Friday, 5 August 2016

Right way for Development!

RIGHT WAY FOR DELOPMENT   (RIWADE)

RIWADE, hii ni asasi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa mwezi Juni 2016, ikiwa na usaili namba  (ooNGO/08696) kwa lengo la kuwasaidia vijana wasio na ajira waweze kufanya kilimo, ufugaji, uvuvi wa kisasa ulio endelevu na mazingira. Na pia  kuwahusisha wakulima katika ngazi zote ili kuweza kushirikiana katika kutatua changamoto zinazokabili kilimo, ufugaji, uvuvi na mazingira kwa ujumla . Hivyo msingi wa RIWADE umejengwa kwenye mahitaji ya wakulima, wafugaji na wavuvi. RIWADE inahusisha wadau wengine kama vile washauri na watalaamu wa  vyuo vikuu, makampuni, serikali na taasisi binafsi katika kutekeleza shughuli zake. Mpango huu shirikishi unatengeneza msingi wa ubunifu ambapo, usambazaji wa elimu, utafiti na ushirikiano hujenga nguzo kuu.

 DIRA YETU. (Vission)

Kuzifikia na kuziboresha huduma za jamii ambazo zitapelekea ukuaji wa hali ya kimaisha kwa wananchi.

DHIMA YETU. (Mission)

Kutengeneza na kutoa fursa kwa watanzania wote ili waweze kupata elimu ya ujasiriamali na namna ya kutengeneza mitaji kwa ajiri ya ukuaji endelevu wa kijamii na kiuchumi.

MISINGI YETU.
Uadilifu
Uwajibikaji 
Uvumbuzi
Uaminifu 
KAULI MBIU.

"Ardhi Ni Mtaji"

    CONTACTS                                                     Managing Director
Eng. Ayubu Massau .
Head Office
P.o. box 682
Morogoro.
Tell. 0763188907

General Secretary 
Shadrack Charles Makaya
Tell. 0752817289

Project Evaluator
Elisaria Swai
Tell. 0788919510

  " IT manager"
Johnson Zablon
     Tell. 0765926368

     
Regional Managers.

Arusha Regional Manager 
Baraka S. Mchomvu
Tell. 0687176587

Lindi Regional Manager 
Shabani Zuberi
Tell. 0783728809

Ruvuma Regional Manager
Sheria Buckley
Tell. 0754424883

Kilimanjaro Regional Manager 
Shadrack Charles Makaya 
Tell. 0752817289.

Mtwara Regional Manager
Pilly Chande 
Tell. 0656635808

  Mbeya & Songwe Regional Manager
Isakwisa Banunu Mwakamoja
Tell. 0752132314.

Njombe Regional Manager
Nafiwe Miho 
Tell. 0769665206

Iringa  Regional  Manager
Vumilia J. Chacky
Tell. 0719056060

Tanga Regional Manager
Bahero Hassan Wema
Tell. 0652020297

Pwani Regional Manager
Khanifa Byamungu
Tell. 0715684196

Tabora Regional Manager
Stephen I. Nyagalu
Tell. 0757888044

Dodoma Regional Manager
Rahim Kalyango
Tell. 0717184731

Morogoro Regional Manager
Elisaria Swai
Tell. 0788919510

Mara Regional Manager
Masatu Bure Salum
Tell. 0759782429

Simiyu Regional Manager
Nkuba Kibayu
Tell. 0759919209

Mwaza & Katavi 
Regional Manager
Diana Joseph Madukwa
Tell. 0754213256

Dar es Salaam Regional Manager
Anitha Said 
Tell. 0719620644

Dar es Salaam Regional Manager
Ochieng Felix Okombo
Tell. 0654092683

Manyara Regional Manager
Batare  Mbaraka
Tell. 0769323117

Manyara Regional Manager
Fredrick Jonas 
Tell. 0682529281

Singida Regional Manager
Juma Ramadhani
Tell. 0756222314

Kigoma Regional Manager
Anton Mwita Kitereri
Tell. 0758382121

Rukwa Regional Manager Paul  Elias  Manzile
Tell.0757313953

Shinyanga Regional Manager
Elikana  Machanya
Tell. 0768011069

Geita Regional Manager
Solo manoni
Tell 0757281331

Kagera Regional Manager
Dativa Paul 
Tell: ,0765571557

Pia tunapatikana

Blog:  riwade.blogspot.com
Facebook: Riwade
Twitter:  Riwadwtz
Instagram:  Riwadetanzania
Email: riwadetanzania@gmail.com

Jinsi ya kujiamini uongeapo mbele za watu!

