lakini ukashindwa. 


Lakini Simore Mult-Sim holder wanakuletea kifaa ambacho kinauwezo wa kutumia Laini hadi 5 katika Simu moja na zote zikawa zinapatikana bila tatizo lolote. Waweza piga simu,tuma meseji au kuwasha data za internet kwa kuchagua laini uitakayo. Pia huhitaji Kuroot Simu yako kwa wale wenye mfumo wa Android katila Simu zao  Wala huhitaji Jailbreaking kwa wale wenye mfumo wa iOS kwenye Simu zao.

Gharama ya hicho kifaa ni dolla $40 ambayo ni sawa na Tsh.87,530/= . kwa maelezo zaidi Fungua website yao  Hapa 

Toa maoni yako

No comments:

Post a Comment