WAFILIPI 4:6
Msijisumbue kwa neno lolote;Bali katika kila neno kwa kusali na kuomba,pamoja na kushukuru,haja zenu na zijulikane na Mungu.
ISAYA 41:21
Haya,leteni maneno yenu,asema BWANA;Toeni hoja zenu zenye nguvu,asema mfalme wa Yakobo.
YEREMIA 33:3
Niite,nami nitakuitikia,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajuwa.
Mpendwa nimekuletea maandiko haya kwa lengo moja tu,kwamba twende mbele za Mungu muda na wakati kama huu,tumpelekee hoja zenu zenye nguvu,yaani tumpe mahitaji yetu.
Mpendwa ninajuwa hapo ulipo una mahitaji mengi ambayo unahitaji Mungu akutendee,hivyo ninakuomba Mpendwa japo kwa mda mfupi tu,twende mbele za Mungu,tumuite naye ni mwingi wa rehema atatuitikia.
Kumbuka yeye anasema
Tazama,mimi ni BWANA,Mungu wa wote wenye mwili;je kuna neno gumu lolote nisiloliweza?
Nakuambia Mpendwa hakuna gumu mbele za BWANA.
Hivyo simama tumwombe Mungu mpendwa,mwambie haja ya moyo wako muda na wakati kama huu,kwa imani naamini utapokea.
Simama mpendwa tuombe na Mungu atakujibu kwa wakati wake.
Najuwa umeomba sana mpendwa,hadi ukaisi kwamba Mungu hayupo,ni kwambia usikate tamaa,maaombi ya mwenye haki yanafaa akiomba kwa bidii.
Hivyo usichoke Mpendwa.
~Tubu kwanza dhambi zako mbele za Mungu.
~Omba kwa imani
~Omba kupitia jina la Yesu Kristo.
~Omba kwa utaratibu
~Omba kwa kumaanisha....
Simama kwa miguu yako Mpendwa, tuombe,paza sauti yako, Mungu anakujibu.
Be blessed, ameen!
No comments:
Post a Comment