Mbinu Saba(7) Za Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Ya Kundi Kubwa!

Katika maisha zipo hofu za aina nyingi zinazomtesa binadamu. Lakini mojawapo ya hofu kubwa ambayo inasumbua sana wengi ni hofu ya kuongea mbele za watu. Hii ni hofu ambayo  huwatesa wengi sana, hasa pale wanaposikia kwamba wanakwenda kuzungumza mbele ya umati wa watu.
Wengi wanaposikia suala la kuongea mbele ya watu hali ya hofu kubwa huwaingia ndani mwao. Kutokana na hofu hiyo husababisha kwa wengine kushindwa kula vizuri, kijasho huwatoka na wakati mwingine kuhisi hata kukimbia kama uwezekano huo upo.

Mara nyingi  hofu hii huwatokea wengi sana. Na ni hali ambayo karibu kila mmoja wetu ameshawahi kukutana nayo katika maisha yake au anayo mpaka sasa. Je, inapotokea unashindwa kuongea mbele za watu huwa unachukua mikakati gani? Je, huwa unaacha kama ilivyo au ni hatua gani ambazo unachukua?

Ni muhimu kujiuliza maswali hayo na kupata majibu kwa sababu suala la kuongea mbele za watu ni la muhimu kwa kila mtu na huwezi kulikwepa. Zipo shughuli nyingi ambazo huwa zinatutaka kuwa wasemaji wakuu, hapo unafanyaje kama huwezi kumudu kuzungumza mbele ya umati? Kama kweli nia yako ni kumudu kuongea mbele za watu makala hii itakupa majibu, kivipi?

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kumudu Kuongea Mbele Ya Kundi Kubwa La Watu.

 1. Jiandae.
Ili uweze kufanikiwa vizuri kuongea mbele za watu, kwanza tambua kwa kina kile unachokwenda kukizungumza. Ikiwezekana ukiweke kwenye maandishi, kisha kifanyie mazoezi mara kwa mara. Unaweza ukafanya mazoezi hayo siku tatu kabla au hata moja.

Kwa kadri utakavyozidi kufanyia mazoezi utajikuta unakimdu vizuri na hiyo haitakupa shida sana wakati wa kuzungumza. Kwa kufanya hivyo akili yako itatulia kuliko ambavyo ungekurupuka na kwenda kuzungumza. Maandalizi ni muhimu sana ili kufanikiwa katika hili.

2. Ondoa mawazo ya kukosolewa.
Wengi wanashindwa kongea mbele za watu wengi kwa sababu ya kuogopa kukataliwa au  kuogopa kukosolewa. Wanakuwa wanaamini kwa vyovyote vile ni lazima watakosolewa. Haya ni mawazo hasi yanayowatesa sana na kuwasumbua wengi.
Lakini kwa vyovyote vile, Ukitaka kumudu kuongea mbele za watu wengi, jiamini kwanza wewe. Amini kuwa unaweza na hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuzungumza mada hiyo kuliko wewe. Acha kuamini sana katika kukoselewa, hilo litakusaidia kusimama imara.

3. Acha kufikiria watu unaongea nao.
Inaweza ikakupa shida sana kuongea mbele za watu hasa kila unapofikiria kundi kubwa la watu unaloongea nalo. Kundi hilo linaweza kuwa ni la wasomi au watu ambao wamekuzidi umri. Sasa kila ukifikiria kundi hilo unaanza kujiona kama hutaweza kuzungumza kitu.

Badala ya kufikiria kundi hilo, jitahidi kuweka mawazo yako yote kile unachokizungumza. Kiamini unachokizungumza kuwa utakizungumza kwa usahihi. Hapo ndipo mawazo yako unatakiwa uweke hapo na siyo sehemu nyingine. Hiyo itakusaidia kukuondolea hofu kwa sehemu kubwa.

4. Epuka kuongea kwa haraka.
Siri kubwa ya mafanikio ya kuongea mbele za watu ni kujifunza kongea polepole na kwa vituo. Wengi wanashindwa kumudu kuongea mbele za watu kwa sababu ya kutaka kuongea haraka haraka ili wamalize. Hii ni sumu kubwa inawafanya watu wengi washindwe kumudu kuongea mbele za watu kwa ufasaha.

Unapoongea kwa haraka kitu kinachokutokea kwanza, unakuwa unashindwa kupangilia maneno vizuri lakini pia inakuwa inakufanya ushindwe kupumua vizuri na kukufanya uongee kwa tabu. Kwa hali hiyo ni lazima kuepuka kuongea kwa haraka ili kufanikiwa kuongea mbele za watu vizuri.

