Thursday, 31 March 2016

SnapChat: Waweza kwenda Jela.

SnapChat: Watumiaji Wa Uk Wanaweza Kwenda Jela Kwa Kunakili Snap!

Utumiaji wa mtandao huu wa kijamii inabidi kuwa wa umakini sana kwani kuna sheria nyingi na sera ambazo zinauongoza.

SnapChat ina misingi nakanunu kadha wa kadha kama mitandao mingine ya kijamii ila kama kawaida yetu tunapenda kuanza kutumia mitandao hii bila kusoma kanuni zake.

Ukiwa ndani ya mtandao wa SnapChat inakubidi kuwa na umakini pindi unapoamua kuchukua ‘Screenshot’ juu ya jambo Fulani ambalo mtu ameliweka katika akaunti yake.

Kitu cha ina yake katika mtandao huu ni kwamba kama umechukua nakala ya kile alichokituma (screenshot) basi mtumiaji atapewa taarifa mara moja na mtandao huu kama umefanya hivyo.

Kumbuka unaweza ukachukua nakala ya kitu ambacho mtu amekiweka katika mtandao wake wa SnapChat na ukaamua kukisambaza kwa watu bila idhini yake. Ukifanya hivyo utakuwa umemkosea sio? Na hasa kama hataki au hapendi kile kitu kionekane nje ya SnapChat.

Ukiwa UK kama umechukua nakala ya kitu alichokituma katika SnapChat bila idhini yake na mbaya zaidi ukaamua kukisambaz akwa watu basi mtu anaweza akaamua kukushtaki katika vyombo vya sheria.

Akishinda kesi hukumu itafutwa. Hii ni kwa sababu vitu ambavyo watu wanavituma katika mtandao huo wa SnapChat vinalindwa na sheria
Sheria hii inasema kuwa “itakua nje ya sheria kwa mtumiaji wa SnapChat kunakili picha na kuifanya ipatikane katika jamii bila ya kupata kibali toka kwa mwenye picha hiyo”

Katika sera ya usiri ya Snapchat inasemma kuwa mara nyingi meseji zinakuwa zinafutwa katika hifadhi zao (server) endapo kampuni inabaini kuwa meseji hiyo imesomwa au imepita muda wake (expire).

Japokuwa jambo hili sio kila saa linawezekana kwa mfano katika kujibu meseji mtu unaweza ukaamua kusevu meseji ili kukupa mwangaza juu ya kitu mnachokiongelea mbeleni (watumiaji wa SnapChat watanielewa zaidi)
Kwa kuwa picha na video zinapotea ndani ya kipindi cha muda mchache basi watumiji wengi wanfurahia kutumia mtandao wa SnapChat katika kutuma na kupokea picha ambazo hazina maadili (mara nyingi)

Mfano Wa Snap Katika SnapChat Lakini hata hivyo watumiaji wanaweza kuchukua nakala (screenshots) za picha hizo, na ikitokea hivyo sera ya kampuni inasema kuwa itakuwa inawatumia wenye akaunti taarifa kama kuna mtu amechukua nakala juu kitu walichokiituma.

Hapo unaweza ukashangaa unaanza kutwangwa maswali kama, Kwa nini umechukua picha yangu bila kibali change? Kutoka kwa mwenye picha.
Sheria kali kama hii ikija na sehemu kama Tanzania sijui itakuaje?

Pengine watu watakuwa wantuma picha ambazo hazina maadili zaidi kwakujua kama wakienda kushtaki kwa serikali watalipwa fidia n.k.

Take care my friend!!!

Now you can add bold, italics and strikethroughs to your whatsap Message!


Bold, Italics, Strikethrough: WhatsApp update adds new formatting to messages WhatsApp, the most popular chatting service, will now let you add the new options of bold, italics and strikethrough to your everyday WhatsApp chat in its latest update.

The new feature was first tested in a beta option but is now available for all users with updates to the iOS and Android app. For most people, those updates should automatically install, and come with version 2.12.17 for iPhones and 2.12.535 for Android handsets.

The new feature is hidden in the app, and needs to be turned on by including certain characters. Here’s how it works:

1. For bold, add asterisks to either side of your text, e.g. *bold*

2. For italics, add underscores to either side of the specific word or words, e.g. _italics_

3. For strikethrough, add a tilde (~) to either side of the word or words, e.g. ~strikethrough~

4. It’s also possible to can surround a word with all three of the characters and have each of the formatting options apply to a word, such as _*bolditalics*_.

These new stylings can also be entered in the WhatsApp web client — which launched last year — but the formatting will only show up in the app-based version of chats.

The move is just the latest in a range of changes to WhatsApp that look to make it into a fully-featured communication tool and allow it to be used in the office, and bring it into line with other chat apps like Slack.

WhatsApp’s latest update, available to beta testers, allows users to reply quickly to messages from the notification panel. One can expect this update to roll out to the wider user base in the near future.

With over one billion regular users, WhatsApp is the world’s largest messaging service. Facebook purchased the platform in 2014 for $19 billion (£13 billion) in 2014, and has continued to run the service parallel to its own standalone Messenger app. On the other hand, WhatsApp hasn’t introduced too many new features since its launch, except for the introduction of voice calling and the blue tick read receipts.

The app recently dropped its annual subscription fee of $1, or for those who downloaded it before July 2013, the upfront fee.

NB: Ni lazima u-update whatsap yako kwanza to the Latest version. Nenda play store.

Google vs Amazon~Automation.

Google kupambana na Amazon katika teknolojia za Automation

Zipo kila dalili za kwamba kampuni kubwa ya Google inaweza kuleta bidhaa ambayo itapambana ama italeta upinzani kwa bidhaa ya Amazon ya Automation ya Echo , taarifa zilizovuja zinadai kwamba Google wanaanza fanyia utafiti kifaa hiki na haijajulikana kama ni lini hasa kitakuwa tayari.

Automation ni sekta ndani ya electronics ambayo inawekea mkazo katika kuhakikisha mitambo na vifaa mbalimbali vinafanya kazi bila ya kumuhusisha binadamu moja kwa moja, mfano ukiingia nyumbani kwako basi taa, feni na TV zijiwashe.

Mpaka sasa katika sekta hii ya Automation ni Amazon pekee ndio wameteka soko hasa kwa bidhaa yao ya Echo ambayo ni spika ya wireless ambayo inaweza kuwa controlled kwa maneno ya mdomo yaani unaweza kuiambia icheze wimbo fulani na ikacheza pia unaweza kuiambia iweke alarm na ikaweka zaidi unaweza kuiambia iwashe vifaa janja ulivyo navyo kama taa feni ama heater.

Baadhi ya huduma ambazo zinawezesha huduma za Automation katika vifaa mbalimbali. Miaka miwili iliyopita Google ilinunua kampuni ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vifaa janja ya NEST kwa Dola za kimarekani bilioni 2.3, kampuni hii hata hivyo haikufanikiwa kuiingizia pesa Google baada ya kutengeneza vifaa ambavyo vilikuwa na matatizo ya kiufundi. inaripotiwa kwamba
NEST hawatashughurika kabisa na mpango huu mpya wa Google kutengeneza bidhaa hiyo mpya pengine ni kwasababu NEST tayari wamejichafua kwa kutengeneza bidhaa mbovu hivyo Gooogle wasingependa kuchafuka.

Google wanahitaji kuingia katika biashara ya
Automation kwa sababu wanazo tayari huduma zote ambazo automation inahitaji,
Google wanayo huduma ya Google now kwa mfano hii inamaana kwamba wakitengeneza kifaa hicho kitatumia Google now kupokea command kutoka kwa mteja ama kwa kutumia huduma ya Chromecast kwaajiri ya kucheza video unazozipenda.

Eneo la automation bado halijafanyiwa uwekezaji wa kutosha na wataalamu wa mambo wanasema kwamba hili eneo la teknolojia litapiganiwa siku za hivi karibuni na makampuni makubwa kama Apple na Google
Nchi zetu za Afrika mashariki bado zipo nyuma katika teknolojia hasa hii ya Home automation , natoa wito kwa wale wote wapenda teknolojia kuangalia upya matumizi ya teknolojia hii hasa katika majumba na maofisi.

Mfano unaweza kuunga taa zako ndani ya nyumba kuwaka pindi tu kuna mtu ndani ya chumba ama kiyoyozi unaweza kukiweka kifanye kazi pale tu kuna mtu ndani ya nyumba, hii itakusaidia pamoja na mambo yote kupunguza gharama za umeme.

Monday, 28 March 2016

NENO LA MUNGU.

WAFILIPI 4:6

Msijisumbue kwa neno lolote;Bali katika kila neno kwa kusali na kuomba,pamoja na kushukuru,haja zenu na zijulikane na Mungu.

  ISAYA 41:21

Haya,leteni maneno yenu,asema BWANA;Toeni hoja zenu zenye nguvu,asema mfalme wa Yakobo.

         YEREMIA 33:3

Niite,nami nitakuitikia,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajuwa.

Mpendwa nimekuletea maandiko haya kwa lengo moja tu,kwamba twende mbele za Mungu muda na wakati kama huu,tumpelekee hoja zenu zenye nguvu,yaani tumpe mahitaji yetu.
Mpendwa ninajuwa hapo ulipo una mahitaji mengi ambayo unahitaji Mungu akutendee,hivyo ninakuomba Mpendwa japo kwa mda mfupi tu,twende mbele za Mungu,tumuite naye ni mwingi wa rehema atatuitikia.

Kumbuka yeye anasema

Tazama,mimi ni BWANA,Mungu wa wote wenye mwili;je kuna neno gumu lolote nisiloliweza?
Nakuambia Mpendwa hakuna gumu mbele za BWANA.
Hivyo simama tumwombe Mungu mpendwa,mwambie haja ya moyo wako muda na wakati kama huu,kwa imani naamini utapokea.

Simama mpendwa tuombe na Mungu atakujibu kwa wakati wake.
Najuwa umeomba sana mpendwa,hadi ukaisi kwamba Mungu hayupo,ni kwambia usikate tamaa,maaombi ya mwenye haki yanafaa akiomba kwa bidii.
Hivyo usichoke Mpendwa.

~Tubu kwanza dhambi zako mbele za Mungu.
~Omba kwa imani
~Omba kupitia jina la Yesu Kristo.
~Omba kwa utaratibu
~Omba kwa kumaanisha....

Simama kwa miguu yako Mpendwa, tuombe,paza sauti yako, Mungu anakujibu.

Be blessed, ameen!

Dar si salama: Makonda

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Makonda--Dar-si-salama/-/1597578/3136210/-/vbbwdmz/-/index.html

Sunday, 27 March 2016

Uvimbe via vya uzazi

Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke na kusababisha maumivu kwao lakini aina hizi saba ndiyo huonekana sana kwa wanawake wengi ambazo ni kama ifuatavyo:

I. Follicular cyst; ni uvimbe ambao hutokea wakati Ovulation isipotokea au baada ya Corpus Luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi.

Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya Ovulation.

Maumivu haya huonekana kwa robo ya wanawake wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.

2.Corpus Luteum cyst; ni uvimbe unaotokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi. Kwa kawaida Corpus Luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwingine inaweza ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii.

Uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.

3. Hemorrhagic cyst; uvimbe huu hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke (kushoto au kulia).

4. Dermoid cyst;  uvimbe huu ambao siyo saratani na pia hujulikana kama Mature Cystic Teratoma, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia inchi 6 kwa upana na ndani yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na Cartilage.

Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi au kujizungusha na hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na hivyo kusababisha maumivu makali sana maeneo ya tumboni.

5. Polycysitic appearing cyst; uvimbe wa aina hii unakuwa ni mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.

6. Cystedenoma: Ni aina ya uvimbe unaotokana kwenye tishu za Ovary na hujazwa na majimaji yenye kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.

7. Endometriomas /Endometrial Cysts: Husababishwa na uwepo wa aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama Endometrium kwenye mayai ya mwanamke. Huathiri wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito na huambatana na maumivu sugu ya nyonga wakati wa hedhi.

Uvimbe huu unakuwa na damu ya rangi nyekundu inayoelekea kuwa kahawia na ukubwa wake ni kuanzia inchi 0.75 hadi 0.8.

Tiba yake na nini husababisha wiki ijayo, usikose kufuatilia blog hii.

Friday, 25 March 2016

IMANI THABITI YENYE TIJA.


Daktari Ahmed, mtaalamu wa ugonjwa wa kansa alikuwa na safari ya kwenda kushiriki mkutano wa muhimu mno katika mji mwingine tofauti na aliopo, mbali na kushiriki mkutano huo pia alikua akitarajiwa kutunukiwa tuzo ya umahili katika tafiti za kiafya.

Alikuwa ameutamani sana huo mkutano na alikuwa akihitaji kufika haraka iwezekanavyo. Amefanya kazi ya utabibu na utafiti kwa muda mrefu hivyo alijiona kweli anahitaji kupata tuzo ambayo alikuwa akiitarajia.

Hata hivyo baada ya masaa mawili ya kukaa angani katika ndege akielekea huko kwenye mkutano, ndege ilipata hitilafu na ikabidi itue katika airport iliyopo karibu.

