NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE
SOMO: UTOAJI SADAKA AINA YA MBEGU UNAVYOJENGA FIKRA ZA KUKUFANIKISHA.
HII NI SUMMARY YA SEMINA, HAKIKISHA UNATAFUTA CD & DVD ZA SOMO HILI. PIGA NO HIZI SAA ZA KAZI SAA 3.00 ASUBUHI HADI SAA 11.00 JIONI. 0754766517 (DAR ES SALAAM) 0754249590 (ARUSHA)
Katika kuweka utangulizi tuangalie Mithali 23:7a
Mithali 23 :7
“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo”
Kwenye tafsiri nyingine za kiingereza lile neno “aonavyo” wametafsiri kama “afikirivyo” na anaposema afikirivyo ni zaidi ya kuwaza hasemi awazavyo bali anasema afikirivyo. Kwa sababu fikra ni tofauti na mawazo.
Fikra _ni mtiririko wa mawazo unaotengeneza msimamo ndani ya mtu._ Mtu anaweza kuwa na mawazo na asiwe na Fikra, maana yake mtu anaweza kuwa na mawazo na asiwe na msimamo. Maana kuwa na fikra ina maana una msimamo. Msimamo ndio unatengeneza mfumo na taratibu za maisha.
Mawazo yakifikia ngazi ya kuwa fikra yanatengeneza Picha. Huwezi kuwa na fikra hadi uone Picha halisi ndani yako, na ikupe hali fulani ya kimaisha ndani yako ili kukuonesha kuwa hiki ndicho unachotaka.
Baada ya hapo unaanza kukitengenezea mikakati ndani yako ili kufikia kile kitu ulichoona. Biblia inasema aonavyo nafsini mwake, na katika tafsiri yetu ya Kiswahili wasingeweza kusema awazavyo nafsini mwake, maana wangekuwa wamepunguza uzito wa neno. Sasa neno lililo karibu na hilo ni afikirivyo.
Sasa fikra ni msimamo wa kimaisha ndani ya mtu, Kwa sababu hiyo tukitaka kujua misimamo yako juu ya maisha tutaangalia aina ya maisha uliyo nayo na tutajua misimamo yako na tutajua fikra ulizonazo na tutajua mawazo ambayo umekaa nayo muda mrefu kwa sababu kuna mtiririko wa aina fulani.
Kitu ambacho unahitaji kufahamu ni kuwa fikra ni muhimu sana katika kufanikiwa kwako. Kwa sababu Mungu anamfanikisha mtu kutoka ndani. Kwa hiyo unajua kabisa kuwa Mungu hulituma neno, na anatumia mawazo ndani yako. Kwa hiyo anapotuma neno ndani yako, anakupa nafasi ya kulitafakari na kujenga msimamo ndani yako ili kuwa na mtiririko wa aina fulani.
Mtu akiwa na msimamo wake, inakuwa ngumu sana kumbandua kutoka katika msimamo wake maana kuna ngome fulani. Wasomaji wa biblia wanaelewa maana kama unataka kushughulika na Fikra za watu wasio muamini Kristo ni lazima ushughulike pia na fikra zao. maandiko yanasema
2 Wakorintho 10 :5
“tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo”
Maana yake kila kitu ndani kinachotengeneza msimamo kinatakiwa kiwe chini ya usimamizi wa Kristo na neno lake.
Kwa hiyo kama hufanikiwi cheki fikra zako. Kama unafanikiwa na maisha yako ni mabaya angalia fikra zako. Maana biblia inasema kufanikiwa kwa mpumbavu kutamwangamiza kwa hiyo hata wapumbavu wanafanikiwa lakini wanaangamia. Kwa hiyo kama unafanikiwa sawa sawa na Mungu anavyotaka, mafanikio yako yatadumu maana hayataishia kwako tu bali yataenda hata kwa wajukuu zako.
