JE UNAJUA KWA NINI HUFANIKIWI?
Una mizigo mingi isiyo ya lazima wala faida ambayo
umeibeba:
1.Umejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya
wengine na umesahau maisha yako!
2.Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya
uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na
maendeleo yako!
3. Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo
kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi
ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa
maslahi yao!
4.Umeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko
kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya
maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.
5.Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna.Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.Maisha ni mipango.
6.Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii.Huna siri hata moja!Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale
uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu
ukibadilika tu watasema “umefulia”
7.Kila aliyefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako
wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao kujifunza mambo mapya.
8.Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki,
hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo.
Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa
kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako.
9.Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.
10.Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe
intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za
mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi
kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako
ya vocha.
ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli unahitaji kusonga mbele! Huu ni ujumbe haumhusu mtu yeyote yule!
Have a nice moment all!
No comments:
Post a Comment