Akiwa na hofu kwamba atachelewa mkutano, Daktari Ahmed akaenda mapokezi pale airport na kukuta kuwa ndege nyingine inayoenda huko anakoenda itaondoka pale baada ya masaa kumi.

Receptionist akamshauri kwama aazime gari na aendeshe mwenyewe mpaka huko anakoelekea kwani ilikuwa ni mwendo wa masaa matatu tu na gari.

Kwakuwa alikuwa hana chaguo jingine, alikubaliana na yule dada wa mapokezi kuazima gari ingawa alikuwa hapendi idea ya kuendesha gari kwa muda mrefu.

Aliazima gari na akaanza safari. Hata hivyo muda mfupi tu baada ya kuondoka hali ya hewa ilibadilika ghafla na kimbunga kikali kikaanza.

Mvua kubwa ikiyoambatana na ukungu ikamfanya apate sana tabu kuona mbele na akapotea barabara aliyokuwa anahitajika kwenda.

Baada ya masaa mawili ya kuendesha gari, akathibitisha kweli amepotea njia. Kuendesha katika mvua kubwa yenye upepo na kimbunga, huku akiwa na njaa na amechoka, ikamlazimu atafute nyumba yoyoye aulizie hapo ni wapi na apate kuelekezwa anakoelekea.

Baada ya muda kidogo hatimaye akaona nyumba ndogo ikiwa kando kidogo mwa barabara. Akaegesha gari pembeni akashuka na kwenda kugonga hodi mlangoni.

Mwanamke mwembamba na mzuri akamfungulia mlango. Daktari Ahmed akamuelezea tatizo lake na akamuomba yule dada kama anaweza akatumia simu yake kuwataarifu kule mkutanoni kilichompata.

Hata hivyo, yule dada akamwambia yeye hana simu wala kifaa chochote cha mawasiliano lakin akamuomba daktari aingie ndani asubiri hali ya hewa itulie vema. Akiwa na njaa, amelowa daktari alikubali kuingia ndani.

Yule mwanamke akampa daktari chai ya moto, na akamwambia anaomba aungane nae katika maombi.

Ambapo daktari alitabasamu na akasema yeye anaamini katika kufanya kazi kwa bidii na sio maombi. Hivyo akamwambia yeye aendelee tu.

Akiwa amekaa akiendelea kunywa chai taratibu, daktari alimwangalia yule mwanamke katika mwanga mdogo wa mishumaa akiwa anasali mbele ya kitu kama kitanda cha mtoto hivi.

Kila muda akimaliza kufanya sala, anaanza sala nyingine. Daktari akahisi labda huyu mwanamke anahitaji msaada fulani hvyo akamsubiri amalize kusali amuulize anasumbuliwa na nini.

Alipomaliza daktari alimuuliza yule mwanamke kuwa ni nini haswa anahitaji kutoka kwa Mungu? Na kama Mungu amemsikia maombi yake. Na akendelea kumuuliza kuhusu mtoto aliyepo katika kitanda ambae amelala hajitambui.

Mwanamke akampa tabasamu la huzuni na kumwambia kwamba mtoto aliyepo kwenye kitanda ni wake ambae anasumbuliwa na kansa kwa muda mrefu.

Na kuna daktari mmoja tu bingwa katika mji mwingine tofauti na huu anaitwa Daktari Ahmed ndio ana uwezo wa kumtibu mwanangu.

Lakini hapa unaponiona sina pesa ya kumtibia mwanangu wala nauli ya kunifikisha huko aliko Daktari Ahmed.

Ni kweli Mungu hajajibu maombi yangu, ila siku zote sikubali woga wangu uzidi imani yangu juu ya Mungu wangu.

Akiwa ameshtushwa na kushangazwa Daktari Ahmed alikuwa akitokwa na machozi, alijiambia kweli Mungu ni mkuu na akajaribu kuunganisha matukio.

Kulikuwa na tatizo katika ndege, nikakodi gari, nako mvua kubwa na kimbunga vikanifanya nipotee njia na kufika hapa.

Yote haya yametokea sio kwa bahati mbaya bali ni makusudi ya Mungu daktari afike hapa kupata nafasi ya kusaidia masikini kama huyu ambae hana pesa ila ana utajiri wa imani juu ya Mungu.

Daktari alijitambulisha kuwa yeye ndio Ahmed, na akakiri kumbe kweli Mwenyezi Mungu hujibu maombi.

Aliwachukua wote wawili na akaenda nao katika mji anakofanya kazi, alimpa matibabu yule mtoto na kwa kipindi kama cha miezi 8 yule mtoto alipona.

FUNDISHO
Sisi kama binadamu tunahitajika kukumbuka hatua hizi muhimu katika maisha.

1. Omba
2. Amini
3. Pokea
4. Toa

Nawatakia Pasaka  njema na Mwenyezi Mungu awabariki.

Saturday, 19 March 2016

Very technical!!

Jinsi Ya Kujitoa Kwenye Group la WhatsApp Na Kulivunja (kulifuta) Kwa Siri!

Utakuta ndani ya WhatsApp ‘Group’ moja lina watu kibao na wanaongea vitu tofauti tofauti na kibaya zaidi wawe wameku Add tuu bila idhini yako. Hii sasa haitakuboa bali itakukasirisha. Au kama uko kwenye ‘Group’ ambalo sio zuri ki maadili labda vitu vinatumwa na kupokewa na watu wa kundi hilo havina maadili hapo vinaweza kukuharibia siku yako.

Sasa basi kama unataka kujitoa katika Group ndani ya Mtandao wa WhatsApp bila ya watu wengine katika lile ‘Group’ kujua kama umejitoa, kuna njia spesheli ya kufanya hivyo.

Katika kutumia njia hii pia utalazimika kuliharibu ‘Group’ kabisa kwani baada ya wewe kujitoa kwa njia hii, ‘Group’ halitaweza kufanya kazi kabisa (litakuwa limeharibika)
Tuifahamu Njia Hiyo
Cha kwanza kabisa itakubidi utumie huduma ya WhatsApp ya kwenye mtandao yaani WhatsApp Web
TeknoKona inashauri utumie kivinjari cha Google Chrome (vingine vina hatihati ya kukwama kuliwezesha hili)

Fungua Simu janja yako na ingia katika WhatsApp. Ukiwa kule nenda eneo la ‘Settings’ na kisha chagua WhatsApp Web kisha skani kodi ya QR katika kivinjari cha kompyuta yako kwa kutumia simu janja yako. Kwa kufanya hivi unaweza ukatumia WhatsApp katika kompyuta yako
Ukiwa unatumia WhatsApp katika Mtandao wa kompyuta (web) fungua ‘Group’ ambalo unataka kujitoa na kulifunga.

Anza kuandika emoji nyingi kadri uwezavyo ili zifike takribani 3000 katika ule uwanja wa meseji. Kwa njia rahisi ili kulifanikisha hili inakubidi uwe una kopi na kupesti taaratibu.
Emoji Takribani 3000
Ukishapata emoji zako takribani 3000 – 4000 (utajua tuu kwani meseji yako itakua ni ndefu sana) bofya ‘Enter’ ili kutuma meseji hiyo.

Na hapa usiwe na haraka sana subiria mpaka Chrome iweze kutuma meseji hiyo na subiri mpaka meseji hiyo ipate tiki moja ikiwa na maana kwamba umetoka(imetumwa).
Baada ya kufanya hivyo sasa unaweza ukafunga WhatsApp Web yako na ukienda katika WhatsApp kwa kutumia simu janja yako, wewe pamoja na watumiaji wengine wa hilo ‘Group’ watapata meseji ifuatayo
“WhatsApp isn’t responding”

Baada ya hapo hilo ‘Group’ la WhatsApp halitawezwa kutumika hata kwa mtu mmoja kati ya wale ambao walikuwa katika ‘Group’ hilo. Hapa kila mtu atalazimishwa kujitoa katika ‘Group’ hilo. Na kizuri ni kwamba hawaatamjua mchawi ni nani kwani kutakuwa hakuna ushahidi juu ya jambo hili.

Wengi watajua ya kuwa labda ni matatizo ya kiufundi kutoka kwa mtandao wa WhatsApp wenyewe. Pia kuna uwezekano ‘Group’ kuweza kufanya kazi endapo njia hii itafanywa kwa kutumia simu janja za iOs kama vile iPhone.

Kwa Android zoezi hili litakamilika mara moja tuu
Lingine la muhimu ni kwamba njia hii sio ya kutumia kwa mzaha. Maana wengine wanaweza wakachukulia kama kamchezo flani. Kabla ya kuifanya fikiria kwanza!!

Tumia busara zaidi!

Friday, 18 March 2016

COCA-COLA SI SALAMA-UTAFITI

Coca-cola ni nembo kubwa sana katika historia ya nembo ya bidhaa na utafiti umeonyesha ni nembo maarufu duniani baada ya “hallo”, Ni neno la pili maarufu Duniani kwa maana hiyo karibia kila mtu katika sayari hii lazima anywe Coca-cola karibu kila wakati. Jambo hili linatisha kwani

imethibitishwa kwamba coca-cola ni hatari kwa mwili wa mwanadamu. Mchanganyiko wa kemikali ambao unakunywa kama kiburudisho kiutendaji inaua umetaboli kutokana na kipimo chake cha uasidi kuwa sawa ni asidi ya betri ya gari.

Sehemu ya tumbo ambapo chakula kinapita kwa ajili ya kuuwa sumu pia inahusisha maradhi kama matatizo ya moyo, kiarusi, pumu, matatizo sugu ya mapafu, nk na ni mbaya zaidi kwa watoto wadogo kwa sababu inaingiliana na mlo bora kuliko kuukamilisha.

Inasemekana kwamba watu wanaokunywa kinywaji hiki chenye sumu wanaangalia utegemezi wa kafeini na upungufu wa madini muhimu kama kalisi, magnesi vitamini A. Usitufikiria vibaya kwani bado tunaamini kwamba

Coca-cola ni kinywaji muhimu ingawaje si kwa ajili ya mwili wa mwanadamu lakini kuna matumizi mengine mengi mazuri ambayo inaweza kutumika na nadhani baada ya kuyajua utaweza kuanza kununua kwa wingi kwa ajili hiyo.

Matumizi 25 halisi ya Coca-cola
Kusafisha Choo: Kusafisha choo ni kazi isiyopendeza na hebu tuwe wakweli – hakuna anayependa kuifanya – hakuna yoyote ispokuwa rafiki

yake mwenye kufoka Coco-cola. Unachohitajika kufanya ni kumimina kinywaji hicho kwenye karo la choo na usubiri baada ya saa moja alafu uanze kusugua na alafu uvute maji – utakuwa umejipatia choo kisafi chenye kumeremeta.

Madoa doa sugu: Fikiria hapo zamani! Kama hutaki ama huna uwezo wa kununua dawa ya kusafishia madoa au uchafu kutokana na gharama, chukua kinywaji cha Coca-cola na umimine pamoja dawa ya kawaida ya

kusafishia au sabuni ya unga: Madoa doa yote yatasafishwa na nguo zako
zitakuwa hazina harufu mbaya: Shukran zote ni kwa asidi ya kaboni na ya forforasi ndani ya kinywaji chenye dioksidi ya kaboni.

Kusafisha vioo vya Madirisha: Mpaka sasa tumeweza kufahamu maajabu ya nguvu ya kusafisha ya Coca-cola – Kitu kingine ambacho kinaweza kusafisha vizuri ni vioo vya madirisha. Kutokana na asidi ya sitriki inayopatikana katika kinywaji hicho, kinasababisha kun’garisha vioo na

inafanyakazi kama linavyofanya kazi tunda la sitriki katika kazi kama hiyo.
Kuuwa Wadudu: Wadudu wengi ni wapenzi wa Coca-cola ina maana hata sisi wenyewe, wanapenda utamu na ufokaji wa kinywaji hicho lakini hatujui/hawajui kama kinaweza kuhatarisha afya au maisha yao na badala yake tunandelea kukinywa. Unaweza kunyunyiza kinywaji hiki katika kichuguu au kabatini kwako na kuwaangamiza kabisa mchwa na mende waliokusumbua.

Kukoleza Rangi inayofifia: Unaweza kutumia kinywaji hiki katika nywele zako kama ulitia rangi nywele zako na zimekolea sana. Coca-cola inafahamika kwa ubora wake wa kufifiza rangi kwenye nywele, kwa maana hiyo kama ulipaka rangi katika nywele kwa namna ambayo uiridhii usishtuke kwa kumwendee msusi mwenye gharama bali fungua fridge yako na utoe kinywaji cha Coca-cola na kitakufanyia kazi nzuri.

Kuondoa Gundi: Kama gundi imen’gan’gania katika nywele zako na unafikiria kwamba njia pekee ya kuiondoa ni kuzinyoa nywele zako basi usipata tabu tena! Kitu cha kufanya ni nyunyiza kinywaji cha Coca-cola katika sehemu iliyopo hiyo gundi na usubiri baada ya dakika chache na utaona kwamba itakuwa rahisi kuiondoa hiyo gundi bila tabu kutoka kwenye nywele zako.

Kuondoa maumivu: Kama umeumwa na mdudu, nyuki, au kiwavi basi usipate hofu, mimina kinywaji cha kufoka foka katika eneo lililoathirika na maumivu yataondoka baada ya sekunde chache, shukrani kwa kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha Coca-cola.