Njia mojawapo ambayo Mungu anaitumia katika kujenga maisha yako ni kwa utoaji wa sadaka aina ya Mbegu.
Isaya 28 :23- 29
“_Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu.Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja? Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake? 26 Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huko na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito.Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri siku zote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi.Hayo nayo yatoka kwa Bwana wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake.
Katika njia ya kuandaa shamba na kupanda na kuvuna Mungu anatumia taratibu hizo katika kufundisha maana si kwamba huyo mtu analima tu. Watu wote wanaojifunza wanajua kuwa mwanafunzi yoyote mzuri, anajifunza kuliko kile ambacho wanafunzi wenzie wanaona Mwalimu kafundisha, ukiwauliza watakueleza kile walichosikia na kujifunza saa hiyo.
Mara nyingi Mwalimu anafundisha cha zaidi. Ukiwauliza wengine watakueleza cha zaidi walichojifunza kutoka kwa mwalimu. Katika kufundisha kuna kufundisha ndani ya kufundisha. Katika kujifunza kuna kujifunza katika kujifunza.
Kwa hiyo mtu wa namna hiyo atapata kitu cha zaidi na hawezi kuishia hapo, kama mkulima mzuri lazima atajifunza katika kulima kwake, na kupanda na kupata kitu cha zaidi.
Mkulima yoyote ambaye anajua tu kulima na kupanda na kuvuna na asijifunze cha zaidi ndani kile kilimo hakimfanikishi. Mkulima hawezi kufanikiwa kwa kulima tu na kupanda, Lazima ajifunze kitu cha zaidi kilichoko ndani ya kilimo.
Si kila mtu anayeuza duka, amefanikiwa anaweza kupata hela, na asifanikiwe maisha. Maana katika kuuza duka kuna kufanikiwa.
Kama wewe una watoto na unataka wasipitie hali uliyopitia unakuwa unawadokezea baadhi ya mambo. Kati ya mambo ambayo huwa nawadokeza watoto wangu nawaambia katika kufanya kazi, nenda kazini kujifunza usiende kazini kupata hela, nenda kujifunza na sio kufanya kazi ili upate hela. Mshahara ni matokeo, nenda kazini kujifunza, Wengi wanafurahia kupata mshahara.
Ndio maana haijalishi mtu anafanya kazi, kama ukimwambia anzisha kazi kama hiyo au mradi kama huo utaona anakwama kwa sababu hakwenda kazini kujifunza bali alienda kufanya kazi tu. Ndio maana usije ukafikiri kwa kuwa unauza duka la mtu na anafanikiwa haina maana ukianzisha la kwako litafanikiwa pia.
Kama unafikiri natania jaribu uone. Ndio maana mchungaji anapokukaribisha kanisani au unakuwa Mchungaji chini yake, au wewe ni Mwinjilisti au ni mzee wa kanisa na unaona watu wanafurahia mahubiri yako pale kanisani. Sasa unataka kuanzisha kanisa lako, ile kwamba unajua kuhubiri haina maana unajua kusimamia kanisa. Lakini hukuenda kujifunza kuwa si kitu chepesi kukusanya watu na ukawakuta hapo kanisani. Sasa kuwakusanya wewe unashindwa, maana si ulizoea kuwakuta. Sasa ni kazi ya kwako kuwakusanya lakini unagundua kuwa kazi hiyo ni ngumu. Lakini unagundua kuwa ulikaa chini ya mchungaji kwa miaka 10 au 5 na hukujifunza namna ya kusimamia watu.
Si suala la kupanda na kuvuna lakini Mungu anataka ujifunze zaidi katika kitendo hicho. Sasa si suala la kupanda na kuvuna bali ni kujifunza zaidi ya hapo kwani Roho Mtakatifu anataka kuachilia kitu cha zaidi ndani yako Upate kujifunza ili Mungu apate kuweka fundisho ndani yako katika kutoa kwako. Fundisho hilo litakusaidia sana katika utoaji wako.
