Monday, 29 February 2016

KASSIM MAJALIWA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-.

Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo kuanzia leo na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Alfred Luanda asimamie zoezi hilo mara moja.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Februari 29, 2016) kwenye kikao cha watumishi wa hospitali hiyo alichokiitisha baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu wenye wagonjwa waliolazwa.

Mara baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa nini wana dirisha moja la kupokelea wagonjwa wote. "Dirisha la wazee lipo?" akajibiwa hakuna. "Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo" nalo pia akajibiwa halipo. "Je wazee wana daktari wao", hakupata jibu.

"Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee  na uhakikishe wana daktari wao. Siyo kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana,"  alisema wakati akimwagiza Mgaga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Shaibu Maarifa.

Akiwa njiani kuelekea wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa waliokuwa wakiimba "tuna jambo, tuna jambo" wakiashiria kutaka kusikilizwa. Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuu alipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei za juu kwenye maduka ya dawa binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.

Lakini kero ya Bi. Tatu Abdallah aliyelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5 ili apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula ndiyo ilimgusa zaidi Waziri Mkuu.

"Februari mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za sh. 85,000/- hapo nje (pharmacy haikumbuki jina) pia uzi wa kushonea kwa sh. 25,000/-. Lakini pia daktari akasema anataka sh. 100,000/- ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji."

"Tarehe 12 Februari  baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000/- na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani".

"Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?" Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza. 

Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.

Akiwa njiani kuelekea theatre, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi umefanyika leo waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo. 

Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika.

"Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu Daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho," alisema. 

Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu amemwagiza RAS, RMO na Afisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi wote wa hospitali hiyo leo saa 9 alasiri na kisha wamletee taarifa.

Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuwa na huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Aliwataka waache tabia ya kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake wanaojifungua kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya Serikali.

Sakata la hospitali ya Ligula lilianza juzi (Jumamosi, Februari 27, 2016) wakati Waziri Mkuu akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa ambapo baadhi yao walikuwa wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya kutumbua.

Waziri Mkuu aliwajibu kuwa amesikia ujumbe wao na ataenda huko lakini alishindwa kutokana na ratiba za siku hiyo kumalizika jioni sana.

Waziri Mkuu amerejea Jijini Dar es Salaam mchana wa leo.

RARE DISEASE DUNIANI

Kila mwaka Siku ya mwisho ya Mwezi Wa Pili huadhimishwa Siku ya 'Rare Disease Duniani. Mwaka huu ni leo tarehe 29 Feb 2016.

Sharifa Mbarak ni mama mwenye watoto wawili ambao waliathirika na magonjwa hayo yasiyotambulika. Kesho ataongea na Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakiwamo na madaktari wa watoto Dr. Mariam wa Agakhan na Professor Kareem wa Muhimbili pamoja na Monica Joseph , mdau kutoka Philips Medical Systems katika hotel ya Serena Dar es Salaam, Saa 4 asubuhi katika kampeni ya kuhamasisha magonjwa yasiyotambulika.

Tunaomba ushiriki wako katika siku hii muhimu kwa Watoto wa Sharifa na watoto wote duniani wanaoteseka na magonjwa haya.

DR. KIGWANGALLA AAGIZA.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA KWA DUKA LA DAWA LA SHINE CARE PHARMACY LA TEMEKE KWA KUKIUKA UENDESHAKI WAKE.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.

Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.

Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n ahata kumsababishia matatizo.

Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.

MSHUKURU MUNGU.

1. Kama upo SINGLE na umekazana kusema "SIAMINI MTU KATIKA MAPENZI" kumbuka rafiki zako wanaoa na kuolewa kila siku. Acha mawazo hasi omba Mungu akujalie mwenza wa maisha ambae unaendana nae.

2. Kama upo ndani ya ndoa na umekazana kusema "NAICHUKIA HII NDOA" huoni wanandoa wengine ambao wanasheherekea jubilei ya miaka 20 ya ndoa zao?  Omba Mungu aiponye ndoa yako.

3. Kama umekazana kusema "NAMWACHA MUME WANGU, KWANI ANANISALITI" tafadhali hebu nenda mjini pita maeneo ya Kona Bar, Kimboka na maeneo kama hayo uone wanawake malaya wenye uchu ambao wanamsubiri kwa hamu mumeo wamchune vizuri ambao kwao hawajali haya ku share mwanaume. Omba Mungu aitengeneze ndoa yako.

4. Usikazane kusema "NAICHUKIA KAZI YANGU" angalia maelfu ya vijana ambao hawana ajira wanazunguka kila siku na mabahasha maofisini! Vipi unataka kujiunga nao? Kuwa na shukrani!

5. Umekazana kusema unapachukia unapoishi, tafadhali sana nenda kawatembelee watoto wa mitaani uone mazingira magumu wanayoishi! Mshukuru Mungu walau unalala hata kwenye godoro.

6. Wengine husema "NIMECHOKA NA HAYA MAISHA" sawa nenda mahospitalini na uone watu wanavyopigania maisha yao, nenda mochwari na utizame na uniambie unafikiri nini! Cha Mihimu ni kushukuru Mungu

Hebu nisikilize kwa makini......