Kuosha vyombo: Kama vyombo vyako vimekuwa vyeusi, mimina kinywaji cha miujiza katika vyombo hivyo na uiache kwa dakika chache. Kemikali zilizopo katika kinywaji hicho kitaondoa uchafu uliopo na baadae unachohitaji ni kusugua na vyombo vyako vitakua safi na vyenye kun’gara.

Kiondoa kutu: Kama unataka kuondoa kutu, tumbukiza kitu kilichokuwa na kutu katika chombo ulichomimina kinywaji cha Coke au kama kitu hicho si kikubwa basi lowesha kipande cha nguo ndani ya coke alafu ufute kila kitu kilichokuwa na kutu. Asidi ya fosforasi iliyopo kwenye kinywaji hicho

kitalainisha kutu iliyopo kwenye kitu hicho na kuiondoa kabisa.
Kuuwa Wadudu Shambani: Huko India baadhi ya wakulima hutumia Coca-cola badala ya dawa za kuuwa wadudu kufanya kazi hiyo, kwa sababu ni rahisi na ufanisi na matokeo yake ni mazuri zaidi. Inasemekana kwamba

kiwango cha juu cha sukari kinachopatikana kwenye kinwyaji hicho 
kinazidisha ubora wa kupambana na wadudu, kitu ambacho kimekanushwa na kampuni hiyo kwani wamesema kwamba hakuna chochote katika kinywaji hicho ambacho kinawezesha uuaji wa wadudu. Lakini mbinu hizo za kupinga zinaonekana kama ni janja ya nyani kwa wakulima wa huko India.
Kiyeyusha Barafu: Coca-cola inaweza kuyayusha barafu ambayo huganda kwenye vioo vya magari wakati wa kipindi cha majira ya baridi. Nyunyiza kinywaji hicho katika sehemu ambayo barafu imeganda na iwacha ikolea kwa dakika chache na hatimae barafu itayayuka.

Kuwatega Wadudu: Kama kunapatikana wadudu wengi kwenye eneo au kwenye bustani yako na inakuwia vigumu kuwaua mmoja mmoja basi weka makopo ya kinywaji cha Coca-cola katika maeneo ya bustani yako au karibu na dirisha na wadudu hao watavutiwa na kujikusanya katika makopo na hivyo kukurahisishia kuwaua kirahisi.

Kuondoa Harufu mbaya: Hauna haja ya kukabiliana na harufu mbaya tena. Kama umepita sehemu na kwa bahati mbaya ukanyewa na dege au mnyama yoyote na unalazimika kuondoa harufu hiyo mbaya basi si lazima kukimbilia kujipulizia au kujipaka mafuta mazuri. Kitu cha kufanya ingia bafuni na ujimwagia kidogo kinywaji hicho katika eneo iliyodhurika na baada ya kujimwagia maji harufu hiyo itakuwa imeondoka.

Msaada katika bustani yako ya majani: Pia huu ni msaada wa mara moja katika bustani yako ya majani. Kama utamwagia kopo moja la coke kila wiki katika vilindo ulivyoviweka katika sehemu mbali mbali za bustani yako ya majani, itasaidia ukuaji wa vidubuni ambayo baadae vitasaidia kunawirisha bustani yako ya majani na kufanya ikuwe vizuri.

Kusafisha Sarafu: Kama wewe ni mkusanyaji wa sarafu basi bila shaka utapenda kidokezi hiki, unaweka kuingiza sarafu zako katika chombo iwe ni glasi au bakuli lililojaa kinywaji cha Coca-cola na uziwacha kwa muda kidogo. Ukitoa baada ya muda utashangaa kwa kuona sarafu zako zikin’gaa na zikiwa kama mpya tena. Cola inasaidia kuondoa samadi au uchafi uliojikusanya.

Kusafisha uchafu vichwa vya betri: Asidi inayopatikana katika kinywaji hiki ni ndogo kiasi ukilinganisha na ile ya kawaida ambayo ikimwaga kwenye betri haiwezi kufifilisha asidi ya betri (H2SO4), ambayo ni asidi haswa, na hii inammainisha inaweza kutumiwa kusafisha betri zilizochafuka. Kwa maana hiyo kama umekwama porini na unahitajika kusafisha betri yako na

hauna cha kusafishia isipokuwa una Coca-cola (tutashangaa kama utashindwa kukichukua kinywaji hiki ukiwa safarini baada ya kusoma makala hii) unaweza kukitumia kwa ajili ya kusafishia.
Kitu cha kulegeza: Unaweza kutumia kinywaji cha Coke kulegeza bolti zilizokaza na zilizoshika kutu. Nyunyiza kinywaji hicho kwenye sehemu hiyo ya bolti na uiwache kwa muda kidogo na baadae unyunyiza maji kidogo alafu uifungue na utagundua imelegea kiasi.

Baada ya kufahamu maajabu ya kuhusu kinywaji cha Coca-cola tunajua unajuta kukitumia na kuhatarisha maisha yako kwa kunywa sumu hiyo kidogo kidogo. Lakini kwa sababu sasa unafahamu kwa hivyo mara nyingine ukiwa katika tafrija ambayo unalazimika kuhudumia kwa sababu
Shangazi yako Maria anakuhitajia, kutohudumua wageni wako kwa Coke

kutainusuru familia yako na wewe mwenyewe na madhara yatokanayo na unywaji wa Coke, kusanya mabaki yote ya kinywaji hiki na umimina katika chombo kimoja kikubwa kwa ajili ya kusafisha uchafu na kutu inayopatikana katika vyombo ili vin’gara.

Take care! Afya yako, maisha yako.

Angalia tv kupitia simu yako!

Angalia tv kupitia simu yako ya mkononi (smartphone) au kifaa chochote chenye access ya internet . All u need is just internet bundle.

1. sky news
http://103.245.167.28/tot/31b003ab7e7749a798fe00424e3dd9ff.m3u8

2. FRANCE 24
http://f24hls-i.akamaihd.net/hls/live/221192/F24_FR_LO_HLS/master_900.m3u8?Wse=4577tr
http://static.france24.com/live/F24_EN_LO_HLS/live_web.m3u8

3. Russia Today (GLOBAL)
http://sat1liveios-i.akamaihd.net/hls/live/205904/ios/rtlive/master002.m3u8

4. ABC News
http://abclive.abcnews.com/i/abc_live4@136330/index_1200_av-b.m3u8

5. ALAZEERA ENGLISH
http://aljazeera-eng-apple-live.adaptive.level3.net/apple/aljazeera/english/appleman.m3u8

6. CNN
http://wpc.c1a9.edgecastcdn.net/hls-live/20C1A9/cnn/ls_satlink/b_828.m3u8
http://wpc.C1A9.edgecastcdn.net/hls-live/20C1A9/cnn/ls_satlink/b_,828,528,264,.m3u8
http://d1hya96e2cm7qi.cloudfront.net/Live/_definst_/sweetbcha1novD177_W_150.sdp/media_7419.m3u8

7. ITV Tanzania
http://ec54.ott.bzdv.net/stream,195,341,830,.m3u8

8. TBC Tanzania
http://bzdv.net.flash.glb.ipercast.net/bzdv.net-live/smil:58.smil/playlist.m3u8

9. CHANNEL TEN Tanzania
http://bzdv.net.flash.glb.ipercast.net/bzdv.net-live/smil:53.smil/playlist.m3u8

10. EAST AFRICA TV Tanzania
http://bzdv.net.flash.glb.ipercast.net/bzdv.net-live/smil:55.smil/playlist.m3u8

11. CITIZEN TV Kenya
http://bzdv.net.flash.glb.ipercast.net/bzdv.net-live/smil:76.smil/playlist.m3u8

12. KTN Kenya
http://ec25.ott.bzdv.net/stream,195,341,830,.m3u8

Thanks be God!

Tuesday, 15 March 2016

CAG BUKOBA-VIWANJA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aende Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufanya upya tathmini na kukagua ugawaji wa viwanja 843 kwenye manispaa hiyo.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa agizo hilo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga mjini Bukoba.

Alifikia hatua hiyo baada ya wananchi kubeba bango lenye ujumbe kuelezea kutopewa viwanja hivyo vilivyopimwa na Manispaa ya Bukoba. Viwanja hivyo vilipimwa na kugawiwa kwa wananchi ambao baadhi yao baada ya kulipa fedha, hawajapewa viwanja hivyo ikiwa ni takriban miaka zaidi ya 10.

Akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu alilazimika kumpandisha jukwaani Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Bw. Wallace Karia ili atoe maelezo ya nini kimekwamisha wananchi kupewa viwanja hivyo.

Katika maelezo yake, Bw. Karia alisema mwaka 2003, vilitengwa viwanja 843, kati ya hivyo 352 vilikuwa eneo la Kyabitembe, 137 Ihungo na Rwome na vingine 132.

Bw. Karia ambaye hana muda mrefu tangu ahamishiwe katika manispaa hiyo, alisema kumbukumbu za ofisi zinaonesha kuwa viwanja 182 ndio wahusika hawajapewa, na viwanja vingine 85 vilikuwa havijapimwa eneo la Kilimahewa na Kashai, huku kukiwa na vingine 5,000 vya mradi.

Aliongeza kuwa walitarajiwa kuwalipa wananchi hao katika mwaka wa fedha 2016/17; kauli ambayo ilisababisha kelele kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Waziri Mkuu.

Kutokana na hilo, Waziri Mkuu aliingilia kati na kumueleza Mkurugenzi huyo kuwa kelele hizo zinaashiria kuwa watu hao hawajaridhishwa na majibu yake.

Alisema anafahamu kuwa mkurugenzi huyo na meya ni wapya, lakini akawaagiza ndani ya mwezi mmoja, kufanya mapitio ya viwanja hivyo 843, na hasa watu 182 ambao hawajapatiwa viwanja wahakikishe wanawapatia kwa sababu viwanja vipo.

“Rais mstaafu alikuja hapa na kupewa kilio cha kupunjwa fedha. Najua wakati huo mtasema ninyi hamkuwepo. Wewe (MD) na Meya wako mkae na kupitia mikataba na mafaili. Nyie na mkoa mkae pamoja na kujua vile viwanja vilivyochukuliwa na JWTZ. Nitamleta CAG hapa, ndani ya mwezi mmoja afanye mapitio ya viwanja tu,” alieleza Waziri Mkuu na kushangiliwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu pia aliwahakikishia wakazi wa Manispaa ya Bukoba kuwa watalipwa fidia zao baada ya kukubali kupisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 31.

Waziri Mkuu aliendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa kutembelea wilaya za Misenyi na Karagwe na leo atakuwa wilayani Ngara.

Friday, 11 March 2016

INJILI YA YESU KRISTO.

Mafundisho ya Mwl. C. Mwakasege.
Dar es Salaam

SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO WALIO NA HAJA YA KUPONYWA

Mistari ya kusimamia
Isaya 61:1
Luka 9:11
Yer 6:14

DAY 5/ SIKU YA 5

UTANGULIZI
Maeneo 4 lazima yapokee uponyaji huu ili uwe uponyaji kamilifu na si wajuu juu ni haya yafuatayo:-
Moyo wenyewe
Mwili wako
Kile kilichosababisha moyo kuvunjika
Chanzo cha chombo kilicho sababisha kujeruhi moyo

...Tunaendelea na kichwa kile cha MOYO ULIOVUNJIKA KUPITIA KWENYE NDOTO ULIOOTA NA MADHARA YAKE YANAYOWEZA KUTOKEA..

5⃣Baadhi ya ishara zitakazokuonyesha ya kuwa ndoto uliyoota unahitaji kuifuatilia
Kumbuka vyanzo ni vingi hivyo lazima kuwepo na ishara zikusaidie ipi ufutalie na kuishikiria

ISHARA HIZO NI KAMA:-
(I)Kuota ndoto hiyo hiyo zaidi ya mara moja
Mwz 41:1,4-5,7,32
Si lazima uote ndoto hiyo hiyo mara mbili kwa usiku mmoja, waweza ota ndo hyo siku nyingine na nyingine hiyo hiyo ama yenye maana hiyo hiyo
Maana MUNGU usema mara moja tena mara mbili na kila asemalo ulithibitisha na ulitimiza. Ayb 33:14

(II) Kukutia hofu
Dan 4:5
Angalia kama ndoto uliyoota imekutia hofu
Hii ni ishara mojawapo ya kutohidharau ndoto hiyo.

(III) Kukufadhaisha au kufadhaisha moyo wako na kukupa maangaiko moyoni
Dan 4:5
Si tu kupata hofu bali itakuletea mafadhaiko moyoni mwako

Mwz 40:5
Ndoto hizi zilikuwa halisi na kuleta mafadhaiko hata nyuso zao zilikosa furaha.
Kuna ndoto zinakuja kama taarifa tu na kuna nyingine ni vigumu kuzizuia kijuu juu tu kama ujapata msaada rohoni zitakusumbua tu.