Fundisho mojawapo ni namna ya kutumia fikra. Kinacho wakwamisha wakulima wengi sana si kulima bali ni Fikra. Kinacho wakwamisha watoaji wengi ni Fikra maana hawadaki saa Mungu anaposema nao. Kwa hiyo hawadaki kitu Mungu anataka wapate ili fikra zao ziwe msaada, hawakai mkao wa kujifunza. Wanasubiri muujiza. Kuna mambo kadhaa yanayojengeka kifikra wakati unatoa sadaka ya mbegu
MAMBO MATANO (5) YANAYOJENGEKA WAKATI UNATOA SADAKA YA MBEGU
JAMBO LA KWANZA.
1.KUFIKIRI JUU YA MATOKEO YA WAZO KABLA YA KUFIKIRI JUU YA KUTEKELEZA WAZO LOLOTE TU.
2 Wakorintho 9 :6
Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
Yohana 12 :20-24
Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
Jambo mojawapo ambalo hufanyika katika fikra zako kama unatoa sadaka aina ya mbegu. Ndani yako kunajengeka aina ya kufikiri, unafikiri kwanza matokeo ya wazo ulilonalo, kabla ya kufikiri kutekeleza wazo lolote. Watu wengi sana wanapokuwa na wazo wanafikiri juu ya wazo tu bila kuangalia matokeo. Lakini mkulima mzuri huwa hawazi juu ya mbegu kwanza bali anawaza juu ya mavuno kwanza. Kwa maana apandaye atavuna.
Kwa hiyo kama wewe ni mkulima huwezi waza juu ya mbegu kwanza, bali utawaza juu ya mavuno kwanza, kwa hiyo aina ya mavuno itaamua aina ya mbegu, sio aina ya mbegu peke yake kwa sababu inawezekana unataka aina ya mavuno angalia aina ya mbegu unayoweka, sasa angalia ndani ya moyo wako unataka nini?.
Jambo la Kilimo cha Parachichi kilinifundisha jambo kubwa sana, kama unapanda parachichi kwa ajili ya kuuza kwa hiyo mavuno yako sio parachichi bali ni hela. Tazama mavuno katika upana wake, biblia inasema Mungu anampa mbegu mwenye kupanda na kama anataka kula anataka kula atampa mkate. Mbegu inatengeneza fikra tofauti ndani yako kwa hiyo lazima ucheki katika upana wake namna ambavyo hizo pesa unazotaka kama zitafika.
Wakati najiandaa kutumia Ardhi niliyonayo, kwa ajili ya kuongeza kipato. Nilitaka kupanda parachichi na nilitazama bei iliyokuwepo sikuona kama itanifaa, na niliongea na yule mtu aliyetaka tupande pamoja na kunitafutia soko, nilimwambia neno gumu kidogo sijui kama alinielewa kitu namaanisha. Nilimwambia sina shida na parachichi la kula kama ni parachichi la kula nitanunua sokoni maana siwezi kutumia ekari 5 kulima parachichi la kula. Maana shida yangu ni hela sio Parachichi.
Nikamwambia na kwa jinsi ulivyoniambia sihitaji kupanda Parachichi maana nilipotazama mavuno, sikuona mavuno niliyokuwa nayahitaji, kwa hiyo nilibadilisha kufikiri. Kwa hiyo nilitafuta mbegu nyingine kufikia hilo lengo. Sasa unisikilize watu wengi sana wanapanda vile vile kwa sababu ukifikiri kimatokeo utafikiria kwa upana wake.
Ukifikiria juu ya kiasi cha mavuno utafikiri juu ya mbegu na kama utafikiri juu ya mavuno utafikiri juu ya mbegu. Ukifikiri juu ya kazi ya mavuno itakusaidia sana kuamua msimu wa kupanda. Ili mavuno yale yaweze kukutana na ile kazi uliyoikusudia. Ukifikiria juu ya umuhimu wa mavuno itakusidia kuamua juu ya umuhimu wa kupanda.
