Thursday, 25 February 2016

BADILI KUFIKIRI KWAKO!

RAFIKI YANGU KIPENZI

Kwako rafiki, rafiki yangu kipenzi maisha ndiyo yapo hivi! Binafsi Ndg. Jack Ma (tajiri wa 33 duniani) ni mfano bora sana kwangu, ni kioo ambacho najitazama, naona nina mengi ya kujifunza toka kwake!

Ningeandika mengi sana juu yake nikimlinganisha na wewe hapo, inawezekana upo katika vita kali sana kuelekea mafanikio na kutimiza mahitaji yako. Lakini shaka kuu bado SPIRIT (ROHO) yako imevunjikavunjika (haina matumaini) sababu inawezekana mazingira uliyozaliwa na kukulia yamepelekea hivyo, toka ukiwa mdogo unaaelezwa UONGO,uongo juu ya maisha (uongo hukutenganisha na amani,furaha na mafanikio).

Maisha hayahitaji akili nyingi sana za darasani, maisha hayahitaji uzuri wa sura wala umbo, wala kifua kinene ili uwe na amani, furaha na mafanikio mengine. Maisha ndiyo haya haya uliyonayo sasa.

Unanafasi kubwa sana ya kuishi maisha unayohitaji au unayotamani, maisha ni wewe,sio baba yako, maisha ni wewe sio mama yako, wala ndugu yako yeyote.

Wangapi wapo leo wana-ishi maisha ya amani, furaha na mafanikio makubwa maishani mwao lakini hamfahamu baba yake ata kwa kwa picha tu,unashangaa? Yes, hamfahamu baba yake, na ajabu ya Mungu mama yake alifariki akiwa bado mdogo kabisa baada ya kumzaa!

Akalelewa na ndugu na jamaa,kisha akakua na maisha yanaendelea. Maisha yanahitaji SPIRIT(ROHO) ISIYO-ONA KUUMIA,maisha yanahitaji SPIRIT (ROHO) INAYO-ONA mahitaji unayo yataka tu, unahitaji ufanye biashara-basi kutwa fikiri juu ya io biashara unayotaka,mfano unataka uanzaje,iweje na uendeshaje, unahitaji nyumba na gari, basi kutwa fikiri juu aina nyumba na aina ya gari unayohitaji, unahitaji mchumba basi muda wote na popote fikiri juu ya aina ya mchumba unaye muhitaji,

LOLOTE UNALOFIKIRIA ndiyo LINALOTOKEA,una kataa? umefikiria hauna pesa...au unapesa kidogo, amini na kwambia lazima katika uhalisia utakuwa hauna pesa au unapesa kidogo kweli, LAZIMA! sio bahati mbaya, bali ndivyo unavyo fikiri muda mwingi zaidi (unafikiria zaidi kukosa pesa). Sasa hizo pesa nyingi zitakujaje wakati muda mwingi unatumia kufikiri juu ya kidogo au kukosa? lazima upate kidogo au ukose kabisa.

Jiondoleee mipaka katika kufikiri juu ya hitaji lako, maana kwa ROHO na KWELI-LOLOTE LINAWEZEKANA.

Tubadili kufikiri kwetu wapendwa!

No comments:

Post a Comment