(IV) Cheki kama uliloota limetokea katika mwili wako wakati huu
Mapambano katika ndoto ni mabaya sana na wengi uyaombea kwa maombi ya kawaida tu

(V) Kukunyima usingizi
Dan 2:1

(VI) Kuwa na hamu ya kutaka kujua tafsiri yake
Mwz 40:7-8
Walipoamka hawakuweza kutulia ndani yao walitaka kutafuta na kujua maana yake

Mwz 41:7-8
Usipuuze msukumo utakao kupata na usilizike mpaka upate na kujua maana sahihi

(VII) Ndoto kutaka kuangaisha imani yako na utumishi wako kwa MUNGU
Yer 23:25-27
Wapo watu wasemao ndoto lakini nia yao ni kuwaondoa watu kwa YESU. Kuwa nao makini

Kumb 13:1-3
Shetani pia utumia sana ndoto kuvuruga imani za watu na utumishi wao
Anatumia ndoto pia kwa kujitengenezea wafuasi na watumishi wake

Hes 12:5-6
MUNGU utumia ndoto na maono kusema na watumishi wake halisi
Na shetani utumia mlango huu huu pia
Lazima ujue kuombea vizuri mlango huu wa ndoto, usipoomba shetani atakuvuruga kweli

(VIII) Moyo wako unakuwaje unapoikumbuka ndoto uliyoota huko nyuma?
Kama hali uliyoipata wakati umeota inakukuta vile vile ukikumbuka basi jua hiyo ni ishara MUNGU anakuambia bado kuna kitu hapo hakijatatuliwa

6⃣Andika ndoto unayoiona inahitaji kufuatiliwa hatakama ni fupi kiasi gani andika
Habakuki 2:2
Andika tarehe,ulikuwa wapi, saa ngapi

7⃣Ikiwa umeota ndoto na ulipo amka umeisahau unafanyeje?
Dan 2:1-19
Msihi ROHO MTAKATIFU akukumbushe maana yeye ndiye atukumbushae yote pia endelea kumsihi MUNGU na yeye atakuotesha tena na tena

8⃣Ikiwa umeota ndoto tafsiri yake huijui ufanyeje?

(I) Omba MUNGU akupe ufahamu juu ya ndoto
Dan 1:17
Omba ufahamu ukae ndani yako ili ukiota ndoto nyingine unapata ufahamu hapo hapo
Ufahamu unakaa ndani, ni wakudumu.

(II) Mwombe MUNGU akupe tafsiri ya ndoto
Tafsiri ni tofauti na ufahamu maana tafsiri ya ndoto moja ni tofauti na ndoto nyingine
Tafsiri huja mara moja na MUNGU ndiye mtafsiri pekee. Dan 2:11, 26-28 na Mwz 40:8

(III)Uwe na NENO la Biblia la kutosha ndani yako katika hekima yote
Ayb 33:14-15
Ndoto ni neno/ujumbe/maelekezo yanayoletwa ktk picha
uja kama neno na kama ni neno basi lipo kwenye Biblia mahali
Neno lina sauti Zab 103:20
Sauti uachilia kitu unachotakiwa kupokea na kupata

Rum 10:17
Si tu kukuletea neno lazima usikie sauti iliyoko ndani ya neno kupata ufunuo, mwongozo, maelekezo, maarifa, hekima, ROHO ya uchaji na mengi mengi

Kol 3:16
Hekima hii ukusidia mahali pa kusema nani wa kumshirikisha hiyo ndoto maana si kila mtu wa kumwambia.

MIFANO YA NDOTO NA TAFSIRI ZAKE KTK BIBLIA
▶Ukiota uko darasani
Unasoma
Umechelewa mtihani
na mengi yahusuyo darasani
Soma Dan 1:1-
Mfalme aliandaa chuo na miaka ya kusoma ilikuwa 3
Darasa ni maandalizi ya hatua iliyoko mbele
Yawezekana umekwama ngazi hiyo uliyopo unahitaji kuvuka.
Muulize MUNGU umekwama eneo gani au wapi hujajiandaa kisawasawa ili uvuke.

▶Unaota mtu anakula
Zab 91:16
Amemaliza siku zake za kuishi ameshiba so ahitaji kuongeza miaka.

Isy 29:8
Moja vita uliyonayo inatoka kwenye nafsi yako we unafikiri inatoka nje
Pili walioko nje wanatumia hali ya nafsi yako kukuletea vita ya kiroho

Luk 22:14-20
Cheki nani anakulisha
Kama unalishwa na watu usiowajua au waliokufa kuna mambo haya:
I. Kuna agano unahusika nalo lililopita kwa hao watu

II. Kuna agano jipya wanataka kukuingiza

Vita hii ni mbaya sana usipopata msaada mapema uharibu hali yako na kuvuruga nyumba yako.

MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI.

Thursday, 10 March 2016

Mwalimu kutoroka kituo cha kazi kisa mimba!

Nyang’hwale. Mwalimu mmoja wa Shule Sekondari Nyugwa wilayani hapa Mkoa wa Geita anadaiwa kutoroka katika kituo chake cha kazi kwa
tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wake wa kidato cha tatu.

Inadaiwa baada ya mwanafunzi huyo
(jina linahifadhiwa) kubainika kuwa na ujauzito, mwalimu huyo aliamua kushirikiana na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Kharumwa kutoa. Inadaiwa Machi 3, ndiyo mimba hiyo ilitolewa kwa ushirikiano wa daktari na muuguzi waliokuwa zamu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa shule hiyo, Henrick Jembe alidai Februari 18, mwanafunzi huyo aliomba ruhusa kwenda hospitali akidai anaumwa.
“Ingawa sikuwapo shuleni siku hiyo, lakini kumbukumbu zinaonyesha mwanafunzi huyu alipewa ruhusu baada ya kukamilisha utaratibu
ikiwamo kuandikiwa daftari la
kumuwezesha kupatiwa matibabu,”alidai mkuu huyo wa shule na kuongeza:

“Alisindikizwa na wanafunzi wenzake wawili, mmoja wa kiume na mwingine
wa kike.”
Alidai waliporejea shuleni, mwanafunzi huyo alisema baada ya vipimo alikutwa
na vimelea vya malaria, hivyo
akaruhusiwa aende nyumbani
kupumzika.

“Lakini baada ya siku mbili nilipokea wito kutoka polisi nikitakiwa kufika na mwalimu anayetuhumiwa ambaye siku
hiyo alikuwa na kazi ya kushughulikia chakula cha wanafunzi, ikabidi niende
mwenyewe na kukuta maelezo kuwa mwanafunzi wangu ana ujauzito na anayetuhumiwa ni huyo mwalimu,” alidai Jembe na kuongeza:

“Nadhani alipopata taarifa kuwa anatuhuma hizo aliamua kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.”

Katibu Mkuu Idara ya Utumishi wa Walimu wilayani hapa, Aron Andrew alisema baada ya kumhoji mwanafunzi
huyo alibaini kuwa alianza uhusiano wa mapenzi na mwalimu wake tangu
mwaka jana.

“Alisema baada ya kutolewa mimba, mwalimu wake alimsafirisha hadi jijini
Mwanza kwa mtu aliyemtambulisha
kwake kuwa ni dada wa mtuhumiwa ili ajiuguze huku akiendelea kunywa dawa
alizoandikiwa hospitali,”alisema.

Hata hivyo, alisema hawawezi
kuchukua hatua yoyote dhidi ya mwalimu huyo kwa sasa kwa sababu wanasubiri taarifa kutoka kwa mwajili
wa mwalimu huyo ambaye ni
mkurugenzi.

Alisema mwajiri huyo akitoa taarifa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi mwalimu huyo kwa kuwa amekiuka sheria na kanuni za utumishi
wa umma.

Kaimu Mkurugenziwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Venance
Ngeleuya alisema ofisi yake pia
haijapokea taarifa za tuhuma hizo na kusisitiza watafuatilia.
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk Lutale Josephat alisema ofisi yake
itachukuwa hatua kama itathibitika kuwa baadhi ya watumishi wa kituo cha afya cha Kharumwa walishiriki
kumtoa mimba mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Ibrahimu Marwa alisema
amewaagiza polisi wilayani hapa kumsaka na kumtia mbaroni mwalimu huyo ili afikishwe mahakamani kujibu
mashtaka ya tuhuma zinazomkabili.

EZEKIEL WENJE

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje 

Kahama/Mwanza. Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje (pichani) anakusudia kuita mahakamani zaidi ya mashahidi 693 kupinga ushindi wa mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula (CCM).

Wakili wa Wenje, Deya Outa aliieleza mahakama kuwa mashahidi hao ni pamoja na waliokuwa wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Tunatarajia kuita mahakamani mashahidi wasiopungua 693 kuthibitisha madai yetu, kulingana na mahitaji ya hoja tunazotaka kuzithibitisha mahakamani,” alidai wakili Outa.

Pande zinazohusika kwenye shauri hilo namba 3 la mwaka 2015, juzi ziliweka wazi hoja wanazokubaliana na zile wanazobishania kabla ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kakusulo Sambo anayesikiliza shauri hilo kuihairisha hadi Machi 14, mwaka huu, itakapoanza kusikilizwa mfululizo.

Pamoja na Mabula, wadaiwa wengine katika shauri hilo linalovuta umati wa wasikilizaji ni aliyekuwa msimamiza wa uchaguzi Nyamagana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kutokana na wingi wa mashahidi na muda wa mwaka mmoja uliowekwa kisheria wa mashauri ya uchaguzi kusikilizwa na kuamuliwa, wakili Outa alisema iwapo muda huo utaisha kabla hawajamaliza kutoa ushahidi wao, wataiomba mahakama kuwaongezea muda wa ziada.

Lembeli apeta

Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini kupitia Chadema, James Lembeli ameruka kihunzi kingine baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga inayosikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo kutupilia mbali pingamizi la mashahidi wa mlalamikaji lililokuwa limewekwa na mawakili wa upande wa mshitakiwa.

Akitoa uamuzi huo jana mjini Kahama, Jaji Moses Mzuna alisema ni kinyume cha sheria na wala siyo haki kuzuia mashahidi wa mlalamikaji kutoa ushahidi wao, hivyo ni vyema wakatoa na haki ikatendeka.

Uamuzi huo ulifuatia mvutano mkali wa kisheria uliotokea Machi 4, mwaka huu, baina ya mawakili wa upande wa utetezi na wakili wa mlalamikaji ambapo Jaji Mzuna aliahirisha shauri hilo, hadi alipolitolea uamuzi jana asubuhi.

Katika mvutano huo, mawakili wa utetezi Anthony Nasimire, Denis Kahangwa na Castuce Ndamugoba walipinga mashahidi wa Lembeli kutoa ushahidi wao kwakuwa walikiuka sheria inayowataka kuwasilisha viapo vyao mahakamani ndani ya saa 48, kabla ya shauri kuanza kusikilizwa.

Pia Jaji Mzuna alisema sheria hiyo ni mpya na kwamba haikujulikana kwake, kwa mawakili wa pande zote, na hata katika rejea za kimahakama nchini ndiyo maana hata mawakili wa utetezi wameiwasilisha wakati ushahidi umekwishaanza kutolewa.

Alifafanua kwamba sheria ya uchaguzi inaelekeza mlalamikaji kutoa ushahidi usioacha mianya ya mashaka, jambo ambalo pia mahakama iliona si vyema mashahidi walioandaliwa kuzuiliwa kutoa maelezo yao, hali itakayobana uwigo wa upatikanaji wa haki.

Kwa upande mwingine Jaji Mzuna aliikataa hoja ya wakili wa Lembeli, Mpale Mpoki kwamba muda wa kuandaa viapo haukuwepo kwa kuwa ilimchukua muda mwingi kuandaa shauri hilo, ambapo Jaji Mzuna alisema haikubaliki kisheria.

Hata hivyo alisema kuchelewa kwa Mpoki kupeleka viapo vya mashahidi hakuwezi kuwa sababu ya Lembeli kupoteza fursa ya kudai haki yake anayohisi alipokonywa, bali muda zaidi umetolewa wa kuandaa viapo hivyo.

Kufuatia hali hiyo Jaji Mzuna aliahirisha shauri hilo hadi Machi 15 mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza maelezo ya mashahidi wa Lembeli waliokuwa wamesubiri uamuzi dhidi ya mvutano huo wa kisheria uliopinga mbunge huyo wa zamani wa jimbo la kahama asipeleke mashahidi wake mahakamani.

Wasira kusubiri uamuzi

Wapiga kura wa Bunda Mjini waliowasilisha maombi ya kuruhusiwa kukata rufaa nje ya muda, kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Ester Bulaya dhidi ya Steven Wasira, wamekumbana na kigingi kingine cha pingamizi.

Maombi hayo namba 25 ya mwaka 2016 yaliwasilishwa na wapiga kura Magambo Masato na wenzake watatu, wakiiomba mahakama hiyo iwaruhusu kukata rufaa nje ya muda baada ya kutupiliwa mbali na mahakama kuu.

Pingamizi hilo liliwasilishwa jana na wakili wa wajibu maombi wa pili na wa tatu, Paschal Malulu akiiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa kiapo kilichoambatanishwa ni batili kwa kuwa aliyeapa ni tofauti na aliyethibitisha.

“Haya makosa yaliyofanyika ni makubwa mno, kiasi cha kutokurekebishika, kwa sababu kiapo kimethibitishwa na wakili Constatine Mutalemwa huku aliyeapa ni wakili James Kahangwa,” alidai Malulu.