Ukiona mtu anakuwa mvivu kupanda ujue hana umuhimu wa mavuno yake na hii ndio sababu wakulima wanabadilisha vitu vya kupanda na ndio maana hata viwanda vinabadilisha matumizi au bidhaa wanaozalisha.
Wakulima wengi sana wanabadilisha, utakuta mkulima huyu analima hiki mwaka huu na mwaka ujao analima kitu kingine. Kwa sababu katazama suala la mavuno katika upana wake na hajaangalia tu mavuno kama wengine walivyotazama suala la mavuno.
Kila wakati unapotoa sadaka aina ya mbegu, angalia aina ya mavuno kwanza maana unapotoa uwe na uhakika Mungu anaanza kushughulika na fikra zako ili uondokane na kutekeleza wazo lolote maadamu lipo, kwa hiyo fikiri kimatokeo kwanza.
JAMBO LA PILI
2.KUFIKIRI JUU YA KUPATA JIBU LA TATIZO UNAPOKUTANA NA TATIZO BADALA YA KULALAMIKA
Habakuki 2 :1-2
“1 Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. 2 Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.”
Huyu ndugu Habakuki ukisoma kwenye ile sura ya kwanza utaona alipitia kwenye mazingira magumu sana yalikuwa na dhuluma hayakuwa mepesi kabisa katika ile sura ya kwanza utaiona. Na alimsemesha Mungu mambo magumu sana na alisema Mungu umenyamazaje unapoona mambo magumu namna hii na inapofika ile sura ya pili alisema nitasimama katika zamu yangu.
Sasa wasomaji wa biblia wanajua huyu ndugu alikuwa ni mlinzi mwombaji na alijikuta na yeye analalamika kama wengine wote na alipogundua aliamua kushika zamu yake, hata alipoomba pia alilalamika. Mungu alimjibu kwanza kulalamika kwake na alimwambia andika njozi hii.
Habakuki 2 :3
“3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.”
Hakumjibu juu ya tatizo bali alimjibu juu ya kulalamika kwake na katika kulalamika kwake alisema kwenye kiingereza wamesema “write down this vision.” andika njozi hii.
Ile njozi inakupa picha ya baadae, njozi inakupa jibu la tatizo wakati tatizo bado lipo. Wakati watu wanalalamika juu ya tatizo wewe utatamani wengine wasione njozi uliyoota kwa sababu ina jibu la tatizo waliloliona. Kwa sababu wakati watu wanalalamika juu ya tatizo wewe utakuwa unakula. Njozi inamfanya mtu mwenye njozi ale wakati wa matatizo na wakati wengine wanalalamika. Njozi inamfanya mtu mwenye njozi astarehe wakati wa matatizo wakati wengine ndio wanalalamika.
Kazi yake kukupa jibu kwenye matatizo, Njozi ni kama mbegu, mbegu ni jibu na njozi ni jibu, kwa hiyo njozi inavyofanya kazi ndivyo na mbegu inavyofanya kazi.
Mwanzo 47 :23-24
23 Yusufu akawaambia watu, Angalieni, nimewanunua leo, ninyi, na nchi yenu, kuwa mali ya Farao; basi mbegu zenu ni hizi, zipandeni katika nchi. 24 Itakuwa wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu wenyewe, kuwa mbegu za nchi, na chakula chenu, na chakula chao waliomo nyumbani mwenu, na chakula cha watoto wenu.
Hii habari tunajua ni ya wakati Mungu alipotoa taarifa kuwa njaa inakuja na kabla haijaja alisema kutakuwa na kipindi cha chakula. Yusufu aliyekuwa amepewa kazi ya kutafsiri ndoto alimueleza Farao na kitu gani cha kufanya. Baada ya kutafsiri ndoto alipewa nafasi ya kutelekeza ile ndoto ili kuhakikisha jambo linatekelezeka.