Kutambua thamani ya miaka minne au mitatu, muulize mhitimu wa chuo kikuu

Kutambua thamani ya mwaka mmoja, muulize mwanafunzi aliyefeli mtihani wake wa mwisho, kutambua umuhimu wa miezi tisa muulize mama aliejifungua mtoto aliye njiti!

Kutambua thamani ya wiki moja muulize mhariri wa gazeti linalotoka kila wiki.

Kutambua thamani ya dakika moja muulize abiria aliyechelewa safari ya ndege, basi au treni.

Na kutambua thamani ya sekunde muulize mtu yeyote aliyenusurika katika ajali!

Furahia kila dakika ambayo mwenyezi Mungu amekupa kuendelea kuvuta pumzi yake! Acha kulalamika maisha ni jinsi wewe unavyoishi!

Kama upo hai mpaka leo shukuru kwa kusema "ASANTE MUNGU"

Sunday, 28 February 2016

GOLI LA KWANZA LA MBWANA SAMATTA.

Jumapili ya February 28 Ligi Kuu Ubelgiji iliendelea tena kwa klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta kushuka katika uwanja wake wa  nyumbani Cristal Arena kucheza mchezo wake wa 28 wa Ligi Kuu dhidi ya vinara wa Ligi Club Brugge.

Licha ya kuwa Club Brugge walikuwa wanarekodi nzuri dhidi ya Genk wamekubali kipigo cha goli 3-2, kwani kabla ya mchezo huo, Genk na Brugge kwa mechi tano zilizopita, Brugge walikuwa wameifunga Genk mara tatu, sare moja na kupoteza mechi moja

Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 31, ikiwa ni dakika 21 zimepita toka Club Brugge wapate goli la kuongoza dakika ya 15 kupitia kwa Thomas Meunier, lakini kasi ya Genk iliongezeka na kupata goli la pili dakika ya 50 kupitia kwa Thomas Buffel.

Mbwana Samatta aliingia dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis aliyefunga goli la kwanza la KRC Genk. mabadiliko ya kuingia Mbwana Samatta yalikuwa na faida kwani, dakika 2 baada ya kuingia alipachika goli lake la kwanza akiwa na Genk lakini pia ni goli la tatu kwa Genk, kabla ya dakika ya 83 Brugge walifanikiwa kupata goli la pili.

Demokrasia barani Africa.

Kwa ufupi

Pamoja na tafsiri nyingi zilizowahi kutolewa na kufundishwa, utekelezaji wa dhana ya demokrasia hapa Afrika una tafsiri maalum kutoka kwa vyama vilivyokaa madarakani muda mrefu au wakuu wa nchi waliosalia madarakani kwa muda mrefu.

Habari
SUNDAY, FEBRUARY 28, 2016
DARUBINI YA MTATIRO :
Demokrasia ya Afrika ni uhuni
mtupu!

Julius Mtatiro
Wengi wetu walipokuwa shule za msingi na sekondari walisikia na kulijua neno demokrasia kwa mara ya
kwanza likitajwa na kupewa maana zake.

Moja ya maana za demokrasia ni “utawala wa watu kwa ajili ya wao wenyewe...” na tena maana nyingine ni “utawala unaowekwa na watu kwa
kufuata misingi waliokubaliana”.

Pamoja na tafsiri nyingi zilizowahi kutolewa na kufundishwa, utekelezaji
wa dhana ya demokrasia hapa Afrika una tafsiri maalum kutoka kwa vyama vilivyokaa madarakani muda mrefu au
wakuu wa nchi waliosalia madarakani kwa muda mrefu.

Kuna demokrasia mbili Afrika, ile ya watawala na ya watawaliwa. Ya watawala haitabiriki na inakuwapo pale wanaposhinda uchaguzi kupitia njia mbalimbali na hasa kwa msaada wa vyombo vya dola, mabavu, rushwa, vitisho, mifumo ya uongozi ya kiupendeleo na tume za uchaguzi zinazoongozwa na wao wenyewe.

Demokrasia hii ya watawala
imeonekana Zanzibar kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 watawala walipoona Maalim Seif Sharif Hamad anaelekea kushinda uchaguzi wakazuia
kwa nguvu matokeo yasiendelee kutangazwa na kisha yakafutwa na ‘mtu’ mwenye dhamana ya kuisimamia tume kwa kufuata kanuni za uchaguzi, sheria na katiba ambavyo hata mara
moja havimpi yeye au tume nzima mamlaka ya kufuta matokeo ya jumla ya uchaguzi na ambayo yamethibitishwa na ngazi za wasimamizi wa uchaguzi.

Matokeo yaleyale yaliyomzuia Maalim Seif kuwa rais wa Zanzibar ndiyo yakampaisha Rais John Magufuli kutangazwa kuwa Rais wa Tanzania.