Alidai kiapo hicho kimekosa nguvu kisheria kwa mujibu wa sheria Na. 19 (1) (2), ni lazima kiwe na mambo ambayo mtu anaweza kuyathibitisha au kuyasimamia, hivyo hii sheria imekiukwa, kwa lugha nyingine kiapo kimekosa uthibitisho.

Malulu alidai kuwa kuna sheria inayosimamia kiapo wala siyo Katiba kwa ujumla wake, kama alivyoitaja Mutalemwa.

Jaji anayesikiliza shauri hilo, Rose Ebrahim aliahirisha shauri hilo hadi Machi 14, mwaka huu atakapolitolea maamuzi pingamizi hilo.    

Wednesday, 9 March 2016

Vyuo vikuu na ubora wake.

UDSM, SUA, MUHAS vinara orodha ya vyuo vikuu Bongo.

 CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeendelea kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya vyuo vikuu
bora nchini Tanzania.

 Katika takwimu zilizotolewa Januari mwaka huu na tovuti ya www.webometrics.info ambayo ni maarufu kwa
kutoa takwimu na orodha za vyuo vikuu duniani iliyopo nchini Hispania, UDSM ndiyo chuo kikuu bora
nchini huku kimataifa kikishika nafasi ya 2035 kikifuatiwa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)
kinachoshika nafasi ya pili huku kimataifa kikiwa namba 3008 na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambayo ipo nafasi ya 3647 kimataifa.

Chuo cha Katavi Polytechnic ndicho kinachoshika nafasi ya mwisho katika orodha hiyo yenye jumla ya vyuo

51 huku kimataifa kikiwa nafasi ya 23728.
Ifuatayo ni orodha hiyo na nafasi za vyuo kimataifa:

1. University of Dar Es Salaam (World rank: 2035)
2. Sokoine University of Agriculture (World rank: 3008)
3. (1) Muhimbili University of Health and Allied Sciences (World rank: 3647)
4. Mzumbe University (World rank: 4052)
5. Mkwawa University College of Education (World rank: 6231)
6. Open University of Tanzania (World rank: 8059)
7. Hubert Kairuki Memorial University (World rank: 8519)
8. Saint Augustine University of Tanzania (World rank: 9422)
9. University of Dodoma (World rank: 9954)
10. DAR University Kampala International University of Uganda Dar es Salaam (World rank: 10179)
11. Ardhi University (World rank: 12120)
12. State University of Zanzibar (World rank: 13314)
13. Nelson Mandela African Institute of Science and Technology (World rank: 14145)
14. Weill Bugando University College of Health Sciences (World rank: 14543)
15. Tumaini University Makumira University College (World rank: 14561)
16. Institute of Finance Management (World rank: 14572)
17. Dar Es Salaam Institute of Technology (World rank: 14978)
18. University of Iringa (World rank: 15444)
19. Saint John’s University of Tanzania (World rank: 16426)
20. College of Business Education (World rank: 16521)
21. Institute of Accountancy Arusha (World rank: 16755)
22. Mount Meru University (World rank: 17033)
23. Kilimanjaro Christian Medical University College (World rank: 17591)
24. International Medical & Technological University (World rank: 17888)
25. Teofilo Kisanji University (World rank: 18649)
26. Zanzibar University (World rank: 18709)
27. Mbeya University of Science and Technology (World rank: 18795)
28. Mwalimu Nyerere Memorial Academy (World rank: 18850)
29. Arusha Technical College (World rank: 19438)
30. University of Bagamoyo UoB Dar es Salaam (World rank: 19790)
31. Sebastian Kolowa Memorial University (World rank: 20142)
32. Muslim University of Morogoro (World rank: 20181)
33. University of Arusha (World rank: 20205)
34. Dar es Salaam University College of Education (World rank: 20349)
35. St Joseph University in Tanzania (World rank: 20471)
36. Tumaini University Stefano Moshi Memorial University College (World rank: 20819)
37. Moshi University College of Co-operative and Business Studies (World rank: 20942)
38. Tanzanian Training Center for International Health (World rank: 21189)
39. Archbishop Mihayo University College of Tabora (World rank: 21424)
40. St Francis University College of Health and Allied Sciences (World rank:21696)
41. Jordan University College (World rank: 21760)
42. Stella Maris Mtwara University College (World rank: 22086)
43. Sumait University (World rank: 22187)
44. Ruaha Catholic University (World rank:22586)
45. Tumaini University Dar es Salaam College (World rank: 22622)
46. (3) Tumaini University Institute of Agriculture (World rank: 22861)
47. Josiah Kibira University College (World rank: 22931)
48. United African University of Tanzania (World rank: 22981)
49. Mwenge Catholic University (World rank: 23139)
50. Tanzania International University (World rank: 23495)
51. Katavi Polytechnic College (World rank: 23728)

Tuesday, 8 March 2016

Magari 213 kulipa kodi TRA

MAGARI 213 yanafuatiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kubainika yameingizwa nchini bila kulipiwa kodi na watu binafsi pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za dini.

Miongoni mwa magari hayo, yamo yaliyoingizwa kwa misamaha ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) ambayo (misamaha) imetajwa kutumika isivyo.

Mamlaka imesema inafuatilia kuhakikisha wahusika sanjari na waliosaidia ukwepaji huo wa kodi, wanachukuliwa hatua.

TRA imetaja majina na taasisi zinazohusika na uingizaji magari hayo, kupitia matangazo kwa vyombo vya habari na imetoa siku nne wajitokeze kulipia ushuru kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Ukaguzi uliofanywa na mamlaka, ndiyo umebaini kuwepo kwa magari hayo yaliyoingizwa nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha hivyo kuyafanya yamilikiwe bila kulipiwa kodi stahili.

Orodha ya magari 213 na namba za usajili, mmiliki na aina ya gari imetolewa katika vyombo vya habari na mamlaka hiyo imewataka wahusika wajitokeze haraka kulipia gharama hizo.

Baadhi ya kampuni, taasisi na watu binafsi, wameingiza magari zaidi ya moja.

Miongoni mwa taasisi zilizotajwa kwenye orodha hiyo zenye magari zaidi ya moja ni JM Hauliers Limited (26), Al-Jabri Co Ltd (16) na Kampuni ya Dhandho Road Hawlage iliyoingiza 18.

Kampuni nyingine na idadi ya magari yaliyoingizwa kwenye mabano ni Bamboo Rock Limited (7) na Dayosisi ya Musoma, ambayo hata hivyo haikufafanuliwa ni ya madhehebu gani ya dini, imeingiza magari manane.

Wengine ni Fai Limited (3), Nam Transport Company (6), Neni Enterprises (2) na Relief Partner International yenye magari matatu.

Kwa upande wa watu binafsi wenye magari zaidi ya moja yaliyoingizwa bila kulipia ushuru ni pamoja na Aloyce Kajijira (6), Mohamed Masoud (5), Mwesige Rwiza (5), Nassor Zakaria (3), Rumishaeli Shoo (3), Ruwaida Ally (4) Simon Mehi (2), Yahya Hilal (5) na Zahor Issa mwenye magari matatu.

Wapewa siku nne
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo aliwataka wamiliki wa magari yaliyoorodheshwa kufika katika ofisi zilizo karibu, wafanyiwe uhakiki walipe ushuru stahiki kabla ya Machi 12 mwaka huu.

Alisema baada ya tarehe hiyo, TRA itachukua hatua ya kufuatilia magari hayo na kuyakamata.

Alisema ufuatiliaji wa magari yaliyoingizwa nchini bila kulipiwa ushuru ni endelevu.

Waliouziwa matatani
Akizungumzia watakaokuwa wameuziwa magari hayo bila kufahamu kama yalitolewa bila kulipiwa kodi stahili, Kayombo alisema pia wanatakiwa kujitokeza.

Alisema walioyanunua magari hayo, ambayo namba zake zimeoneshwa, wanapaswa kujitokeza wapigiwe hesabu, walipe kiasi kinachodaiwa na mamlaka.

Kwa mujibu wa Kayombo, watakapofika katika ofisi za TRA, zitafanyika taratibu kuangali jinsi ya kulipa, kwani yapo magari ambayo hayakulipiwa kabisa au yamelipiwa kidogo kutokana na kufanya udanganyifu katika malipo.

Waliosaidia ukwepaji kodi
Hata hivyo, Kayombo alisema baada ya kulipa gharama hizo, hatua nyingine zitachukuliwa.

Hatua hizo za kisheria, zitahusu waliopitisha magari hayo na waliosaidia katika kufanya udanganyifu wa kulipa kodi stahiki kwa magari hayo.

Mwl auawa kwa risasi Dar

DAR ES SALAAM: Mwalimu wa Shule ya Msingi Msigani, Kimara wilayani Kinondoni jijini Dar, Grace Benedicto 32, (pichani) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakati alipokuwa akijiandaa kwenda kumpokea mume wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, mauaji hayo yalitokea saa mbili usiku wa Februari 27, mwaka huu huko Msigani, Mbezi, Dar hatua chache kutoka shule aliyokuwa akifundishia mwalimu huyo.

Kwa mujibu wa majirani wa eneo hilo, siku hiyo watu watatu walifika kwenye duka la huduma ya pesa na vocha la mwalimu huyo wakiwa kwenye pikipiki moja, mmoja wao alitoa shilingi elfu kumi ali apewe vocha, mwingine alihitaji Luku.

“Lakini ghafla wakamuweka mwalimu chini ya ulinzi. Hata hivyo, alipambana nao, wakamzidi nguvu na ndipo mwingine aliyejificha mahali akatoa bunduki na kumfyatulia risasi mbili mwalimu.

“Risasi moja ilimpiga bega la kushoto, nyingine tumboni. Alidondoka chini huku akipiga kelele ya kuomba msaada lakini tulipofika tulikuta wale majambazi wameshakimbia,” alisema jirani mmoja.

Aliendelea kusema kuwa, polisi walitaarifiwa na walifika katika eneo la tukio muda mfupi na kumchukua mwalimu kumkimbiza Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani lakini daktari alipomchunguza akagundua alishafariki dunia.

Uwazi lilifika msibani, Kimara ya Stop Over jijini Dar na kuzungumza na mdogo wa marehemu aitwaye Benard Benedicto ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Ninachojua mimi siku hiyo dada alikuwa akifunga duka ili akampokee shemeji uwanja wa ndege lakini muda mfupi kabla ya kuondoka, ndipo walifika hao majambazi.

“Dada alikuwa akiwasiliana na mume wake hadi pale mume wake alipozima simu baada ya kupanda ndege. Aliposhuka na kuwasha simu ili ampigie dada, akapokea taarifa ya mkewe kupigwa risasi, lakini muda huohuo akapigiwa simu kuwa, amefariki dunia.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Dustan Kuzirwa katika mahojiano na Uwazi ofisini kwake wiki iliyopita alisema kuwa, wamesikitishwa na mauaji hayo ya kinyama ya mwalimu Grace.

“Mwalimu Grace alikuwa mchapa kiazi na mwenye ushirikiano mkubwa na wenzake. Alikuwa kitengo cha kompyuta na alianza kazi mwaka 2006. Tunalaani mauaji hayo na tunaliomba jeshi la polisi kuwasaka wahusika,” alisema Dustan.

Hata hivyo, mume wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Kimati alipohojiwa alisema waliomuua mkewe siyo majambazi bali kuna siri nyuma yake. Hakuitaja.

Mazishi ya mwalimu huyo yalifanyika katika makaburi ya Banda la Mkaa, Mbezi Jumatano ya Machi 2, mwaka huu.

WAZIRI LUKUVI NA RUSHWA.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza alipofanyiwa mahojiano maalumu na waandishi wa Mwananchi, ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 

Dar es Salaam.  Waziri wa  Ardhi, William Lukuvi amesema rushwa imekithiri kwenye sekta ya ardhi kiasi kwamba wafanyabiashara wawili walimuahidi rushwa ya Sh5 bilioni afanikishe mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi kwenye eneo linalotakiwa kujengwa mji wa kisasa wa Kigamboni.

Mji huo kabambe wa Kigamboni unajumuisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila na eneo lote lina ukubwa wa takribani ekari 6,000.

Awali mradi huo ulitarajiwa kugharimu Sh13 trilioni ambazo zingetolewa na Serikali, lakini ikaamua kushirikisha sekta binafsi ili zishiriki kuujenga na Serikali ishughulikie uwezeshaji wa awali.

Lukuvi, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa takriban miaka mitano kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ardhi mapema mwaka jana na kubakizwa wizara hiyo na Rais John Magufuli, alitoa siri hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu.

Mbunge huyo wa miaka mingi wa Isimani mkoani Iringa alisema amegundua kuna mtandao mkubwa wa rushwa unaoanzia ngazi ya halmashauri mpaka wizarani ambao unahusisha maofisa wa Serikali na viongozi wa wizara.

Waziri Lukuvi alisema mtandao huo ni hatari na unaweza kusababisha mtu ashindwe kufanya kazi ya wananchi iwapo ataendekeza rushwa.

“Hapa (Wizara ya Ardhi) fedha ipo,” alisema Lukuvi ambaye amekuwa mbunge wa Isimani tangu mwaka 1995.