Kwa hiyo wale watu walijua kitu kilichokuwa kinaendelea na hawakuwa na kitu cha kusingizia kwa sababu
i) Ile nafasi ilitengenezwa na haikuwepo katika uongozi wa Farao na kwa sababu sio nafasi waliyoizoea Farao alitangaza nchi nzima na kwa hiyo alipokuwa anapokelewa alitangaza nchi nzima.
ii) Hata miji ilianza kuandaliwa kwa ajili ya mahali pa kuweka nafaka. Wakajenga maghala makubwa na kila mtu alijua maana walikuwa wananunua kwa watu maana Farao alikuwa hana shamba.
Baada ya miaka saba, njaa ikaja, na njaa ilipoanza wale watu walikuwa hawana nafaka ya kutosha na iliisha mwaka wa kwanza tu, na akiba yao pia ilikuwa ni hela na wanyama, nazo hazikuwatosha na ziliisha mapema sana, kwa hiyo waliuza hata wanyama, waliuza ardhi yao na walijiuza na wao wenyewe.
Walipofikia kiwango hicho, alichukua Ardhi yao yote kuwa ya Farao isipokuwa ya makuhani na aliwapanga katika matuo maana ardhi tayari walikuwa wameiuza kwa Farao. Biblia inasema Yusufu alipowanunua watu na ardhi yao alisema
“ Yusufu akawaambia watu, Angalieni, nimewanunua leo, ninyi, na nchi yenu, kuwa mali ya Farao; basi mbegu zenu ni hizi, zipandeni katika nchi. [Mwanzo 47 :23].
Sasa utajiuliza kwanini hakuwapa chakula maana siku zote alikuwa anawapa chakula na sio mbegu. Walipokuwa wanaenda na mifugo yao alikuwa anawapa chakula na sio mbegu lakini walipoachilia ardhi yao na wao wenyewe akawapa mbegu, maana alibadilisha namna ya kutatua tatizo lao na alisema “basi mbegu zenu ni hizi, zipandeni katika nchi”24 Itakuwa wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu wenyewe, kuwa mbegu za nchi, na chakula chenu, na chakula chao waliomo nyumbani mwenu, na chakula cha watoto wenu. [Mwanzo 47 :23c, 24]
Hawa watu walikuwa na mashamba ila hawana mbegu maana walikuwa na fursa ila walikuwa hawana mbegu.
2 Wakorintho 9 :10-11
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
Tazama vizuri hiyo mistari ,Mungu hatoi mbegu kwa wenye kula , anatoa mbegu kwa mtu ambaye fikra zake zimekaa mkao wa kupanda ,lakini yule ambaye fikra zake zimekaa mkao wa kula anampa chakula.
Mstari unaofuata anasema “mkitajirishwa katika vitu vyote” anamzungumzia mtu gani, sio anayekula ni anayepanda yeye anayekula tu hatajirishwi bali anayepanda anatajirishwa
Turudi kwa farao. “Wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakaposalia zitakuwa zenu wenyewe, kuwa mbegu za nchi, na chakula chenu, na chakula chao waliomo nyumbani mwenu, na chakula cha watoto wenu.” Mwanzo 47:24
Na ukiendelea hapo wale watu
“Wakasema, Umeyaokoa maisha yetu, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao.
Mwanzo 47:25
Huyu ndugu anazungumza nao masuala ya kupanda wao wanazungumza masuala ya utumwa ,kwa nini , kwa sababu kulima kwao ni utumwa , kwa hiyo walikuwa wanajua kulima kwao ni utumwa, ndio maana wanazungumza tutakuwa watumwa wa Farao.
Sasa unaweza ukaelewa kwanini mashamba walikuwa nayo lakini hawapandi, kwao kupanda ni utumwa,mpaka walipofika mahali wakaanza kufikiri, hamhitaji kumpa Farao kila kitu, anazungumza nao juu ya fikra ziweze kuwasaidia , kwa sababu mtu anapopita kwenye njaa fikra zake zinavurugwa.
