Saturday, 27 January 2018

Madhara ya kutumia ant-virus mbili.

MATATIZO YANAYOTOKANA NA KUTUMIA “ANT-VIRUS” MBILI TOFAUTI KWENYE KOMPYUTA MOJA.

“Ant-virus” ni software ambayo husaidia katika ulinzi wa Kompyuta zidi ya shambulio la virusi kwenye Kompyuta.  Hapa tunazungumzia Ant-virus kama Kaspersky, Escan, Microsoft Security Essentials, Defender AVG, n.k. Mara zote hutumika kama mlinzi/askari kwenye Kompyuta ili kuiweka katika hali nzuri ya usalama.

Lakini katika matumizi hayo watumiaji wengi wa Kompyuta wamekuwa wakitumia ant-virus mbili kwenye Kompyuta moja, kitendo ambacho hupelekea kutokea kwa matatizo mbalimbali kwenye Kompyuta, kama;

1. Vita/msuguano, hapa utakuta kila ant-virus kwenye Kompyuta inataka kuwa juu ya nyingine, na mara zote “mafahari wawili wakigombana kinachoumia ni nyasi” hivyo utakuta kinachoumia ni Program/ mafaili mbalimbali kwenye Kompyuta yako.

2. Kuzima kwa Kompyuta, msuguano unaotokea wa Ant-virus mbili kupambana kwenye Kompyuta hupelekea Kompyuta kuzima ghafla maana Kompyuta hushindwa kuhimili ugomvi unaotokea baina ya Ant-virus hizo mbili.

3. Kompyuta kufanya kazi polepole (Computer working slowly), hii hutokea hasa pale ambapo muda mwingi ukiwa una scan kitendo ambacho hutumia muda mrefu sana katika utendaji mzima.

4. Msuguano baina ya Ant-virus mbili tofauti pia unaweza kusababisha Ant-virus hizo mbili moja kuikamata nyingine kama Virus mwishowe kusababisha mataizo mengine kwenye Kompyuta.
Ushauri  ni kwamba ni vyema ukatumia Ant-virus moja ili kuondoa mkanganyiko na mgongano unaojitokeza ndani ya Kompyuta yako.

Lakini pia elewa kuwa ni muhimu sana pia kutumia Ant-virus ili kuweza kuikinga vyema na matatizo mbalimbali kwenye Kompyuta yako, kama kupotea kwa mafaili, kuliwa kwa baadhi ya Program n.k.
Kumbuka “Ant-Virus” ni ulinzi madhubuti wa Kompyuta yako.

1 comment:

  1. Fullz/Pros/Leads

    SSN DOB
    SSN DOB DL
    High CS Fullz

    Fresh Spammed CC's
    Many other leads & stuff

    Spamming, Hacking, Carding Stuff
    Legit stuff with Guarantee

    Loan methods/Carding methods
    All Hack Tools
    Tutorials
    Mailers
    Brutes

    & many more

    What's app +92 317 2721122
    Tele.gram @leadsupplier
    ICQ 752822040
    exploit.Tools4U AT GMAIL (DOT) COM

    ReplyDelete