“Kama ukiwa na tamaa huwezi fanya kazi uliyotumwa. Kuna wakati walikuja wafanyabiashara wawili wakubwa na kutaka wanipe Sh5 bilioni ili nikubali kupitisha mradi wao wa mabilioni ya shilingi na walitangaza kwa marafiki zangu kuwa wangenipa fedha, lakini hapa hawawezi” alisema Lukuvi.

“Wakati naingia tu wizara hii, nilikuta harakati za kukamilisha mradi wa Kigamboni ukiwa katika hatua za mwisho na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Lakini nilipopitia vizuri, nilikataa kuwalipa wafanyabiashara hao. Cha ajabu hazikupita siku mbili wafanyabiashara hao walipata taarifa wakaja mbio kutaka kuniona.”

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, wafanyabiashara hao walitaka walipwe kiasi cha Sh141 milioni kwa kila ekari wakati wao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa Sh5 milioni kwa ekari, jambo ambalo alisema lilishapitishwa awali.

“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue kutoka kwa wananchi ekari moja kwa Sh5 milioni, kisha Serikali tumlipe Sh141 milioni kwa ekari kwa kuvuka pantoni tu. Ni wizi mkubwa. Kama kweli Serikali ina fedha hizo kwa nini tusimlipe mwananchi moja kwa moja?” alihoji.

Waziri Lukuvi alisema endapo njama hizo zingefanikiwa, Serikali ingetumia zaidi ya Sh84 bilioni kuwalipa wawekezaji hao hewa kwa kuwa mmoja anamiliki takribani ekari 200 na mwingine 400.

“Niliwaambia Serikali haiwezi kuwalipa fedha hizo na badala yake waende kuiendeleza ardhi wenyewe kulingana na mradi unavyotaka. Walitaka kutajirika kwa ujanja ujanja,” alisema Lukuvi.

“Eti walidai wamekopa benki kwa ajili ya mradi huo. Haiingii akilini mtu utumie Sh5 milioni, halafu uje uvune mabilioni ya fedha kwa kuvuka pantoni tu.”

Hata hivyo, Lukuvi alikataa kutaja majina ya wafanyabiashara hao.

Akiongea na gazeti moja la kila wiki mwaka 2013, Profesa Anna Tibaijuka, waziri aliyemtangulia Lukuvi kwenye wizara hiyo, alisema tayari kampuni mbili za Miworld kutoka Dubai na China Hope (China) zilishasaini mkataba wa maridhiano na Serikali wa kujenga nyumba takriban 20,900 kwenye eneo hilo.

Miworld ilisaini mkataba wa kujenga nyumba 5,000 wakati China Hope ilitaka kujenga nyumba 15,900 kwenye eneo hilo la mradi wa mji mpya.

Profesa Tibaijuka aliliambia gazeti hilo wakati huo kuwa wananchi wangefidiwa kwa bei za soko kwa mujibu wa sheria, akisema ekari moja ingefidiwa Sh141 milioni kwa ajili ya kumuwezesha kulipia gharama ya nyumba mpya mbadala.

Akizungumzia migogoro ya ardhi, Waziri Lukuvi alisema amegundua mingi inasababishwa na maofisa na viongozi wa wizara hiyo wasio waaminifu, lakini pia wawekezaji wenye tamaa ya kumiliki kiasi kikubwa cha ardhi hata kama hawana shughuli nayo.

“Nimegundua kuna watu hapa wanataka kumiliki ardhi kila sehemu. (Mtu huyo) Atafanya kila njia ashirikiane na watumishi wasio waaminifu ili wampatie eneo hata kama limeshauzwa,” aliongeza.

Lukuvi alisema wengi wao ni wafanyabiashara wenye asili ya Kiarabu na Asia ambao kwa muda aliokaa wizarani hapo amegundua wamehodhi  mashamba katika miradi yote ya viwanja au mashamba iwe ya halmashauri au wizara.

“Wanasiasa na viongozi wa Serikali wanaohodhi maeneo wapo, lakini siyo wengi ukilinganisha na hawa wafanyabiashara wengi wenye tamaa ambao wakishapata ardhi wanatumia kukopa mabilioni ya fedha ndani na nje ya nchi kisha wanawekeza katika miradi yao mingine ikiwamo kujenga majumba katika nchi za Dubai na Ulaya na kuyatelekeza maeneo hayo kuwa mapori hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wasio na maeneo.

Waziri Lukuvi alikuwa ameambatana na maofisa na wakurugenzi wa vitengo mbalimbali wa wizara hiyo na aliwauliza mbele ya waandishi wa Mwananchi iwapo anachokisema si sahihi wamsute.

Kutokana na kauli huyo, naibu mkurugenzi wa mipango miji na vijiji, Immaculate Senje alisema kwa sasa heshima ya wizara imeanza kurejea na kwamba wanasikia fahari kujitambulisha kuwa watumishi wa wizara hiyo.

“Kuna watu wengi wameumizwa na watumishi wa wizara. Tunachofanya sasa ni kutibu vidonda vya muda mrefu. Natamani ifike wakati kila aliyeumizwa apate haki yake na hilo linawezekana chini ya utawala wangu, hapa mambo ya rushwa hayana nafasi,” alisema Senje.

Akizungumzia matarajio yake, Waziri Lukuvi alisema endapo Rais John Magufuli ataendelea kumuweka katika wizara hiyo anatamani amalize migogoro yote baina ya wananchi katika kipindi cha miaka mitano

Mtumishi mwingine, Idrisa Kyera alisema awali mfumo uliokuwepo ilikuwa hautendi haki kwa wananchi, jambo lilosababisha migogoro kukithiri.

“Awamu iliyopita ilikuwa aibu kujitambulisha mbele za watu kuwa ni mtumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Mkazi. Lakini sasa hivi kazi inafanyika vizuri na wananchi wameanza kutuamini,” alisema.

Lukuvi alizaliwa mkoani Iringa Agosti 15, 1950 na kupata elimu yake ya msingi kwenye Shule ya Msingi ya Kitanewa. Alianza kazi serikalini kwa kuwa mkuu wa wilaya kuanzia mwaka 1994 hadi 1995 alipogombea ubunge wa Isimani.

Kati ya mwaka 1995 na 2000 alikuwa Naibu Waziri na katika Bunge la Nane (2000-2005) aliendelea na wadhifa huo hadi Bunge la Tisa (2005-2010) alipoteuliwa kwa nyakati tofauti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Dar es Salaam.

Katika Bunge la Kumi aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ardhi katika mabadiliko ya mwisho ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.

Monday, 7 March 2016

Huyo ndo Makonda.

Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, akisimamia zoezi la wanafunzi kupanda kwenye daladala pamoja na walimu

PAUL Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ametangaza mpango mpya wa kuanzisha mtaa maalum utakaokuwa ukihusika na biashara ya uuzaji wa vinywaji vikali na baridi (Bar).

Makonda ameweka wazi mpango huo mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa pia ndiyo siku ambayo utekelezwa wa mpango wa walimu wa shule za msingi na sekondari kusafiri bure kupitia usafiri wa umma (daladala) unaanza rasmi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema mpango huo ni muendelezo wa ubunifu na uthubutu wa mipango ya maendeleo ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukikosekana miongoni mwa Watanzania na hivyo kufanya kasi ya maendeleo hapa nchini kuwa ndogo tofauti na matarajio ya wananchi.

“Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhi. Nasubiri muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na bar mpaka nyuma ya misikiti na nyuma ya makanisa,” ameeleza Makonda.

Wilaya ya Kinondoni ndiyo wilaya yenye watu wengi zaidi hapa nchini ambapo kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya hiyo ina jumla ya watu milioni 1.7 na kwasasa ikikadiriwa kufikia watu milioni 1.9.

Katika hatua nyingine pia Makonda ameeleza kuridhishwa na zoezi la walimu wa jiji la Dar es Salaam kuanza kusafiri bure hii leo huku akibainisha changamoto mbalimbali alizozishuhudia hii leo wakati alipotembelea vituo mbalimbali za daladala kuangalia zoezi hilo.

Makonda amesema: “Changamoto zipo ikiwemo baadhi ya walimu kuficha vitambulisho vyao wakati nimewambia wavivae, lakini kiukweli makondakta wote katika vituo vya mawasiliano na Tegeta nilivyotembelea wana hamasa kubwa ya kuwasafirisha walimu kila mahali wanaita, walimu! walimu!!!

Sunday, 6 March 2016

Katibu wa CWT asema upangaji matokea kwa division ni batili.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Ezekiel Olouch amesema upangaji matokeo ya kidato cha nne kwa mfumo wa divisheni uliofanywa na Wizara ya Elimu, ni batili na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako anatakiwa kushtakiwa.

Mwalimu Olouch aliitoa kauli hiyo juzi kwenye kongamano la walimu Kitengo cha Wanawake Manispaa ya Dodoma kuwa, Profesa Dk Ndalichako anapaswa kushtakiwa.

Pia, alipinga suala la kutumbua majipu kwani linakwenda kinyume na haki za binadamu.

“Mambo mengi yanafanywa kwa pupa hasa yanayofanywa na manaibu waziri, na baadhi ya wakuu wa wilaya nchini,” alisema Mwalimu Olouch.

Kuhusu matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa Februari, alisema kitendo cha waziri kuamua kufuta mfumo wa GPA na kurudisha divisheni, kilikuwa kizuri lakini aliufanya kwa kukurupuka.

Mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma, Profesa Ndalichako alitangaza kubadilisha mfumo wa matokeo kutoka GPA kurudi wa zamani wa divisheni ikiwa ni wiki chache kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo.

“Hapa tuelezane ukweli kwamba Ndalichako amevunja sheria na mimi ningekuwa na mtoto aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana, lazima ningemfikisha mahakamani haiwezekani kuwa na elimu ya kukurupuka, kitaaluma ni matokeo feki lakini kisiasa ni matokeo halali,” alisema Mwalimu Oluoch.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Waziri anaruhusiwa kubadilisha lakini lazima aaandike kanuni na mwongozo jambo alilodai halikufanyika.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Dodoma, Augustino Njamasi alimtaka chama kuendelea kupigania masilahi ya walimu ikiwamo madeni.

Chadema yaichambua siku 120 za Magufuli.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezichambua siku 120 za Rais John Magufuli tangu ashike wadhifa huo kikidai kuwa uongozi wake umetawaliwa na ukiukwaji wa haki, demokrasia na utawala bora.

Aidha, Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana hivi karibuni imeitisha mkutano wa Baraza Kuu utakaofanyika Machi 13 jijini Mwanza ambao utatoa msimamo wa jinsi chama hicho kikuu cha upinzani kitakavyoidai haki badala ya kuiomba na kuweka mkakati wake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Kasoro zilizotajwa kushikia hatamu katika siku hizo zilizotimia jana ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha uchaguzi kwa upendeleo na haki kutotendeka Zanzibar baada ya kufutwa kwa uchaguzi, kuingiliwa kwa uchaguzi wa wenyeviti wa halmashauri na mameya, kuthibiti Bunge na uundwaji wa kamati na viongozi wake, polisi kuzuia mikutano ya hadhara na wabunge na madiwani wa Chadema kukamatwa kwa sababu zisizo za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao hicho, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliitaka mamlaka husika kutangaza tarehe ya uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam, siku saba kabla ya kufanyika kwake.

“Hatutaomba tena kumpata meya wa Jiji la Dar es Salaam, tutadai kumpata. Serikali isifikiri wao ndiyo wanapanga tarehe. Mara nyingi wamekuwa wakitushtukiza ila kwa mujibu wa kanuni tarehe inapaswa kutangazwa siku saba kabla ya uchaguzi. Siku hiyo tutachagua meya na kama asipochaguliwa tusilaumiane,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, demokrasia imekuwa ikikua kwa kasi licha ya kuwa na changamoto kadhaa lakini miezi minne ya utawala wa Rais Magufuli, demokrasia hiyo inatoweka taratibu.

Kuhusu uchaguzi wa Zanzibar, alisema wagombea walioshinda kihalali kwa kupigiwa kura na wananchi hawakupewa fursa ya kuongoza jambo ambalo linaweza kuathiri masuala ya kisiasa, kiuchumi na kiutawala ndani ya nchi.

Akizungumzia Bunge, Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema kumekuwa na udhibiti wa mhimili huo kutekeleza wajibu wake wa kikatiba, kisheria na kikanuni wa kuisimamia Serikali na jambo hilo limefanyika katika maeneo matatu; kuzuia urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya kupitia Televisheni ya Taifa (TBC), jambo alilodai kuwa limefanywa kibabe na Serikali ya CCM bila kujali kuwa “televisheni hiyo ni mali ya wananchi siyo chama tawala.

“Aidha, Serikali ya CCM imeingilia kwa kiwango kikubwa uundwaji wa uongozi wa kamati za Bunge zinazosimamia fedha za umma. Hapa kuna (Hesabu za Serikali) PAC na (Hesabu za Serikali za Mitaa) Laac,” alisema Mbowe.

Alisema kamati hizo zinapaswa kuongozwa na Kambi ya Upinzani Bungeni lakini CCM ilijiwekea utaratibu wa kuwapangia wapinzani viongozi wa kuongoza kamati hizo mbili.