Na kama unatoa sadaka aina ya mbegu uwe na uhakika inapofika wakati wa matatizo, Mungu atahakikisha fikra zako zinakuvusha katikati ya matatizo na utafikiri in terms of solutions. Utafikiria jibu badala ya kufikiria tatizo ulilonalo na kuanza kulalamika,kwa hiyo hata kufanya kazi utakuwa unaona ni shida,unaona ni utumwa kwa nini,unataka upewe tu chakula
Maandiko yanasema ule mstari wa 26.
Yusufu akaifanya kuwa sheria ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.
Ilibidi iwekwe sheria ya sehemu ya tano, kwa nini sehemu ya tano, ili kesho na kesho-kutwa fikra zao zikirudi kila mtu akivuna kama hataweka akiba ,Farao awe na mahali pa kuwagawia chakula, najaribu kuzungumza juu ya fikra, huwezi kuwa unatoa sadaka aina ya mbegu na unaona matatizo ukalalamika, kama unatoa sadaka aina ya mbegu na bado unaona matatizo unalalamika endelea kutoa mpaka fikra zako zijengeke. Wakati wenzako wanatafuta kila neno la kulalamika lakini wewe utakuwa unatafuta kila fursa ambayo inaweza kutokea mahali hapo, kwa sababu wewe ndani yako unaona tofauti.
Mkulima yeyote anayefanikiwa ni yule anaye lima na kilimo chake ni jibu la matatizo yake ,lakini kama analima kama alivyolima mwaka jana huwezi pata kitu na utaishi kama mwaka jana , kwa sababu mkulima ambaye mwaka juzi yuko vilevile, mwaka huu naye yuko vilevile shida sio yeye ni fikra.
Kwa hiyo kama unatoa sadaka yako ya mbegu kila mwaka upo vile vile tatizo lipo kwenye fikra,maana yake hujifunzi kitu ndani ya utoaji wako. Basi achilia Roho Mtakatifu afanye kazi yake kwa sababu hawezi kumpa mbegu mwenye kupanda kama hana fikra za kupanda. Maana anakutengeza na anapokupa mbegu maana yake umeiva. Kuna watu wengine ambao watapewa mbegu watakula na watasizingizia watasema Mungu unajua sehemu ninayopita… Kwani unafikiri Yusufu alikuwa hajui mahali wanapopita siku zote anawapa chakula siku hiyo akawapa mbegu, usile kitu ambacho Mungu amekuletea kama mbegu ya jibu la matatizo ya maisha yako, upate laki tano leo, kesho upate milioni moja , haiko hivyo. Mungu hakutuleta duniani tuishi kwa miujiza ametuita tuishi katika Neno lake na baraka zilizopo katika agano
Muujiza ni intervation Mungu anaingilia kati kushughulika na tatizo lako. Ukisharudi kwenye hali yako ya kawaida ana withdraw , unaanza kuishi sawa sawa na neno alilokupangia kwenye agano, kawaulize wana wa Israeli ,walipovuka mto mana ilikoma na wamekaa miaka 40 hawajui kulima,wakitaka tu chakula mana inashuka wakitaka nyama upepo unavuma wanapata kware.
Sasa anawaambia hamna kware nendeni mkafuge, hamna nafaka mkalime, wanasema hivi tukipanda leo tutavuna lini
Glory to God, Glory to God! Ameen.
Fullz/Pros/Leads
ReplyDeleteSSN DOB
SSN DOB DL
High CS Fullz
Fresh Spammed CC's
Many other leads & stuff
Spamming, Hacking, Carding Stuff
Legit stuff with Guarantee
Loan methods/Carding methods
All Hack Tools
Tutorials
Mailers
Brutes
& many more
What's app +92 317 2721122
Tele.gram @leadsupplier
ICQ 752822040
exploit.Tools4U AT GMAIL (DOT) COM