Thursday, 10 March 2016

Mwalimu kutoroka kituo cha kazi kisa mimba!

Nyang’hwale. Mwalimu mmoja wa Shule Sekondari Nyugwa wilayani hapa Mkoa wa Geita anadaiwa kutoroka katika kituo chake cha kazi kwa
tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wake wa kidato cha tatu.

Inadaiwa baada ya mwanafunzi huyo
(jina linahifadhiwa) kubainika kuwa na ujauzito, mwalimu huyo aliamua kushirikiana na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Kharumwa kutoa. Inadaiwa Machi 3, ndiyo mimba hiyo ilitolewa kwa ushirikiano wa daktari na muuguzi waliokuwa zamu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa shule hiyo, Henrick Jembe alidai Februari 18, mwanafunzi huyo aliomba ruhusa kwenda hospitali akidai anaumwa.
“Ingawa sikuwapo shuleni siku hiyo, lakini kumbukumbu zinaonyesha mwanafunzi huyu alipewa ruhusu baada ya kukamilisha utaratibu
ikiwamo kuandikiwa daftari la
kumuwezesha kupatiwa matibabu,”alidai mkuu huyo wa shule na kuongeza:

“Alisindikizwa na wanafunzi wenzake wawili, mmoja wa kiume na mwingine
wa kike.”
Alidai waliporejea shuleni, mwanafunzi huyo alisema baada ya vipimo alikutwa
na vimelea vya malaria, hivyo
akaruhusiwa aende nyumbani
kupumzika.

“Lakini baada ya siku mbili nilipokea wito kutoka polisi nikitakiwa kufika na mwalimu anayetuhumiwa ambaye siku
hiyo alikuwa na kazi ya kushughulikia chakula cha wanafunzi, ikabidi niende
mwenyewe na kukuta maelezo kuwa mwanafunzi wangu ana ujauzito na anayetuhumiwa ni huyo mwalimu,” alidai Jembe na kuongeza:

“Nadhani alipopata taarifa kuwa anatuhuma hizo aliamua kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.”

Katibu Mkuu Idara ya Utumishi wa Walimu wilayani hapa, Aron Andrew alisema baada ya kumhoji mwanafunzi
huyo alibaini kuwa alianza uhusiano wa mapenzi na mwalimu wake tangu
mwaka jana.

“Alisema baada ya kutolewa mimba, mwalimu wake alimsafirisha hadi jijini
Mwanza kwa mtu aliyemtambulisha
kwake kuwa ni dada wa mtuhumiwa ili ajiuguze huku akiendelea kunywa dawa
alizoandikiwa hospitali,”alisema.

Hata hivyo, alisema hawawezi
kuchukua hatua yoyote dhidi ya mwalimu huyo kwa sasa kwa sababu wanasubiri taarifa kutoka kwa mwajili
wa mwalimu huyo ambaye ni
mkurugenzi.

Alisema mwajiri huyo akitoa taarifa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi mwalimu huyo kwa kuwa amekiuka sheria na kanuni za utumishi
wa umma.

Kaimu Mkurugenziwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Venance
Ngeleuya alisema ofisi yake pia
haijapokea taarifa za tuhuma hizo na kusisitiza watafuatilia.
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk Lutale Josephat alisema ofisi yake
itachukuwa hatua kama itathibitika kuwa baadhi ya watumishi wa kituo cha afya cha Kharumwa walishiriki
kumtoa mimba mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Ibrahimu Marwa alisema
amewaagiza polisi wilayani hapa kumsaka na kumtia mbaroni mwalimu huyo ili afikishwe mahakamani kujibu
mashtaka ya tuhuma zinazomkabili.

No comments:

Post a Comment