Kidemokrasia (Demokrasia ya
Tanzania) kwa tafsiri ya dola na chama kinachoongoza dola ni pale ambapo wagombea wa CCM wangelikuwa wanaongoza wote, lakini pia bila aibu aliposhindwa mmoja wakashindwa kujibaraguza ilimradi wazuie matokeo yote ya Zanzibar kwa chaguzi zote
(urais wa Jamhuri na ule wa Zanzibar) na kwa hivyo uchaguzi wa marudio
unaokwenda kufanyika Zanzibar (huku vyama vyenye nguvu kama CUF vikiwa vimeususia) ungelifanyika kwa nafasi zote za urais wa Jamhuri na ule wa Zanzibar.

Ndiyo kusema hadi leo wakati fukuto la Zanzibar linaendelea Jakaya Kikwete angepaswa kuwa madarakani huku
John Magufuli (aliyekuwa anaongoza kura za urais wa Jamhuri wakati matokeo ya Zanzibar yanafutwa) akisubiri apigiwe kura upya Zanzibar
kabla ya kutangazwa mshindi wa jumla wa uchaguzi wote.

Kwa vyama vilivyoongoza Afrika muda mrefu demokrasia ni jambo la upande mmoja, ni jambo la wao wanataka kupata nini, ni jambo la wanachokipata
kinawatosha kiasi gani!

Watawala wa Afrika huitafsiri demokrasia yao na kuilazimisha ikubalike hivyo ilivyo kwa kadri watakavyoamua, na hapo
ndipo bara hili linakwama.

Kwenye shule zetu watoto wanaendelea kufundishwa demokrasia ni maamuzi
ya wananchi na wengine wanadhani jambo hilo ni dhahiri, kwenye utekelezaji demokrasia ya Kiafrika ni
tofauti na kile kinachofundishwa na
labda kinachofanywa na wenye demokrasia wenyewe, huko nchi za Magharibi.

Mwalimu Kitila Mkumbo (Profesa) mara kadhaa amepata kuandika juu ya
“dhana ya demokrasia ya Afrika” na amekuwa akihoji ikiwa kuna haja ya
Afrika kuendelea na demokrasia hiyo ya maigizo badala ya kukaa chini na
kuamua moja na hata kuanzisha demokrasia ya Afrika na kuijulisha dunia “hii ndiyo demokrasia yetu!”

Kitila anaongelea dhana pana ya unafiki mkubwa unaofanywa na viongozi wa Afrika kuanzia kwenye ngazi ya chama kimoja kimoja (kilichoshika dola na visivyoshika dola) na ngazi ya nchi ambapo vyama vyote
hukutana na kushindana ili kimoja kipate ushindi wa jumla.

Hii ni wiki ambayo nchini Uganda kumekuwa na gumzo la Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni na wakati
wananchi wa kawaida wanaimba mabadiliko wayatakayo, vyombo vya
dola na rais aliyeko madarakani,
Yoweri Museveni wanasimamia kile
wanachokiamini kama “ni lazima Museveni aendelee kutawala”. Katika wiki ya mwisho ya uchaguzi, kiongozi
mkuu wa upinzani nchini Uganda, Kiza Besigye, alikamatwa na kushikiliwa mara tatu.

Mara ya mwisho ni siku ya
uchaguzi yenyewe tena akiwa katika mizunguko ya kufuatilia mienendo ya uchaguzi. Kiongozi mwingine wa
upinzani, Amama Mbabazi naye aliwekwa jela ya nyumbani kwake siku
ya uchaguzi.

Haya yote yakifanywa na majeshi ya Uganda yakishirikiana na walinda
usalama wengine, hii ndiyo demokrasia ya Afrika. Museveni hana mpango wa
kuondoka madarakani na kwake yeye na wanaonufaika moja kwa moja na utawala wake ‘demokrasia sahihi ni
yeye kutawala!”

Ukihamia pale Burundi utakumbana na matatizo makubwa, Pierre Nkurunziza
amekatalia madarakani, alifanya uchaguzi wa upande moja akajihalalisha kuendelea kuwa mtawala wa Burundi. Kwa Nkurunzinza, tafsiri
ya demokrasia ni yeye kuendelea kuitawala Burundi.
Mamia ya watu waliouawa kwenye machafuko yaliyoongozwa na vyombo
vya dola ili kuwanyamazisha
wapinzani wa Nkurunziza, hakujali, kwake demokrasia ni “kusalia madarakani” hata kama watu wanakufa!

Majirani zetu Wanyarwanda wanapita kwenye yaleyale, Rais Paul Kagame anaamini hakuna Mnyarwanda mwenye uwezo wa kuongoza nchi hiyo,
amekaa madarakani miongo miwili na bado yumo tu, yeye tu! Vyama vilivyosajiliwa pale Rwanda vinafanya kazi kama wakimbizi.

(Julius Mtatiro ni mchambuzi wa masuala ya Kijamii na Kisiasa (Adv Cert in Ling, B.A, M.A, L LB) +255787536759,

juliusmtatiro@yahoo.com).

WALIMU DAR HIACE BURE

Walimu wa shule za msingi na sekondari za umma mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paulo Makonda na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar wanazungumza na wanahabari hivi sasa.

