Saturday, 5 March 2016

Semina ya neno la Mungu.

SEMINA YA NENO LA MUNGU.
                                                           UPONYAJI WA MOYO ULIOVUNJIKA
                                                           NA MWL MWAKESEGE.
                                                           MOSHI MJINI
                                                           TAR 17/2/2016
                                                                   DAY-2
Isaya 61:1 ‘’ Roho wa BWANA Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu BWANA amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwaganga WALIOVUNJIKA MOYO, kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao’’
Jana tuliangalia kwa sehemu na hapa leo nataka tuone kwa sehemu somo la jana, kama haukuwepo jitahid tafuta kanda na sikiliza na sikiliza. ‘’Somo la siku ya kwanza sijaweza kufanikiwa kulipata na sikupata nafasi ya kusikiliza hili nimelifuatilia kwa njia ya internet’’.
Tuendelee na semina sasa.
Summary ya somo la jana.
Maana ya moyo kibiblia.
1. Moyo ambao ni kiungo cha mwili wa mwanadamu ambao unasukuma
2. Moyo –roho ya mtu
3. Moyo nafsi ya mtu
4. Moyo kiini cha uhai wa mtu.

TUANGALIE MAANA YAKE NINI KUVUNJIKA MOYO.
Ni kuharibika kwa moyo kutokana na kuzidiwa na kitu ulichokibeba.
Mahali pengine ni moyo kujeruhika.
Waefeso 4:26-27 ‘’ Muwe na hasira ila msitende dhambi, wala jua lisichwe  na uchungu wenu bado haujawatoka. 27wala msimpe ibilisi nafasi’’.
Kwa hiyo ujue kabisa moyo haujaumbwa kukaa na hasira kwa Zaidi ya masaa 12.

MAGONJWA YA MWILI YANAYOSABABISHWA NA MOYO KUJERUHIWA.
Roho yako ikizidiwa  nayo nafsi yako itazidiwa na mwili wako pia utazidiwa.
Yeremia 51:52’’ 52‘‘Lakini siku zinakuja,’’ asema BWANA, “nitakapoadhibu sanamu zake, na katika nchi yake yote WALIOJERUHIWA WATALIA WATAUGUA.’’
Kuwa na majeraha ndani ya moyo wa ndani husababisha kuugua kwa mwili. Ndio maana kuna baadhi ya magonjwa daktari atakuuliza anaweza kukuuuliza maswali ya kiroho  maana magonjwa mengine sababu zae ni za kiroho au mwingine atakuuliza sababu za kisaikolojia.

1. UBOVU WA MIFUPA.
Mithali 17:22 ‘’ 22Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyonyong’onyea HUKAUSHA MIFUPA’’
Mithali 14:30 ‘’ 30Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu HUOZESHA MIFUPA
Mithali 3:5-8 ‘’ 5Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe, 6katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako. 7Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe, mche BWANA ukajiepushe na uovu. 8Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako’’.

Tukiangalia maneno hayo hapo juu tunajifunza ya kuwa hali ya moyo wako inaathiri sana mifupa. Na tatizo kubwa sana la mifupa ni kukauka kwa mafuta, ndio maana miguu au viungo vinaanza kukuuma sana kwa sababu mafuta hamna kwenye mifupa nayo yamekauka.

Na kila hali inayokutokea jaribu kutafuta sababu za moyo kuvunjika kwenye biblia nazo utazipata.
WAFILIPI 4:6-7 ‘’ 6Msijisumbue kwa jambo lo lote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itawalinda MIOYO YENU NA NIA ZENU KATIKA KRISTO YESU.’’
Kwa hiyo jua ya kuwa akili iko kwenye nafsi na ubongo upo kwenye mwili. Kwa hiyo Mungu katuruhusu kutumia akili na sio tuzitegemee ndio maana anatusisitiza kuwa tumtegee Mungu bali tutumie akili zetu vizuri huku tukimtegemea Mungu wetu.
Na ukiona moyoni mwako una pressure au stress basi ujue kuwa kuna kitu hakiko sawa na cheki vizuri hili.

2. VIDONDA VYA TUMBO.
Mithali 26:22, 28, 20-22.  22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu, HUINGIA SEHEMU ZA NDANI SANA ZA TUMBO 28Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu. 20Bila kuni moto huzimika, pasipo uchongezi ugomvi humalizika. 21Kama makaa juu ya makaa yanayowaka na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi. 22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu, huingia sehemu za ndani sana za mtu. 
Nataka uone neno hili la sehemu za ndani sana za tumbo kwa hiyo chanzo cha vidonda vya tumbo pia ni kusikia maneno ambayo yanakujeruhi na moyo wako.

Ayubu 34:6 ‘’ Ingawa niko sawa, ninaonekana mwongo, nami ingawa sina kosa, kJeraha langu haliponyeki.
Zaburi 69:20 ‘’ 20Laumu zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata ye yote, wa kunituliza, lakini sikumpata ye yote.
Watu wengi baada ya kulaumiwa huwa wanavunjika moyo , na kilichosababisha kuvunjika moyo ni kwa sababu umelaumiwa sana. Au watu wengine wakisingiziwa huwa hali yake ya ndani inaharibika kabisa yaani anaumia na mwisho wake ni kukata tamaa. Moyo watu mtu hauwezi ustahimili lawama maana madhara ya kulaumiwa ni kuvunjika moyo na ndio maana biblia imekataza kualumu.