5. Fikiria unaongea na mtu mmoja tu.
Sumu kubwa ya wengi kushindwa kuzungumza mbele za watu ni kuchukulia unazungumza na kundi kubwa la watu sana. Huu unaweza ukawa ndiyo ukweli halisi, lakini ili uweze kufanikiwa katika hili ni lazima kwako kujidanganya na kuchukulia kuwa unaongea na mtu mmoja.

Hapa ndipo siri ya mafanikio ilipo. Jifanye unaongea na mtu mmoja binafsi ingawa mbele yako lipo kundi kubwa. Wakati wa mazungumzo unaweza ukasisitiza jambo kwa kusema ‘unanielewa ninachosema’ badala ya kusema ‘mnanielewa ninachosema’ Hiyo itakupa nguvu ya kuondoa hofu ndani mwako.
.
6. Tuliza akili na mawazo yako.
Kwa kuwa utakuwa umeshajua kwamba unaonenda kuongea na watu wengi ni vizuri ukajua kuituliza akili yako. Kabla ya kile unachokwenda kuongea kunywa maji mengi, hiyo haitoshi unaweza ukalala zaidi usiku wke kabla ili kuiweka akili yako sawa.

Hayo yanaweza yakawa ni sehemu ya maandalizi ya kile unachokwwenda kukiongea. Ukumbuke pia akili yako inahitaji utulivu huu, ili usiwe na papara za hapa na pale. Hiyo itakusaidia kumudu zoezi zima la kuongea mbele za watu, ikiwa utakuwa makini kwa hilo.

7. Jifunze.
Tafuta namna ya kujifunza na kuweza kuongeza ujuzi wako wa kuongea mbele za watu. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu mbalimbali au unaweza ukatafua ‘mentor’ au mshauri ambaye ameboboa katika hilo eneo na akakuongeza na kukusaidia kufikia hatua yaw ewe kuweza kumdu kuongea mbele za watu bila wasiwasi.

Haijalishi wewe ni mbovu kiasi gani wa kuongea mbele za watu. Lakini, kwa makala hii itakuwa chachu au hamasa kwako ya kuweza kukusaidia kuweza kumudu kuongea mbele za watu bila woga. Kitu kikubwa endelea kujifunza, fanyia mazoezi na mwisho wa siku utamudu hili pia na kuwa mshindi.

Tuesday, 2 August 2016

Mikojo ya walevi kutengenezewa bia!

Mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia!

GHENT, Ubeligiji
WATUMIAJI wa pombe sasa wataweza kupata auheni ya bei ya vinywaji hivyo, baada ya wanasayansi kugundua kifaa maalumu kitakachotumika kubadilisha mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia.

Kugunduliwa kwa kifaa hicho ni mkombozi kwa wamiliki wa viwanda vya pombe ambapo wataweza kupata malighafi ya kutengenezea bia kwa urahisi.

Kinatarajiwa kufungwa kwenye vyoo vya baa mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa mikojo hiyo ya walevi.

Kifaa hicho ambacho kitakuwa kikitumia umeme wa jua pia kitakuwa na uwezo wa kubadili mikojo hiyo kutumika kama maji ya kunywa.

Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubeligiji, walisema kifaa hicho kitaanza kutumika hususan maeneo ya mijini kwenye nchi zinazoendelea.

Licha ya kuwepo kwa mashine maalum yenye uwezo wa kutibu maji machafu ikiwemo mkojo kisha kutumika kwa matumizi mengine muhimu ya binaadamu, wataalamu hao wamesema kifaa hicho walichokigundua kinauwezo zaidi wa kuyatibu maji hayo bila kutumia nguvu ya umeme.

Dk. Sebastiaan Derese, alisema kifaa hicho kitakuwa kikitunza mikojo kwenye tangi maalum ambalo litatumika kutibu kisha kutumika kama malighafi ya kutengenezea bia.

Kwa mara ya kwanza kifaa hicho kilianza kutumika kwenye tamasha la muziki ililofanyika mjini humo ambapo jumla ya lita 1000 za mikojo, zilikusanywa kisha kutengenezewa bia.

Alibainisha kuwa, bia zilizotengenezwa kupitia mikojo hiyo imewavutia wanywaji wengi hususan kwenye matamasha mbalimbali.

Je, bado utaendelea kunywa bia?

Sunday, 31 July 2016

Udukuzi-programu kampeni ya Hillary Clinton

Programu ya kampeni za Hillary Clinton yadukuliwa

Maafisa wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.

Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.

Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.

Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.

Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.

Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.

Yaan IT ni shidaah aise!!!

Friday, 29 July 2016

Watu wasiingilie mapenzi yenu!

Fahamu mambo ya kufanya ili kuzuia watu wasiingilie mapenzi yenu

Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako.

 Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.  Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.

1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:  
Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako.

Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.

2. Upekee wa mambo:
 Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako.

Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.

3. Mwenye maamuzi ni wewe:
Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua.

4. Kuwa na subira:
Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza  kuzitumia kupata suluhu ya tatizo.

5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu:
Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa  nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine.

6. Kuweni peke yenu: 

Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni  kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako.

Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi.

 Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao  kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.

7. Nenda ‘darasani’ :  Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu.

Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu.

NB: Kuweni watu wa imani, mshirikisheni MUNGU ktk ndoa yenu! Msali na kuomba.

Mikopo Elimu ya Juu.

Waombaji wa Mikopo Elimu ya juu Wafikia 69,820 Mpaka Sasa.

JUMLA ya wanafunzi 69,820 wameomba mikopo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) hadi sasa ikiwa zimebaki siku tatu kufikia mwisho wa kupokea maombi hayo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam , Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisoga, alisema mwaka jana walioomba kupewa mikopo walikuwa 65,000, hivyo waombaji wa mwaka huu wameongezeka.

Mwaisoga alisema tofauti na awali, mchakato wa sasa wa kuomba unafanyika kwa njia ya mtandao na baada ya kutumwa kwao, watayapitia na kwa yale yenye kasoro, wahusika wataitwa ili wayarekebishe.

Alisema dirisha la uombaji wa mikopo linatarajia kufungwa Jumapili hii.

Katika hatua nyingine, alisema idadi ya wanaorejesha mikopo imeongezeka maradufu baada ya kutakiwa kufanya hivyo.

“Kwa sasa ni vigumu kutaja idadi yao kwa sababu huwa tunaitoa mwishoni mwa mwezi kwa hiyo kesho tutakuwa na idadi kamili ya waliorejesha, lakini ikilinganishwa na huko nyuma, sasa hivi mwitiko wa wanaorejesha umeongezeka,” alisema.

Mwaisoga alisema sheria inamtaka aliyekopa aanze kurejesha baada ya mwaka mmoja wa kuhitimu masomo yake, lakini anapochelewesha, kila mwaka kunakuwa na penati ya ongezeko la asilimia sita.

Thursday, 28 July 2016

Maziwa ya mende na faida zake!!!

Maziwa ya mende chanzo bora cha protini!

Mende wa Diploptera puncata hujifungua

Wengi huenda wakawa hawawezi kuwavumilia mende, hata kuwatazama pekee, lakini wanasayansi nchini India wanasema huenda mende wakatoa tumaini kwa binadamu, katika lishe.

Wamegundua kwamba chembe za protini za maziwa kwenye mende ambazo zina virutubisho„vingi ajabu”.

Wanasema vinasema kutumiwa kama tembe ama chakula chenye virutubisho vya protini kwa kiwango cha juu.

Wanasayansi katika taasisi ya sayansi ya seli katika mji wa Bengaluru, wamefanya ugunduzi huo baada ya kutafiti muundo wa chembe za protini zinazopatikana katika utumbo wa aina ya mende wajulikanao kama Diploptera puncata, ambao ndio pekee hujifungua.

Ingawa mende kwa kawaida hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera puncata huwa wanatengeneza aina fulani ya maziwa yenye protini kwenye utumbo, ambayo hutumiwa kulisha watoto wake.

Chembe moja ya protini hiyo inakadiriwa kuwa na kiwango mara tatu cha nguvu ya mwili ikilinganishwa na kiasi sawa cha maziwa ya nyati.

Chembe hizo zina nguvu mara nne kushinda maziwa ya ng’ombe.

“Ni chakula kamili, unapata protini, mafuta na sukari,” amenukuliwa mmoja wa watafiti waliohusika, Sanchari Banerjee, na gazeti la The Times of India.

Mende huliwa katika maeneo mengi duniani hasa Mashariki ya Mbali

Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la International Union of Crystallography.

Ramaswamy anasema kwa kutumia ufahamu wao wa muundo wa protini hizo, wanaweza kutumia hamira kuzalisha chembe kama hizo kwa wingi kwenye maabara.

Isitoshe, anasema muundo wa chembe hizo unaonesha matumaini kwamba zinaweza kuundwa na kutumiwa katika vidonge vya dawa.

Je, wewe utakunywa? Toa maoni yako!