Walimu watatengenezewa vitambulisho maalum ili kuwaondolea usumbufu.
Huduma hiyo ni katika kuwapunguzia adha ya usafiri na ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure.

Muda wa kuwasafirisha bure ni saa 11.30 hadi 2 asubuhi na saa 9 hadi 11 jioni.

HAPANA CHEZEYA MAKONDA.

CWT MPYA YAJA.

Chama Kipya cha Walimu Chasajiliwa Kikiwa na Wanachama zaidi ya 9,000 | CWT Tumbo Joto Mpasuko Unakuja!

CHAMA kipya cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kimesajiliwa rasmi na kupata cheti cha usajili wa kudumu kutoka Wizara ya Kazi na Ajira.

Akizungumza na FikraPevu, Katibu Mkuu wa Chakamwata, Mwalimu Meshack Kapange, anasema chama hicho kipya kinaundwa na walimu nchini waliojiondoa kutoka mikononi mwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). 

Kapange amesema mchakato wake wa kukisajili chama hicho ulianza miaka minne iliyopita, hadi hivi juzi kilipopewa usajili wa kuendelea na shuhuli zake kisheria.

“Ni furaha iliyoje kupata usajili huu wa chama chetu cha kutetea haki na maslahi ya walimu? Huu ni ukombozi kwa walimu wanaokatwa asilimia mbili za mishahara yao bila kurejeshewa wanapostaafu,” anasema Katibu Mkuu huyo.

Kuundwa kwa chama kipya hicho kumetajwa na wachambuzi wa mambo kwamba kunaweza kuipasua CWT na pia kutahitimisha ukiritimba wa muda mrefu wa chama hicho. Aidha, chama hicho kitatoa fursa sasa kwa walimu nchini kuwa na hiyari ya kujiunga na chama ambacho wataona kina maslahi kwao badala ya ilivyo sasa ambapo walimu walikuwa hawana chaguo zaidi ya kujiunga na CWT.

Kwa mujibu wa Mwalimu Kapange, Makao Makuu ya sasa ya chama hicho yatakuwa Jijini Mbeya. Anasema walimu watakaohitaji kujiunga na chama hicho kipya, watafanya hivyo kwa hiari yao kama sheria za kazi zinavyoelekeza tofauti na CWT ambayo kila mwalimu anayepata ajira serikalini alikuwa analazimishwa kujiunga na kuanza kukatwa fedha zake kutoka kwenye mshahara wake bila ridhaa yake na kinyume cha sheria za ajira.

“Kila mwanachama atachangia asilimia moja tu ya mshahara wake kwa kila mwezi badala ya asilimia mbili kama ilivyo kwa CWT. Wakati mwanachama anapostaafu, atapewa ‘bonus’ kama asante kwa kuchangia Chama,” anasema Mwalimu Kapange.

Mbali na hilo, Kapange anasema Chakamwata kitafanya jitihada za kuwajengea wanachama wake uwezo wa kutambua wajibu wao, haki zao na jinsi ya kuzidai, badala ya kutambua wajibu pekee kama ilivyo ndani ya CWT, kwa maelezo kwamba hakuna wajibu kwa mtumishi yeyote wa umma usiokwenda sambamba na haki yake.

“Tulipokuwa tukiomba usajili kwa mara ya kwanza Mei, 2012, tulikuwa wanachama 400 ingawa masharti ya kisheria ya kuanzisha vyama kama hivi yanataka wanachama 20 tu.

Nashukuru kwamba hadi tunapata usajili huu, wanachama wetu wanafikia 9,743, wengi wao wakitokea mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Arusha, Mara, Morogoro, Singida na Kagera,” amesema.

Chama kipya hicho, kabla hakijasajiliwa, kilikuwa kikijulikana kwa jina la Umoja wa Maofisa Elimu Tanzania (UMET). Hata hivyo, uongozi wa muda wa chama hicho ulikaa tena na kukipa chama hicho jina la Chakamwata.

Chama hicho kimepewa usajili kwa namba 031, huku cheti chake kikiwa kimesainiwa na Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri nchini, Doroth Uiso.

FikraPevu inaendelea kumtafuta Rais wa CWT, Gratian Mukoba, pamoja na maoni ya walimu mbalimbali nchini, ili pamoja na mambo mengine, waweze kuelezea ujio wa chama kipya hicho cha walimu nchini na athari zake katika mstakabali wa mshikamano na utengamano wa walimu nchini katika siku za usoni.

Toa maoni yako hapo chini

 

IJUE SIMU YAKO.

JINSI YA KUJUA SIMU ORIGINAL NA FEKI

Kabla hujanununa simu mpya hakikisha unaandika namba hii *#06# , itaonyesha namba ya pekee (serial number ) au IMEI (International Mobile Equipment Identity) namba ambayo ni lazima ziwe namba 15 au zaidi, na ni lazima ianze na namba 35.