Ukisika tumbo limechafua basi ujue moyo wako umezidiwa, yaani tumbo lako kuchafuka baada ya kusikia habari Fulani. Hii huweza kukudhuru sana usipojua namna ya kushughulika na habari mabay zinazokujia.
Pia jua kabisa kama moyo wako hauwezi kusatihimili hilo jambo basi ujue tu itasukumia kwenyenafsi nayo nafsi itasukumia kwenye mwili wako na hapo ndipo unaanza kuona madhara kabisa mwili mwako.

Ndio maana kuna aina ya vidonda ambavyo madaktari hawawezi kutibu na chanzo kikuu ni sababu za kiroho ndani ya mtu. Ndio maana biblia imesema vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kushindana siku ya uovu. Maana shetani anatumia mbinu nyingi sana ili kuweza kuwaangamiza watu.
Na ndio maana mtu akizidiwa sana na majeraha sana moyoni mwake mara ataanza kuona tumbo linajaa gesi tumboni, na nyango humwagika sana tumboni mwako. Na sababu zake kubwa sana ni hali za kiroho ,ndicho chanzo kikuu.

3. KUISHIWA NA NGUVU MWILINI.
Zaburi 38:5-10, 5Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.6Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.7Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu.8Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni.9Ee BWANA, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani sana kwangu hakufichiki mbele zako. 10Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia, hata macho yangu yametiwa giza.

Moyo wako ukiumia unaishiwa na nguvu.
Kwa mfano mtu alikuwa na duka lake na limejaa sana na aje apewe taarifa kuwa duka lake limeungua na utoana kuwa anaanza kulia na wengine utaona wanapoteza na fahamu na muda mwingine hali inaweza ikawa mbaya Zaidi. Na sababu kubwa ni kuwa moyo wako umeumia kiasi kikubwa sana.

4. UGONJWA WA NGOZI YA USO.
Mithali 15:13 ‘’ 13Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.’’
Mithali 14:10-13 ‘’ Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, wala hakuna ye yote awezaye kushiriki furaha yake.11Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. 12Iko njia ionekanayo sawa kwa mtu, bali mwishoni huelekea mautini. 13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.
Ndio maana mtu kama ni mlevi angalia sana sura yake utagundua tu sura yake inaanza kuzeeka kabisa na afya ya uso wake inadhurika kabisa.

Mithali 10:10-13 ‘’ 10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia. 11Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.12Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote. 13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.

Ndio maana mtu akiwa na jambo zito au huzuni moyoni mwake au akiwa na hai ngumu suluhu sio kuanza ulevi bali nenda mbele za Mungu na Mungu akusaidie na ndio maana katika Mathayo Yesu alisem a njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo name ntawapumzisha.

Mungu akikupa mzigo, mzigo wake unabebeka kabisa. Moyo wako ukiumia basi peleka mzigo wako kwa Bwana usikae nao maana utakulemea kabisa. Moyo wako ukiumia na afya ya uso wako inaharibika na unazeeka kabla ya wakati.

Ndio maana mtu akiumia moyo wako Mungu hataki uponye juu juu anataka uponye hadi na chanzo chake. Yeremia 6:14 ‘’ 14Hufunga majeraha ya watu wangu kama vile hawakuumia sana. Husema, ‘Amani, amani,’ wakati hakuna amani.’’

MPAKA MTU ANAKATA TAMAA UJUE VITU HIVI VITATU VINATOKEA.
1.Kuna chanzo cha kuvunjika moyo,
2.Moyo uankuja kujerehiwa
3.Ndipo unaona matokeo ya moyo kuvunjika.

Jifunze kushughulika na chanzo na sio matokeo.

TUANGALAIE VYANZO VYA MOYO KUVUNJIKA/KUKATA TAMAA.
1.Uchungu uliozidi, husababisha magonjwa kama kuuma mifupa, kuharibika kwa sura yako.n.k
2.Huzuni, huzuni kwa mwanadamu ni kitu kigeni yaani hutoka kwa Mungu au kwenye mazingira nayo huleta madhara
3.Hasira, ukiwa na hasira sana nayo pia itadhuru tu mwili wako.
4. Kutikusamehe, kama nafsi yako imembeba mtu na hujaweza kumsamehe angali matokeo yake utiana kabisa kuna vitu vinakwama maishani mwako.
5. Kujisikia vibaya moyoni au tumboni unaposingiziwa au kusemwa vibaya. Jifunze namna ya kusonga mbele.
6.Kusikia habari mbaya.kwa mfano mtu wa karibu yako amekufa  na angalia ulishughulikaje, ndio maana ukitokea msiba mwingine unakuwa unakumbuka tu lileliliokufika  hivyo nenda kwene biblia tafuta namna ya kushughulika nayo.
Ndio maana Yesu alisema farijianeni kwa maneno haya.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

No comments:

Post a Comment