“Tunastahili kuwa na mamlaka kamili ya kuchagua viongozi wa kamati hizi. Serikali pia imedhibiti uundwaji wa kamati za Bunge... Katika Bunge hili, Serikali na uongozi wa Bunge wametengeneza kamati bila kuthamini ujuzi, uzoefu na taaluma za wabunge. Hii itafanya Bunge kukosa meno,” alisema Mbowe.

Alidai kuwa polisi kwa maelekezo ya Serikali, imezuia mikutano ya siasa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Alisema mikutano inayoruhusiwa ni ya wabunge tu, si ya viongozi wala vyama vya siasa ambavyo vinahitaji kushukuru wananchi baada ya kumalizika kwa uchaguzi.

“Leo ni miezi minne baada ya uchaguzi bado tunazuiwa kufanya mikutano. Licha ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kulitolea ufafanuzi suala hili bado tunazuiwa kufanya mikutano,” alisema Mbowe.

Alisai kuwa polisi imewafungulia mashtaka viongozi mbalimbali wa Chadema, wakiwamo wabunge na madiwani kwa kudai masuala ya msingi kuhusu haki zinazokiukwa.

Alisema mkutano wa Baraza Kuu utakaokuwa na wajumbe zaidi ya 600, wakiwamo wabunge na wenyeviti wote wa chama hicho utatoa msimamo na mwelekeo.

Akitolea mfano wa uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam alisema: “Kuongoza Dar es Salaam si mapenzi ya Mbowe ni wananchi. Woga kwetu ni mwiko na kauli ya amani bila haki haiwezekani. Tunaiambia Serikali na dola kwamba amani itapatikana tukiheshimiana na haki kuchukua mkondo wake kwa kufuata utawala wa sheria na Katiba.”

Alipoulizwa kuhusu madai ya Chadema, Waziri wa Habari, Nape Nnauye aliwataka viongozi wa chama hicho kutangaza hadharani kuwa wanamkubali Rais Magufuli kabla ya kuchambua siku 120 za utawala wake.

“Hawa Chadema walimkataa Magufuli, walisema hawamtambui na hata bungeni walimsusia, leo wanawezaje kuchambua kazi zake?” alihoji Nape.

Nape ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alisema Watanzania wanajua kazi nzuri ya Dk Magufuli na kuwataka Chadema wauchambue utawala wake baada ya kumkubali.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene alisema haoni kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu katika utumbuaji wa majipu kwani umelenga kusaidia wananchi wa hali ya chini.

“Hata hivyo, kama kuna anayeona ameonewa hajazuiwa kwenda mahakamani kupinga na kupata haki yake. Ni lazima Serikali ifanye kazi yake,” alisema.

Kuhusu umeya, Mwambene alisema CCM haina kosa katika hilo, bali inafuata kanuni na taratibu akisema Chadema inajua kilichotokea na inachofanya sasa ni kutafuta visingizio tu na wala si kingine.

“Mbona waliposhinda umeya Ubungo CCM hawakuenda mahakamani? Waache taratibu zifanye kazi,” alisema.

Ummy aagiza utumbuaji majipu idara ya Afya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amezipa meno taasisi za idara ya afya, wakuu wa mikoa na wilaya kuwashughulikia wahudumu wa afya watakaokwenda kinyume na maadili ya kazi zao.

Ummy aliziagiza taasisi hizo ikiwamo Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT), Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC), makatibu tawala na wakurugenzi kuchukua hatua zinazostahili.

Waziri huyo alitoa tamko hilo jana, ikiwa ni wiki moja tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutumbua majipu kadhaa katika Hospitali ya Ligula mkoani Mtwara na baadaye Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamis Kigwangalla kufanya hivyo katika Hospitali ya Temeke.

Ummy aliyaagiza mabaraza hayo kuwachukulia hatua na kuwafutia usajili na leseni zao wahusika iwapo watabainika kwenda kinyume na maadili ya kazi zao.

Katika tamko hilo, alisema wizara haitawavumilia watumishi wa sekta ya afya watakaokwenda kinyume na matakwa ya maadili ya taaluma zao katika vituo vya kutolea huduma.

“Katika utoaji wa huduma za afya yapo maadili ambayo mtoa huduma anapaswa kuyajua na kuyazingatia ikiwamo faragha, uaminifu, usawa, usiri na uhusiano,” alisema.

Pia, alisema mtoa huduma anatakiwa kumheshimu mgonjwa.

Saturday, 5 March 2016

Semina ya neno la Mungu.

SEMINA YA NENO LA MUNGU.
                                                           UPONYAJI WA MOYO ULIOVUNJIKA
                                                           NA MWL MWAKESEGE.
                                                           MOSHI MJINI
                                                           TAR 17/2/2016
                                                                   DAY-2
Isaya 61:1 ‘’ Roho wa BWANA Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu BWANA amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwaganga WALIOVUNJIKA MOYO, kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao’’
Jana tuliangalia kwa sehemu na hapa leo nataka tuone kwa sehemu somo la jana, kama haukuwepo jitahid tafuta kanda na sikiliza na sikiliza. ‘’Somo la siku ya kwanza sijaweza kufanikiwa kulipata na sikupata nafasi ya kusikiliza hili nimelifuatilia kwa njia ya internet’’.
Tuendelee na semina sasa.
Summary ya somo la jana.
Maana ya moyo kibiblia.
1. Moyo ambao ni kiungo cha mwili wa mwanadamu ambao unasukuma
2. Moyo –roho ya mtu
3. Moyo nafsi ya mtu
4. Moyo kiini cha uhai wa mtu.

TUANGALIE MAANA YAKE NINI KUVUNJIKA MOYO.
Ni kuharibika kwa moyo kutokana na kuzidiwa na kitu ulichokibeba.
Mahali pengine ni moyo kujeruhika.
Waefeso 4:26-27 ‘’ Muwe na hasira ila msitende dhambi, wala jua lisichwe  na uchungu wenu bado haujawatoka. 27wala msimpe ibilisi nafasi’’.
Kwa hiyo ujue kabisa moyo haujaumbwa kukaa na hasira kwa Zaidi ya masaa 12.

MAGONJWA YA MWILI YANAYOSABABISHWA NA MOYO KUJERUHIWA.
Roho yako ikizidiwa  nayo nafsi yako itazidiwa na mwili wako pia utazidiwa.
Yeremia 51:52’’ 52‘‘Lakini siku zinakuja,’’ asema BWANA, “nitakapoadhibu sanamu zake, na katika nchi yake yote WALIOJERUHIWA WATALIA WATAUGUA.’’
Kuwa na majeraha ndani ya moyo wa ndani husababisha kuugua kwa mwili. Ndio maana kuna baadhi ya magonjwa daktari atakuuliza anaweza kukuuuliza maswali ya kiroho  maana magonjwa mengine sababu zae ni za kiroho au mwingine atakuuliza sababu za kisaikolojia.

1. UBOVU WA MIFUPA.
Mithali 17:22 ‘’ 22Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyonyong’onyea HUKAUSHA MIFUPA’’
Mithali 14:30 ‘’ 30Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu HUOZESHA MIFUPA
Mithali 3:5-8 ‘’ 5Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe, 6katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako. 7Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe, mche BWANA ukajiepushe na uovu. 8Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako’’.

Tukiangalia maneno hayo hapo juu tunajifunza ya kuwa hali ya moyo wako inaathiri sana mifupa. Na tatizo kubwa sana la mifupa ni kukauka kwa mafuta, ndio maana miguu au viungo vinaanza kukuuma sana kwa sababu mafuta hamna kwenye mifupa nayo yamekauka.

Na kila hali inayokutokea jaribu kutafuta sababu za moyo kuvunjika kwenye biblia nazo utazipata.
WAFILIPI 4:6-7 ‘’ 6Msijisumbue kwa jambo lo lote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itawalinda MIOYO YENU NA NIA ZENU KATIKA KRISTO YESU.’’
Kwa hiyo jua ya kuwa akili iko kwenye nafsi na ubongo upo kwenye mwili. Kwa hiyo Mungu katuruhusu kutumia akili na sio tuzitegemee ndio maana anatusisitiza kuwa tumtegee Mungu bali tutumie akili zetu vizuri huku tukimtegemea Mungu wetu.
Na ukiona moyoni mwako una pressure au stress basi ujue kuwa kuna kitu hakiko sawa na cheki vizuri hili.

2. VIDONDA VYA TUMBO.
Mithali 26:22, 28, 20-22.  22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu, HUINGIA SEHEMU ZA NDANI SANA ZA TUMBO 28Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu. 20Bila kuni moto huzimika, pasipo uchongezi ugomvi humalizika. 21Kama makaa juu ya makaa yanayowaka na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi. 22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu, huingia sehemu za ndani sana za mtu. 
Nataka uone neno hili la sehemu za ndani sana za tumbo kwa hiyo chanzo cha vidonda vya tumbo pia ni kusikia maneno ambayo yanakujeruhi na moyo wako.

Ayubu 34:6 ‘’ Ingawa niko sawa, ninaonekana mwongo, nami ingawa sina kosa, kJeraha langu haliponyeki.
Zaburi 69:20 ‘’ 20Laumu zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata ye yote, wa kunituliza, lakini sikumpata ye yote.
Watu wengi baada ya kulaumiwa huwa wanavunjika moyo , na kilichosababisha kuvunjika moyo ni kwa sababu umelaumiwa sana. Au watu wengine wakisingiziwa huwa hali yake ya ndani inaharibika kabisa yaani anaumia na mwisho wake ni kukata tamaa. Moyo watu mtu hauwezi ustahimili lawama maana madhara ya kulaumiwa ni kuvunjika moyo na ndio maana biblia imekataza kualumu.

Ukisika tumbo limechafua basi ujue moyo wako umezidiwa, yaani tumbo lako kuchafuka baada ya kusikia habari Fulani. Hii huweza kukudhuru sana usipojua namna ya kushughulika na habari mabay zinazokujia.
Pia jua kabisa kama moyo wako hauwezi kusatihimili hilo jambo basi ujue tu itasukumia kwenyenafsi nayo nafsi itasukumia kwenye mwili wako na hapo ndipo unaanza kuona madhara kabisa mwili mwako.

Ndio maana kuna aina ya vidonda ambavyo madaktari hawawezi kutibu na chanzo kikuu ni sababu za kiroho ndani ya mtu. Ndio maana biblia imesema vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kushindana siku ya uovu. Maana shetani anatumia mbinu nyingi sana ili kuweza kuwaangamiza watu.
Na ndio maana mtu akizidiwa sana na majeraha sana moyoni mwake mara ataanza kuona tumbo linajaa gesi tumboni, na nyango humwagika sana tumboni mwako. Na sababu zake kubwa sana ni hali za kiroho ,ndicho chanzo kikuu.

3. KUISHIWA NA NGUVU MWILINI.
Zaburi 38:5-10, 5Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.6Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.7Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu.8Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni.9Ee BWANA, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani sana kwangu hakufichiki mbele zako. 10Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia, hata macho yangu yametiwa giza.

Moyo wako ukiumia unaishiwa na nguvu.
Kwa mfano mtu alikuwa na duka lake na limejaa sana na aje apewe taarifa kuwa duka lake limeungua na utoana kuwa anaanza kulia na wengine utaona wanapoteza na fahamu na muda mwingine hali inaweza ikawa mbaya Zaidi. Na sababu kubwa ni kuwa moyo wako umeumia kiasi kikubwa sana.

4. UGONJWA WA NGOZI YA USO.
Mithali 15:13 ‘’ 13Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.’’
Mithali 14:10-13 ‘’ Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, wala hakuna ye yote awezaye kushiriki furaha yake.11Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. 12Iko njia ionekanayo sawa kwa mtu, bali mwishoni huelekea mautini. 13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.
Ndio maana mtu kama ni mlevi angalia sana sura yake utagundua tu sura yake inaanza kuzeeka kabisa na afya ya uso wake inadhurika kabisa.

Mithali 10:10-13 ‘’ 10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia. 11Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.12Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote. 13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.

Ndio maana mtu akiwa na jambo zito au huzuni moyoni mwake au akiwa na hai ngumu suluhu sio kuanza ulevi bali nenda mbele za Mungu na Mungu akusaidie na ndio maana katika Mathayo Yesu alisem a njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo name ntawapumzisha.

Mungu akikupa mzigo, mzigo wake unabebeka kabisa. Moyo wako ukiumia basi peleka mzigo wako kwa Bwana usikae nao maana utakulemea kabisa. Moyo wako ukiumia na afya ya uso wako inaharibika na unazeeka kabla ya wakati.

Ndio maana mtu akiumia moyo wako Mungu hataki uponye juu juu anataka uponye hadi na chanzo chake. Yeremia 6:14 ‘’ 14Hufunga majeraha ya watu wangu kama vile hawakuumia sana. Husema, ‘Amani, amani,’ wakati hakuna amani.’’

MPAKA MTU ANAKATA TAMAA UJUE VITU HIVI VITATU VINATOKEA.
1.Kuna chanzo cha kuvunjika moyo,
2.Moyo uankuja kujerehiwa
3.Ndipo unaona matokeo ya moyo kuvunjika.

Jifunze kushughulika na chanzo na sio matokeo.