1. Sasa angalia kwa makini kama namba unazoziona zinafanana moja kwa moja na namba zilizoandikwa katika simu yako sehemu ambayo betri inakaa (battery base). Namba hizi zinapaswa kufanana kwa simu ambayo ni origino.

2. Simu yaweza kuwa origino lakini katika viwango nya ubora(qualities ) tofauti . Sasa tuanze kuchambua IMEI ili kujua ubora. Katika namba hizo namba ya saba(7) na ya nane (8) ndizo zinazohakikisha ubora wa simu yako.

= Kama namba ya saba na ya nane ni 00 inamaana kuwa simu yako imetengenizwa kwa ubora wa juu kabisa katika viwanda vya kuaminika.

= Kama namba ya saba na y a nane ni 01 au 10 inamaana simu yako imetengeneza Finland na ina ubora wa juu pia.

=Kama namba ya saba na ya nane ni 13 inamaana simu yako imeunganishwa katika nchi ya Azerbaijan na ni hatari sana kwa matumizi na afya yako.

=kama namba ya saba na ya nane ni 02 au 20 inamaana simu yako imeunganishwa katika nchi ya Emirates hivyo ina kiwango cha chini sana.

= Kama namba ya saba nay a nane ni kati ya 03 au 30 au 04 au 40 inamaana simu yako imetengenezwa China lakini ina ubora mzuri ila haijafikia zile zenye 00 , 01 au 10.

=Kama namba ya saba na ya nane ni 05 au 50 inamaana simu yako imatengenezwa labda Brazil ama USA ama Finland.

= Kama namba ya saba na ya nane ni 06 au 60 simu yako imetengenezwa Hong Hong, China au Mexico.

= Kama namba ya saba na ya nane ni 08 au 80 simu yako imetengenezwa Germany na ina ubora wa kawaida.

Unaweza pia kuangalia simu uliyonayo sasa kujua kama unatumia simu origino au feki na yenye kiwango gani!!

JOB VACANCY

Jhpiego JOB ADVERTISEMENT

Kindly circulate widely.

The Sauti Program is a USAID-funded initiative to improve the health of all Tanzanians through a sustained reduction in new HIV infections in support of the Government of the United Republic of Tanzania.  Sauti uses vulnerability-tailored evidence-based interventions to bring high-quality HIV prevention, HIV adherence support, and family planning promotion and service delivery to key and vulnerable populations (KVPs) in selected regions of mainland Tanzania.

The Sauti program has a Research Portofolio with the following vacant positions for immediate
hiring [successful candidates must be able to start working on 14th  March 2016]

Position: Regional Coordinator – 5 positions – [1 position in each of the following regions: Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Njombe, Shinyanga regions]

Contractual duration: Six Months [From March 14, 2016]

Required Qualifications:
At least an undergraduate  degree
At least two years of research experience.
Experience of working with Key Population would be an added advantage
Have to be inhabitant of the region choosing to apply for. 

Roles and responsibilities:
Maintain liaison between the field teams and the Field Coordinator
Plan all field activities and ensure logistic and communication support within each region;
Assist the technical team in developing and training the field team;
Ensure that data collection proceeds according to given protocol and assure the quality of data;
Conduct regular meetings with the teams to highlight field problems and provide solutions;
Provide regular updates to the Field coordinator and technical team on weekly basis.

Position: Teams/Field Supervisors – 5 positions – [1 position in each of the following regions: Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Njombe, Shinyanga regions]

Contractual duration: Six Months [From March 14, 2016]

Required Qualifications:
At least an undergraduate  degree
At least one years of research experience.
Experience of working with Key Population would be an added advantage
Have to be inhabitant of the region choosing to apply for. 

Roles and responsibilities:
The team supervisor is responsible for overview and managing field work for a specific key population groups. Separate team supervisors will be hired for different key population teams. The following are typical roles.
To conduct daily meetings and brief the team about the day’s work in the morning meeting;
Plan field activity along with the team leader in such a manner that it can be completed in the required time frame;
Debrief the team during evening meetings, discuss field issues and suggest appropriate solutions;
Arrange for social mobilizers, and introduce team members to the various social mobilizers in order to facilitate the field work/interviewing process;
Maintain close contact with team members in order to closely monitor and support data collection at each stage including sampling specifications (sampling points, selection of respondents), and interviewing specifications. This is necessary to ensure quality and consistency throughout the data collection process;
Supervision of interviews being conducted on regular basis ;
Review and edit a random number of completed questionnaires to ensure that all questionnaires filled by the team members are complete and according to guidelines;
Edit forms daily along with the data coder and apprise the team about mistakes;
Maintain records and dispatch of filled questionnaire to the Data Manager
Monitor the work-in-progress, prepare and submit weekly reports to the Field Coordinator.

Position: Virtual Mapper – 2 positions – [Based in Mwanza]

Contractual duration: Six Months [From March 14, 2016]

Required Qualifications:
Bachelor of Computer science
At least one year of research experience
Have to be inhabitant of the region choosing to apply for. 

