MATATIZO YANAYOTOKANA NA KUTUMIA “ANT-VIRUS” MBILI TOFAUTI KWENYE KOMPYUTA MOJA.
“Ant-virus” ni software ambayo husaidia katika ulinzi wa Kompyuta zidi ya shambulio la virusi kwenye Kompyuta. Hapa tunazungumzia Ant-virus kama Kaspersky, Escan, Microsoft Security Essentials, Defender AVG, n.k. Mara zote hutumika kama mlinzi/askari kwenye Kompyuta ili kuiweka katika hali nzuri ya usalama.
Lakini katika matumizi hayo watumiaji wengi wa Kompyuta wamekuwa wakitumia ant-virus mbili kwenye Kompyuta moja, kitendo ambacho hupelekea kutokea kwa matatizo mbalimbali kwenye Kompyuta, kama;
1. Vita/msuguano, hapa utakuta kila ant-virus kwenye Kompyuta inataka kuwa juu ya nyingine, na mara zote “mafahari wawili wakigombana kinachoumia ni nyasi” hivyo utakuta kinachoumia ni Program/ mafaili mbalimbali kwenye Kompyuta yako.
2. Kuzima kwa Kompyuta, msuguano unaotokea wa Ant-virus mbili kupambana kwenye Kompyuta hupelekea Kompyuta kuzima ghafla maana Kompyuta hushindwa kuhimili ugomvi unaotokea baina ya Ant-virus hizo mbili.
3. Kompyuta kufanya kazi polepole (Computer working slowly), hii hutokea hasa pale ambapo muda mwingi ukiwa una scan kitendo ambacho hutumia muda mrefu sana katika utendaji mzima.
4. Msuguano baina ya Ant-virus mbili tofauti pia unaweza kusababisha Ant-virus hizo mbili moja kuikamata nyingine kama Virus mwishowe kusababisha mataizo mengine kwenye Kompyuta.
Ushauri ni kwamba ni vyema ukatumia Ant-virus moja ili kuondoa mkanganyiko na mgongano unaojitokeza ndani ya Kompyuta yako.
Lakini pia elewa kuwa ni muhimu sana pia kutumia Ant-virus ili kuweza kuikinga vyema na matatizo mbalimbali kwenye Kompyuta yako, kama kupotea kwa mafaili, kuliwa kwa baadhi ya Program n.k.
Kumbuka “Ant-Virus” ni ulinzi madhubuti wa Kompyuta yako.
Fullz/Pros/Leads
ReplyDeleteSSN DOB
SSN DOB DL
High CS Fullz
Fresh Spammed CC's
Many other leads & stuff
Spamming, Hacking, Carding Stuff
Legit stuff with Guarantee
Loan methods/Carding methods
All Hack Tools
Tutorials
Mailers
Brutes
& many more
What's app +92 317 2721122
Tele.gram @leadsupplier
ICQ 752822040
exploit.Tools4U AT GMAIL (DOT) COM