TUANGALAIE VYANZO VYA MOYO KUVUNJIKA/KUKATA TAMAA.
1.Uchungu uliozidi, husababisha magonjwa kama kuuma mifupa, kuharibika kwa sura yako.n.k
2.Huzuni, huzuni kwa mwanadamu ni kitu kigeni yaani hutoka kwa Mungu au kwenye mazingira nayo huleta madhara
3.Hasira, ukiwa na hasira sana nayo pia itadhuru tu mwili wako.
4. Kutikusamehe, kama nafsi yako imembeba mtu na hujaweza kumsamehe angali matokeo yake utiana kabisa kuna vitu vinakwama maishani mwako.
5. Kujisikia vibaya moyoni au tumboni unaposingiziwa au kusemwa vibaya. Jifunze namna ya kusonga mbele.
6.Kusikia habari mbaya.kwa mfano mtu wa karibu yako amekufa  na angalia ulishughulikaje, ndio maana ukitokea msiba mwingine unakuwa unakumbuka tu lileliliokufika  hivyo nenda kwene biblia tafuta namna ya kushughulika nayo.
Ndio maana Yesu alisema farijianeni kwa maneno haya.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

Mwigulu Nchema vs TASGA

MUUNGWANA BLOG / 25 minutes ago

Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba ameusimamisha uongozi wa chama cha wakulima wa miwa Tanzania (TASGA) baada ya kubaini kuwepo vitendo vya unyanyasaji.

Tuhuma nyingine ni kushindwa kuwasaidia wakulima wa miwa na kusababisha migogoro kati wakulima na kiwanda cha sukari cha Kilombero.

Akizungumza katika mkutano wa wakulima wa miwa wa bonde la Ruhembe waziri Mwigulu amesema serikali haiwezi kuvumilia viongozi wanaotumia madaraka yao kuwanyanyasa na kuwagandamiza wakulima.

Mwigulu ameagiza mkuu wa mkoa na uongozi wa wilaya kuwasimamia wakulima hao kuhakikisha wanapata uongozi wa muda ndani ya siku mbili huku akiwataka wawekezaji kuwalinda wakulima kimaslahi ili waweze kunufaika na rasilimali zilizopo nchini kwa kuzingatia masharti ya serikali.

Awali wakitoa kilio chao mbele ya waziri huyo, wakulima hao wamemwambia waziri kuwa pamoja na changamoto lukuki zinazowakabili mwenyekiti wao amekuwa kikwazo cha maendeleo ya wakulima wa Ruhembe ikiwa ni pamoja na kubadilisha katiba ya chama kwa lengo la kuendelea kubaki madarakani.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mikumi mheshimiwa Joseph Haule ameshukuru ujio wa waziri wa kilimo kwani hali ya wakulima wa miwa wa bonde hilo ni mbaya kutokana na unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vyao pamoja na wawekezaji kwa kuwanyima haki wakulima wa miwa.

NDOA YA RAYUU YAVUNJIKA NDANI YA WIKI MOJA.

Baada ya kutamba kuwa tayari amepata mume wa maisha, mambo yameharibika msanii wa filamu Rayuu, kwani sasa hatoki nje wale hapokei simu za shoga zake.

Wiki moja iliyopita msanii huyo aliiteka mitandao ya kijamii hasa instagram, kwa picha zake za harusi huku akiwa na bwana ake ambaye sasa si bwana tena.

Chanzo kikubwa cha kuvunjika kwa ndoa hiyo inadaiwa kuwa mwanaume ambaye alimuoa ni mume wa mtu, ambaye tayari mke wake ana ujauzito wa miezi mitatu, lakini pia inadaiwa kuwa ni kutokana na matukio kadhaa ya msanii huyo.

Rayuu alitafutwa ili kujibu tuhuma za kuachika, alijibu yote ni matokeo na kuachika kwake isiwe sababu ya yeye kusemwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Sina muda wa kuzungumzia mambo hayo kwani nilipofunga ndoa sikusema, sitaki nasema sitaki, maana watu wanaona ni jambo la kuzungumzwa mbona wapo wanaoolewa kifahari na wanaachika,” alisema kwa ukali kisha akakata simu.

JIDE NDOA TENA.

 Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide.

Dar es Salaam: Siku chache baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’, mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja na ujio mpya alioubatiza jina la Naamka Tena, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide amedaiwa kupata mwanaume mwingine ambaye yupo kwenye mikakati kabambe ya kumuoa, Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.

Jide ambaye amekuwa kimya kimuziki kwa zaidi ya miaka miwili, Februari mwaka huu alipewa talaka katika Mahakama ya Manzese-Sinza jijini Dar baada ya mvutano uliodumu kwa muda mrefu tangu wawili hao washindwe kuishi pamoja.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Jide alimpata mwenza muda mrefu tangu walipomwagana na Gardner lakini mipango ya ndoa ikashindwa kwenda haraka kwa sababu hakuwa amepewa talaka hiyo aliyoidai mahakamani.

“Mbona Jide kitambo tu alishapata mtu sema alikuwa hawezi kufanya mambo ya ndoa kwani hakuwa amepewa talaka na Gardner ila sasa hivi yupo huru na mwaka huuhuu huenda kikaeleweka,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Sema Jide kama unavyomjua, mtu wa usiri sana. Anatumia nguvu nyingi kweli kumficha mchumba wake wa sasa. Hataki watu wamjue.”

Mwanahabari wetu alijaribu kumvutia waya Jide kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopatikana aliomba  asizungumzie mambo ya uhusiano na badala yake akadai aulizwe kuhusu ujio wake mpya.

“Niulize kuhusu program yangu ya Naamka Tena, nipo bize kuandaa ngoma hiyo na kama unavyoona siku chache zijazo natarajia kuiachia, inanifanya niwe bize sana please niache kwanza,” alisema Jide.

Hata hivyo, mmoja wa mameneja wa msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kile alichoeleza kuwa hapaswi kumsemea Jide katika masuala ya uhusiano, alikiri Jide kuwa na mchumba ambaye wapo katika hatua nzuri ya kuyaanza maisha ya ndoa.

Mbowe kuzungumza na Taifa kupitia waandishi wa habari leo

Mbowe Kuzungumza na Taifa Kupitia Waandishi wa Habari Makao Makuu CHADEMA Leo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe leo atazungumza na Taifa kupitia mkutano wa waandishi wa Habari.

Mkutano huo wa waandishi utafanyika saa 6 mchana makao makuu Kinondoni Ufipa.

Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini anatarajiwa kutoa tamko rasmi la maazimio ya Kamati kuu ya chama iliyokutana Machi 1

Tayari vyombo vya ndani na nje ya nchi vimealikwa kwenye mkutano huo na imetakiwa ifikapo saa 5 asubuhi waandishi wote wawe wamekaa kwenye nafasi zao.

Mwenyekiti huyo anabashiriwa mbali na mambo kadhaa lakini atatoa msimamo rasmi wa chama kuhusiana na hujuma ya watawala dhidi ya uchaguzi wa meya wa DSM

Friday, 4 March 2016

Kiwanda cha rangi chateketea kwa moto.

Ghara la kuhifadhia rangi kwenye kiwanda cha Sadoline kilichopo maeneo ya tazara  Dar es salaam,   baada ya kuungua  moto ambao bado haujafahamika mpaka sasa nini chanzo chake. Kwa mujibu wa mkaguzi msaidizi wa jeshi la zima moto wilaya ya Kinondoni adam hamisi ngao amesema moto huo ulianza  kuwaka muda wa saa moja za usiku .

Walimu wasimamishwa kazi Mwanza.

 Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi.

Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013.

Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel.

Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga.

Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambulisho (passport size).

Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, kuchunguza tuhuma dhidi ya walimu hao kujihusisha na mapenzi na wanafunzi imebaini ukweli baada ya kuwahoji wanafunzi kadhaa.

“Ni fedheha na haivumiliki kuona walimu wakifanya mapenzi na wanafunzi wao. OCD wakamate walimu wote na uanze uchunguzi mara moja na kukusanya ushahidi utakaowezesha wahusika kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Mulongo.

Amri hiyo ilitekelezwa mara moja kwa walimu hao kuwekwa chini ya ulinzi.

Mulongo pia alimwagiza Katibu wa Idara ya Utumishi wa Walimu Mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani kuwaandikia barua za onyo walimu wa kike shuleni hapo kwa kushindwa kulinda na kutetea masilahi ya wanafunzi wa kike waliokuwa wakidhulumiwa kingono na walimu wenzao kiasi cha baadhi yao kuathirika kisaikolojia.

Pia, alimwagiza Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Khamisi Maulid kuangalia uwezekano wa kuwahamishia shule nyingine wanafunzi waliodhulumiwa kingono na walimu wao ili kuwaepusha na matatizo ya kisaikolojia.

Maulidi alisema wanafunzi walioathirika zaidi ni wale wa kidato cha nne.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Mwanza, Said Mselem alisema kitendo hicho kimeifedhehesha taaluma ya ualimu na kuahidi kuwa ofisi yake itatanua wigo wa uchunguzi hadi kwenye shule nyingine.

Kinachosababisha macho kutokuona!

Dk Isaack Maro 

Macho ni moja ya milango mitano ya fahamu. Kazi yake ni kuhakikisha binadamu anaona mazingira yanayomzunguka. Bila macho huwa ni vigumu kwa binadamu kuyatawala mazingira yake.

Ili kuweza kutawala vyema mazingira yake binadamu anahitaji macho ambayo yanaona vizuri na mfumo wa fahamu ambao unaweza kutafsiri mwanga wa taswira ambao unafikishwa kwenye ubongo kupitia macho.

Kwenye makala yetu leo hii tunaangalia changamoto mbalimbali ambazo zinasababisha macho kushindwa kuona vizuri na matokeo yake kusababisha taswira yenye kasoro kwa ajili ya kutafsiriwa na ubongo. Macho kushindwa kuona vizuri husababisha mwanga wa taswira unaopelekwa kwenye ubongo kupitia mshipa maalumu wa fahamu wa macho kuwa na upungufu.

Ingawa tatizo linaweza kuwa kwenye jicho moja mara nyingi madhara yake kwenye tafsiri inayofanywa na ubongo huhusisha macho yote.

Dalili ni kama vile kuona taswira mbili tofauti kutokana na jicho moja kuona vizuri na jingine kutoona vizuri, kushindwa kuona au kupata matatizo ya kuona kwenye eneo lenye mwanga mdogo.

Dalili nyingine ni kushindwa kuona wigo mpana zaidi ya eneo ambalo jicho limedhamiria kutazama na kuona ukungu na kushindwa kutambua kitu vizuri. Kwa kawaida kushindwa kuona vizuri huwa ni tatizo la macho lakini mara nyingine hali hii hutokea pamoja na dalili nyingine. Inapotokea tatizo la kuona vizuri likaambatana na dalili nyingine mara nyingi huashiria tatizo kubwa linalohitaji kufanyiwa vipimo na kupatiwa ufumbuzi.

Dalili mbaya zinazoambatana na tatizo la kuona vizuri ni kama vile kichwa kuuma sana, kushindwa kuongea vizuri kunakoambatana na kushindwa kuona vizuri na kukosa nguvu mwilini; hususani kupoteza nguvu kwenye upande mmoja wa mwili

Dalili nyingine mbaya ni upande mmoja wa uso kushindwa kufanya kazi kabisa, maumivu makali ya macho na tatizo la kushindwa kuona vizuri kadiri siku zinavyoenda.

Kuna sababu nyingi zinazosababisha mtu kushindwa kuona vizuri. Baadhi ya sababu ni kama vile mtoto wa jicho, mkwaruzo au uambukizo kwenye jicho, kama vile korinea na retina, mbele wa jicho, maradhi yatokanayo na umri, kipanda uso, kisukari, kiharusi na majeraha.

Tatizo hili kwa watu wengi huanza taratibu na ili kuweza kujua chanzo cha tatizo ni muhimu sana kwa daktari kuuliza historia ya tatizo na kufanya vipimo vya kawaida vya macho na mwili kabla ya kumshauri mgonjwa kufanya vipimo vikubwa zaidi vya macho. Historia ya maradhi mengine ni muhimu pia kwa daktari kuifahamu kwa kuwa inaweza kuwa sababu ya tatizo a kutoona vizuri.

Vipimo vitakavyofanyika sio tu vitahusisha macho lakini pia inaweza kuhusisha mifumo mingine ya mwili kama damu na kadhalika.

Matibabu ya matatizo ya macho hutegemea matokeo ya vipimo vya chanzo vya tatizo. Chanzo cha tatizo hutoa mwanga wa kama tatizo linatibika ama halitibiki. Kwa wengi wenye tatizo la kutoona vizuri matibabu ya tatizo huhusisha tiba ya chanzo halisi.

Matibabu hulenga kutatua chanzo cha tatizo na kutatua tatizo la macho. Kinga ya matatizo mengi ya macho huhusisha ulinzi wa macho kwa kuyakinga na madhara ya moja kwa moja.

Kutokana na sababu za tatizo kuhusisha mifumo mingine pia ni vyema tutambue kuwa kulinda afya kwa ujumla kunaweza kusaidia kukinga macho na tatizo hili.

Vaa miwani ya kuzuia mwanga mkali, kula mlo wenye virutubisho muhimu kwa macho na nawa mikono kabla ya kugusa macho kwa vidole.