Roles and responsibilities:
Administer a questionnaire/form to KIs to develop a list of websites and apps that particular key population group in the region use to meet sexual partners. If possible, specify where these sites and apps are used (e.g. specific cities or other geographic entities)

Visit the site or app to list the list the following
Name of the website/app
Type of site (geo-social site using GPS or not)
Expected days of the week and times of the day when the volume of men on the site is expected to be high. 
Subscription fee for an active profile
Description of search criteria to use on the site

Description of how to distinguish between people registered on the site and people online/active during the scheduled observation.

Position: Research Assistant/Interviewers – 20 positions – [4 position in each of the following regions: Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Njombe, Shinyanga regions]

Contractual duration: Six Months [From March 14, 2016]

Required Qualifications:
Hi School or equivalent
At least one years of research experience.
Have to be inhabitant of the region choosing to apply for. 

Roles and responsibilities:
Conduct interviews according to the provided training and guidelines;
Be prepared, and have all the necessary supplies: e.g. questionnaires, guidelines, a pen or pencil, required administrative forms (such as log books which may vary from one setting to another);
Ensure confidentiality of information, and eliminate any apprehensions and fears from the minds of the study subjects;
Field edit and complete all questionnaires;
Hand over completed questionnaires to the team supervisors after field editing;
Develop a strong working relationship with the social mobilizers and provide them any field assistance if required.

Position: Social Mobilizers – 10 positions – [2 position in each of the following regions: Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Njombe, Shinyanga regions]

Contractual duration: Six Months [From March 14, 2016]

Required Qualifications:
Should be active members of the key population group and should be willing to participate and facilitate field work.
Preferably graduates in social sciences
Have to be inhabitant of the region choosing to apply for. 

Roles and responsibilities:
To make key populations approachable for the field teams so that interviews can be conducted. .
Facilitates the field team in approaching the high risk groups.
To help the field team in recruiting genuine high risk groups from different spots in each region.

Position: Data Clerks – 10 positions – [2 position in each of the following regions: Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Njombe, Shinyanga regions]

Required Qualifications:

Diploma/certificate in IT, EMR, Social Work or other relevant area.
At least 1 years of experience working with data management.
Proven analytical and numerical capabilities.
Must demonstrate self-management (i.e. motivation, dealing with pressure, adaptability)
Have to be inhabitant of the region choosing to apply for

Roles and responsibilities:

To enter data to the  Database provided for the Task
To ensure appropriate recording of qualitative Data
To be ethical and professional during data collection process
To organize and store all documents and tools for the survey program as directed by  their supervisor

Jhpiego offers a competitive package to the selected candidate in line with salary history, academic qualifications and relevant experience. If you feel you are the right candidate, apply in confidence, indicating the post you are applying for and the location you want to be based. Please include your up-to-date CV with three contactable professional references, covering letter and your salary history.

Send the Application to the office you saw this advertisement [NIMR or Jhpiego Office]: 

BUT:
Should be addressed to:
The Director of Human Resource
Jhpiego, PO Box 9170, Plot 72, Block 45B, New Bagamoyo road, Victoria
Dar es Salaam, Tanzania

Or through email at: HRTZ@jhpiego.org 

Please note that, only shortlisted candidates will be contacted. These positions are for immediate hiring, the advert will close on 4th March 2016

KINDLY CIRCULATE WIDELY TO YOUR NETWORK.

JARIBU BAHATI YAKO.

Thursday, 25 February 2016

BADILI KUFIKIRI KWAKO!

RAFIKI YANGU KIPENZI

Kwako rafiki, rafiki yangu kipenzi maisha ndiyo yapo hivi! Binafsi Ndg. Jack Ma (tajiri wa 33 duniani) ni mfano bora sana kwangu, ni kioo ambacho najitazama, naona nina mengi ya kujifunza toka kwake!

Ningeandika mengi sana juu yake nikimlinganisha na wewe hapo, inawezekana upo katika vita kali sana kuelekea mafanikio na kutimiza mahitaji yako. Lakini shaka kuu bado SPIRIT (ROHO) yako imevunjikavunjika (haina matumaini) sababu inawezekana mazingira uliyozaliwa na kukulia yamepelekea hivyo, toka ukiwa mdogo unaaelezwa UONGO,uongo juu ya maisha (uongo hukutenganisha na amani,furaha na mafanikio).

Maisha hayahitaji akili nyingi sana za darasani, maisha hayahitaji uzuri wa sura wala umbo, wala kifua kinene ili uwe na amani, furaha na mafanikio mengine. Maisha ndiyo haya haya uliyonayo sasa.

Unanafasi kubwa sana ya kuishi maisha unayohitaji au unayotamani, maisha ni wewe,sio baba yako, maisha ni wewe sio mama yako, wala ndugu yako yeyote.

Wangapi wapo leo wana-ishi maisha ya amani, furaha na mafanikio makubwa maishani mwao lakini hamfahamu baba yake ata kwa kwa picha tu,unashangaa? Yes, hamfahamu baba yake, na ajabu ya Mungu mama yake alifariki akiwa bado mdogo kabisa baada ya kumzaa!

