Saturday, 27 January 2018

Matatizo ya PC na suluhisho lake.

MATATIZO YANAYOIKUMBA KOMPYUTA, PAMOJA NA SULUHISHO LAKE.

VIRUSI(VIRUSES)
Virus ni “software” ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuharibu “software” nyingine ambazo zinakuwa kwenye mfumo wa utendaji kazi wa Kompyuta.

Kirusi cha kwanza kilijulikana kama “Brain” ambacho kilitengenezwa mwaka 1986, kirusi hiki kiliandikwa na vijana wawili wa huko Lahore nchini Pakistan ambao wanajulikana kwa majina ya Basit Farooq Alvi na Amjad Farooq Alvi.

Kirusi hiki cha Brain kiliharibu Kompyuta za IBM, Kirusi hiki kilibadilisha “boost sector” ya ‘” floppy disk” na kutengeneza kopi ya Virusi mbalimbali.
Aina za virusi ni kama ifuatavyo, “Trojan horse”,” Spyware”, “Adware” “Worms” n.k.

DALILI ZINAZOONESHA KOMPYUTA IMESHAMBULIWA NA VIRUSI.
(i)Kompyuta kuwa nzito katika utendaji wa kazi.
(ii) Kupotea kwa baadhi ya mafaili na Program kwenye Kompyuta.

Zipo njia mbalimbali ambazo huwa ndicho chanzo kikuu cha kusambaza virusi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

(i) Barua pepe (email attachment), mara nyingi huwa zinaingia barua pepe kwenye barua pepe ya mtu mwingine, na hapo ukiiifungua barua pepe kama hauna “Ant-virus” itakupekelea kupokea virusi hivyo bila kukamatwa na “Ant-virus”.

(ii) Tofuti mbalimbali ambazo sio nzuri kwa matumizi ya mwanadamu, ambazo zimetengenezwa kwa lengo hilo la kusambaza virusi.

(iii) Hard disk, flash, memory cards, ambazo zimehathirika/ haribiwa na virusi.

(iv) Hackers/Ant-virusi zisizo rasmi, mbovu ambazo zinatengenezwa kuharibu mfumo wa Kompyuta.

(v) Kupitia simu, hii ni pale ambapo simu inapounganiswa na Kompyuta hasa kutoa au kuingiza taarifa mbalimbali kwenye simu au Kompyuta, mwingiliano huu unaweza kusababisha virusi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
         Yafuatayo ni madhara yasababishwayo na Virusi kwenye Kompyuta.

(a) Kupotea kwa files/ taarifa kwenye Kompyuta., hapa kirusi kikishaingilia file kina uwezo wa kulifuta, kuficha, kutafuna au kuliondoa kabisa kwenye Kompyuta.

(b) Kuharibu mfumo wa Utendaji wa Kompyuta (Operating System corrupt). Hapa hutokea kwa sababu hivi virusi vinakuwa na nguvu kubwa kuliko mfumo wa utendaji wa Kompyuta.

(Operating System). Kompyuta kuwa nzito sana(slowly) ambapo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa sababu mfumo mzima wa utendaji unakuwa umelemewa na virusi.

Jambo muhimu la kuelewa ni kuwa virusi hivi huongezeka kwa kujizalisha haraka na kushambulia mafaili mbalimbali kwenye Kompyuta.

JINSI YA KUTATUA TATIZO LA VIRUSI KWENYE KOMPYUTA.

(i) Weka “ Ant-virus” ambayo na nguvu kukabiliana na virusi mbalimbali kwenye Kompyuta yako.

(ii) Epuka kuingia kwenye Tofuti(website) ambazo hazieleweki, ambazo zinaweza kuwa chanzo cha virusi kwenye Kompyuta yako.

(iii) Usifungue Barua Pepe (email attachment) bila” kuzi- scan” hizo barua pepe ulizopokea kwenye Kompyuta yako.

(iv) Iweke Kompyuta yako kwenye mfumo wa “Automatic scan”

1 comment:

  1. Hello to all

    Fullz with good credit scores are available
    CC's with cvv & Dumps
    SSN DOB USA Fullz/Pros
    EIN Fullz
    COmbos/Logs

    Legit fullz with guarantee results
    Fresh spammed & valid info
    -----------------------------------------
    ICQ/Telegram @killhacks
    WA +92 317 2721122
    Email exploit dot tools4u @ gmail dot com
    Wickr/Skype @peeterhacks
    -----------------------------------------
    Tools & tutorials are also available
    Hacking Carding Spamming Scripting Stuff
    Mailers Senders C-panels
    Brutes Crackers

    Legit tools & tutorials
    Fresh & verified tools

    ReplyDelete