Akalelewa na ndugu na jamaa,kisha akakua na maisha yanaendelea. Maisha yanahitaji SPIRIT(ROHO) ISIYO-ONA KUUMIA,maisha yanahitaji SPIRIT (ROHO) INAYO-ONA mahitaji unayo yataka tu, unahitaji ufanye biashara-basi kutwa fikiri juu ya io biashara unayotaka,mfano unataka uanzaje,iweje na uendeshaje, unahitaji nyumba na gari, basi kutwa fikiri juu aina nyumba na aina ya gari unayohitaji, unahitaji mchumba basi muda wote na popote fikiri juu ya aina ya mchumba unaye muhitaji,

LOLOTE UNALOFIKIRIA ndiyo LINALOTOKEA,una kataa? umefikiria hauna pesa...au unapesa kidogo, amini na kwambia lazima katika uhalisia utakuwa hauna pesa au unapesa kidogo kweli, LAZIMA! sio bahati mbaya, bali ndivyo unavyo fikiri muda mwingi zaidi (unafikiria zaidi kukosa pesa). Sasa hizo pesa nyingi zitakujaje wakati muda mwingi unatumia kufikiri juu ya kidogo au kukosa? lazima upate kidogo au ukose kabisa.

Jiondoleee mipaka katika kufikiri juu ya hitaji lako, maana kwa ROHO na KWELI-LOLOTE LINAWEZEKANA.

Tubadili kufikiri kwetu wapendwa!

10 BEST STUDENTS 2015

NECTA CSEE 2015: Best Top Ten Performing Students

This is a List of students that performed best than any other students in Tanzania Form Four Results 2015!

1. Butogwa Charles Shija- Canossa Girls
2. Congcong Wang -Feza Girls
3. Innocent Lawrence -Feza Boys
4. Dominick Marco Aidano – Msolwa
5. Sang’udi E Sang’udi -Ilboru Boys
6. Asteria Herbert Chilambo -Canossa Girls
7. Belinda Jackson Magere – Canossa Girls
8.Humfrey Martine Kimanya-Msolwa
9. Bright B Mwang’onda – Marian Boys
10. Erick R Mwang’ingo – Marian Boys

Wednesday, 24 February 2016

NGELI ZA KISWAHILI

Kufahamu ngeli za Kiswahili kunamwezesha mwanafunzi kuelewa upatanisho wa kisarufi katika sentensi, kutambulisha maumbo ya umoja na uwingi pia kufahamu uhusiano wa Kiswahili na lugha zingine.

Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.

Kufahamu ngeli za Kiswahili kunamwezesha mwanafunzi kuelewa upatanisho wa kisarufi katika sentensi, kutambulisha maumbo ya
umoja na uwingi pia kufahamu uhusiano wa Kiswahili na lugha zingine.

Ngeli ya A–WA hutumika kurejelea viumbe vilivyo hai (wanyama na watu). Majina mengi katika ngeli ya A-WA huanza kwa sauti M- kwa umoja na sauti WA- kwa wingi.

Hata hivyo baadhi ya majina huchukua miundo tofauti.
Mifano; mgonjwa - wagonjwa, mchungaji - wachungaji, mwizi-wezi, mtu- watu.
Muundo ulio tofauti na maelezo hapo juu ni kama mbuzi-mbuzi, kwale - kwale  nyati - nyati kifaru – vifaru.

Ngeli ya LI-YA husimamia nomino zenye miundo mbalimbali. Licha ya majina ya vitu visivyo hai, ngeli hii pia hutumika kwa majina yote katika hali ya ukubwa (yakiwamo ya watu au wanyama). Majina mengi huanza kwa JI- au J- kwa umoja na hubadilishwa kuanza
na MA- au ME- kwa wingi.

Majina mengine
ambayo huanza kwa sauti nyingine kama vile /b/, /d/, /g/, /k/, /z/ n.k ambayo huwekwa katika wingi kwa kuongeza kiungo MA-
Mifano; jimbo - majimbo, jicho - macho, jiko - majiko, jino - meno, maua, umbo - maumbo,
bati - mabati.

Ngeli ya KI - VI hurejelea vitu visivyo hai ambavyo majina yao huanza kwa KI- au CH-
(umoja) na VI- au VY- (wingi).
Mifano; kijiko - vijiko, kikapu - vikapu, kioo- vioo, choo - vyoo, chumba - vyumba, chuma -
vyuma, chungu - vyungu.

Ngeli ya U - I
huwakilisha nomino za vitu visivyo hai na ambavyo majina yake huanza kwa sauti M -
(umoja).
Mifano; mfupa - mifupa, mtambo - mitambo,
mfuko – mifuko.
Ngeli ya U - ZI hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI-
kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Mifano; ufunguo - funguo, ukuta – kuta.

Majina ya silabi mbili katika ngeli hii huongezwa NY katika uwingi. Mifano; uzi - nyuzi, uso – nyuso.

Ngeli ya I - ZI hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (wingi).

Aghalabu haya ni majina ya vitu ambayo huanza kwa sauti N, NG, NY, MB, n.k
Mifano; nyumba - nyumba, nguo - nguo, mbegu - mbegu, nyasi - nyasi, nyama – nyama.

Ngeli ya U - YA hujumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u-katika umoja na ma-
katika uwingi. Mifano; unyoya - manyoya.

Ngeli ya KU huwakilisha majina yanayotokana na vitenzi kwa vitenzi vinavyoanza na ku-
(huitwa vitenzi jina). Mfano Kusoma kwetu kumetusaidia, Kusema uongo kumemponza.

Ngeli ya mahali PA - KU – MU. Ngeli ya PA hurejelea mahali maalumu, padogo au palipo
wazi. Ngeli ya KU hurejelea mahali fulani kwa jumla au eneo fulani. Ngeli ya MU - hutumika kurejelea mahali ndani ya kitu kingine kama vile ndani ya nyumba, shimo n.k.

Ngeli za mahali hubaki vivyo hivyo katika umoja na wingi Hivyo, mwanafunzi anaweza kufanya mazoezi kadiri awezavyo kwa kutunga sentensi umoja na uwingi kwa kutumia neno au kitenzi jina ili kubaini kundi husika la neno au maneno.

Mwandishi ni mtaalamu wa
Kiswahili.chanzo.KISWAHILI KWA WANAFUNZI: Ngeli tisa za Kiswahili na upatanisho wa kisarufi - Makala - mwananchi.co.tz

Tujifunze kiswahili yetu!

Tuesday, 23 February 2016

WIZI WA SIMU BASI!

Hakuna kuibiwa simu tena...

If u lose your mobile you can trace it back.

Most of us always fear that our Mobile may be stolen at any time.

Each mobile carries a unique
IMEI no. i.e. International Mobile Equipment Identity No which can be used to track your mobile anywhere in the world.

This is how it works!!

1. Dial *#06# from your mobile.

2. Your mobile shows a unique 15 digit.

3. Note down this number at a secure place except in your mobile phone itself as this is the Number which will help trace your mobile in Case of a theft.

4. Once stolen you just have to E-mail this 15 digit IMEI No. to cop@vsnl.net with details as below.
  
Your name:____________________
Address:______________________
Phone model:_________________
Make:_________________________
Last used No.:_________________
E-mail for communication:_____
Missed date:___________________
IMEI No :_______________________

5. No need to go to the police.
 
6. Your Mobile will be traced within next 24 hrs via a complex system of GPRS and internet, You will find where your hand set is being operated and the new user's no. will be sent to your email.

Let's be very carefully friends.

JIFUNZE KISWAHILI

Leo tujifunze lugha teule ya Kiswahili.
1. password- Nywila.
2. juice - sharubati.
3. chips - vibanzi.
4. PhD - uzamifu.
5. Masters - uzamili.
6. Degree - shahada.
7. Diploma - stashahada.
8. Certificate - Astashahada.
9. keyboard - kicharazio.
10. scanner - mdaki.
11. Flash disk - diski mweko.
12. Mouse - kiteuzi.
13. Floppy disk - diski tepetevu.
14. Computer virus - mtaliga.
15. Distillation- ukenekaji.
16. Evaporation - mvukizo.
17. Synthesis- uoanishaji.
18. Oesphagus- umio.
19. Green house - kivungulio.
20. Femur - fupaja.
21. Germ cell - selizazi.
22. Humus - mboji.
23. Nector - mbochi.
24. Nector - Ntwe.
25. Nutrients - virutubisho.
26. Appetizers - vihamuzi.
27. ATM - Kiotomotela.
28. Bussiness card - kadikazi.
29. scratch card - kadihela.
30. simcard - kadiwia/mkamimo.
31. memory card - kadi sakima.
32. micro wave - Tanuri ya miale.
33. Laptop - kipakatarishi.
34. power saw - msumeno oto.
35. Duplicating machine - kirudufu.
36. photocopier- kinukuzi.
37. cocktail party - Tafrija mchapulo.
38.Air conditioner- Kiyoyozi.
39. lift- kambarau

Let's learn Swahili language.

MCHUMBA HASOMESHWI.

Kijiji cha Bulongwa, wilayani Makete mkoani Njombe mwanaume anayetambulika kwa jina la Sylvester Mgowolwa amejinyonga baada ya kumyonga mchumba wake hadi kumuua.

Kahimu RPC Njombe SSP JohnTemu amedhibitisha kutokeea kwa tukio hilo. Kamanda Temu amesema kuwa Marehemu aliacha ujumbe kwamba sababu ya kujiua na kumuua mpenzi wake ni kwa kuwa alimsomesha chuo cha Nursing, akamfungulia duka la dawa baridi, na kumjemgea nyumba ya kuishi mjini Njombe.

Lakini baada ya muda mpenzi wake huyo akaanza kubadilika. Mgogoro huo ulikua mkubwa na mwanaume akaomba kuachana lakini kwa kugawana mali ambazo alimnunulia mchumba wake. Mchumba alikataa na ndipo kijana huyo alipoamua kumnyonga na kumuua kabla ya kujinyonga yeye mwenyewe!

Let's be care wapendwa!!!